Ukweli uliofichwa: Divai aliyotengeneza Yesu haikuwa ya kulevya

Kunywa pombe na kulewa ni vitu viwili tofauti..
Kunywa na kulewa vyote viwili vimekatazwa.⛔
Mambo ya Walawi 10:9
"Usinywe divai wala kileo chochote, wewe, wala wanao pamoja nawe, hapo mwingiapo ndani ya hema ya kukutania, ili kwamba msife; amri hii itakuwa ni amri ya milele katika vizazi vyenu."
Efe 5:18-20
"Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho..."
 
"Usinywe divai wala kileo chochote, wewe, wala wanao pamoja nawe, hapo mwingiapo ndani ya hema ya kukutania, ili kwamba msife; amri hii itakuwa ni amri ya milele katika vizazi vyenu."
Sasa hapo hiyo Divai iliyokatazwa ni juice ...? Na hilo fungu linaongelea mazingira gani, wakati gani na mahali gani usinywe pombe... Maana pia kuvaa viatu kuliwa ni marufuku wakati unajiandaa kuingia hemani... je tusivae viatu..?? Musipende kusoma maandiko kwa mihemko...
 
Mbona yeye alitengeneza divai huko mjini kana ?

Na kikombe Cha divai alichokichukua na kukitwaa kilikuwa kipi ?
 
Endelea tu kuukataa ukweli, to your own disadvantage.

"Kwa sababu hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo; ili wahukumiwe wote wasioamini ile kweli, bali walifurahia udhalimu." (2 Wathesalonike 2:11–12)
Umeanza lini kupingana na biblia unaelewa nini kuhusu mvinyo? Wale watu walimfuata mama yake wakamwambia sisi tunataka masanga mwambie Mwamba afanye miujiza hapa patokee kitu cha tungi, km unavyojua mama akawaambia kila atakachowaambia fanyeni kweli jamaa akafanya muujiza wa kutengeneza tungi bila kutumia kiwanda chochote sasa imekuaje unaanza kubishana na biblia lakini?
 
Watu wanashindwa kutofautisha kati ya divai na mvinyo. Divai ikihifadhiwa kwa muda mrefu ndo inakuwa mvinyo.
 
Okay.
Soma Matendo 2:13-21, Isaya 28:7 na. 1 Timotheo 5:23-25

Jihakikishie kabla ya kubandika.
 
Mathayo 11v18-19 Maana Yohama alikuja hali wala hanywi wakasema ana pepo
Mwana wa Adamu alikuja akila na kunywa wakasema mlafi huyu na mlevi .........

Luka 7v34 Mwana wa Adamu amekuja,anakula na kunywa nanyi mwasema ,Tazama mlafi huyu na mnywaji wa divai ,rafiki wao watoza ushuru na wenye dhambi ......

Sikia hii
Mathayo 15v16-17 Yesu akasema hata sasa ninyi nanyi mngali hamna akili ?Hamjafahamu bado ya kuwa kila kiingiacho kuinyani hupita tumboni kikatupwa chooni?

Marko 7v14-15 Akawait makutano tena, akawaambia, Nisikieni nyote na kufahamu .Hakuna kitu kilicho nje ya mtu kikimwingia chaweza kumtia unajisi(kumfanya kuwa na dhambi ),bali vile vimtokavyo .......

Siyo kwamba natetea pombe,ila kunywa pombe siyo dhambi
na usimtetee Yesu ,
Yesu alitamka tu na maji yakaw pombe
 
Hiyo Biblia inayosema Yesu alitengeneza tungi labda umeiandika mwenyewe. Ya kwangu inasema alitengeneza divai njema(non-alcoholic)
 
Hiyo Biblia inayosema Yesu alitengeneza tungi labda umeiandika mwenyewe. Ya kwangu inasema alitengeneza divai njema(non-alcoholic)
Divai njema si ndio hio hio tungi mtoto wa Mzee bwaksi
 
Hio kwako babu
 
Nenda ujifunze historia ya Biblia vizuri.
 
Ni vema pia kuwathibitishia wasomaji kuwa pombe yoyote ile ya kiwango chochote kile cha kilevi, kitaalamu au kisayansi, haina manufaa yoyote mwilini. Haina lishe au virutubisho vyovyote vya kusaidia kuujenga, kuupa nguvu au kuulinda mwili.

Ni kama zilivyo sigara zote zina madhara hatarishi kwa afya ya mwili. Hayo yote yamethibitishwa na madaktari bingwa duniani kote.

Yeyote anayetaka kulinda afya ya mwili wake na kuwa na akili timamu wakati wote, pamoja na mambo mengine, ajiepushe na unywaji pombe au uvutaji sigara na dawa zozote za kulevya. Akishindwa kujinasua nashauri atubu na kumwomba Yesu amwokoe na uraibu wa pombe wa kiwango chochote kile, ikiwemo kuonja.
 
Yohana 6v63 Roho ndiyo itiayo uzima ,mwili haufai kitu.Maneno haya niwaambiayo ni roho tena ni uzima

So. Paulo anaposema msilewe kwa mvinyo bali mjazwe Roho
haongelei mvinyo kama pombe,bali kuna kitu anamaanishasha hapo

kwasababu Roho hawezi kuwa mbadala wa pombe kama pombe hii konyagi

Warumi 14v17 Maana ufalme wa Mungu si wa kula wala kunywa bali ni haki amani na Furaha katika Roho Mtakatifu

ishu siyo kwamba unakunywa au haunywi ,note hiyo
 
Divai njema si ndio hio hio tungi mtoto wa Mzee bwaksi
Nimeishakuambia Yesu hawezi kutengeneza tungi halafu aseme wapiga tungi hawataurithi ufalme wa Mungu(1 Wakorintho 6:9-10)

Au ulipiga tungi nini, kabla ya kusoma huu uzi? Maana wanaopiga tungi macho yao yanaona mauzauza, kama Maandiko yanenavyo katika Mithali 23:33
 
Asante Gwappo Mwakatobe kwa kupigilia msumari 🔨
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…