Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

Siku mwili wa kambona ukishuka uwanja wa ndege nyerere akwea pipa kwenda butiamaaaaa......alikua na bifu za kijinga
 
Nimesoma maandiko mengi sana yanayomuhusu kambona hata katika nadharia nyingi kuhusiana na Vita Ya Biafra kule Nigeria.Kweli katika jambo ambalo najutia na ninalichukia kupita kiasi ni kuimbishwa nyimbo za kumkashfu na kumtukana kambona nikiwa Nursery school.

Halafu kuna tawala nyingine ni za ajabu kweli kweli.hivi makosa ya ndugu inakuaje wakamatwe ndugu halafu wafungwe mika 10 na wengine waendelee kukamatwa na kufungwa hata baada ya mahakma kutoa hukumu ya kuwaachia huru?

Kwangu serikali ya Tanzani hadi leo imeonyesha Usaliti wa hali ya juu kutomuenzi Oscar kambona.Kwangu huyu ni shujaa hata kama nitamuona hivyo peke yangu kama ninavyoamini kwenye Ushujaa wa Kasim Hanga,Abdulrahaman Babu,Muammar Ghaddafi na Robert Mugabe
Kuna mambo mengi sana yanayoashiria kwamba Nyerere aliongoza nchi kibabe sana. Alikuwa ni a kind of a dikteta, ni vile tu kwamba yeye hakutumia sana jeshi. Kwa mfano watu wanasimulia operation sogeza ilivyofanywa kibabe, plus namna ambavyo alikuwa anawaweka kwenye vizuizi watu waliokuwa wanaonekana kukosoa fikra zake. Ndiyo akaanzisha na slogan ya zidumu fikra za mwenyekiti wa chama. Akiamini yeye ndiye mwenye fikra sahihi kuliko wengine.
Na kwa bahati mbaya sana mfumo wa siasa za kibabe na kionezi zimerithishwa kwa viongozi wengine ndani ya CCM ambao waliofuata baada ya Nyerere, kwa kumchukulia Nyerere kama mfano wa kiongozi bora. Lakini kusema ukweli ukiangalia katika mengi ambayo Kambona aliyatetea, unagundua kwamba huyu Nyerere alikuwa na vision mfu, zilizolitia taifa katika umasikini huu.
 
Neema yupo London na amejiunga na CHADEMA tawi la London siku za hivi karibuni.

Okey ..na wale watoto wengine wa kiume wawili?..ni kama hawapo. Nadhani neema ndie mtoyto pekee wa mzee kambona ambaye anayejua ukweli wa mambo maana hata katika maandiko mengi inaonesha Baba yake alikuwa akiandikiana mashairi na mwanaye huyo.. Wakati Kambona anarudi Dar toka uingereza aliambatana na Neema..nimesoma cover story yake jarida la femina(2004).. Kuna sehemu anasema "niliogopa sana sikujua nini kingetukuta, nilijiandaa kwa chochote. Nilimshikilia mkono baba na nikaapa sitamwacha. Kama wangempeleka jela ningekwenda pia"
 
Kuna mtu hapa ananidokeza kua uhuru wa Tanganyika ulipiganiwa na watu wengi sana ila kwa bahati mbaya historia zao zilifunikwa makusudi na muheshimiwa mwalimu.
Jamani wenye data mtumwagie.
 
Ni wakati sasa Oscar Nathaniel Kambona....one time Nyerere best friend na bestman kwenye ndoa yake na Florah ...apewe nafasi stahiki kwenye historia ya nchi hii

Inasemwa pia kuwa kawawa alimchongea sana kambona kwa mwalimu Katika kugombea kuwa right hand wa mwalimu........mwalimu alimuamini kawawa baada ya uasi wa jeshi....ambapo wanajeshi walimsikiliza kambona Huku kawawa na nyerere wakijificha kwenye secret house za usalama wa Taifa ,kigamboni....wanajeshi walitaka kumtangaza awe Rais ...aka kataaa

Baada ya uasi uhusiano ulianza kuzorota .....kupeleka kutofautiana mitazamo kwenye Azimio la Arusha....inasemekana nyerere alifahamu kutoroka kwa kambona na akaagiza apewe safe exit.
 
Kuna mambo mengi sana yanayoashiria kwamba Nyerere aliongoza nchi kibabe sana. Alikuwa ni a kind of a dikteta, ni vile tu kwamba yeye hakutumia sana jeshi. Kwa mfano watu wanasimulia operation sogeza ilivyofanywa kibabe, plus namna ambavyo alikuwa anawaweka kwenye vizuizi watu waliokuwa wanaonekana kukosoa fikra zake. Ndiyo akaanzisha na slogan ya zidumu fikra za mwenyekiti wa chama. Akiamini yeye ndiye mwenye fikra sahihi kuliko wengine.
Na kwa bahati mbaya sana mfumo wa siasa za kibabe na kionezi zimerithishwa kwa viongozi wengine ndani ya CCM ambao waliofuata baada ya Nyerere, kwa kumchukulia Nyerere kama mfano wa kiongozi bora. Lakini kusema ukweli ukiangalia katika mengi ambayo Kambona aliyatetea, unagundua kwamba huyu Nyerere alikuwa na vision mfu, zilizolitia taifa katika umasikini huu.

Kwa mfano operation ya Ujama vijijini ilikua na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.watu walihamishwa kwa lazima.Tunashukuru Mungu hii imeingia katika mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu kwamba kuhamisha watu kwa lazima ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

Hata operation ya CHINA ya vijini pia iliambatana na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.Leadership ni Inspiration.Akina Vladmir Lenin pamoja na uwezo na jeuri kubwa waliyokuwa nayo lakini katika operation yao ya ujamaa hakufanya ukiukwaji mkubwa ukilinganisha na wa Chairman Mao.Huko ndiko tulikua tunaelekea

Kitu kimoja nilichogundua kwenye utawala wa awamu ya kwanza spinning na high class propaganda zilitumika sana hasa propaganda ya kijivu ambayo hadi leo imeliathiri Taifa letu
 
Ni wakati sasa Oscar Nathaniel Kambona....one time Nyerere best friend na bestman kwenye ndoa yake na Florah ...apewe nafasi stahiki kwenye historia ya nchi hii

Inasemwa pia kuwa kawawa alimchongea sana kambona kwa mwalimu Katika kugombea kuwa right hand wa mwalimu........mwalimu alimuamini kawawa baada ya uasi wa jeshi....ambapo wanajeshi walimsikiliza kambona Huku kawawa na nyerere wakijificha kwenye secret house za usalama wa Taifa ,kigamboni....wanajeshi walitaka kumtangaza awe Rais ...aka kataaa

Baada ya uasi uhusiano ulianza kuzorota .....kupeleka kutofautiana mitazamo kwenye Azimio la Arusha....inasemekana nyerere alifahamu kutoroka kwa kambona na akaagiza apewe safe exit.

Nyerere,Kambona na Kawawa naona ushirika wao ulikua unaelekea kuja kufanana na uhusiano wa Lenin,Trosky na Joseph Stalin
 
WaTanzania tuna bahati mbaya sana historia ya hawa wazee wetu haikuandikwa sawasawa.Kambona kafa na historia yake sijui kwanini wasomi wetu hawapendi kuandika vitabu ambavyo vingeweza kutusaidia kujua walikotoka na makosa gani walifanya ili kuepuka kujirudia siku za usoni.

Siku hizi wanajitokeza wanahistoria uchwara wanapotosha kama anavyofanya mohamed Said.Kawawa katutoka hakuna kitabu chake,Chief Abdallah Fundikira,.....hakuna vitabu vyao.
 
Fasali Kambona yeye mewesa kukimbia, Sujaa Moringe Sokoine yeye imesokoinewa mapema.
 
Hivi huyu Kambona hayuko kwenye lile kundi la wazee wa Gerezani.Ni wazi kabisa tofauti zake na Mwl Nyerere zilimsababishia mateso makubwa ikiwemo kuishi uhamishoni kwa miaka 27.Mzee wa ngano za Gerezani sijui kama kamtia kwenye kile kitabu chake au kwakuwa ni mgalatia anaweza kumsahau.

Mkuu Ngongo,

Mtendee haki Oscar Kambona.
 
Last edited by a moderator:
... Mleta mada umenikumbusha enzi hizo tulikuwa tunaimbishwa wimbo usemao
"kambona, aa x2, ameolewa"
"na nani, na na x2, na mwingereza"
"wapi? U u x2 huko Ulaya"

kwa ujumla, nilikuwa sijui historia ya huyu jamaa, na kwa nini tulikuwa tunaimbishwa wimbo huo.
 
Siyo unasikia kitu kimoja tu unaconclude mkubwa. Vile vile tafuta upande wa pili. Kwa nini huyu jamaa alikimbilia Uingereza na wala siyo China?

Wewe kwanini usitafute na kutuletea vya upande wa pili? yeye katafuta upande wa kwanza.

Wewe tuambie kwanini asikimbilie Uingereza na akimbilie China?
 
Halafu huyo Nyerere ndiye anaetaka kupewa "utakatifu" kwa lipi jema aliloifanyia nchi hii?
 
... Mleta mada umenikumbusha enzi hizo tulikuwa tunaimbishwa wimbo usemao
"kambona, aa x2, ameolewa"
"na nani, na na x2, na mwingereza"
"wapi? U u x2 huko Ulaya"

kwa ujumla, nilikuwa sijui historia ya huyu jamaa, na kwa nini tulikuwa tunaimbishwa wimbo huo.
Hata mimi nakumbuka shule ya msingi tulikuwa tunaimba wimbo wa kumlaani Kambona kama muasi.
Nakumbuka tulikuwa tunaimba
Kambona mhaini huyoooo x 2
sasa yupo wapi (mwimbishaji)
Yupo Uingereza (waitikiaji).
Yaani Kambona alikuwa anaonekana ni jamaa wa hovyo vibaya sana. Those days nilikuwa naimba tu hata sielewi kwanini natakiwa kuimba hivyo. Sasa ndiyo tunatambua who was Kambona. Nyerere alikuwa na itikadi za kijinga sana ukijaribu kuchunguza. Katika suala la kutumia mabavu zaidi kuliko akili, katu sitamuunga mkono Nyerere.
 
Halafu huyo mfu Nyerere ndiye anaetaka kupewa "utakatifu" kwa lipi jema aliloifanyia nchi hii?
Hili la kumpa utakatifu ni kampeni za Mseveni! Sijui anataka kumshukuru Nyerere kwa kumuwezesha kuwa Rais, hata sielewi. Lakini kama kuna watu wanatakiwa kupata utakatifu ndani ya kanisa katoliki, kutokea hapa Tanzania, basi Nyerere atakuwa wa mwisho kupata huo utakatifu. He totally doesn't deserve it. Tunashukuru tu kwamba kanisa Katoliki lipo stable, haliyumbishwi na siasa. Tunaamini halitajipaka matope kwa kumpa utakatifu mtu asiyestahili.
 
kulikuwa na msuguano mkali, kiasi kwamba ilimlazimu Kambona alijiuzulu ... na hatimaye yeye na familia yake wakakimbilia Nairobi
Hapo ndo kuna missing pieces of the puzzle. Hivi leo hii ukisikia, kwa mfano, Taso kakwaruzana na Invisible halafu Taso kakimbia. Nini kinakujia mawazoni? Taso kaharibu!

Hadithi ya Kambona ina gap kubwa sana, hapo pa "akajiuzulu, hatimaye akakimbia." Tunaambiwa akakimbia lakini hatuambiwi alikuwa anatafutwa. Umeshajiuzulu, unakimbia, kwa nini unakimbia? Hivi wewe ukisema Ubeberu ndio mzuri kwa nchi yetu halafu mimi nikasema hapana nadhani Ubwanyenye ndio mzuri. Kwa nini sasa wewe ukimbie?

Kwa kweli nikifika hapo pa "akajiuzulu hatimae akakimbia" huwa nacheka sana. It doesn't make any sense. Halafu kwa nini wadogo zake Kambona nao walifungwa? Walihukumiwa kwa kosa gani katika mahakama gani masikini ya Mungu?
 
Kwa mfumo wa enzi za Nyerere hili halishangazi, kwa kuwa ilikuwa ukikwaruzana na kupingana naye kidogo anahisi utampindua. Kutokana na aina yake ya utawala alikuwa anamwogopa kila mtu. Na hii ndiyo sababu iliyopelekea akina Bibi Titi Mohamed kufungwa jela na baadaya wakaja kukata rufaa kwenye mahakama kuu ya Africa mashariki, ndiyo wakatolewa. Ni wazi mahakama za wakati ule zilikuwa zinafanya kazi kama hizi za sasa, ambapo hukumu inatolewa kwa amri ya Rais na si ya sheria za nchi.

Nyerere mwenyewe aliwahi kusema siku moja kwamba kuna waziri wake alikula rushwa, akaamuru achapwe viboko kumi na mbili wakati wa kuingia jela na wakati wa kutoka, sasa utajiuliza Nyerere aliamuru kama nani ilihali mahakama ndizo zinazojua adhabu? Kiujumla nafikiri baada ya kujiuzulu Kambona alitambua kwamba kutokana na visasi vya Nyerere, anaweza kumtia jela. Siamini na sijaona popote panapoonyesha kwamba Kambona alipanga kumpindua Nyerere in anyway. Kama angetaka kufanya hivyo, basi ni dhahiri wakati ule Nyerere na Kawawa wamekimbia angeweza kujitwalia nchi na kuwaulia mbali hao akina Nyerere huko mafichoni.

Mimi naamini Nyerere alikuwa na misimamo ya kijinga, na alikuwa anapenda umungu mtu. watu wamuimbe wamsifie, bendi za mziki zimuimbe yeye. Na akajiita mtukufu Rais. Upumbavu kabisa. Tunamsfia bure tu.
 
Ulevi wa madaraka una sura nyingi sana,mojawapo ni kutoshaurika,au kushindwa kuona upande mzuri wa ushauri wa watu wengine ni ulevi tu na ni mbya sana pia.
 
A campaign by the government was started to vilify him again. First was the claim that he was not a citizen of Tanzania and had
never been one even though he had served as the country's minister of home affairs, minister of defence, and minister of foreign
affairs, and even led the struggle for independence with Nyerere in the 1950s. Yet nothing was said in all those years that he was not a citizen of Tanganyika. It was only decades later, in the 1990s, that the government said he was not a Tanzanian but a Malawian. Others said he was a Mozambican.

The government even withdrew his passport on the same grounds that he was not a Tanzanian citizen.He could not even travel
outside the country after his passport was withdrawn. The vilification campaign against him by the Tanzanian government made the government look bad and it finally relented and gave the passport back to him. Kambona himself had his own "revelations"concerning the national identities of other Tanzanian leaders including President Nyerere himself.

He said Nyerere's father was a Tutsi from Rwanda who was a porter for the Germans and settled in Tanganyika and that he could prove it. He also said Vice President Rashid Kawawa came from Mozambique, and John Malecela - who once served as Tanzania's foreign affairs minister, prime minister and vice president among other posts at different times -came from Congo where his grandparents were captured as slaves before they settled in Dodoma, central Tanzania. But few people took any of those claims seriously any more than they did the claim that Kambona himself was not a Tanzanian citizen but a Malawian, from Likoma Island, or a Mozambican.

en.m.wikipedia.org/wiki/Oscar_Kambona/
 
Back
Top Bottom