Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

Hey hey. Hakuna free lunch. Misaada ilikuwa direct proportional na invenstment ya nchi inayokusaidia.

Baada ya kutaifisha invenstments zao, ulitaka watusaidie?

Na nani aliwapa ruksa ya kuchukua mashamba kwa nguvu? Nani aliwapa ruksa ya kuiba mali zetu asili? Kweni tuliwaomba waje kututawala?

Sio watusaidie bali warudishe pesa walizoiba wakati wa ukoloni!
 
Na nani aliwapa ruksa ya kuchukua mashamba kwa nguvu? Nani aliwapa ruksa ya kuiba mali zetu asili? Kweni tuliwaomba waje kututawala?

Sio watusaidie bali warudishe pesa walizoiba wakati wa ukoloni!

Maswali,
Ukweli unaujua kuhusu utaifishwaji wa mali za watu enzi za azimio la Arusha........ule ulikuwa ni "mchemsho" na nina shukuru mungu kwamba alipata maisha marefu kuona sera zake za kipuuzi zikiwa a total failure!!!..........lazima kuwe na majority ya middle class ktk nchi ili yawepo maendeleo ya kweli. Kuindoa middle class, kutegemea peasants, na njia za uchumu zinazo endeshwa na serikali kuu ni recipe ya disaster. Bwana "fikra sahihi" hakuliona hilo, ndio maana tupo hapa tulipo.

Hata kama wakoloni wangeturudishia hizo mali unazosema, kwa sera za kijamaa za Nyerere angeharibu tu.
 
Nakuunga mkono ndugu yangu, mfano mzuri ni huo hapo chini toka ktk article flani hivi.......... hiyo ni pick ya paragraph mbili tu ambazo zina dissect Tanzania, ukweli ni kwamba li-ujamaa la Nyerere ndio limeua "timu". James Carville angesema' "it's ujamaa stupid."!!!! Well, mtu anaweza ku-spin atakavyo...............

In fact, ujamaa villages were generally failures as satisfactory human communities and, above all, as units of production. What the high-modernist planners of the Tanzanian state failed to realize was that the prior dispersion and movement of the population was a finely-tuned and long-practiced response to a very stingy semi-arid environment. Similarly, the complex forms of poly-cropping they practiced were generally quite productive and ecologically sound, despite having been judged, partly on aesthetic grounds, to be "backward" by agricultural planners. The mono-cropping mandated in its place typically failed. As the failures of the ujamaa became more manifest and the fiscal capacity of the regime to subsidize them weakened, communal production was abandoned and many of the villages broke up altogether. Where the new villages persisted it was due more to the improvisational skills and kinship networks of those resettled than to the logic of the planners' design.

Like the Soviet state, the Tanzanian state had replaced an independent, migratory, and illegible rural population with a regimented, fixed peasantry. In the process it damaged, if not destroyed, a preexisting human capital of working knowledge and social connective tissue. By making an abstraction of the peasant farmer and insisting on a vastly simplified, mono-cropping regimen, its own scheme proved a recipe for failure.

There u go!!!!.

Hicho ndicho nachokielewa mimi. Lakini Ndugu yangu mwanakijiji anataka kuleta vita baridi, hali ya hewa na vita vya Kagera kama sehemu ya matatizo ya uchumi wetu.

Vita baridi viingizia hasara duniani nzima. Marekani ilipigana vita katika front nyingi. Urusi nayo iliongeza matumizi ya kijeshi. Matumizi ya kijeshi hayasaidii maendeleo ya nchi. Hivyo mwenye kutumia sababu za vita baridi kama kisingizio cha kushindwa kwetu, ni lazima akubali Darwin theory Natural selection or Survival of the fittest ikiwa applied katika social science. Ujamaa umeshindwa kwa sababu ni INFERIOR.

Hali ya hewa ni matatizo ya kidunia na binadamu yoyote anayekubali kuishi dunia ni lazima akubali kuwa atapambana na matatizo ya hayo. Na matatizo ya hewa mara nyingi yanaji-correct yenyewe. Matatizo ya hali ya hewa yalishindwa kuji-correct yenyewe kwa sababu yalitokea wakati wakazi wengi wa nchi wanahamia katika vijiji vya ujamaa. Lakini kama watu wangekuwa katika vijiji vyao asilia, wangeweza kukabiliana nayo kama walivyofanya kabla ya mkoloni kuja au wakati tunatawaliwa. Kwanini matatizo ya hewa ya athari kubwa sana kiuchumi miaka ya 70 na mwanzo mwa 80 ? Mwaka 94 kulikuwa na ukame, 98 Al-nino na 2006 Ukame na tumeweza kuvipita bila ku-athirika sana kiuchumi.

Vita vya Kagera vilichukua kama miezi minne. Gharama ya vita vya miezi minne katika sehemu kipande kidogo sana cha nchi hazifanyi nchi iwe masikini kwa miaka 30.

Hasara ilipatikana kwa sababu ya kutaka kumrudisha OBOTE madarakani na ikalazimisha jeshi la Tanzania kukaa Uganda kwa zaidi ya miaka miwili. Na katika kipindi cha miaka hiyo miwili tutumie sehemu ya pato letu kuwafanya waganda wanyamaze, hii ni sawa na wamarekani wanavyofanya sasa Iraq.
 
Nimesema hapo juu kuwa siupendi ujamaa na pia simpendi Nyerere. Ila kama tutafanya mada ya kujadili historia kuwa nafasi ya kuponda na kubeza viongozi waliopita (wote Nyerere na Kambona kama inavyofanywa hapa), wote mwisho wa siku tunaonekana kuwa tu na utoto kama wa huyo mwafrika wa kike na pumba zake.

Yaani wewe huwezi kusema point zako bila kuingiza jina langu? au ndio yale yale ya kutafuta umaarufu kwa kumpondea Mwafrika wa kike. Come on now..... grrrrrrrrrrrr

Unaanza kusema kuwa huupendi ujamaa wakati unamtetea Nyerere. Wewe hujaona concept hapa JF ni kuwa kila anayemtetea Nyerere ni mshabiki wa ujamaa.... do your math damn it
 
Na nani aliwapa ruksa ya kuchukua mashamba kwa nguvu? Nani aliwapa ruksa ya kuiba mali zetu asili? Kweni tuliwaomba waje kututawala?

Sio watusaidie bali warudishe pesa walizoiba wakati wa ukoloni!

Sasa hiyo siasa na sio uchumi. Bila kufanya hayo maovu ungekuwa bado unavaa vipande vya ngozi. Dini ya ukristo au uislamu usingejua. Ungekuwa Mbumbumbu mpaka leo. Njia za treni na mabarabara usingeyajua. Na cha maana zaidi nchi inayoitwa Tanzania isingekuwepo.

Na kama tunaona kuwa walituibia basi tuliboronga kutumia process ya kutaifisha. Katika kutaifisha, serikali ilibidi inunue mashamba kwa lazima. Kwanini unanunua kitu chako ulichoibiwa, huo ni upumbafu. Kitu kilicho chako chukua tu bila malipo yoyote.
 
Mkuu MMJ,

Heshima mbele mkuu, haya matatizo uliyoyasema mkuu huoni kuwa ya;likuwa ni kujitakia kuliko ya natural?

Mkuu MWK,

Nimeskusikia mkuu, ila it is nice for once wewe na Mkuu MMJ, kuwa kwenye defense, I am enjoying it, ingawa in the process ninajifunza cha kumtetea Mwalimu mbele ya foregners, unajua hii ni sisi kwa sisi tu yaani nigger kuita nigger mwenziwe nigger, lakini sio mzungu, Na mimi pia mkuu siwezi mponda Mwalimu, mbele wageni au nikakubali akapondwa na wageni wasiokuwa wabongo, atakufa mtu ndio maana ninasema tunachota arguments hapa,

Ila Respect kwenu wote mnaoshiriki kwamba finally, inatolewa elimu na that is all tunachoomba!

Mkuu FMES,

Kumbe issues ni kumweka somebody kwenye fence? Mbona hiyo ndiyo game ya JF all day all night? kuna wakati unakuwa kwenye fence na kuna wakati unakuwa kwenye kikapu. Ni kama basketball game, mchezaji mmoja unatumika kushambulia na kukaba.

Kitu kimoja naona labda wengi wameshindwa kuelewa hapa ni kuwa. Mimi kama mpinzani wa serikali si-gain chochote kwa kumtetea Nyerere. Nyerere ni muasisi wa CCM, Binafsi naona kama Nyerere alichangia sana mzee wa Kiraracha na Seif Sharif kukosa urais wa Tanzania na Zanzibar mwaka 1995.

Of all people, mimi ndio ningemchukia Nyerere zaidi. Nilipokuwa shule nilielezwa kila aina ya stori mbaya kuhusu Nyerere hadi nikamchukia mzee wa watu kuliko hata shetani. Wapinzani wengi wa CCM wangependa sana sumu ya Nyerere iondoke maana kuna sehemu nyingi Tanzania CCM ni popular kwa sababu watu wanaihusisha na Nyerere. Mimi ndio nina kila sababu ya kumpondea Nyerere hapa JF.

Sasa kwa nini simpondei Nyerere?

1. Siamini kuwa kuna chochote cha Nyerere miaka 22 baadaye
2. Siamini kuna chochote mfu wa miaka 8 kaburini atafanya
3. Mimi sio apologist - Sitafuti visingizio kwa kufeli kwangu
4. Nimegundua mengi niloambiwa shuleni juu yake ni uongo
5. Sifaidiki na chochote hata nikimpondea
6. Nilikutana na mama maria nikagundua kuwa she is so sweet
7. Ufisadi wa ccm utamfuta Nyerere automatically kwenye historia
8. Baada ya Kichaka kumnyonga Sadam, nani atasema NO kwa jamaa
9. # 8 hapo juu, Nyerere alisema NO kwa jamaa na that's hot!
10. Nikiandika sana utachoka kusoma.......
 
Nakuunga mkono ndugu yangu, mfano mzuri ni huo hapo chini toka ktk article flani hivi.......... hiyo ni pick ya paragraph mbili tu ambazo zina dissect Tanzania, ukweli ni kwamba li-ujamaa la Nyerere ndio limeua "timu". James Carville angesema' "it's ujamaa stupid."!!!! Well, mtu anaweza ku-spin atakavyo...............

In fact, ujamaa villages were generally failures as satisfactory human communities and, above all, as units of production. What the high-modernist planners of the Tanzanian state failed to realize was that the prior dispersion and movement of the population was a finely-tuned and long-practiced response to a very stingy semi-arid environment. Similarly, the complex forms of poly-cropping they practiced were generally quite productive and ecologically sound, despite having been judged, partly on aesthetic grounds, to be "backward" by agricultural planners. The mono-cropping mandated in its place typically failed. As the failures of the ujamaa became more manifest and the fiscal capacity of the regime to subsidize them weakened, communal production was abandoned and many of the villages broke up altogether. Where the new villages persisted it was due more to the improvisational skills and kinship networks of those resettled than to the logic of the planners' design.

Like the Soviet state, the Tanzanian state had replaced an independent, migratory, and illegible rural population with a regimented, fixed peasantry. In the process it damaged, if not destroyed, a preexisting human capital of working knowledge and social connective tissue. By making an abstraction of the peasant farmer and insisting on a vastly simplified, mono-cropping regimen, its own scheme proved a recipe for failure.

There u go!!!!.

Ni vizuri kujenga hoja wewe mwenyewe. Unapocopy na kupaste mawazo ya mtu mwingine na kuyafanya yawe ya kwako na hivyo watu wanakupongeza kana kwamba ni ya kwako, kwenye akademia wana jina lao... na inapogundulika mtu anaweza hata kufutwa shule.. sasa natoa wazo tu cite the source ama sivyo you'll be guilty of ....
 
Thanks FMES,

hiyo conclusion ndiyo ukweli wenyewe (maneno yako kwenye red).

Matatizo yetu yote ni kwa sababu ya huyu dikiteta Nyerere. Taratibu tu kila kitu kumhusu yeye itabidi kifutwe ili taifa lianze upya bila Nyerere wala wafuasi wake.

Rest in Peace our hero Kambona.

Burn in Hell the dictator Nyerere
.

Baada ya hapo....

Mimi napendekeza uwanja wa michezo wa Kambarage shinyanga ubadilishwe jina kuitwa Yasin Memba na ndugu yake kwa vile waliteka ndege ili kumtoa dikiteta Nyerere madarakani

Inabidi pia mtoto wa Nyerere Makongoro avuliwe uenyekiti wa ccm huko musoma ili apewe binti wa Kambona.

Unajua hawa madikiteta inabidi kuwaadhibu hadi watoto wao kama Nigeria wanavyofanya kwa familia za madikiteta
.

Kishaaa.....

Yaani hapa FMES umekamilisha kila kitu.

Akaimbiisha wanafunzi nchi nzima kuimba nyimbo za kumsifia (talk about Nyerere kuwa all over the country).

Yaani huyu dictator baada ya kutupa watu huko mafia, akaanza kuiba madini na pesa zote za nchi na kuziweka kwenye mabenki ya nje.

This guy, inabidi kwanza mwili wake ufukuliwe pale ulipozikwa kisha awekwe huko kisiwani mafia ili asikie uchungu wa kuweka mamilioni ya watanzania huko mafia!

grrrrrrrrr

Baadae.......

hakuishia hapo.....

Mkuu Kafara,

Tanzania ya leo inaonekana hakuna kitu kitafanyika kama Dikiteta Nyerere ataendelea kuenziwa. Mkulu FMES amekumbusha kuwa kitendo cha Nyerere kuwaamulia watanzania cha kufanya miaka yote hii ndio kimesababisha viongozi leo wanasaini mkataba kama Buzwagi.

Inabidi huyu Nyerere awe -exposed na aadhibiwe au ikiwezekana afutwe kwenye historia kwa vile inaonekana kuwa as longer as this guy yupo kwenye historia ya Tanzania hakuna chochote kile kitakachofanyika! nchi itaendelea kuwa mbovu na masikini.

Mwelekeo wa hii thread ndio dawa ya matatizo ya Tanzania. Futa anything about this Dictator Nyerere ili watu waanze upya. Kisha badili historia ya Tanzania ili watu tuliozaliwa miaka mingi baada ya shujaa Kambona kwenda uhamishoni tumuenzi vilivyo.

Kwanini lakini?

Mkuu Icadon,

Imeshaonekana kuwa Nyerere ndiye anakwamisha maendeleo ya Tanzania leo hii. Hii thread ilianza kwa nia ya kumuenzi shujaa Kambona lakini ikachukua very strong turn kuwa anti-Nyerere (it should be).

1. Inaonekana bila kufuta historia ya Nyerere, Tanzania haiwezi kusaini mikataba bora ya madini leo.

2. Inaonekana bila kufuta historia ya Nyerere, Kikwete hawezi kuondoa mafisadi kwenye baraza lake la mawaziri.

3. Inaonekana bila kufuta historia ya Nyerere, wizi BOT hauwezi kuisha.

4. Inaonekana bila kufuta historia ya Nyerere, miundo mbinu Tanzania haiwezi kujengwa.

5. Inaonekana bila kufuta historia ya Nyerere, watoto na vitukuu vyetu wataendelea kuwa masikini mpaka siku this guy akiadhibiwa.

Mimi naona haya yanayoendelea hapa ni sawa tu maana ndio suluhisho la matatizo ya Tanzania (kwa mtazamo wa wana-JF).

So hii ni muhimu sana kwa memba wa JF!

Now you are kidding hunhh

Kwi kwi kwi,

yani wewe naona unahangaika kumtetea dikiteta Nyerere, huchoki tu na ukubali yaishe?

Kwanza nimepata idea mpya ya kumfukuza mama Maria kutoka Msasani na kisha ile nyumba ya Butiama iliyojengwa na Jeshi inabidi itaifishwe ili ipewe familia ya shujaa wetu Kambona.

No way.......
 
Ni vizuri kujenga hoja wewe mwenyewe. Unapocopy na kupaste mawazo ya mtu mwingine na kuyafanya yawe ya kwako na hivyo watu wanakupongeza kana kwamba ni ya kwako, kwenye akademia wana jina lao... na inapogundulika mtu anaweza hata kufutwa shule.. sasa natoa wazo tu cite the source ama sivyo you'll be guilty of ....

Mkjjj,

Kumbe hukuambiwa kuwa inapokuja suala la kupigana kufuta historia ya Nyerere kila silaha inatumika? Si umeona wameanza kukuita mjamaa (socialist)?

Ilianza kwa kumsifia Kambona, Ikawa Kambona VS Nyerere, na sasa ni ujamaa Vs Ubepari. Chochote utakachosema kizuri kuhusu Nyerere basi wewe ni mtetezi wa ujamaa. Kila article inayopondea ujamaa itaelekezwa kwako regardless.

Get ready for the muziki. FMES amesema anaenjoy kukuona kwenye fence mwenzangu. Kazi unayo ya kutetea mwana-ccm Nyerere!
 
BTW,

Nimepata idea nyingine itakayofuta kabisa mabaya yote ya Nyerere na ujamaa wake na hasara zake kwa Tanzania.

Inabidi wale wote wanaomtetea Nyerere sehemu yoyote hata kama ni hapa JF kama Mwanakijiji, wakamatwe na wawekwe kizuizini au mafia kwa miezi saba bila mashtaka. Baadaye wataifishwe mali zao zote ili deni la Tanzania lililosababishwa na Nyerere lilipwe.

Nadhani baada ya hapo nchi itatulia maana so far naona hakuna kitakachoendelea Tanzania mpaka Nyerere ameadhibiwa big tyme.
 
Mkjjj,

Kumbe hukuambiwa kuwa inapokuja suala la kupigana kufuta historia ya Nyerere kila silaha inatumika? Si umeona wameanza kukuita mjamaa (socialist)?

Ilianza kwa kumsifia Kambona, Ikawa Kambona VS Nyerere, na sasa ni ujamaa Vs Ubepari. Chochote utakachosema kizuri kuhusu Nyerere basi wewe ni mtetezi wa ujamaa. Kila article inayopondea ujamaa itaelekezwa kwako regardless.

Get ready for the muziki. FMES amesema anaenjoy kukuona kwenye fence mwenzangu. Kazi unayo ya kutetea mwana-ccm Nyerere!

sisi wengine dear wangu, tunauwezo wa kusimama peke yetu! Ukweli unabakia kuwa ukweli hata watu 1000 wakiupinga na kusema uongo. Ila baadhi ya mapendekezo unayoyatoa nadhani yatawasaidia sana.. ila hilo sisi wengine kuswekwa Lupango naona ni zuri kwani hatutakuwa na sababu ya kutoroka kama Kambona. Tatizo miaka 22 baadaye wakijikuta na matatizo yale yale watamlaumu nani sasa?
 
Miaka 22 baadate wao watakuwa wamezeeka sana na watoto wao wataanza kukulaumu wewe kwa kupoteza muda mwingi kumtetea Nyerere badala ya kutumia muda huo kuzuia nchi isiuzwe kwa mara ya pili kwa wazungu kupitia mikataba mibovu.

Kazi unayo baba watoto!
 
sasa muda watakaokuta wanatumia kunilaumu mimi, kwanini watoto wao wasiwe wameweza kuijenga nchi miaka 44 baada ya Nyerere?
 
MWK - Mbona unaharibu mada bibie? Katika kipindi cha siku 3 ambacho ulipotea, hii mada ilikuwa kwenye mkondo mzuri sana. Wengi wetu tumekuwa tunaelimika sana na hii mada kuhusu sehemu ya historia ya nchi yetu. Pia, michango ya Mwafrica, Bin Maryam, na Maswali imetusaidia sana kuelewa kwa kifupi historia ya ujamaa vs upebari. Sasa bibie umeibuka tena basi du unaanza kuipeleka mada kwenye mkondo wa kejeli na dharau. Kwa nini lakini?? Hivi kuna ugumu gani ukiwa msomaji tu, kama hauna cha kuchangia? It really won't make any less of who you are!

Mkjj - Inawezekana ni kweli unapima kila neno unalo andika, lakini pengine haupimi kila post unayochangia au support. C'mon, you should know better.
 
QuickMover,

Samahani sana kama kuwepo kwangu hapa kumekufanya uone kama mada imeharibika. Mada kuharibika ni tafsiri kubwa sana kwani hata mimi naweza kuona walioifanya hii mada kuwa Nyerere vs Kambona waliharibu mada. Au hao kina Mwafrika (sijui hata ametokea wapi huyu kuanza kuniita mtoto mwenye pumba) walioanza kuifanya hii mada kati ubepari vs ujamaa wanaweza kuwa wameharibu mada ya kutafuta nafasi ya Kambona kwenye historia.

Usijali ndugu yangu, hii ndio namna yangu ya kuchangia mada hapa JF, unaweza tu kuamua kutosoma ninachoandika na maisha yakawa safi tu bila matatatizo. Jifunze tu kuishi na mimi kwani I will be for a long time as longer niko hai na JF iko hewani.

Endelea tu na mchango wako hapa na kwa nchi. Nakuhakikishia kuwa kinachosemwa hapa juu ya Nyerere (miaka 22 baada ya kustaafu) kina nafasi kidogo sana ya kubadili mwelekeo wako binafsi wa kimaisha au familia na nchi yako.

Samahani na asante pia kama utanielewa.
 
MWK - Mbona unaharibu mada bibie? Katika kipindi cha siku 3 ambacho ulipotea, hii mada ilikuwa kwenye mkondo mzuri sana. Wengi wetu tumekuwa tunaelimika sana na hii mada kuhusu sehemu ya historia ya nchi yetu. Pia, michango ya Mwafrica, Bin Maryam, na Maswali imetusaidia sana kuelewa kwa kifupi historia ya ujamaa vs upebari. Sasa bibie umeibuka tena basi du unaanza kuipeleka mada kwenye mkondo wa kejeli na dharau. Kwa nini lakini?? Hivi kuna ugumu gani ukiwa msomaji tu, kama hauna cha kuchangia? It really won't make any less of who you are!

Mkjj - Inawezekana ni kweli unapima kila neno unalo andika, lakini pengine haupimi kila post unayochangia au support. C'mon, you should know better.

Very perceptive, guilty as charged. Will do better next time. Thanks for friendly observation.
 
sasa muda watakaokuta wanatumia kunilaumu mimi, kwanini watoto wao wasiwe wameweza kuijenga nchi miaka 44 baada ya Nyerere?

Wewe kama Kikwete anaunda kamati ya kuchunguza kamati iliyochunguza kamati ya kutoa mapendekezo kwa kamati ya madini ndio utashangaa watu wakilaumu kuhusu waliolaumu kuhusu wale ambao hawakulaumu kuhusu kulaumu yale ambayo yalilaumiwa na wale wanaolalamika?
 
YourName,Maswali,Bin Maryam,Mwanakijiji,QuickMover,

Naona hii mada imegeuka tena kuwa VIBWEKA...i will see you over the weekend!!
 
Maswali,
Ukweli unaujua kuhusu utaifishwaji wa mali za watu enzi za azimio la Arusha........ule ulikuwa ni "mchemsho" na nina shukuru mungu kwamba alipata maisha marefu kuona sera zake za kipuuzi zikiwa a total failure!!!..........lazima kuwe na majority ya middle class ktk nchi ili yawepo maendeleo ya kweli. Kuindoa middle class, kutegemea peasants, na njia za uchumu zinazo endeshwa na serikali kuu ni recipe ya disaster. Bwana "fikra sahihi" hakuliona hilo, ndio maana tupo hapa tulipo.

Hata kama wakoloni wangeturudishia hizo mali unazosema, kwa sera za kijamaa za Nyerere angeharibu tu.

Siwezi kupoteza muda wangu kutetea kwamba baadhi ya sera za Ujamaa zilikuwa mbovu. Sio zote. Hilo nimeshasema. Kitu ambacho baadhi ya watu hapa hawataki kuona ni kwamba Tanzania iliadhibiwa kiuchimi kwasababu ya siasa zake za ndani na mambo ya nje. Kwa wale ambao wamelala kwenye mambo ya "economic warfare" wakasome kitabu kinaitwa Confessions of an Economic Hitman. Haongelei Tanzania, lakini najua for a fact kwamba Tanzania ilikuwa victimized kiuchumi.
 
Back
Top Bottom