Arnoldinho
Senior Member
- Jan 14, 2013
- 119
- 24
Siku mwili wa kambona ukishuka uwanja wa ndege nyerere akwea pipa kwenda butiamaaaaa......alikua na bifu za kijinga
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuna mambo mengi sana yanayoashiria kwamba Nyerere aliongoza nchi kibabe sana. Alikuwa ni a kind of a dikteta, ni vile tu kwamba yeye hakutumia sana jeshi. Kwa mfano watu wanasimulia operation sogeza ilivyofanywa kibabe, plus namna ambavyo alikuwa anawaweka kwenye vizuizi watu waliokuwa wanaonekana kukosoa fikra zake. Ndiyo akaanzisha na slogan ya zidumu fikra za mwenyekiti wa chama. Akiamini yeye ndiye mwenye fikra sahihi kuliko wengine.Nimesoma maandiko mengi sana yanayomuhusu kambona hata katika nadharia nyingi kuhusiana na Vita Ya Biafra kule Nigeria.Kweli katika jambo ambalo najutia na ninalichukia kupita kiasi ni kuimbishwa nyimbo za kumkashfu na kumtukana kambona nikiwa Nursery school.
Halafu kuna tawala nyingine ni za ajabu kweli kweli.hivi makosa ya ndugu inakuaje wakamatwe ndugu halafu wafungwe mika 10 na wengine waendelee kukamatwa na kufungwa hata baada ya mahakma kutoa hukumu ya kuwaachia huru?
Kwangu serikali ya Tanzani hadi leo imeonyesha Usaliti wa hali ya juu kutomuenzi Oscar kambona.Kwangu huyu ni shujaa hata kama nitamuona hivyo peke yangu kama ninavyoamini kwenye Ushujaa wa Kasim Hanga,Abdulrahaman Babu,Muammar Ghaddafi na Robert Mugabe
Neema yupo London na amejiunga na CHADEMA tawi la London siku za hivi karibuni.
Kuna mambo mengi sana yanayoashiria kwamba Nyerere aliongoza nchi kibabe sana. Alikuwa ni a kind of a dikteta, ni vile tu kwamba yeye hakutumia sana jeshi. Kwa mfano watu wanasimulia operation sogeza ilivyofanywa kibabe, plus namna ambavyo alikuwa anawaweka kwenye vizuizi watu waliokuwa wanaonekana kukosoa fikra zake. Ndiyo akaanzisha na slogan ya zidumu fikra za mwenyekiti wa chama. Akiamini yeye ndiye mwenye fikra sahihi kuliko wengine.
Na kwa bahati mbaya sana mfumo wa siasa za kibabe na kionezi zimerithishwa kwa viongozi wengine ndani ya CCM ambao waliofuata baada ya Nyerere, kwa kumchukulia Nyerere kama mfano wa kiongozi bora. Lakini kusema ukweli ukiangalia katika mengi ambayo Kambona aliyatetea, unagundua kwamba huyu Nyerere alikuwa na vision mfu, zilizolitia taifa katika umasikini huu.
Ni wakati sasa Oscar Nathaniel Kambona....one time Nyerere best friend na bestman kwenye ndoa yake na Florah ...apewe nafasi stahiki kwenye historia ya nchi hii
Inasemwa pia kuwa kawawa alimchongea sana kambona kwa mwalimu Katika kugombea kuwa right hand wa mwalimu........mwalimu alimuamini kawawa baada ya uasi wa jeshi....ambapo wanajeshi walimsikiliza kambona Huku kawawa na nyerere wakijificha kwenye secret house za usalama wa Taifa ,kigamboni....wanajeshi walitaka kumtangaza awe Rais ...aka kataaa
Baada ya uasi uhusiano ulianza kuzorota .....kupeleka kutofautiana mitazamo kwenye Azimio la Arusha....inasemekana nyerere alifahamu kutoroka kwa kambona na akaagiza apewe safe exit.
Hivi huyu Kambona hayuko kwenye lile kundi la wazee wa Gerezani.Ni wazi kabisa tofauti zake na Mwl Nyerere zilimsababishia mateso makubwa ikiwemo kuishi uhamishoni kwa miaka 27.Mzee wa ngano za Gerezani sijui kama kamtia kwenye kile kitabu chake au kwakuwa ni mgalatia anaweza kumsahau.
Siyo unasikia kitu kimoja tu unaconclude mkubwa. Vile vile tafuta upande wa pili. Kwa nini huyu jamaa alikimbilia Uingereza na wala siyo China?
Hata mimi nakumbuka shule ya msingi tulikuwa tunaimba wimbo wa kumlaani Kambona kama muasi.... Mleta mada umenikumbusha enzi hizo tulikuwa tunaimbishwa wimbo usemao
"kambona, aa x2, ameolewa"
"na nani, na na x2, na mwingereza"
"wapi? U u x2 huko Ulaya"
kwa ujumla, nilikuwa sijui historia ya huyu jamaa, na kwa nini tulikuwa tunaimbishwa wimbo huo.
Hili la kumpa utakatifu ni kampeni za Mseveni! Sijui anataka kumshukuru Nyerere kwa kumuwezesha kuwa Rais, hata sielewi. Lakini kama kuna watu wanatakiwa kupata utakatifu ndani ya kanisa katoliki, kutokea hapa Tanzania, basi Nyerere atakuwa wa mwisho kupata huo utakatifu. He totally doesn't deserve it. Tunashukuru tu kwamba kanisa Katoliki lipo stable, haliyumbishwi na siasa. Tunaamini halitajipaka matope kwa kumpa utakatifu mtu asiyestahili.Halafu huyo mfu Nyerere ndiye anaetaka kupewa "utakatifu" kwa lipi jema aliloifanyia nchi hii?
Hapo ndo kuna missing pieces of the puzzle. Hivi leo hii ukisikia, kwa mfano, Taso kakwaruzana na Invisible halafu Taso kakimbia. Nini kinakujia mawazoni? Taso kaharibu!kulikuwa na msuguano mkali, kiasi kwamba ilimlazimu Kambona alijiuzulu ... na hatimaye yeye na familia yake wakakimbilia Nairobi
Kwa mfumo wa enzi za Nyerere hili halishangazi, kwa kuwa ilikuwa ukikwaruzana na kupingana naye kidogo anahisi utampindua. Kutokana na aina yake ya utawala alikuwa anamwogopa kila mtu. Na hii ndiyo sababu iliyopelekea akina Bibi Titi Mohamed kufungwa jela na baadaya wakaja kukata rufaa kwenye mahakama kuu ya Africa mashariki, ndiyo wakatolewa. Ni wazi mahakama za wakati ule zilikuwa zinafanya kazi kama hizi za sasa, ambapo hukumu inatolewa kwa amri ya Rais na si ya sheria za nchi.Hapo ndo kuna missing pieces of the puzzle. Hivi leo hii ukisikia, kwa mfano, Taso kakwaruzana na Invisible halafu Taso kakimbia. Nini kinakujia mawazoni? Taso kaharibu!
Hadithi ya Kambona ina gap kubwa sana, hapo pa "akajiuzulu, hatimaye akakimbia." Tunaambiwa akakimbia lakini hatuambiwi alikuwa anatafutwa. Umeshajiuzulu, unakimbia, kwa nini unakimbia? Hivi wewe ukisema Ubeberu ndio mzuri kwa nchi yetu halafu mimi nikasema hapana nadhani Ubwanyenye ndio mzuri. Kwa nini sasa wewe ukimbie?
Kwa kweli nikifika hapo pa "akajiuzulu hatimae akakimbia" huwa nacheka sana. It doesn't make any sense. Halafu kwa nini wadogo zake Kambona nao walifungwa? Walihukumiwa kwa kosa gani katika mahakama gani masikini ya Mungu?