Ukweli unaoogopwa kusemwa kuhusu bwawa la umeme la Nyerere

Ukweli unaoogopwa kusemwa kuhusu bwawa la umeme la Nyerere

Ni Trilioni 11
Acha uongo. Imepanda lini?
Screenshot_20221222-094057.png
 
Kiufupi ni kwamba huko ulaya walisha haribu mazingira sana na bado wanaendelea kuharibu kupiti mioshi ya viwandani. Lakini Africa ikitaka kufanya jambo la maendeleo utasikia wana harakati wanapinga sababu wanajua mradi ukikamilika kwa namna flani tutapunguza utegemezi. Bomba la mafuta wanapinga lakini waulize bomba la mafuta kutoka Urusi kwenye Germany pamoja na kupita baharini eneo flani lakini limepita pia aridhini hilo hawakumbuki. Waulize kuhusu miradi mikubwa ya nyukria inafanyikaje?. Kama inafanyika bila kukata miti sawa itakua ni huko angani.

Siku ukijua kwa nini wanasema kuoa wanawake wengi ni vibaya lakini mwanaume kuolewa na mwanaume mwenzake ni haki za binadamu basi utaelewa hii post.

Tuache kushikiwa akili. Ndio maana hata neno 'democracy' inatakiwa tulitafsiri kiafrica sio kimagharibi. Sio kila kitu kinachofanya kazi Europe kinaweza kufanya kazi africa pia.

Tumevunja utaratibu wetu wa zamani wa chiefdom tukaanz akufuata sijui ndio democracy kwamba tunachagua viongozi lakini wao hapo uingereza tu wana endelea na utaratibu wao wa kuwa na mfalme au malkia.

Kuna watu wanajfanya wanaharakati kwa kua wanapata vihela vya NGOs kutoka nje ndio wanaleta agenda zao z kijinga humu.

Kila siku mikutano ya kulinda mazingira haipati suluhisho sababu wakiacha kuzalisha viwandani uchumi wao utashuka sana. Sasa ikiwa wao wanaharibu mazingira kwa 78 Africa kwa asilimia 8 nani anatakiwa kuangaliwa zaidi
1. Sio kweli kwamba wanapinga miradi ya Afrika tu wanaharakati wa climate change kina Greta Thurnberg ni mara ngapi wanafanya maandamano kupinga carbon emissions za mashirika makubwa? Mara ngapi wanafanya glue mikono Yao maeneo kadhaa Kama protests? So miradi yote ya fossil fuels inapingwa na wanaharakati duniani. Hata Messi tu alitolewa povu alipotumia ndege badala ya Basi kusafirisha familia yake!!

2. Demokrasia Ina misingi 11 embu niambie msingi hata mmoja ambao haufai kutumika Afrika. Tulikua tunatumia u chief lakini ulitusaidia Nini? Rwanda na Uganda Zina machief umeona ukabila uliopo? Demokrasia ndio imeleta uwajibikaji kwamba mafisadi yanaogopa mahakama, uchaguzi, bunge, ukaguzi n.k. when practiced to its fullness.
 
LEO Rais Samia Suluhu Hassan, atakuwa mgeni rasmi katika tukio la kujaza maji kwenye Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere (JNHPP). Hatua muhimu kwenda kuzalisha umeme.

JNHPP itakuwa na uwezo wa kufua umeme megawati 2,100 na kuuingiza gridi ya taifa kila siku. Hatua kubwa kuelekea nchi kujitosheleza katika nishati ya umeme.

Kukamilika kwa JNHPP bila shaka utakuwa mwanzo wa kupotea kwa hisia na maneno kuwa mradi huo ulikuwa unahujumiwa usifike mwisho. Muda ni tiba thabiti.

Pamoja na kipengele hicho chanya, upo ukweli ambao si Rais Samia Suluhu Hassan wala Waziri wa Nishati, January Makamba, wanaweza kuusema.

Kwamba JNHPP ni mradi ambao hawakuwa na namna zaidi ya kuukamilisha kwa sababu waliukuta umeshakaribia nusu na tayari ulishateketeza fedha nyingi za Watanzania.

Ukweli ni kuwa mradi wa JNHPP ulikuwa uamuzi wa hovyo kuwahi kutokea. Kwanza unakuja na athari kubwa ya kimazingira. Ushauri wa wataalamu ulipuuzwa. Mradi ukajengwa kwa kulazimisha.

Karibu miti milioni tatu imekatwa. Eneo la msitu la kilometa za mraba 1,500 limeharibiwa (deforestation).

Yaani, Serikali iliamua kujenga mradi wa umeme wa maji kwa kuharibu vyanzo vya maji.

Hivi sasa kuna mabadiliko ya tabia nchi. Mvua hazinyeshi. Mto Rufiji umekuwa mkavu. Je, sio athari za kuharibu msitu wa Selous.

Mtangulizi wa Rais Samia, Dk John Magufuli, alipoingia madarakani, alikuta mradi mkubwa wa gesi Mtwara. Nchi ilikuwa ina tabasamu kuelekea uchumi wa gesi.

Fedha zaidi ya Sh11 trilioni zilizotumika kujenga JNHPP, nusu yake tu ungewekezwa kwenye gesi Mtwara, sasa hivi nchi ingekuwa na umeme wa gesi, nishati ya kupikia ya gesi na kufanya mauzo ya gesi nje ya nchi. Tungeepuka janga la vita ya Ukraine na Urusi.

Umeme wa gesi ndio wa kisasa. Umeme wa maji sio wa uhakika. Ndio maana mara kwa mara nchi ikitetereka kidogo kupata mvua, umeme unakuwa shida.

Changamoto ya umeme wa maji na kukauka kwa mabwawa ya kuzalishia umeme ndio matokeo ya nchi kuingia mikataba ya hovyo ya IPTL na Richmond kwa sababu ya uhitaji wa umeme wa dharura.

Pamoja na kutambua hayo, bado Serikali ya Magufuli ikafanya uamuzi wa kujenga mradi wa umeme wa maji.

Maswali ni mengi mno, unawezaje kujenga mradi wa umeme wa maji katika nchi ambayo tayari ina gesi ya kutosha?

Kuutelekeza mradi wa gesi Mtwara, ilikuwa kumkomoa nani? Hii hulka ya Rais akiingia madarakani anatelekeza miradi ya mtangulizi wake inaumiza mno wananchi.

Ingekuwaje Rais Samia angeamua kutoendelea na JNHPP? Fedha za Watanzania zingetolewa maelezo gani? Yatolewe maelezo ya kutelekezwa gesi Mtwara na miradi mingine yote ambayo ipo njiani miaka saba sasa.

Mwisho tuhoji; miti milioni tatu iliyokatwa Msitu wa Selous kupisha mradi wa JNHPP, ilipelekwa wapi? Iliuzwa? Fedha ilikwenda wapi? Uchunguzi maalum unahitajika katika hili.

Kuna harufu kubwa ya ufisadi wa miti milioni tatu iliyokatwa Selous.

Ndimi Luqman MALOTO
View attachment 2454151View attachment 2454152

Unataka kunambia serikali mzima na viongozi wote ni vipofu wasione ulichokiona ww?

Sometimes tunatakiwa kuheshim maamuzi ya viongozi wetu, ndio maana wakawa viongozi

Maybe hata ww ungekuwa kwenye nafasi ya uongozi wa juu ungetumia zaidi ya hizo trion 11

Ishu ya miti au misitu, unataka kunambia ni msitu wa rufiji Tu ndio ulikuwa unaleta mvua?

Misitu mingapi ipo Tanzania?

Hapo kwenye swala la Gesi kuna sarakasi nyingi Sana ambazo watu wengi hawajui
 
Mbona Sasa mnalialia.

Gesi Ile ni mradi wa watu Wala sio watanzania. Gasi yenyewe Bei juu .. hakuna hata faida.

Siku tukipata tena mtu wa aina ya JPM tutafaida sana.

Hawa msoga wao ni watu wa deal tu.

Una uhakika gani umeme wa maji hautakuwa bei juu? Unajua terms za mkopo wa ujenzi wa hilo bwawa? Mbona ndege ni zetu, lakini nauli ni bei gali kulinganisha na fastjet? Acheni utapeli wa kijinga.
 
Una uhakika gani umeme wa maji hautakuwa bei juu? Unajua terms za mkopo wa ujenzi wa hilo bwawa? Mbona ndege ni zetu, lakini nauli ni bei gali kulinganisha na fastjet? Acheni utapeli wa kijinga.
Wivu tu ..

Mimba ya Mwendazake kiboko
 
Kwani umeme wa Gas Principle ni ipi? Si kuchemsha maji? Sasa kama hamna maji ya kuchemsha si sawa tu kukosa maji kwa ukame? Ile mitungi mirefu inawekwa nini?

Hydro haihitaji mitungi na kuchemsha maji, inahitaji "gravity" tu kuziendesha Turbines na umeme unawake, kipi gharama rahisi kati ya hivi viwili?

Mto au bwawa la Maji => Gravity = Turbines au
Gasi = mitungi ya maji kuchemsha mvuke halafu ukapige turbines na coolers vile vile!

Shule nzuri
Mkuu naona unachanganya kati ya steam power plant na gas power plant.
Kwenye gas power plant, gas inaunguzwa na kwenda moja kwa moja kuendesha turbine. Ni kama turbo charger inavyofanya kazi kwenye magari.

Ila steam power plant ndio ulivyoelezea hapo maji yanachemshwa kwa fuel yeyote either kwa makaa ya mawe, kuni, Uranium, mabaki ya miwa especially kwenye viwanda sukari etc.
 
1: Maji yatakauka ? Duh sasa yakikauka si tutakufa kabisa hata kabla ya kukosa giza ?

2: Ukame utakuja maji hayana uhakika gesi ndio uhakika ? ; Kwamba hio gesi ndio haitaisha ?

3: Tungekuwa na gesi mpaka ya kupikia ?; Hio gesi ingekuwa bei gani production cost na tunanunua kwa kiasi gasi ili tuuziwe kwa kiasi gani? Na hizo infrastructure za pipes mpaka majumbani kwa watu kule milimani ni kiasi gani and is it even feasible let alone doable ?

4: Sipingi energy mix ila hili Bwawa ndio the centre ya mambo yote na likitumika vizuri linaweza likatutoa hapa na kutupeleka pale....

Acha kumvisha maneno mama ambayo yeye hana,naona mlisubiri mradi ukwame mpate cha kusema ,sasa mradi unasonga mbele unakuja na brah brah mama hautaki ,ohh waziri hautaki.

Urais ni taasisi kama mama asingekuwa anautaka huu mradi basi taasisi ya urais ingemwambia.

Acheni kumlisha hisia na maneno rais wetu
 
Miradi mingi ya pesa nyingi Tanzani imejaa usiri na kwa vile Wananchi wetu ni matahira basi hakuna chochote cha ukweli tunaweza kufahamu zaidi ya hadaa za majukwaani za Wanasiasa na Rais.

Labda vizazi vyetu vikakuja kuhoji na kufanya maamuzi kwa sasa sisi tutulie tu tupelekeshwe na familia za Wanajeshi wastaafu za Kikwete,Makamba,Nnauye & Kinana.
 
Kiufupi ni kwamba huko ulaya walisha haribu mazingira sana na bado wanaendelea kuharibu kupiti mioshi ya viwandani. Lakini Africa ikitaka kufanya jambo la maendeleo utasikia wana harakati wanapinga sababu wanajua mradi ukikamilika kwa namna flani tutapunguza utegemezi. Bomba la mafuta wanapinga lakini waulize bomba la mafuta kutoka Urusi kwenye Germany pamoja na kupita baharini eneo flani lakini limepita pia aridhini hilo hawakumbuki. Waulize kuhusu miradi mikubwa ya nyukria inafanyikaje?. Kama inafanyika bila kukata miti sawa itakua ni huko angani.

Siku ukijua kwa nini wanasema kuoa wanawake wengi ni vibaya lakini mwanaume kuolewa na mwanaume mwenzake ni haki za binadamu basi utaelewa hii post.

Tuache kushikiwa akili. Ndio maana hata neno 'democracy' inatakiwa tulitafsiri kiafrica sio kimagharibi. Sio kila kitu kinachofanya kazi Europe kinaweza kufanya kazi africa pia.

Tumevunja utaratibu wetu wa zamani wa chiefdom tukaanz akufuata sijui ndio democracy kwamba tunachagua viongozi lakini wao hapo uingereza tu wana endelea na utaratibu wao wa kuwa na mfalme au malkia.

Kuna watu wanajfanya wanaharakati kwa kua wanapata vihela vya NGOs kutoka nje ndio wanaleta agenda zao z kijinga humu.

Kila siku mikutano ya kulinda mazingira haipati suluhisho sababu wakiacha kuzalisha viwandani uchumi wao utashuka sana. Sasa ikiwa wao wanaharibu mazingira kwa 78 Africa kwa asilimia 8 nani anatakiwa kuangaliwa zaidi
Hawa jamaa wanatuona kama sisi hatuna akili kabisa tunaishi under control yao .Mambo mengi wanayo resist yana maslahi kwao na sio kwetu.Ki ukweli wenzetu hawa ndio number mojamoja kwa uharibifu wa mazingira nje ya huu wa kukata miti.

Wameharibu mazingira mpaka wametibua Ozon layer.....najiuliza tu kwa sauti uharibifu wa ozon layer causative ingekuwa nchi za kiafrika tungepata pa kupumulia?

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Wewe bogus kaa kimya, mkaa unakatwa toka miaka ya 90 hadi leo. Lini mvua iliacha kunyesha? Una record ya miti million ngapi imekatwa toka 1991 hadi leo kwa ajili ya mkaa?
Alafu mwambie pia aende kule iringa aone mamilioni ya miti yanavyovunwa na mamilioni mengine kupandwa!

Hawa watoto wa miaka ya 90 kwa mujibu wa mama yao ni wa hovyo
 
1. Sio kweli kwamba wanapinga miradi ya Afrika tu wanaharakati wa climate change kina Greta Thurnberg ni mara ngapi wanafanya maandamano kupinga carbon emissions za mashirika makubwa? Mara ngapi wanafanya glue mikono Yao maeneo kadhaa Kama protests? So miradi yote ya fossil fuels inapingwa na wanaharakati duniani. Hata Messi tu alitolewa povu alipotumia ndege badala ya Basi kusafirisha familia yake!!

2. Demokrasia Ina misingi 11 embu niambie msingi hata mmoja ambao haufai kutumika Afrika. Tulikua tunatumia u chief lakini ulitusaidia Nini? Rwanda na Uganda Zina machief umeona ukabila uliopo? Demokrasia ndio imeleta uwajibikaji kwamba mafisadi yanaogopa mahakama, uchaguzi, bunge, ukaguzi n.k. when practiced to its fullness.
Ghana ni roli mode wenu kwenye democrasia ila anafirisika!
 
Mradi wa umeme trillions 7.
Mradi wa reli,trillions 15.
Mikopo trillions-90

Makusanyo kwa mwaka USD 67 =15 trillions

Kwenye hayo makusanyo hujalipa mishahara ya civil servant,hujapeleka fedha za maendeleo na hujalipa deni la Taifa.
 
Back
Top Bottom