Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

Pascal,
Wala mimi sishangai kwa wewe kusema hayo uliyosema kwani hao waliokuja
kuingia TANU 1954 hapo ndipo ulipo ukomo wao wa kujua mambo mtu hawezi
kuwalaumu kwani hawakuwapo na hawajui kilikuwapo nini kabla yao.

Lakini ukienda kwa waliokuwapo na wa miaka ya 1920 watakuambia kuwa
alikuwa Dr. Aggrey ndiyo aliyempa Kleist Sykes fikra ya kuanzisha African
Association alipokuja Tanganyika 1924.

Hii ni historia na kwa mtu mwenye ubongo uliokaa vyema atataka kumjua huyu
Aggrey ni nani, katoka nchi gani na vipi alikutana na Kleist na kumpa fikra hiyo
na huyi Kleist ni nani katika historia ya uhuru wa Tanganyika?

Ikiwa ubongo wako una maradhi basi utajilazimisha uridhike na TANU bila ya
kuifahamu African Association na waasisi wake wala kujiukiza imekuwaje ndugu
wawili Abdul na Ally Sykes wote wawe waasisi wa TANU na kadi zao za ziwe
zimefuatana na kadi ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere?

Kadi no. 1 Julius Nyerere, no. 2 Ally Sykes na no. 3 Abdul Sykes na kadi
zote hizo tatu ziwe na sahihi ya Ally Sykes?

Hakika haiwezekani kuwa haya yalikuja hivi hivi pasi ya kuwa na sababu.
Waarabu wana msemo: ''Ukiijua sababu huondoka ajabu.''

Sasa ukiwa haya yote huyataki nani mwenye hasara.

Mwenye hasara utakuwa wewe unaebakia na ujinga ilhali elimu ipo wazi na
kwa kuhitimisha nukta hii chembelecho Maalim Faiza, ''Elimu bila khiyana,''
elimu ipo na ukitaka utawezakuipata bure.

Hassan Upeka aliliambia jopo la Chuo Cha Kivukoni la waandishi wa historia
ya TANU kuwa haiwezekani mkamfikia Nyerere katika TANU bila ya kupita kwa
Abdul Sykes, hiyo haitakuwa historia ya TANU.

Lakini wewe unasema historia hii ya Kivukoni ndiyo iliyokupa alama ''A'' katika
mtihani.

Sawa wala mimi sistaajabu.
Leo tuaona nchi inavyohangaika na vyeti vya kughushi.

Haya ndiyo matokeo yake.

Vyuo vyenye kughushi na shule zake na vitabu vya kughushi vitatoa ''A'' kama hiyo
yako na wala mimi sikulaumu wewe.

Itatuchukua muda kukaa vyema.

Lakini Chuo Kikuu Cha Harvard na Oxford University Press baada ya kusoma historia
ya Kleist Sykes wamemtia katika Dictionary of African Biography (DAB).

Ukipenda unaweza kusoma hapo chini ukalinganisha na historia unayoijua wewe:
Mohamed Said: KLEIST SYKES (1894 - 1949) KATIKA DICTIONARY OF AFRICAN BIOGRAPHY (DAB) OXFORD UNIVERSITY PRESS, NEW YORK

DSCN1159.JPG
Hongera sana mkuu uko sahihi sana nimekukubali kwa historia nzuri kabisa.
 
Hongera sana mkuu uko sahihi sana nimekukubali kwa historia nzuri kabisa.
Sheikh Hamidu ahsante sana. In Shaa Allah nitamueleza Paskali udhaifu wa Chuo Cha Kivukoni kwa kumwangalia Mkuu wa Chuo hicho Dr. Magotti aliyeandika kitabu cha maisha ya Mzee Kawawa. Nataka aangalie aliyoandika Dr. Magotti na niliyoandika mimi nikitoa taarifa zangu ndani ya Nyaraka za Sykes. Subiri nitoke kwenye simu nihamie ofisini maktaba.
 
Tatizo ukweli hawaukubali ila ubishi tuu usio na faida yoyote. Kwa ulivyofafanua wala hapakupaswa kuwe na tofauti ila nikukumbushana zaidi na zaidi ili tuliotokea nyuma tuzidi kujifunza lakini mtu anakatisha mambo muhimu na mengi kama hayo bila hata haya.

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Sheikh Said kinachowachoma ni kuwa Tanganyika ilikombolewa na Waislam.
 
Sheikh Hamidu ahsante sana. In Shaa Allah nitamueleza Paskali udhaifu wa Chuo Cha Kivukoni kwa kumwangalia Mkuu wa Chuo hicho Dr. Magotti aliyeandika kitabu cha maisha ya Mzee Kawawa. Nataka aangalie aliyoandika Dr. Magotti na niliyoandika mimi nikitoa taarifa zangu ndani ya Nyaraka za Sykes. Subiri nitoke kwenye simu nihamie ofisini maktaba.
Paskali/Hamidu
Nakuomba uangalie haya maelezo hapa chini ili upate picha kamili
ya Chuo Cha Kivukoni na uwezo wake wa kuandika historia ya nchi
hii:

LW013K1LkQSY-ksQJMIfrLluBCK19y57yhYU-j_BY8cl-cwkVVtJ0aGvjZjYwlKPlwcWsMzMYgiGqjCjm8fQL_F3DbDFXcb0H88lMHZMEvypsbsmC_dZg48dxd2lCWkmhzzBziAJ4dt1eD8ykoC2Z905bagButKmxHxS1d-VfYiPinqFPrVM3nZ7OOFfbW7nqQ-eG6CSK7qoYlc7WcYHDQW35kOANKQk0jmvX8Kn-FsPioIpZqTiCckBELGHw9gszEZo7DnSZpBt5vNTrYMheFZgtY0eowMYpOA7XiyUxUJyDW4X0kzp-QUP7z27tE_iLPAB-3nyjIt3HsuHcDyk0CCO_70lE5ayaUYWyv8ddi2NLA_ff33LEWcGI2Qhl3-iQgT8iimVy5VKsMmYcij0lk--el0WI48G8CrJeS45zE34C6VvC-fTJ1ibu_Bj_s4IOFuEkiBatncaeGMCvAVFDiXKngmnrna-4V2V1v7Z5rEKtqYOR54LhMwSqII-_VZUpZA2nxOJvm-CMORXaaPoGr0PdGZg-cO5qbTNxMXAqigwQaNbXVSqpC4f9M7CP1t-6XAI=w407-h615-no

Kwa mara ya kwanza Tanzania ilishuhudia kuandikwa kwa historia ya mmoja wa viongozi wakuu wake kupitia kitabu “Simba wa Vita Katika Historia ya Tanzania Rashidi Mfaume Kawawa” kilichoandikwa na Dk. John M. J. Magotti. Sidhani kama katika historia ya Tanzania kuna kumbukumbu ya kuandikwa kwa kitabu kinachohusu maisha ya kingozi yoyote achilia mbali kufanyika kwa sherehe ya kukizindua kitabu hicho Ikulu ikiongozwa na rais mwenyewe. Kwa hakika sherehe ilifana sana na tukakisubiri kwa hamu kitabu madukani ili tupate kunufaika na kumbukumbu za Mzee Kawawa.

Msomaji anaweza kukisoma kitabu chote chenye kurasa 127 kwa muda wa saa moja akawa kakimaliza chote na atakapokiweka chini akawa hakubakia na chochote cha maana katika fikra yake. Kwa nini iwe msomaji asibaki na kumbukumbu yoyote ya kiongozi mkubwa kama Mzee Kawawa mtu aliyeshuhudia kwa macho yake mwenyewe harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika na si hivyo tu yeye mwenyewe ni mmoja wa wale waliopigania uhuru wa Tanganyika na kushika nyadhifa kubwa za uongozi chini ya Mwalimu Julius Nyerere. Kwa kawaida vitabu vya maisha ya viongozi hasa wapigania uhuru huwa vina mambo mengi sana ambayo kwa muda mrefu huwa siri, hayafahamiki hadi hapo kitabu kitakapoandikwa ama kwa mkono wake kiongozi mwenyewe au kuandikwa na muandishi. Mifano ipo mingi. Kitabu kama “Mahatma Gandhi” klichoandikwa na Robert Payne au “Long Walk to Freedom” alichoandika Nelson Mandela mwenyewe au “Seeds of Freedom” alichoandika Bildad Kaggia hakika unapomaliza kusoma vitabu hivi lazima urudi nyuma kufungua kurasa hapa na pale kuzisoma upya zile sehemu zinasosisimua.

Huwezi kupata haya katika kitabu cha Mzee Kawawa. Huwezi kuyapata haya kwa kuwa mwandishi hakuandika kitu. Hakuandika kitu si kama Mzee Kawawa hana historia ya kusisimua na kuwa hana mengi ambayo wengi hawayajui katika maisha yake, nadhani mwandishi hakuwezakuja na jipya labda kwa sababu hakufanya utafiti wa kutosha kuweza kuandika kitabu kinachomuhusu simba wa vita aneunguruma. Kuna msemo wa Kiswahili usemao “Aungurumapo simba mcheza ni nani?” Kwa hakika simba wa vita hakuunguruma kabisa katika kitabu hiki. Sijui lawama zielekezwe wapi.

Mimi simjui Mzee Rashidi Kawawa kwa kiwango cha kusema naweza kunyanyua kalamu na kufanya pitio la kitabu kilichoandikwa kuhusu yeye. Nathubutu kuandika kuhusu kitabu chake kutokana na kumjua kwangu mimi nikiwa kama mwandishi na mtafiti ambae katika kutafiti kwangu nimekutana na jina la Mzee Kawawa hapa na pale katika nyaraka zilizo katika hifadhi ya ukoo wa akina Sykes. Nitatumia uzoefu wangu huu kueleza yale niliyoyaona katika nyaraka hizi na ninayojua kuhusu Mzee Kawawa na kufanya tathmini kwa yale niliyoyasoma katika kitabu cha Magotti.

Miaka kama ishirini iliyopita nikiwa kijana mdogo nilipata hamu ya kuandika historia ya kudai uhuru wa Tanganyika. Sikuona mtu wa kumuendea isipokuwa Ally Sykes. Nilipomueleza kuwa nia yangu ni kuandika kitabu kuhusu marehemu kaka yake Abdulwahid Sykes (1924- 1968) Ally Sykes alinambia kuwa atanipa nyaraka zake zote nizipitie kisha ndiyo nakaenae chini kwa mahojiano ya ana kwa ana. Katika nyaraka alizonikabidhi ndani yake nilikuta barua ya mkono aliyoandika Rashid Kawawa mwaka 1952 kutoka Bukoba akimletea Ally Sykes aliekuwa Dar es Salaam. Barua hii ya Mzee Kawawa kwa Ally Sykes ilikuwa ikimfahamisha Ally Sykes hali ya siasa Kanda ya Ziwa. Hii barua hadi leo ipo katika nyaraka za akina Sykes. Nilipokaa na Ally Sykes kutaka maelezo ya barua ile aliyoandikiwa na Kawawa, Ally Sykes alinipa kisa hiki:

Mwaka 1951 nilichaguliwa kuwa katibu mkuu wa Tanganyika African Government Servants Association (TAGSA). Chama hiki kiliundwa mwaka wa 1927 kwa lengo la kuendeleza maelewano mazuri baina ya serikali ya Malkia na sisi watumishi Waafrika. Rashid Kawawa alikuwa mwana kamati. Mimi nilichaguliwa pamoja na Thomas Marealle kama rais wa TAGSA. Katiba ya TAGSA iliamuru uchaguzi wa kila mwaka, na mimin nilirudishwa madarakani kama katibu mara nne hadi Oktoba, 1954 nilipojiuzulu baada ya kuhamishwa kwenda Korogwe kamaadhabu kwa kuwa miongoni mwa wale wanachama 17 waliounda TANU. Watu kadhaa walishika urais. Stephen Mhando na Dr Wilbard Mwanjisi wote hao waliwahi kuchaguliwa kuwa marais wa TAGSA. Miongoni mwa wanachama watendaji wa TAGSA walikuwa Dr Michael Lugazia na Rashid Kawawa ambao alichaguliwa kuwa katibu baada ya mimi kujiuzulu. Kupitia TAGSA, Kawawa alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Tanganyika Federation of Labour (TFL).

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa ulipokuja kuzuru Tanganyika Agosti, 1951 kwa mara ya tatu, vyama vyote viwili, TAA na TAGSA, viliwakilisha malalamiko kwa ujumbe huo. TAGSA iliwakilisha malalamiko yake kuhusu ubaguzi katika utumishi serikalini kwa mujibu wa kupanga mishahara kufuatana na rangi ya ngozi. Mshahara wa Mwafrika ulikuwa wa chini zaidi kuliko ule aliokuwa akipokea Mzungu au Muasia kwa kazi hiyo hiyo. Kwa mfano Mwandishi wa hati mkato Mzungu alikuwa akipata mshahara mkubwa kuliko Mwafrika aliyekuwa na shahada au digrii kutoka chuo Kikuu cha Makerere. TAGSA vilevile tulilalamika kuhusu kuajiri makarani wa kutoka India na hali walikuwepo Waafrika kutoka Afrika ya Mashariki na Nyasaland ambao wangeweza kujaza nafasi hizo kwa urahisi.

Vyama vyetu hivi viwili TAA na TAGSA viliwakilisha malalamiko haya tukifahamu fika kwamba Uingereza ilikuwa ikiitawala Tanganyikachini ya vifungu nambari 76 na 77 vya Umoja wa Mataifa ambavyo viliwekwa ili kuendeleza maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ya nchi zilizokuwa chini ya udhamini. Kama mdhamini Uingereza ilitakiwa kuhimiza na kuheshimu haki za binadamu na uhuru wa kwa wote bila kubagua kwa misingi yajinsia, lugha au dini. Lakini Uingereza ilikuwa ikipuuza vifungu hivi bila aibu. TAGSA tuliwakilisha malalamiko haya ili Umoja wa Mataifa ujue matatizo halisi ya ukoloni nchini Tanganyika.

Mimi nikiwa katibu wa TAGSA nilifuatilia serikalini masuala yaliyoainishwa ndani ya malalamiko yetu. Suala lililokuwa likituhangaisha sanawakati ule ilikuwa uajiri wa Wahindi kutoka India, jambo ambalo niliieleza serikali halikuwa na faida, maadam kulikuwako na Waafrika ndani ya nchi ambao wangeweza kujaza nafasi zile. Jambo hili lilikuwa likisababisha manugíuniko makubwa miongoni mwa Waafrika. Hakuna majibu maridhawa yaliyopatikana kutoka kwa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa. Barua tulizoandika serikalini juu ya masuala hayo zilipuzwa na Chief Secretary, Bruce Hutt. Katika kufuatilia malalamiko haya, Niliandika barua moja kali sana na kwa mara ya kwanza bila kutafuna maneno niliuliza uhalali wa Waingereza kututawala Waafrika wa Tanganyika. Nillimwambia Katibu Mkuu kuwa kwa kuwa serikali imeshindwa kupata ufumbuzi kwa matatizo ya Waafrika, Uingereza lazima ijitoe Tanganyikana Umoja wa Mataifa utawale Tanganyika. Barua hiyo ilimkasirisha Katibu Mkuu na siku chache baadaye nilipokea barua kutoka serikalini iliyokuwa imejaa vitisho, dharau, stihizai na makemeo. Nikajibiwa kuwa hakuwa na suala la Umoja wa Mataifa kutekeleza utawala wa moja kwa moja Tanganyika.

Dkt Mwanjisi alikuwa amegusa suala nyeti sanakwa kuzungumzia matatizo ya ubaguzi wa rangi uliokuwa ukitukabili Waafrika wa . Kawawa, kama mjumbe wa kamati, akaniandikia barua akanitahadharisha nisichapishe ile hotuba ya Dkt Mwanjisi katika jarida la TAGSA bila idhini ya kamati ya utendaji. Kufuatia majibishano haya kati ya TAGSA na serikali, Dkt Mwanjisi kama alivyofanyiwa Dk Kyaruzi kabla yake, akahamishwa kutoka hospitali ya Sewa Haji mjini Dar es Salaamhadi Kingolwira Prison Hospitalkaribu na Morogoro. Kawawa na yeye akapewa uhamisho kwenda Bukoba na mimi nikapewa uhamisho kwenda Mtwara. Dk Mwanjisi na Kawawa walikubali uhamisho wao na wakaondoka Dar es Salaam. Mimi nilikataa uhamisho na nikabakia Dar es Salaam kupinga uhamisho wangu.

Alipokuwa Bukoba ndipo Kawawa akamwandikia Ally Sykes barua ile ya mwaka 1952 akimweleza hali ya siasa kamaalivyoikuta Kanda ya Ziwa. Huyu ndiye Kawawa niliyemjua mimi kupitia nyaraka na mahojiano na Ally Sykes. Kwa kweli inasikitisha kuwa Dk Magotti hakupata fursa ya kuziangalia nyaraka hizi muhimu sana katika siyo historia ya Kawawa bali katika historia ya kuundwa kwa TANU na kudai uhuru wa Tanganyika. Endapo angepata nafasi ya kuziona hizi nyaraka zingempelekea katika kuwajua wazalendo wengine waliotajwa mle ndani kama Dk. Kyaruzi, Dk. Wilbard Mwanjisi ambao Kawawa alikuwanao katika harakati za TAGSA. Katika majina hayo angeweza kudodosa mengi kutoka kwa Mzee Kawawa na hivyo kuandika yale ambayo hayafahamiki kwa wengi. Hii imgekifanya kitabu kiwe cha maana.

Mathalan Kawawa angeeleza mtafaruku kati ya Mwalimu Nyerere na Dk. Mwanjisi nini chanzo chake na nini ikajakuwa matokeo yake. Halikadhalika angempa fursa Mzee Kawawa kumuhadithia mchango wa Dk. Michael Lugazia katika kuasisi kwa TANU hasa kipindi kile cha 1953 wakati TAA ilipokuwa inatayarisha rasimu ya katiba ya TANU. Kwa ufupi ni kuwa Dk Lugazi alikuwa akijaribu kuamsha ari ya TAA Bukoba ari iliyokufa kutokana na kufungwa kwa kiongozi wa TAA Bukoba Ali Migeyo. Kisa cha Ali Migeyo ni moja ya visa vinavyosikitisha sana katika historia ya Tanganyika kwani aliwekwa kizuizini na Mwalimu Nyerere kama alivyofungwa na Waingereza. Haiwezekani kuwa Kawawa asiwe na habari na kile kilichopelekea mpigania uhuru hodari kama Ali Migeyo aishie jela tena wakati nchi ikiwa huru. Migeyo alifungwa na wakoloni kwa kuwahamasisha Watanganyika kudai uhuru labda Mzee Kawawa angeulizwa angeeleza ni nini kilitokea wakaamua kumfunga Migeyo kama walivyomfunga Waingereza.

Kitabu kimegusia kazi alofanya Kawawa kama mtumishi wa serikali ya kikoloni katika kambi za raia wa Kenyawalioshukukiwa kuwa ni Mau Mau. Katika hawa wafungwa walikuwawepo wananchama wa TANU ingawa hawa walikuwa Wakenya. Maarufu katika hawa alikuwa Dome Okochi Budohi (ambae kadi yake ya TANU ilikuwa na 6) na Patrick Aoko. Budohi alicheza senema pamoja na Kawawa iliyoitwa “Wageni Wema.” Kawawa na Budohi walikuwa wakifahamiana vizuri sana kwa sababu wote walikuwa wasanii. Budohi alikuwa mmojawapo katika bendi ya vijana wa mjini iliyojulikana kama Skylarks. Bendi hii baadaye ilibadilisha jina na kuitwa Blackbirds. Matangazo ya radio yalipoanza Tanganyika, Blackbirds midundo ya Blackbirds ilikuwa haikosekani kusikika radioni katika Sauti ya Dar es Salaam. Kawawa kama walivyo vijama wote wa Dar es Salaam wa wakati ule alikuwa mmmoja wa wapenzi wa bendi hii na alikuwa hakosekani Ukumbi wa Arnatouglo bendi hii ikitumbuiza katika ile miaka ya 1950. Ilikuwa katika ule upigaji muziki wa Budohi ndipo alipoungana na Kawawa katika kutengenezwa kwa senama hiyo ya “Wageni Wema” ambayo mwandishi kaitaja lakini aliishia hapo tu.

Budohi na Aoko ni kati ya wafungwa wa Mau Mau waliokuwa Handeni ambako Kawawa alikuwa na jukumu la kuwaangalia. Budohi ndiyo alikuwa mtu wa kati baina ya TAA na KAU na kuanzia hali ya hatari ilipotangazwa Kenya mwaka 1952 Budohi na Aoko wakawa katika jicho kali la makachero. Makachero hawa Waafrika wanafahamika na wengine walikuja kufanya kazi hiyohiyo katika Tanganyikahuru. Hiki ndicho kipindi ambacho Kaimu Rais wa TAA na Katibu wa TAA Abdulwahid Sykes alipokutana na Kenyatta Nairobi. Wakati Wakenya hawa wanafungwa Tanganyika, viongozi wa KAU akina Bildad Kaggia, Jomo Kenyatta, Kun’gu Karumba, Achieng Oneko, Paul Ngei na Fred Kubai walikuwa wamekamatwa Kenya. Kawawa ni mmoja kati ya viongozi hawa na ingependeza sana kama kupitia kwake tungeelezwa jinsi KAU na TAA ilivyokuwa ikishirikiana kwani haiwezekani kuwa Budohi na Kawawa uswahiba wao ukaishia kwenye kucheza senema tu.

Wanaharakati wote walishtushwa na kutiwa mbaroni kwa Budohi na Aoko. Haiwezekani kuwa iwe Mzee Kawawa kasahau matukio haya muhimu. Budohi na Aoko walikuwa wamefungwa minyororo walipokuwa katika selo pale Kituo cha Kati cha Polisi kwa sasa jumba hiloliko kituo cha mabasi kinachojulikana kama“station.” Waliwekwa pale kwa miezi sita muda wote wakiwa na minyororo miguuni. Waliwekwa pale kwa miezi sita wakihojiwa kabla hawajapelekwa Handeni walipomkuta Kawawa. Hivi ndivyo vitu ambavyo kwa hakika vingeongeza ladha ya kitabu cha Mzee Kawawa endapo mwandishi angechukua muda kutafiti na kuzungumza na watu waliokuwa katika harakati wakati ule ambao bado wa hai kama Ally Sykes na mdogo wake Balozi Abbas Sykes na wengine wengi ambao walikuwepo wakati ule kama Mzee Chipaka.

Katika migomo ya wakati wa kudai uhuru hakuna mgomo uliofanikiwa na kuvuta hisia za wananchi kama mgomo wa reli wa mwaka 1960 uliodumu kwa siku 62. Ukiachia kutajwa tu kama sehemu ya historia undani wake na jinsi mipango yake ilivyokwenda na nafasi ya viongozi wa Tanganyika Railway African Union (TRAU) walivyopata misaada kutoka nchi za Mashariki hivi havijawekwa wazi. Si treni, meli wala mabasi ya railway yaliyotembea kwa mieizi mitatu. Mipango ya mgomo huu ilifanyika Tabora ambako ndiko palikuwa na karakana kuu ya reli na hapo ndipo palipokuwa makao makuu ya viongozi wa TRAU, Salum Abdallah mwenyekiti na Kassanga Tumbo katibu. Kawawa ana mengi katika kadhia hii kwa kuwa yeye wakati ule ndiye alikuwa Katibu Mkuu wa TFL. Inasemekana mgomo huu miezi michache kabla Tanganyika haijapata uhuru ndiyo ilikuwa kama zinduo kwa Mwalimu Nyerere kutambua kuwa hakuwa peke yake na sauti kwa wananchi. Walikuwapo viongozi wengine pembeni yake ambao nao wakipiga wananchi wanacheza. Ilimdhihirikia kuwa huko mbeleni wanakokwenda ipo siku atapambana na viongozi hawa. Hivyo ndivyo ilivyotokea.

Inasemekana Mwalimu Nyerere akimtumia Kawawa alianza mipango kabambe ya kujitayarisha hilo lisitokee. Hii ilikuwa nukta muhimu sanakwani haukupita muda baada ya uhuru kupatikana mwaka wa 1961 viongozi hawa wa vyama vya wafanyakazi wakajikuta wamewekwa kizuizini. Wasomaji wangependa kujua Kawawa alijihisi vipi wakati viongozi wenzake wa vyama vya wafanyakazi aliofanya nao kazi wakati wa kudai uhuru wakishirikiana na TANU kama Victor Mkello, Paul Pamba, Abdallah Mwamba, Hassan Khupe, Salum Abdallah na wengine wengi walipokamatwa mwaka wa 1964 na kuwekwa kizuizini kwa amri ya Mwalimu Nyerere. Maelezo ya Mzee Kawawa katika mambo haya yangetia mwanga katika yale mengi yasiyofahamika katika historia ya Tanzania.

Waislam wangependa sana kujua hisia za Kawawa kama muumini alihisi vipi wakati makachero walipomvamia mzalendo aliyepigania uhuru wa Tanganyika Mufti wa TanganyikaSheikh Hassan bin Amir usiku wa manane na kumrudisha Zanzibar na kuwekewa masharti kuwa hana ruhusa kurejea Tanzania Bara. Nilitegemea kusoma sakata zima la kukamatwa kwa Sheikh Hassan bin Amir na kuvunjwa kwa East African Muslim Welfare Society (EAMWS) jumuia ya Waislam iliyokuwa ikipanga kujenga Chuo Kikuu Dar es Salaam.

Nilitegemea halikadhalika kusoma mchango wa Mzee Kawawa katika kuunda Bakwata. Mengi yamesemwa kuhusu hujuma hii kwa Waislam moja wapo ni kuwa EAMWS ilivunjwa kwa shinikizo la Kanisa Katoliki likimtumia Mwalimu Nyerere. Hili si jambo la siri tena tafiti mbalimbali zimefanywa na vitabu kuandikwa na waandishi kutoka nje ya Tanzania kuhusu tatizo hili la kujitokeza udini mapema baada ya uhuru kupatikana. Kwa kuwa Kawawa alikuwa pamoja na Mwalimu Nyerere na alishiriki katika kuunda Bakwata wananchi hasa Waislam wangenufaika kusoma hisia zake wakati maamuzi hayo yanapitishwa na serikali. Kwa hakika kuna maamuzi mengi sanaambayo Kawawa alishiriki yaliwaumiza sanaWaislam katika juhudi zao za kujitafutia elimu. Waislam wangependa sana kujua ni kipi kilikuwa kinamsukuma kufanya vile.

Kwa yeyote atakaepata bahati ya kusoma kitabu cha maisha ya Mzee Kawawa ni wazi hatakuta jipya ambalo hakuwa akilijua kabla. Kwa ajili hii basi mlango bado uko wazi kwa watafiti wengine kuandika kitabu kuhusu Rashidi Mfaume Kawawa kwani maisha ya Mzee Kawawa bado hayajaandikwa. Hata hivyo tumpongeze mwandishi kwa kazi hii kwani ni baada ya yeye kutuandikia kitabu ndipo nasi tumepata nguvu ya kunyanyua kalamu zetu na kusema.

Mohamed Said
3rd January 2010

Ukipenda unaweza ukaingia hapa:Mohamed Said: TUNAMKUMBUKA MZEE RASHID MFAUME KAWAWA ALIYETUTOKA TAREHE 31 DESEMBA 2009
 
Hayo majina yasiyojulikana ya hao mashujaa/Machief yalifichwa kwa sababu ni ya Kiarabu? Na wewe umeyeweka ili kutufahamisha majina hayo au kutufahamisha kuwa walikuwa Waislam?
Kituko walioyaficha majina yale waliyopewa na baba zao hawakupenda wajulikane kama hawa walikuwa Waislam na mimi nimeyarejesha katika historia ili wajulikane kuwa walikuwa Waislam.
 
Kituko walioyaficha majina yale waliyopewa na baba zao hawakupenda wajulikane kama hawa walikuwa Waislam na mimi nimeyarejesha katika historia ili wajulikane kuwa walikuwa Waislam.

So walikiwa wanapigania Uislam au haki yao kama binadamu?
 
So walikiwa wanapigania Uislam au haki yao kama binadamu?
Kituko,
Hii post iko nyuma hapo hebu isome hapa itakusaidia kuelewa:

bonge ya stori
ni vizuri kujua hao wapigania uhuru kama hivi, umekuwa neutral hujahusianisha maisha yake ya kupigania uhuru na udini wala ukabila, wala hujasema alikuwa baba ako mdogo, na wala hujatumia article hii ku diminish role mwalimu Nyerere au kumdis kwa namna yyte.

hivo ndio historia hupaswa kuandikwa big up, tukitaka kufichua historia zilizo fichwa tuwe impartial tutoe facts kama hivi.
RIP Waziri Kambona
Iceman,
Dini, kabila na vinginevyo vyote ni sehemu ya siasa.

Huwezi kuandika historia ya Kenya mathalan, ukaacha kuwataja Wakikuyu
hata kama huwapendi.

Na ukithubutu kufanya hivyo utamega na kukitupa nje kipande kikubwa cha
historia kwani vipi utamfikia Dedan Kimathi na wapiganaji wa Mau Mau?

Mchango wa Wakikuyu uko wazi kabisa.
Na sababu kwa nini iwe wao ziko wazi pia.

Msome Bildad Kaggia, ''Roots of Freedom.''

Hali kadhalika katika historia ya uhuru wa Tanganyika.
Vipi utaikwepa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na uifikie historia ya TANU?

Na sababu kwa nini iwe Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika ziko wazi pia.

Waliothubutu kuikwepa historia hiyo matokeo yake hii leo wewe unayajua ingawa
yanakutisha.

Utawajua vipi walioasisi TANU ikiwa huitaki historia ya Al Jamiatul Islamiyya?
 
Muelezaji wa historia hii umeelezea kwa weledi mzuri kama msomi mzuri kabisa... Ukiacha wale kwa kukosa kujiamini kila historia huingiza iman zao binafsi au huelezea kwa minajiri ya kuonesha wanaonewa na kumbe ni asili yao toka kitambo kulalamika na kujikuta kila kona duniani wanalalamika tu.

Nakupongeza sana. Tunahitaj watu wenye elimu ya kuelezea Historia kama ilivyo pasipo kuweka mihemko na kushadadia na story za vijiwe vya kahawa au mabarazan
 
Ninakumbuka nyimbo za mchaka mchaka sekondari tuliimba "Kambona ameolewa huko ulaya" propaganda ni kitu kibaya sana.​
Kuondoka Kwa Kambona lilikuwa ni pigo kubwa Kwa ustawi wa nchi yetu. Madhara ya kuondoka kwa Kambona tunayapata mpaka sasa
 
Pascal,
Wala mimi sishangai kwa wewe kusema hayo uliyosema kwani hao waliokuja
kuingia TANU 1954 hapo ndipo ulipo ukomo wao wa kujua mambo mtu hawezi
kuwalaumu kwani hawakuwapo na hawajui kilikuwapo nini kabla yao.

Lakini ukienda kwa waliokuwapo na wa miaka ya 1920 watakuambia kuwa
alikuwa Dr. Aggrey ndiyo aliyempa Kleist Sykes fikra ya kuanzisha African
Association alipokuja Tanganyika 1924.

Hii ni historia na kwa mtu mwenye ubongo uliokaa vyema atataka kumjua huyu
Aggrey ni nani, katoka nchi gani na vipi alikutana na Kleist na kumpa fikra hiyo
na huyi Kleist ni nani katika historia ya uhuru wa Tanganyika?

Ikiwa ubongo wako una maradhi basi utajilazimisha uridhike na TANU bila ya
kuifahamu African Association na waasisi wake wala kujiukiza imekuwaje ndugu
wawili Abdul na Ally Sykes wote wawe waasisi wa TANU na kadi zao za ziwe
zimefuatana na kadi ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere?

Kadi no. 1 Julius Nyerere, no. 2 Ally Sykes na no. 3 Abdul Sykes na kadi
zote hizo tatu ziwe na sahihi ya Ally Sykes?

Hakika haiwezekani kuwa haya yalikuja hivi hivi pasi ya kuwa na sababu.
Waarabu wana msemo: ''Ukiijua sababu huondoka ajabu.''

Sasa ukiwa haya yote huyataki nani mwenye hasara.

Mwenye hasara utakuwa wewe unaebakia na ujinga ilhali elimu ipo wazi na
kwa kuhitimisha nukta hii chembelecho Maalim Faiza, ''Elimu bila khiyana,''
elimu ipo na ukitaka utawezakuipata bure.

Hassan Upeka aliliambia jopo la Chuo Cha Kivukoni la waandishi wa historia
ya TANU kuwa haiwezekani mkamfikia Nyerere katika TANU bila ya kupita kwa
Abdul Sykes, hiyo haitakuwa historia ya TANU.

Lakini wewe unasema historia hii ya Kivukoni ndiyo iliyokupa alama ''A'' katika
mtihani.

Sawa wala mimi sistaajabu.
Leo tuaona nchi inavyohangaika na vyeti vya kughushi.

Haya ndiyo matokeo yake.

Vyuo vyenye kughushi na shule zake na vitabu vya kughushi vitatoa ''A'' kama hiyo
yako na wala mimi sikulaumu wewe.

Itatuchukua muda kukaa vyema.

Lakini Chuo Kikuu Cha Harvard na Oxford University Press baada ya kusoma historia
ya Kleist Sykes wamemtia katika Dictionary of African Biography (DAB).

Ukipenda unaweza kusoma hapo chini ukalinganisha na historia unayoijua wewe:
Mohamed Said: KLEIST SYKES (1894 - 1949) KATIKA DICTIONARY OF AFRICAN BIOGRAPHY (DAB) OXFORD UNIVERSITY PRESS, NEW YORK

DSCN1159.JPG
Mohammed said, what are your motives?
 
Paskali/Hamidu
Nakuomba uangalie haya maelezo hapa chini ili upate picha kamili
ya Chuo Cha Kivukoni na uwezo wake wa kuandika historia ya nchi
hii

... Katika majina hayo angeweza kudodosa mengi kutoka kwa Mzee Kawawa na hivyo kuandika yale ambayo hayafahamiki kwa wengi. Hii imgekifanya kitabu kiwe cha maana.Kwa yeyote atakaepata bahati ya kusoma kitabu cha maisha ya Mzee Kawawa ni wazi hatakuta jipya ambalo hakuwa akilijua kabla. Kwa ajili hii basi mlango bado uko wazi kwa watafiti wengine kuandika kitabu kuhusu Rashidi Mfaume Kawawa kwani maisha ya Mzee Kawawa bado hayajaandikwa. Hata hivyo tumpongeze mwandishi kwa kazi hii kwani ni baada ya yeye kutuandikia kitabu ndipo nasi tumepata nguvu ya kunyanyua kalamu zetu na kusema.
Mohamed Said
3rd January 2010

Ukipenda unaweza ukaingia hapa:Mohamed Said: TUNAMKUMBUKA MZEE RASHID MFAUME KAWAWA ALIYETUTOKA TAREHE 31 DESEMBA 2009
Mkuu Maalim Mohamed Said, kwanza asante kwa haya machache kumhusu Simba wa Vita, Mzee Rashid Mfaume Kawawa. Uandishi wa biography ni kama ulivyo usandishi wa bibliography, mwandishi anaandika yale tuu yanayotakiwa kufahamika in public, hivyo hicho alichoandika Magotti ndicho Kawawa alitaka kiandikwe. Tofauti ya biography na bibliography, biagraphy inaandikwa na mwingine na bibliography unaandika mwenyewe, sasa pale historia inapoandikwa na mwingine, itasadifu nia na malengo ya mwandishi wa historia hiyo, ndio maana kunaweza kuandikwa mengi kumhusu mtu huyo huyo mmoja mfano Nyerere, mwanmdishi mmoja mwenye lengo la kumtukuza, atamuandika kwa mema na kama kuna ubaya wowote hatauandika kutokana na malengo kusudiwa, mfano biography ya Nyerere ikiandikwa na wafia dini wa Wakristu Wakatoliki, tumeaminishwa Nyerere alikuwa Mtakatifu, kumaanisha ni mtu ambaye hakutenda dhambi yoyote na sasa hivi tuko kwenye mchakato wa canonization kumtaangaza Mwenye Heri ambayo ni hatua moja kabla ya kutangazwa Mtakatifu Mwalimu Juliasi Kambarage Nyerere, ambapo baada ya hapo Watoliki tutakuwa tunasali kupitia yeye na kuzifikisha sala zetu moja moja kwa Mungu Baba. Biography ya Nyerere ikiandikwa na wafia dini wa Kiislamu, Muslim fundamentalist kama ..., watamwandika Nyerere kwa ubaya na kumueleza ni mdini na dikiteta wa hatari aliyeifutilia mbali EAMWS, waandishi wote watakuwa right kwa mujibu wa kusudio la mwandishi, hivyo Dr, Magotti is very right kumuandika Kawawa hivyo alivyomuandika.

Ila mimi kama kawaida yangu ni kusoma, in between the lines kwa kubaini the motive behind ukosoaji wako wa andiko la Magoti.

Mathalan Kawawa angeeleza mtafaruku kati ya Mwalimu Nyerere na Dk. Mwanjisi nini chanzo chake na nini ikajakuwa matokeo yake.
Hapa the motive ulitaka hoja ya mtafaruku!. Sii nia ya mwandishi kuelezea kuhusu mitafaruku!

Kisa cha Ali Migeyo ni moja ya visa vinavyosikitisha sana katika historia ya Tanganyika kwani aliwekwa kizuizini na Mwalimu Nyerere kama alivyofungwa na Waingereza. Haiwezekani kuwa Kawawa asiwe na habari na kile kilichopelekea mpigania uhuru hodari kama Ali Migeyo aishie jela tena wakati nchi ikiwa huru. Migeyo alifungwa na wakoloni kwa kuwahamasisha Watanganyika kudai uhuru labda Mzee Kawawa angeulizwa angeeleza ni nini kilitokea wakaamua kumfunga Migeyo kama walivyomfunga Waingereza.
Hapo the motive ni kueleza kuwa Nyerere alimtia kizuizini Ali Migeyo, hivyo kuonyesha na Kawawa alihusika!.
Kitabu kimegusia kazi alofanya Kawawa kama mtumishi wa serikali ya kikoloni katika kambi za raia wa Kenya walioshukukiwa kuwa ni Mau Mau. Katika hawa wafungwa walikuwawepo wananchama wa TANU ingawa hawa walikuwa Wakenya. Maarufu katika hawa alikuwa Dome Okochi Budohi (ambae kadi yake ya TANU ilikuwa na 6) na Patrick Aoko. Kawawa ni mmoja kati ya viongozi hawa na ingependeza sana kama kupitia kwake tungeelezwa jinsi KAU na TAA ilivyokuwa ikishirikiana kwani haiwezekani kuwa Budohi na Kawawa uswahiba wao ukaishia kwenye kucheza senema tu.
hapa the motive ni kuonyesha jinsi Kawawa alivyowatosa maswahiba wake!.
Wanaharakati wote walishtushwa na kutiwa mbaroni kwa Budohi na Aoko. Haiwezekani kuwa iwe Mzee Kawawa kasahau matukio haya muhimu. Budohi na Aoko walikuwa wamefungwa minyororo walipokuwa katika selo pale Kituo cha Kati cha Polisi kwa sasa jumba hiloliko kituo cha mabasi kinachojulikana kama“station.” Waliwekwa pale kwa miezi sita muda wote wakiwa na minyororo miguuni. Waliwekwa pale kwa miezi sita wakihojiwa kabla hawajapelekwa Handeni walipomkuta Kawawa. Hivi ndivyo vitu ambavyo kwa hakika vingeongeza ladha ya kitabu cha Mzee Kawawa endapo mwandishi angechukua muda kutafiti na kuzungumza na watu waliokuwa katika harakati wakati ule ambao bado wa hai kama Mzee Chipaka.
Hapa unalazimisha kuwa haiwezekani Kawawa kusahau tukio hili unaloliita muhimu, ni muhimo kwako na sio kwake, kuna baadhi yetu tumefunza kuweka kumbukumbu za mambo mema tuu na sio mabaya!, lengo ni kuonyesha Kawawa ndie alikuwa korokoroni wa Bodohi na Aoko!
Katika migomo ya wakati wa kudai uhuru hakuna mgomo uliofanikiwa na kuvuta hisia za wananchi kama mgomo wa reli wa mwaka 1960 uliodumu kwa siku 62. Inasemekana Mwalimu Nyerere akimtumia Kawawa alianza mipango kabambe ya kujitayarisha hilo lisitokee. Hii ilikuwa nukta muhimu sanakwani haukupita muda baada ya uhuru kupatikana mwaka wa 1961 viongozi hawa wa vyama vya wafanyakazi wakajikuta wamewekwa kizuizini. Wasomaji wangependa kujua Kawawa alijihisi vipi wakati viongozi wenzake wa vyama vya wafanyakazi aliofanya nao kazi wakati wa kudai uhuru wakishirikiana na TANU kama Victor Mkello, Paul Pamba, Abdallah Mwamba, Hassan Khupe, Salum Abdallah na wengine wengi walipokamatwa mwaka wa 1964 na kuwekwa kizuizini kwa amri ya Mwalimu Nyerere. Maelezo ya Mzee Kawawa katika mambo haya yangetia mwanga katika yale mengi yasiyofahamika katika historia ya Tanzania.
Hapa the motive behind ni kumuonyesha Kawawa kuwa was a snitch!.
Waislam wangependa sana kujua hisia za Kawawa kama muumini alihisi vipi wakati makachero walipomvamia mzalendo aliyepigania uhuru wa Tanganyika Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Amir usiku wa manane na kumrudisha Zanzibar na kuwekewa masharti kuwa hana ruhusa kurejea Tanzania Bara. Nilitegemea kusoma sakata zima la kukamatwa kwa Sheikh Hassan bin Amir na kuvunjwa kwa East African Muslim Welfare Society (EAMWS) jumuia ya Waislam iliyokuwa ikipanga kujenga Chuo Kikuu Dar es Salaam.
Hapa the motive ni kumchonganisha Kawawa na Waislamu, kwa vile alikuwa Mwislamu, alitegemewa kuingilia kati hizo issues za udini kwa kutetea Uislamu!.
Nilitegemea halikadhalika kusoma mchango wa Mzee Kawawa katika kuunda Bakwata. Mengi yamesemwa kuhusu hujuma hii kwa Waislam moja wapo ni kuwa EAMWS ilivunjwa kwa shinikizo la Kanisa Katoliki likimtumia Mwalimu Nyerere. Hili si jambo la siri tena tafiti mbalimbali zimefanywa na vitabu kuandikwa na waandishi kutoka nje ya Tanzania kuhusu tatizo hili la kujitokeza udini mapema baada ya uhuru kupatikana. Kwa kuwa Kawawa alikuwa pamoja na Mwalimu Nyerere na alishiriki katika kuunda Bakwata wananchi hasa Waislam wangenufaika kusoma hisia zake wakati maamuzi hayo yanapitishwa na serikali. Kwa hakika kuna maamuzi mengi sanaambayo Kawawa alishiriki yaliwaumiza sanaWaislam katika juhudi zao za kujitafutia elimu. Waislam wangependa sana kujua ni kipi kilikuwa kinamsukuma kufanya vile.
Hili pia ni uchonganishi wa dini ili kuonyesha Kawawa had a hand kwa kutozuia!.

Naomba niishie hapa kwa sababu kila tunapokutana katika minakasha humu na ukachomekea udini, kiukweli tunakuwa mbali mbali nisije kukuvunjia heshima kwa kukuita mrongo kuwa ni Kanisa Katoliki lilitumika kuivunja EAMWS simply kwa vile Mwalimu ni Mkatoliki!.

Kwa taarifa tuu Mzee wangu Andrew Mayalla, ambaye ni Mkatoliki na akitokea kanda moja na Nyerere, akiwa RSO wa Mwanza mwaka 1976, aliwekwa sana kizuizini na Mwalimu. James Mapalala ni Mkristu Mkatoliki akisali misa moja na kanisa moja na Nyerere, lakini Nyerere alimuweka sana kizuizini. Hii maana yake kila aliyewekwa kizuizini na Nyerere aliwekwa kwa sababu, regardless jina lake ni Ali, Juma au Joni!. Kawawa hakuwa na sababu ya kuyaeleza haya!.

Paskali
 
Mohammed said, mbona unakuwa mbaguzi mkuu, lengo lako tutambue mchango wa uislamu katika kupigania na kuleta Uhuru wa nchi Hii. Tujaribu kuweka kando kidogo hizi habari za imani zetu.
Imani zetu ni kubwa kuliko akili zetu na zinaweza kutusababishia madhara mkubwa.
 
Mkuu Maalim Mohamed Said, kwanza asante kwa haya machache kumhusu Simba wa Vita, Mzee Rashid Mfaume Kawawa. Uandishi wa biography ni kama ulivyo usandishi wa bibliography, mwandishi anaandika yale tuu yanayotakiwa kufahamika in public, hivyo hicho alichoandika Magotti ndicho Kawawa alitaka kiandikwe. Tofauti ya biography na bibliography, biagraphy inaandikwa na mwingine na bibliography unaandika mwenyewe, sasa pale historia inapoandikwa na mwingine, itasadifu nia na malengo ya mwandishi wa historia hiyo, ndio maana kunaweza kuandikwa mengi kumhusu mtu huyo huyo mmoja mfano Nyerere, mwanmdishi mmoja mwenye lengo la kumtukuza, atamuandika kwa mema na kama kuna ubaya wowote hatauandika kutokana na malengo kusudiwa, mfano biography ya Nyerere ikiandikwa na wafia dini wa Wakristu Wakatoliki, tumeaminishwa Nyerere alikuwa Mtakatifu, kumaanisha ni mtu ambaye hakutenda dhambi yoyote na sasa hivi tuko kwenye mchakato wa canonization kumtaangaza Mwenye Heri ambayo ni hatua moja kabla ya kutangazwa Mtakatifu Mwalimu Juliasi Kambarage Nyerere, ambapo baada ya hapo Watoliki tutakuwa tunasali kupitia yeye na kuzifikisha sala zetu moja moja kwa Mungu Baba. Biography ya Nyerere ikiandikwa na wafia dini wa Kiislamu, Muslim fundamentalist kama ..., watamwandika Nyerere kwa ubaya na kumueleza ni mdini na dikiteta wa hatari aliyeifutilia mbali EAMWS, waandishi wote watakuwa right kwa mujibu wa kusudio la mwandishi, hivyo Dr, Magotti is very right kumuandika Kawawa hivyo alivyomuandika.

Ila mimi kama kawaida yangu ni kusoma, in between the lines kwa kubaini the motive behind ukosoaji wako wa andiko la Magoti.

Hapa the motive ulitaka hoja ya mtafaruku!. Sii nia ya mwandishi kuelezea kuhusu mitafaruku!

Hapo the motive ni kueleza kuwa Nyerere alimtia kizuizini Ali Migeyo, hivyo kuonyesha na Kawawa alihusika!.
hapa the motive ni kuonyesha jinsi Kawawa alivyowatosa maswahiba wake!.
Hapa unalazimisha kuwa haiwezekani Kawawa kusahau tukio hili unaloliita muhimu, ni muhimo kwako na sio kwake, kuna baadhi yetu tumefunza kuweka kumbukumbu za mambo mema tuu na sio mabaya!, lengo ni kuonyesha Kawawa ndie alikuwa korokoroni wa Bodohi na Aoko!
Hapa the motive behind ni kumuonyesha Kawawa kuwa was a snitch!.

Hapa the motive ni kumchonganisha Kawawa na Waislamu, kwa vile alikuwa Mwislamu, alitegemewa kuingilia kati hizo issues za udini kwa kutetea Uislamu!.
Hili pia ni uchonganishi wa dini ili kuonyesha Kawawa had a hand kwa kutozuia!.

Naomba niishie hapa kwa sababu kila tunapokutana katika minakasha humu na ukachomekea udini, kiukweli tunakuwa mbali mbali nisije kukuvunjia heshima kwa kukuita mrongo kuwa ni Kanisa Katoliki lilitumika kuivunja EAMWS simply kwa vile Mwalimu ni Mkatoliki!.

Kwa taarifa tuu Mzee wangu Andrew Mayalla, ambaye ni Mkatoliki na akitokea kanda moja na Nyerere, akiwa RSO wa Mwanza mwaka 1976, aliwekwa sana kizuizini na Mwalimu. James Mapalala ni Mkristu Mkatoliki akisali misa moja na kanisa moja na Nyerere, lakini Nyerere alimuweka sana kizuizini. Hii maana yake kila aliyewekwa kizuizini na Nyerere aliwekwa kwa sababu, regardless jina lake ni Ali, Juma au Joni!. Kawawa hakuwa na sababu ya kuyaeleza haya!.

Paskali
Pascal,
Nashukuru kuwa umesoma yaliyokuwapo katika historia ya uhuru wa Tanganyika na umeyajua.

Nimeyaeleza na wengine pia wameyajua na watakuja watafiti wengine watayasoma na kama sisi watafanya uchambuzi wao na wataandika kama tulivyoandika sisi.

Muhimu kwangu ni kuwa chano kimefunuliwa uwanjani na kila mtu kakiona kilichokuwa kimefunikwa.
 
Mohammed said, mbona unakuwa mbaguzi mkuu, lengo lako tutambue mchango wa uislamu katika kupigania na kuleta Uhuru wa nchi Hii. Tujaribu kuweka kando kidogo hizi habari za imani zetu.
Imani zetu ni kubwa kuliko akili zetu na zinaweza kutusababishia madhara mkubwa.
Tejateja mbaguzi ni yule aliyefuta historia ya Waislam. Mimi nilichofanya nimeirejesha historia hiyo huu si ubaguzi.
 
bonge ya stori
ni vizuri kujua hao wapigania uhuru kama hivi, umekuwa neutral hujahusianisha maisha yake ya kupigania uhuru na udini wala ukabila, wala hujasema alikuwa baba ako mdogo, na wala hujatumia article hii ku diminish role mwalimu Nyerere au kumdis kwa namna yyte.

hivo ndio historia hupaswa kuandikwa big up, tukitaka kufichua historia zilizo fichwa tuwe impartial tutoe facts kama hivi.
RIP Waziri Kambona
Hii historia ya kambona mbona imejaa viraka vingi vyenye rangi tofauti?????!!!!! Hebu tupe asili ya taarifa yako.kwani hakuna historia isiyo na kalenda
 
Mohammed said, je wajua kuwa mambo ya dini/imani, hayatumii akili??
 
Back
Top Bottom