Bin Maryam
JF-Expert Member
- Oct 22, 2007
- 685
- 13
Mkuu hiyo statement ya kuongopa ni kali sana ila naona inakurudia wewe maana umesema kuwa ameongopa bila kutoa "ukweli" ili kuhakikisha vingine (prove otherwise).
Kwa kushindwa kutoa namba tofauti, inaonekana ni kweli kuwa nchi ilikuwa na wazawa 2, 12, 15% kama alivyosema Maswali hapo juu na hii ni big deal sana kwa nchi inayotaka kuendelea. Je wakati Nyerere akistaafu hiyo number ilikuwa imefikia wapi? (yaani kulikuwa na mainjinia na madakitari wazawa wangapi? na 15% ilikuwa imefikia ngapi?).
Bado nakusubiri upinge au ukubali hoja kuwa hakuna nchi duniani iliyotumia ubepari pekee au ujamaa pekee katika kuleta maendeleo na pia ujibu kama NASA nk ni uzalishaji wa kibepari au kijamaa
Nchi inafanya kazi kwa workforce iliyopo ndani ya nchi bila kujali utaifa wa watu hao. Na hiyo ndio point yangu. Tanzania ilikuwa na madaktari wa kihindi, kigiriki na kizungu na walifanya kazi zilizoleta maendeleo.
Chukua mfano wa ujenzi wa reli Tanzania wakati wa kipindi cha mjerumani. Ni injinia wangapi walitumika? Hata 10 hawafiki.
Nyerere amesomesha ma-injinia wa ujenzi wa reli kibao lakini kama wanashindwa kufanya wanachotakiwa, hakuna sababu ya kuwapeleka shule.
Wakati Nyerere ana-staafu, kuliwa na madaktari wengi na ma-injinia wengi lakini kulikuwa hakuna mtaji (CAPITAL) wa kuwafanya wawe productive.
Ujamaa sio mfumo wa kuleta maendeleo. Ni mfumo wa watu kuishi kwa raha na kutumia mali ya umma kama wako peponi (Kasome DAS KAPITAL by Karl Marx).
Nchi zote za Scandinavia, Marekani ya Kaskazini, Ulaya Magharibi walishautumia ubepari kuleta maendeleo kwanza. Na wanachokifanya ni kujaribu quasi-Ujamaa kugawana matumizi ya mali ya umma.
Kuhusu NASA sina la kusema unachanganya madawa sawa. NASA ni idara ya serikali kama vile magereza au polisi. Hata Mtwa Mkwawa alikuwa na idara zake za serikali. Idara za serikali hazina uhusiano wowote na mada.