mike2k
JF-Expert Member
- May 12, 2016
- 1,571
- 3,448
LEO Rais Samia Suluhu Hassan, atakuwa mgeni rasmi katika tukio la kujaza maji kwenye Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere (JNHPP). Hatua muhimu kwenda kuzalisha umeme.
JNHPP itakuwa na uwezo wa kufua umeme megawati 2,100 na kuuingiza gridi ya taifa kila siku. Hatua kubwa kuelekea nchi kujitosheleza katika nishati ya umeme.
Kukamilika kwa JNHPP bila shaka utakuwa mwanzo wa kupotea kwa hisia na maneno kuwa mradi huo ulikuwa unahujumiwa usifike mwisho. Muda ni tiba thabiti.
Pamoja na kipengele hicho chanya, upo ukweli ambao si Rais Samia Suluhu Hassan wala Waziri wa Nishati, January Makamba, wanaweza kuusema.
Kwamba JNHPP ni mradi ambao hawakuwa na namna zaidi ya kuukamilisha kwa sababu waliukuta umeshakaribia nusu na tayari ulishateketeza fedha nyingi za Watanzania.
Ukweli ni kuwa mradi wa JNHPP ulikuwa uamuzi wa hovyo kuwahi kutokea. Kwanza unakuja na athari kubwa ya kimazingira. Ushauri wa wataalamu ulipuuzwa. Mradi ukajengwa kwa kulazimisha.
Karibu miti milioni tatu imekatwa. Eneo la msitu la kilometa za mraba 1,500 limeharibiwa (deforestation).
Yaani, Serikali iliamua kujenga mradi wa umeme wa maji kwa kuharibu vyanzo vya maji.
Hivi sasa kuna mabadiliko ya tabia nchi. Mvua hazinyeshi. Mto Rufiji umekuwa mkavu. Je, sio athari za kuharibu msitu wa Selous.
Mtangulizi wa Rais Samia, Dk John Magufuli, alipoingia madarakani, alikuta mradi mkubwa wa gesi Mtwara. Nchi ilikuwa ina tabasamu kuelekea uchumi wa gesi.
Fedha zaidi ya Sh11 trilioni zilizotumika kujenga JNHPP, nusu yake tu ungewekezwa kwenye gesi Mtwara, sasa hivi nchi ingekuwa na umeme wa gesi, nishati ya kupikia ya gesi na kufanya mauzo ya gesi nje ya nchi. Tungeepuka janga la vita ya Ukraine na Urusi.
Umeme wa gesi ndio wa kisasa. Umeme wa maji sio wa uhakika. Ndio maana mara kwa mara nchi ikitetereka kidogo kupata mvua, umeme unakuwa shida.
Changamoto ya umeme wa maji na kukauka kwa mabwawa ya kuzalishia umeme ndio matokeo ya nchi kuingia mikataba ya hovyo ya IPTL na Richmond kwa sababu ya uhitaji wa umeme wa dharura.
Pamoja na kutambua hayo, bado Serikali ya Magufuli ikafanya uamuzi wa kujenga mradi wa umeme wa maji.
Maswali ni mengi mno, unawezaje kujenga mradi wa umeme wa maji katika nchi ambayo tayari ina gesi ya kutosha?
Kuutelekeza mradi wa gesi Mtwara, ilikuwa kumkomoa nani? Hii hulka ya Rais akiingia madarakani anatelekeza miradi ya mtangulizi wake inaumiza mno wananchi.
Ingekuwaje Rais Samia angeamua kutoendelea na JNHPP? Fedha za Watanzania zingetolewa maelezo gani? Yatolewe maelezo ya kutelekezwa gesi Mtwara na miradi mingine yote ambayo ipo njiani miaka saba sasa.
Mwisho tuhoji; miti milioni tatu iliyokatwa Msitu wa Selous kupisha mradi wa JNHPP, ilipelekwa wapi? Iliuzwa? Fedha ilikwenda wapi? Uchunguzi maalum unahitajika katika hili.
Kuna harufu kubwa ya ufisadi wa miti milioni tatu iliyokatwa Selous.
Ndimi Luqman MALOTO