Ukweli tuuweke hapa kuhusu Kassim Mganga!

Ukweli tuuweke hapa kuhusu Kassim Mganga!

Kama huu wimbo wake mpya jamani kajamaa kameimba vizuri sana aiseee
Najua ushaumizwa mengi sana, ushakutana na ma-heart breaker,
Ila sio mimi, I am a good boy.
Walishazichezea hisia zako mpenzi wangu,
mwisho wa siku wakakuacha ukilia
Mapenzi ukayachukia,
ila sio mimi....;I am a good boy, I am a good boy.....
 
Najua ushaumizwa mengi sana, ushakutana na ma-heart breaker,
Ila sio mimi, I am a good boy.
Walishazichezea hisia zako mpenzi wangu,
mwisho wa siku wakakuacha ukilia
Mapenzi ukayachukia,
ila sio mimi....;I am a good boy, I am a good boy.....
Don't call me lover........I am innocent baby......
Yani naupenda hatari
 
Ligi Imeahamia kwa
Diamond VS Kassim Mganga
 
Kassim anajua sana...sanaaaa!
Kwa nyimbo za mahaba hafai huyu mtu.
Moja kati ya nyimbo zake nizipendazo ni Usiende kwa mganga.
Eeeh bwana,anavyoimba taratibu...na ile video walivyoweza kuuvaa uhusika acha kabisa.

Shkamoo Kassim [emoji119]
jamani hebu tumwagieni hapa hayo ya Kassim!
 
Natamani kukujibu ila naogopa heshima yangu kama inashuka vileee.....anyway ka mbway na iwe mbwayiii banaaaa....sie wenyewe utafiti unatutambua 1 out of 4...ahahahaha.

Tako na hips kajaaliwa sema babako kamzidiiiii.
Nahisi una umbo kama la jamaa ndo mana ume panick
 
Habari zenu wakuu!

Nimefikiria kitu kuhusu huyu jamaa, katika tasnia ya mziki hapa Tanzania! Huyu jamaa yupo vizuri, ukisikiliza nyimbo zake kuna tungo nzuri kwa lugha yetu ya kiswahili fasaha pasipo kuchanganya lugha za kigeni, pia ana mashairi yaliyotulia pasipo kuwa na matusi au misamiati ya kipuuzi!

Hakika jamaa anatisha sana kuliko hata hawa 'waramba midomo' wa sasa.

Ongeza ulichoona kutoka kwa huyu jamaa!
Huyo ni mdigo wa mkoa wa Tanga, halmashauri ya wilaya ya mkinga kwa yule jamaa aliyemtishia askari bastola, kwao kwaitwa MANZA BAY, ni mahali pazuri sana kwa utalii wa fukwe lakini viongozi wa mkinga wanazurura na kutishia wenzao.

Wadigo wapo njema sana kwa lugha ya Kiswahili na mashairi yakutongozea wanaongoza, mdigo anaweza kumuimbia mwanamke akalazimika lainiiiii akikaaasawa keshaliwa, hatari sana.
 
wimbo wake mpya ni mzuri sana lakini nashangaa kwanini haupati air time ya kutosha...jamaa ana kipaji sana?
Hivi Honey Faith huwa unakula ndizi au senene? kuna kitu nimegundua...
Yani ni mzuri sana kwa kweli sema tu nyota hana.
Sema kama unataka kuniletea ndizi na senene atiiiii acha maongezi marefuuuuu[emoji1] [emoji6]
 
Yani ni mzuri sana kwa kweli sema tu nyota hana.
Sema kama unataka kuniletea ndizi na senene atiiiii acha maongezi marefuuuuu[emoji1] [emoji6]
teh teh unajua kuna kitu nimekiangalia nikafikiri utakuwa unatumia ndizi na senene. Hongera...
Basi ntawasiliana na atoto atakuletea ndizi na senene
 
Aaah Awena sasa

Niliapa ukiondoka mpenzi, ntaondoka nawe
Sikuahidi kukufuta machozi, bali ntalia nawe
Ina maana hata kugeuka kunitazama hutaki Awena
Basi kama nakosa kwako nililofanya, nieleze Awena
Chozi langu la thamani unaliacha lianguke eeeh
Mti nilopanda zamani ina maana si chochote...........


Maneno matamu ulonipa chumbani, huku kichwa chako umelaza kifuani
Machozi yakikutiririka mashavuni
Kwamba hutoniacha mimi labda nitoweke duniani. ........
dah! haya mashairi bwana yanakonga sn aisee, jamaa ni mtaalamu wa mashairi, kuimba mpaka sauti, namkubali sn huyu kaka
 
Maneno matamu ulonipa chumbani huku kichwa chako umelaza kifuani machozi yakikutiririka mashavunii..... Dah kitu awena
 
Tajiri wa mahaba napenda anavyousifia sana mkoa wa Tanga na raha zake. Hapo tu ndo ninapomkubali mimi yani hata nikipita mtaani kifua mbele nikiulizwa mtoto wa wapi najibu bila wasiwasi mimi ni mgosi
 
Watu povu linawatoka kumsifia jamaa kajaliwa..mbona domo hua mnasema
 
Back
Top Bottom