Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

Nabii hakubaliki nyumbani kwake. Hata Jesus alipigwa mawe, leo hii tunachoringia Tanzania sio kinachofanyika na viongozi wa sasa.

Nyerere angekuwa dictactor Salim A. Salim angekuwa rais na che nkapa asingeona kitu hata Mwinyi angeishia Zanzibar tu.
 
Nyani, a leader who doesn't have such tendencies would not be a leader of a nation! It just tell us he is just human! But calling Nyerere a dictactor is an insult to history, a hateful attempt to demonize him, and indeed don't tell me the millions of people who lined up at his funeral, those who cried at his passing didn't know what kind of a dictactor Nyerere was; Don't tell me when John Malecela led with the then VP to retrieve Mwalimu's remains from London he was happy that a "dictator" died! Don't tell me when JM called himsef in the presence of Mama Nyerere that "Baba ametutoka" and that he (Malecela) was a astudent of Mwalimu too! C'mmon I mean Nyerere had many shortcomings and human flaws but a dictator? I mean mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni! He WAS NOT A DICTATOR.. no Sir he was not!

Look here...he was not a dictator in the strict sense of the word. At least I'm not ready to call him that. But, when you look at the powers that he had, he could have easily become one. Now, question is, why didn't repeal those powers that he could have used to oppress others if he didn't enjoy the safeguards they provided? Isn't that a dictatorial tendency?
 
Nabii hakubaliki nyumbani kwake. Hata Jesus alipigwa mawe, leo hii tunachoringia Tanzania sio kinachofanyika na viongozi wa sasa.

Nyerere angekuwa dictactor Salim A. Salim angekuwa rais na che nkapa asingeona kitu hata Mwinyi angeishia Zanzibar tu.

Maelezo yako, yana-prove kwamba alikuwa dikteta. Kwani hata leo hii lau kama angelikuwa hai, basi tusingekuwa na "muungwana" kwenye state house. The dude ran the show hata baada ya kutoka madarakani!!!!. Kwani si ni yeye aliebadili katiba na kukaa madarakani kwa miongo miwili na ni yeye tena aliyebadili katiba kuweka terms limit......hiyo ni double standard na ni tabia ya ki-dikteta. Kama isingekuwa hali mbaya ya kiuchumi, kusambaratika kwa sovieti, eastern bloc na ujamaa/ukomunist kwa ujumla basi babu bin dikteta kifimbo angefia ikulu akiwa kashika hatamu.

Hakuna aliyezaliwa dikteta, u-dikteta ni tabia progressive, ambayo inaweza kuwa stunted kwa kufikwa na guilty consciousness........Nyerere alikuwa ni dikteta, ambaye alifikia mahali akaona "hii inatosha," ili asi-fit kwenye typical definition ya neno!!!.
 
1. Don't tell me when John Malecela led with the then VP to retrieve Mwalimu's remains from London he was happy that a "dictator" died! Don't tell me when JM called himsef in the presence of Mama Nyerere that "Baba ametutoka" and that he (Malecela) was a astudent of Mwalimu too!

Wooow! kwanza ilikuwa dictionary, sasa imekuwa Malecela, sio thread ya Mwalimu tena? yote ili kumsafisha tu Mwalimu kuwa alikuwa malaika! Mkuu Malecela anayo thread yake na haihusinani in anyways na hii thread, unless kuihamisha hapa hii thread haikutohsa sasa unataka ifutwe kabisaa, lakini hata kama anahusiana haibadili mawazo ya baadhi yetu wananchi kama mimi kuwa Mwalimu alikuwa dikteta, maana mamuzi mengi ambayo yamelididimiza taifa letu kiuchumi na kisiasa, yalianzishwa na kupitishwa na yeye binafsi bila ridhaa zetu wananchi, lakini alikuwa mjanja enough ku-cover his back ili aonekane kuwa ni wananchi ndio walioamua tena under the law, ndio maana viongozi wetu walipopata nafasi tu ya kufanya maamuzi yao bila ya kuingiliwa na Mwalimu, cha kwanza walivunja Azimio La Arusha, waliomkatalia Salim asiwe rais walikuwa ni wa-Zanzibari ambao Mwalimu siku zote za uwatwala wake alikuwa akipata taaabu nao sana kuwaweka kwenye mstari wake, tunajua yaliyowapata Seif, Seif Bakari, Jumbe, Idrisa, na wengineo,

Ni Mwalimu, aliyetupatia the frauds kina Mwinyi, na Mkapa, tena akatuchagulia kwa nguvu, bila ridhaa zetu, mimi sihitaji kusoma maana ya u-dikteta kwenye vitabu wakati nimeuona mwenyewe kwa macho yangu na kuuishi, nimelimishwa shuleni kama punda bila sababu, nimesoma Europe sikulimishwa hata siku moja, to this day sielewi kwa nini nilikuwa ninalimishwa mazao ambayo baadaye Mwalimu mkuu aliyauza na kutia hela mfukoni mwake bila yaa kuulizwa na mtu yoyote,

2. C'mmon I mean Nyerere had many shortcomings and human flaws but a dictator? I mean mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni! He WAS NOT A DICTATOR.. no Sir he was not!

The ishu sio udikteta wa Mwalimu, kwani as long unailazimisha hiyo ishu kuwa dikteta badala ya shortcomings za Mwalimu kiuongozi na the outcome kwa taifa letu, basi utakuwa na a lot to say, lakini ukweli ni kwamba pamoja na kusiaidia nchi yetu Mwalimu, ndiye aliyeiuua nchi yetu kisisasa na kiuchumi, hakuwa dikteta if that makes you happy, lakini lawama za matatizo yetu as a nation yanakwenda miguuni kwake, he was a fraud ndio maana leo tumekuwa a national of fraud people, wanafiki, waongo, wapenda sifa bila matendo,

I mean ni taifa gani duniani linalofanana na sisi bongo? Viongozi wanasema one thing in public halafu wanafanya mengine kabisa behind the scene? Wananchi wanaandamana kupinga mafisadi halafu wanaichagua CCM?


3. C'mmon I mean Nyerere had many shortcomings and human flaws

Mkuu ni kwenye hii statement yako ya mwisho ndio matatizo yote ya nchi yetu yalipoanzia, sasa cha kusikitisha ni kwamba kuna waliojaribu kumfahamisha kuwa he was on the wrong track, wakaishia kuhamishiwa ubalozini nje ya nchi, au kupumzishwa kabisaa, Nyerere was the greatest, lakini pia he wa a flawed human being ambaye hakutaka ushauri, I mean kuwa flawed ni one thing, lakini kukataa ushauri ni absolutely another ishu ambayo ndio hasa bongo we are paying for mpaka leo! Lakini at the same token he was good politicain wa kuweza ku-shift the blame kwa Kawawa na Malecela, Kawawa ndiye aliyeamua maduka ya ushirika na kuvunja co-operatives, lakini sio mimi mimi nilimwambia asifanye alivyofanya, Malecela ndiye anayeleta matatizo ya taifa maana hapendi muungano, na ndio maana taifa linadidimia kiuchumi!
 
Nyerere angekuwa dictactor Salim A. Salim angekuwa rais na che nkapa asingeona kitu hata Mwinyi angeishia Zanzibar tu.

Asingekuwa, basi baaada ya wa-Zanzibari kumkatalia Salim, basi angamua kuacha ili wananchi waamue wenyewe, lakini hakukubali kushindwa akawalizimisha wamchague Mwinyi, ilipokuja mwisho wa Mwinyi huyo akaja tena Dodoma tena akifanya kampeni usiku usiku kwa kutembelea majumba ya wageni walikofikia wajumbe wa mkutano mkuu l;azima Mkapa, akachaguliwa siku ya sherehe ya Birthday yake aliyofanyiwa na Mkapa, ninayakumbuka maneno ya kejeli ya Mwalimu, kuwa

"..Sisi kina Nyerere tuna tabia ya kuishi kwa muda mrefu sana, kwa hiyo nitaishi long enough kushuhudia uchaguzi wa rais ujao baada ya Mkapa, kuna wanaotaka kunizunguka ili wagombee urais huko mbele nitakutana nao tu!......"

the next thing akaamua cheo cha makamu wa rais kitenganishwe na waziri mkuu, ikawa!, rais wa visiwani asiwe makamu wa kwanza, ikawa!, makamu wa rais lazima atoke Pemba, ikawa! uchaguzi wa Visiwani matokeo CCM ikashindwa yeye akasema CCM imeshinda, ikawa! Mkapa akaamua kuwa hataki kuwa mwenyekiti wa CCM, Mwalimu akasema akawa, Mkapa akauza NBC kwa bei poa kwenye dhana ya ubinafsishaji, ukawa ndio mwanzo na mwisho wa Mwalimu kusema hadharani tena!

Mungu Amuweke Mahali Pema Peponi!
 
hii kali
"...Mungu aibariki nchi yetu kwa watu wenye mawazo kama ya kwako ambao kutokana na chuki binafsi wanataka kuikana historia yao na kujaribu kwa nguvu zote kushetanisha (demonize) Nyerere just because they hate his guts! Mungu aibariki nchi hii kwa sababu watu hao wanainua kipimo cha juu kumpima Nyerere na hawako tayari kukubali kuwa Mwalimu alikuwa ni binadamu aliyefanya makosa kama wengine lakini he was not an evil man (that is what dictators become if you didn't know). Watu hawa ambao leo kwa sababu wanazozijua wao wanataka kumfuta Mwalimu kwenye historia na kumuinua mzugaji kisiasa ili waonekana wameachana na historia yao! Mungu aibariki nchi yetu kwa sababu watu hawa wanajaribu bila ya mafanikio kuandika upya historia ambayo wameitengeneza wao wenyewe! Ati mwalimu Dikteta! Jamani tuwe wa kweli. Alikuwa na makosa na mapungufu, kumuita dikteta pamoja na chuki mlizonazo you all know it is not fair! it is not true, and it has no any factual basis! Ila kwa sababu ya chuki, you can go on calling him a dictactor while praising a political conman and a fraud, Oscar Kambona."
__________________

inapokuja kwa mwalimu na makosa aliyofanya inaitwa "ubinadamu" lakini makosa ya kambona yanaitwa "political fraud na yanafuta kabisa mchango wake kwa taifa"
 
inapokuja kwa mwalimu na makosa aliyofanya inaitwa "ubinadamu" lakini makosa ya kambona yanaitwa "political fraud na yanafuta kabisa mchango wake kwa taifa"

Good point!
 
cha kushangaza ni pale mtu anatoa hoja zake na kisha kutangaza ushindi! kwangu mimi japokuwa mada hii imehamishwa na kuwekwa kwenye vibweka nimefurahi kuona mitazamo mbali mbali ikielezwa hapa na nimejifunza mengi na mengine nimekumbuka ambayo niliisha yasahau.

naamini kabisa utafika wakati watanzania tutatizama nyuma na kuwaenzi vilivyo viongozi wetu waliopigania uhuru wa nchi hii. aidha utafika wakati ambapo tutakubali kwamba viongozi waanzilishi wa taifa hili walifanya makosa ama kwa makusudi au kwa kukosa uzoefu na tutajifunza kutokana na makosa hayo na kuendelea kulijenga taifa.

mola ibariki tanzania
 
Wasee,
Mtoto wa Gamal Nasser kwenye lile gazeti lake al nanilii(jina limenitoka), kwenye article moja anasema "Nyerere was African Dictator" ingawa kuna vitu anakubaliana nae ambavyo baba lake alipingana na Nyerere.

Ali Mazruhi wa Kenya pale Cornelly University, alikuwa short wa kusema Nyerere was a dictator kwa sababu alikuwa rafiki yake toka Makelele....ila aliita Tanzania ya Nyerere, "ROMANTIC TANZAPHILIA." Well haikuwa bahati mbaya, Prof Mazruhi alikuwa na rationale.......think vita vya Kagera na kuitambua Biafra, the rumor has it at least according to Mazruhi "udini." Kama ni kweli basi huo ni udikteta, kuweka maslahi ya taifa nyuma(hasa inapohusu usalama......kumbuka kisa cha Saddam wa Tikriti) kwa mambo binafsi!!.
 
Dictator Mwalimu Nyerere Mungu ampumzishe kwa amani.. ni aibu ni aibu tu, there is no defence. Watu wanazungumza kana kwamba ni wao peke yao walikulia miaka ya shida na njaa; wanazungumza kama ni wao peke yao waliojipanga kwenye "duka la kaya"; wanazungumza kama ni wao peke yao waliokuwa wakihangaika na mabasi ya Relwe na yale ya KAMATA; Wanazungumza kana kwamba ni wao pekee waliotoa baba zao na kuwapoteza kwenye vita ya Nduli huku watoto wakihangaika kuchimba mahandaki! Watu wanazungumza kana kwamba ni wa peke walikuwa dona, yanga, kuendesha gari jumapili hadi kibali cha Polisi! Wao wanazungumza kwa sababu wanaamini ni wao peke wanaujua ugumu ambao taifa hili limepitia! Leo watu wanavuna wallipopanda wengine! Bila haya hata aibu wanadiriki kumuweka Nyerere kwenye kundi la madikteta huku wakijaribu "kumuenzi" kwa mazuri machache!

Kweli tuna kazi, Nyerere alikuwa dikteta? yaani hata uzito wa maneno yao hawaupimi. Chuki dhidi ya Mwalimu kwa sababu matarajio ya watu hayakutimizwa imegeuzwa kuwa ni Udikteta. Leo wasimame basi viongozi mashujaa ambao wanaamini ndani ya mioyo yao kuwa Nyerere alikuwa ni dikteta! Binafsi, sina tatizo na yote mnayosema kuhusu mapungufu ya Mwalimu na makosa ya hapa na pale lakini kuliweka jina la Nyerere na Hitler, kuliweka jina la Nyerere na Milosevic, kuliweka jina la Nyerere na Saddam, na Mabotu, na Idi Amin.. yaani

Dikteta Adolf Hitler
Dikteta Saddam Hussen
Dikteta Nduli Idi Amin Dada
Dikteta Slobodan Milosevic
Dikteta Mobutu Seseseko
Dikiteta Mwalimu Julius K. Nyerere

really??????

Kafara, Kuhusu Kambona, nani kati yenu kasema Kambona alifanya makosa yoyote? Kwenu Kambona was the hero, hajakosea hata mahali pamoja na ni shujaa mtupu. Kama mnajua makosa ya Kambona yatajeni!

Kwa hili nasikia kukata tamaa. Leo hii Wamarekani wasimame na kumuita their founding father George Washington kuwa ni Dikteta kwa sababu alipigana vita, alifanya maamuzi mabaya na aliruhusu Utumwa kuendelea leo wamuite Dikteta!!? Leo tunafurahia taifa moja, amani, utulivu; tunasema ni matunda ya Dikteta! I'll give you guys all the other victories, I'll let call Nyerere any other name, I'll even grant you majina ambayo hata yeye mwenyewe aliyajua "mchonga, Haambiliki"... lakini kweli Dikteta?

Najua kuna chuki dhidi yake kwa sababu mnazozijua wenyewe lakini hili la Udikteta hapana bwana.
 
Do you really believe Nyerere was a dictator?

Mwanakijiji hilo wala sio swali la kuuliza.

Nyerere ni bonge la dictator na hii thread ni one of the best things vimetokea hapa JF kujifunza kuhusu mchonga meno na kifimbo wa Butiama.

Inafurahisha sana kujua ukweli huu ambao ulikuwa haujulikani miaka yote hii kuwa Nyerere alikuwa dictator, mbinafsi, na muovu. Ni vizuri pia imeonekana kuwa Nyerere ndiye chanzo cha matatizo yote ya nchi yetu - yaliyopita, yaliyopo na yajayo.

Ikija wakati wa action sasa - huyu dictator Nyerere sijui aadhibiwe vipi sasa. Maana the guy ameleta Buzwagi, IPTL na Kiwira. The same guy ameleta Richmonduli, Rada nk.

Dictator Nyerere ameuza migodi yote ya dhahabu ya Tanzania. The same guy amezuia Zanzibar kutojiunga OIC. The same guy ameuza Serengeti.

Huyu Dictator na mwovu kabisa Nyerere amefanya Tanzania itakuwa maskini for the rest of her history.

Huyu Nyerere sijui inabidi ashtakiwe absentia na ahukumiwe kufa kwa kunyongwa kama Sadam husein.

Dictator Nyerere. uko wapi?
 
Dikteta Adolf Hitler
Dikteta Saddam Hussen
Dikteta Nduli Idi Amin Dada
Dikteta Slobodan Milosevic
Dikteta Mobutu Seseseko
Dikiteta Mwalimu Julius K. Nyerere

really??????

You gat that right!

Dikiteta Mwalimu Julius K Nyerere.

Yeye ndiye chanzo cha matatizo yote ya Tanzania na ni yeye ndiye anasababisha ufisadi wote wa Tanzania. Kulingana na account ya hii thread;

Nyerere was nothing. The hero should Kambona, Malecela and the like. Hayo mengine ya Nyerere aliyafanya kwa ubinafsi tu na wivu.

Nyerere inabidi atafutwe aadhibiwe na azuiwe kabisa kukwamisha maendeleo ya Tanzania. Kumtetea Nyerere hapa unapoteza muda. This Nyerere ndio mkosi kwa Tanzania. So live with it Mkjj.
 
Dear wangu, nimeshakubali hoja zao, Nyerere ni Dikteta na historia ya TAnzania ingeandikwa vizuri pasipo huyu Dikteta. Dikteta kawaachia nchi miaka 22 iliyopita hadi leo ati hawajui kuongoza! Leo wanakimbilia kwenye Ulaya kuomba wataalamu wa Mikataba kwa sababu ya Dikteta hakuwapeleka shule! Huko nyuma nilifikiri Bunge lilikuwa linashinda kubadili sheria na Katiba kwa sababu wajumbe walikuwa wanamuogopa Dikteta. Leo hii sheria zile zile zipo kitabuni na Dikteta kawaachia waongoze miaka 22 iliyopita.

Wakati umefika Tanzania iache kukumbuka siku ya kufa Dikteta huyu mkubwa!
 
kawaachia nchi miaka 22 iliyopita hadi leo ati hawajui kuongoza! Leo wanakimbilia kwenye Ulaya kuomba wataalamu wa Mikataba

Very strong point indeed, na ndio hasa tatizo letu kubwa kitaifa lilipo, ni taifa lililozoea kuamuliwa maamuzi yake na mtu mmoja, hatukutayarishwa kuamua maaamuzi yetu wenyewe, sasa yule muamuzi hayupo tena, tizama tunavyohangaika!
 
wakuu,

binafsi nimesikitika sana kuona kwamba hoja hii imechukua mkondo ulionao sasa. siamini kabisa kwamba kuwapachika majina viongozi wetu waanzilishi wa taifa hili ni sahihi. wote walifanya makosa na nadhani ni vyema tuyatambue makosa yao kama makosa ambayo hatustahili kuyarudia.

wakuu, tuwaenzi viongozi wetu waliopita. tuwaombee malazi mema peponi, kwa wale waliotangulia mbele ya haki ambako huko kila mmoja atahukumiwa kwa haki. kwa wale ambao bado tunao tuwaombee maisha marefu na kuwahamasisha kuweka historia sawa. watueleze kama kuna makosa yalifanyika huko nyuma ni yapi na nini kilikuwa kiini au misingi yake na tusaidiane kutoyarudia makosa hayo. tusiwape imani kwamba mara watakapotutoka (kama watatangulia) huku nyuma wataanza kuitwa majina kama au yanayofanana na yaliyojitokeza katika mjadala huu.

kweli mola ibariki tanzania
 
Hakuna mtu aliyemweka Mchonga kwenye league na kina Saddam, tena kuna post huko juu nimegusia hilo.......acha ku-sensantionalize na ku-slant fwacts za maneno ya watu ktk hoja zako!!!. That's cheap...shame on you!.

Yes, kuna watu tena wengi tu wana amini kwamba George alikuwa mbaya na yupo criticized kama kawa....nicknamed "George the terrible"........ni democracy hommies!!.

Issue ya mabasi ya Kamata, sijui kuendesha gari jumapili, bora ungekaa kimya tu, kwani ume-sound kama "regular joe" ktk main street somewhere in Romantic Tanzaphilia. Why I say so?, kwasababu hata mwaka 2010 ktk uchaguzi the so called Vasco da Gama will be re-elected!!! does that make him a good leader? hell no! hiyo inakuambia nini kuhusu Tanzania?. Hiyo ni kama ile equation ya Shroendiger, halafu variable moja ina miss...!!! kaazi kweli.

Kama alikuwa saint kama unavyojaribu kusema hapa, basi angeliomba msamaha na ku-disappear ktk thin air baada ya kujiuzuri, badala yake ilikuwa opposite.......halafu leo unashangaa kuona kuna "mwendo mdundo." Irresponsibility ni legacy ya Nyerere alowachia wa Tanzaphilia!!!.

Mimi nimesema Nyerere alikuwa Dikteta, naweza ku-support hoja zangu na kuna watu wanaweza kukubaliana na mimi. Najua kuwa ni unpopular kwenda after Nyerere, lakini hey.....ndio matunda ya domo-kracy, live with it and stop being emotional......atleast acha kugeuza maneno ya watu, ebo.!!!
 
Kafara,
Ni hao jamaa ambao walianza kuwa "Nasty"........kwani nani hapa aloleta story za "ballz" na kadhalika?? They started name calling, finger point etc...we're just following suit!!.
 
Duh yameshakuwa haya, anyways kwa kifupi nadhani kila mtu ana mtizamo wake kutokana na kilichomtokea wakati wa utawala wa Nyerere, nadhani umefika wakati wa kumove on kutoka kwenye hizi yengele za alikuwa dikteta or hakuwa dikteta na kuangalia Taifa letu linaelekea wapi maana kwa kusoma historia inaonyesha Mwalimu alikuwa na vision na Taifa kulinganisha na hawa viongozi wetu wa siku hizi.
Weekend njema and Happy 46th Independence.

*MIaka 46 iliyopita watu walikuwa wanabishania Uhuru, Leo tunabishania sijui nini?
 
Taifa linalopinda historia yake na ni taifa lisilojua linakotoka na lisilofahamu limefikaje hapa; ni taifa lisilojua wapi linataka kwenda.
 
Ebwana si nilidhani wewe umeacha kupost kwa vile hamna jipya....kulikoni?
 
Back
Top Bottom