Naona mauzauza tu Yesu hakufungua Bar pale Kana aligawa Pombe bure hakuchukua hata 100 ya mtuNimeishakuambia Yesu hawezi kutengeneza tungi halafu aseme wapiga tungi hawataurithi ufalme wa Mungu(1 Wakorintho 6:9-10)
Au ulipiga tungi nini, kabla ya kusoma huu uzi? Maana wanaopiga tungi macho yao yanaona mauzauza, kama Maandiko yanenavyo katika Mithali 23:33
View attachment 3311218
DR Mambo Jambo pitia hapa...Katika kitabu cha Yohana 2:1-25 kuna habari ya muujiza alioufanya Yesu wa kubadili maji kuwa divai - wakati wa arusi ya Kana. Hiyo divai aliyotengeneza Yesu, ilikuwa non-alcoholic; haikulewesha. Huu ni ukweli ambao shetani hapendi uujue ili uangamie kwa dhambi ya ulevi. Twende pamoja sasa nikufichulie ukweli wenyewe.
Watu wamekuwa wakitumia Andiko hilo kuhalalisha unywaji wa pombe. Hebu leo tujifunze sababu zinazoonyesha wazi kuwa divai aliyotengeneza Yesu haikuwa pombe(kileo).
Kulingana na muktadha, neno “divai” katika Biblia linamaanisha ama:
1. Juisi ya zabibu isiyo na kilevi(non-alcoholic) au
2. Pombe
Mstari wenye maana ya kwanza ya divai upo katika Isaya 65:8. Huo mstari unazungumzia juisi mpya ya zabibu, isiyo na alcohol.
“BWANA asema hivi, Kama vile divai mpya ipatikanavyo katika kichala, na mtu mmoja husema, usikiharibu kwa maana mna baraka ndani yake...”
Katika Mithali 20:1 tunasoma maana ya pili ya divai:
"Divai huleta dhihaka na kileo huleta ugomvi; Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima.”
Katika andiko hilo "divai' inamaanisha mvinyo au pombe(alcohol).
Yesu alitengeneza aina ya kwanza ya divai isiyolewesha. Kwanini? Kwa sababu kama angetengeneza pombe, asingesema:
“Wala msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi.”(Waefeso 5:18)
Yesu asiye na dhambi, asingeweza kutengeneza kinywaji kitakachowafanya watu waanguke dhambini. Divai aliyotengeneza Yesu ilikuwa mpya, tamu, na yenye baraka—sio ya kulevya.
Kama ile divai ingekuwa pombe, Yesu asingesema:
"Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wezi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi."(1Kor 6:9-10)
So dear brother/sister, don’t be fooled—Jesus never endorsed drinking alcohol.
Hicho kitabu kipo kwenye biblia ya kikatoliki ?Sira 31 : 28
Pombe ni kama uhai kwa mtu ukinywa kwa kiasi. Maisha yafaa nini bila pombe? Imeumbwa iwafurahishe watu.
Moja ya vitabu 72 vya Biblia Takatifu, Hekima ya Yoshua bin siraHicho kitabu kipo kwenye biblia ya kikatoliki ?
Kitabu cha Sira hakikubaliki. Hakina uvuvio wa Roho Mtakatifu(not divinely inspired). Wanaokitumia ni wale tu walioko msibani sasa - ameondoka Mkuu wao😢Sira 31 : 28
Kunywa pombe wakati wake na kwa kiasi,
kwaleta shangwe moyoni na furaha rohoni.
Sema biblia ya wakatoliki..Moja ya vitabu 72 vya Biblia Takatifu, Hekima ya Yoshua bin sira
Madhehebu ya Kiprotestanti, yanatambua vitabu 66 tu, ndivyo vilivyoandikwa kwa uongozi wa Roho Mtakatifu. Vitabu 66 ndivyo vinavyokubalika kama Maandiko Matakatifu ya kweli(Biblia). Hicho cha Sira ni cha wapiga tungi tu.Moja ya vitabu 72 vya Biblia Takatifu, Hekima ya Yoshua bin sira
Akili yako iko sawa kweli? Biblia ina vitabu 72 vilivyoandikwa, kuchambuliwa kwa umakini na Kanisa, Wewe ni nani uje uchambue hiki kinafaa kile hakifai wakati hata hivyo unavyoona vinafaa pia umepewa na Kanisa?Kitabu cha Sira hakikubaliki. Hakina uvuvio wa Roho Mtakatifu(not divinely inspired). Wanaokitumia ni wale tu walioko msibani sasa - ameondoka Mkuu wao😢
Biblia Takatifu ya Kikristu iliyokamilika na vitabu 72.Sema biblia ya wakatoliki..
Biblia ya Warumi hiyo..Biblia Takatifu ya Kikristu iliyokamilika na vitabu 72.
Protestant no mtoto wa Catholic, Hajui wala haelewi hiyo Biblia iliandaliwaje, Halafu mnakuja kuchambua vitabu vyenu 66 mnavyoona vinawafaa 😀😀 haujasoma Sylabus nzima alafu unasema upo konki, Uko serious unataka kwenda mbinguni kweli??Madhehebu ya Kiprotestanti, yanatambua vitabu 66 tu, ndivyo vilivyoandikwa kwa uongozi wa Roho Mtakatifu. Vitabu 66 ndivyo vinavyokubalika kama Maandiko Matakatifu ya kweli(Biblia). Hicho cha Sira ni cha wapiga tungi tu.
Biblia ya Kikristu, Nyie mnayo nyingine mpya mliyoandika?Biblia ya Warumi hiyo..
Warumi waliutumia Ukristo kujieneza duniani na kutanua himaya yao tu...Biblia ya Kikristu, Nyie mnayo nyingine mpya mliyoandika?
Umemaliza yote. Hawa watu sijui wakoje. Na watakuja na excuse kwenye hiloMathayo 11v18-19 Maana Yohama alikuja hali wala hanywi wakasema ana pepo
Mwana wa Adamu alikuja akila na kunywa wakasema mlafi huyu na mlevi .........
Luka 7v34 Mwana wa Adamu amekuja,anakula na kunywa nanyi mwasema ,Tazama mlafi huyu na mnywaji wa divai ,rafiki wao watoza ushuru na wenye dhambi ......
Sikia hii
Mathayo 15v16-17 Yesu akasema hata sasa ninyi nanyi mngali hamna akili ?Hamjafahamu bado ya kuwa kila kiingiacho kuinyani hupita tumboni kikatupwa chooni?
Marko 7v14-15 Akawait makutano tena, akawaambia, Nisikieni nyote na kufahamu .Hakuna kitu kilicho nje ya mtu kikimwingia chaweza kumtia unajisi(kumfanya kuwa na dhambi ),bali vile vimtokavyo .......
Siyo kwamba natetea pombe,ila kunywa pombe siyo dhambi
na usimtetee Yesu ,
Yesu alitamka tu na maji yakaw pombe