Ukweli unaoogopwa kusemwa kuhusu bwawa la umeme la Nyerere

Tena hapo pa kikamilika patatokea uoto mzuri sana!
20221007_171704.jpg

Yeah patakua fresh sana
 
LEO Rais Samia Suluhu Hassan, atakuwa mgeni rasmi katika tukio la kujaza maji kwenye Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere (JNHPP). Hatua muhimu kwenda kuzalisha umeme...
ujinga ni mzigo mkubwa sana. vyanzo vya maji yale sio kule yanapokusanywa, ni mikoani huko, huko ndiko walikotakiwa kulima miti na kuhifadhi mazingira. kule stigners ni maandalizi ya kumwaga maji baharini yaende zake. hebu tueleze, ni athari gani za mazingira unazozielea ili tuone kama ni tofauti na zile zinazosemwa na wazungu wanaotaka kutuuzia gas wanayoichimba kwetu sisi wenyewe?

weka kwenye mzani, miti hiyo ikikatwa upande mmoja na megawati zaidi ya 2000 za umeme upande mwingine, wapi kuna faida zaidi kwa wananchi? ni kwamba hiyo miti kukatwa ndio kweli kumeharibu kabisa mazingira hatutasavaivu?

Au unaongelea kuharibu mazingira ya wanyama wa selous game reserve ambao ndio watapata raha zaidi kwa kuja kunywa maji pembezoni mwa ziwa, na mamba watashiba sana kwa kuwala hivyo utalii pande ile unaweza kuongezeka pia. ilikuwa ni lazima iwe usiku au mchanga bwawa lile lijengwe ili tuondokane na utumwa wa umeme. umeme ni kitu muhimu kuliko hata hiyo miti unayoipenda ambayo tunaweza kucompensate kupanda sehemu zilizobaki.

mwisho, mapimbi wengi kasori mikia wanaupinga sana huu mradi kwasababu wanataka wazungu wanaochimba gas kwetu watuuzie gas hiyo kwa garama ili wao wapate faida kwasababu wana chao huko, ili umeme wetu utegemee tu gas, ambayo haipo mikononi mwetu, kama gas ipo mikononi mwa wazungu hao ndio watatuamulia chochote watakachotaka, hata wakisema leo hii tuukubali ushoga ama la wataondoka na utaalamu wao hatuna la kufanya. tuna safari ndefu sana kuishi na watu kama wewe.
 
Sasa hapa Kuna hoja gani ya kujenga umeiweka wewe?

Ni kweli mradi huwezi kuacha kwa Sasa lakini haiondoi ukweli kwamba Mwendazake alikosea Sana na kaisababishia Nchi hasara..

Unatumia Til.11 kuzalisha megwt 2115 na kuharibu Mamilioni ya hekta za misitu na vyanzo vya maji.

Ni akili hiyo?
NaJulius Nyerere alikosea ? Muaasisi wa hili bwawa ni Julius Kambalage Nyerere.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
LEO Rais Samia Suluhu Hassan, atakuwa mgeni rasmi katika tukio la kujaza maji kwenye Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere (JNHPP). Hatua muhimu kwenda kuzalisha umeme...
Kwaio unatak kusema hilo la nusu ya 11T kumaliza mradi wa gesi #Chuma hakuliona?

Kukatwa kwa miti 3M kumesababisha ukame.Mabadiriko ya tabia ya nchi miaka ilyopita yalisababishwa na nn?

Serikali inakemea ukataji wa miti kwa matumiz ya mkaa kama chanzo kikuu cha ukame, unatak kusema hili la 3m miti kweny BWAWA LA NYERER hawajaliona?

Umeme wa maji umepitwa na wakat How,Dunia inajenga hayo mabwawa kila kukicha mfano Ethiopia na china.

Bonde la ihefu linachangia maji 3% kweny mto ruvu ajabu na lenyew limekauka, unatak kusema hio miti 3m pwani ndo inasababisha ukame mbeya?Mbona mbeya mvua zinanyesha
 
We mleta mada ni mpumbavu,kama shida ni miti milion 3 kukatwa waambie hao waliokutuma watanzania wako zaidi ya 60 milion chukua nusu ya watanzania na kila mmoja apande mti wake popote pale alipo ndani ya nchi yake.

Bwawa hatuwezi kuachana nalo kisa hiyo miti,nilitegemea muweke nguvu kubwa kwenye uhamasishaji wa upandaji wa miti kwakuwa nyie ni watunza mazingira wazuri kumbe sio [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23],
leo hii mnaulizia ile miti iliyokatwa iko wapi na kama iliuzwa hela yake iko wapi!!
mbona hamuulizii ile miti inayokatwa kwenye ujenzi wa barabara nayo inaenda wapi?
 
LEO Rais Samia Suluhu Hassan, atakuwa mgeni rasmi katika tukio la kujaza maji kwenye Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere (JNHPP). Hatua muhimu kwenda kuzalisha umeme...
Sikujua wewe ni mpumbavu kiasi hiki,baada ya kusoma komenti yako wewe ni [emoji706][emoji706][emoji706][emoji706][emoji706][emoji706][emoji706]
 
Pale Kama Zitatoka Megawatts Nyingi ni 600mw, Nani atatukagulia kwamba Bwawa lile linao uwezo wa kuproduce 2000+ mw at peak, Vipi izo Turbines ni za kuweza Kuzalisha 2000Mg?

Je kiwango cha chini kabisa cha uzalishaji ni Mw Ngapi Kwa Siku?
 
Ghana ni roli mode wenu kwenye democrasia ila anafirisika!
Faida ya demokrasia ni kwamba ukija uchaguzi hicho Chama kitaondolewa kitakuja chama kingine kuleta fikra na sera mpya ila tatizo nchi ya kidkteta mkipata kiongozi mbovu ndio mnajua miaka 40 matatizo hayo hayataisha!!

Demokrasia ipo kwa ajili ya uwajibikaji, mfano Kenya hapo zaidi ya 80% ya wabunge hawakurudi chaguzi iliyopita ikimaanisha ingekua nchi ya kidkteta yangeteuliwa tu kuongoza majimbo kwa miaka hata 50 licha ya zero output!!
 
LEO Rais Samia Suluhu Hassan, atakuwa mgeni rasmi katika tukio la kujaza maji kwenye Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere (JNHPP). Hatua muhimu kwenda kuzalisha umeme.

JNHPP itakuwa na uwezo wa kufua umeme megawati 2,100 na kuuingiza gridi ya taifa kila siku. Hatua kubwa kuelekea nchi kujitosheleza katika nishati ya umeme.

Kukamilika kwa JNHPP bila shaka utakuwa mwanzo wa kupotea kwa hisia na maneno kuwa mradi huo ulikuwa unahujumiwa usifike mwisho. Muda ni tiba thabiti.

Pamoja na kipengele hicho chanya, upo ukweli ambao si Rais Samia Suluhu Hassan wala Waziri wa Nishati, January Makamba, wanaweza kuusema.

Kwamba JNHPP ni mradi ambao hawakuwa na namna zaidi ya kuukamilisha kwa sababu waliukuta umeshakaribia nusu na tayari ulishateketeza fedha nyingi za Watanzania.

Ukweli ni kuwa mradi wa JNHPP ulikuwa uamuzi wa hovyo kuwahi kutokea. Kwanza unakuja na athari kubwa ya kimazingira. Ushauri wa wataalamu ulipuuzwa. Mradi ukajengwa kwa kulazimisha.

Karibu miti milioni tatu imekatwa. Eneo la msitu la kilometa za mraba 1,500 limeharibiwa (deforestation).

Yaani, Serikali iliamua kujenga mradi wa umeme wa maji kwa kuharibu vyanzo vya maji.

Hivi sasa kuna mabadiliko ya tabia nchi. Mvua hazinyeshi. Mto Rufiji umekuwa mkavu. Je, sio athari za kuharibu msitu wa Selous.

Mtangulizi wa Rais Samia, Dk John Magufuli, alipoingia madarakani, alikuta mradi mkubwa wa gesi Mtwara. Nchi ilikuwa ina tabasamu kuelekea uchumi wa gesi.

Fedha zaidi ya Sh11 trilioni zilizotumika kujenga JNHPP, nusu yake tu ungewekezwa kwenye gesi Mtwara, sasa hivi nchi ingekuwa na umeme wa gesi, nishati ya kupikia ya gesi na kufanya mauzo ya gesi nje ya nchi. Tungeepuka janga la vita ya Ukraine na Urusi.

Umeme wa gesi ndio wa kisasa. Umeme wa maji sio wa uhakika. Ndio maana mara kwa mara nchi ikitetereka kidogo kupata mvua, umeme unakuwa shida.

Changamoto ya umeme wa maji na kukauka kwa mabwawa ya kuzalishia umeme ndio matokeo ya nchi kuingia mikataba ya hovyo ya IPTL na Richmond kwa sababu ya uhitaji wa umeme wa dharura.

Pamoja na kutambua hayo, bado Serikali ya Magufuli ikafanya uamuzi wa kujenga mradi wa umeme wa maji.

Maswali ni mengi mno, unawezaje kujenga mradi wa umeme wa maji katika nchi ambayo tayari ina gesi ya kutosha?

Kuutelekeza mradi wa gesi Mtwara, ilikuwa kumkomoa nani? Hii hulka ya Rais akiingia madarakani anatelekeza miradi ya mtangulizi wake inaumiza mno wananchi.

Ingekuwaje Rais Samia angeamua kutoendelea na JNHPP? Fedha za Watanzania zingetolewa maelezo gani? Yatolewe maelezo ya kutelekezwa gesi Mtwara na miradi mingine yote ambayo ipo njiani miaka saba sasa.

Mwisho tuhoji; miti milioni tatu iliyokatwa Msitu wa Selous kupisha mradi wa JNHPP, ilipelekwa wapi? Iliuzwa? Fedha ilikwenda wapi? Uchunguzi maalum unahitajika katika hili.

Kuna harufu kubwa ya ufisadi wa miti milioni tatu iliyokatwa Selous.

Ndimi Luqman MALOTO
View attachment 2454151View attachment 2454152
Wewe ni Mpuuziiiiiii
 
Kuna watu humu JF wakiamua wanaongea point nzuri hadi raha!
 
The main point I have seen in your opinions ni MITI ILIYOKATWA.

Serikali ianze kampeni ya kupanda MITI Ili tufanye recovery ya MITI iliyopotea.

Ethiopians ambao Wana mradi kama huu wanasema nini?

Bandiko nyingine tunazianzisha bila kuwa na exposure.

Everything has merits and demerits for this project merits is very high.

Mtoa mada Mimi siungani na hayo mawazo yako.
 
Kwa ukubwa wa Hilo bwawa Leo ndio nimeamini waliosema miti minginimekatwa sio mchezo.

Km 100,kubwa kwa ujazo wa Maji kuliko Ziwa Rukwa
Hivi Chande kwa akili aliyonayo anaona hilo ni jambo la kujisifia? Hakupaswa hata kulisema. Ni sawa na kusifia ndugu yako alivyokufa kwa ajali wakati akiwa kwenye mashindano ya magari
 
Alafu mwambie pia aende kule iringa aone mamilioni ya miti yanavyovunwa na mamilioni mengine kupandwa!

Hawa watoto wa miaka ya 90 kwa mujibu wa mama yao ni wa hovyo
We naye unampoteza tu!! Nani kakwambia madhara ya tabianchi yanakua felt ndani ya mwaka mmoja?? Ukataji miti unaosifia siku ukijibu ni miaka hata 30 ijayo ndio utaona madhara yake.

Tukubali kwamba tumeona faida za umeme ni kubwa kuliko madhara ya ikolojia ila kupinga hakuna madhara kisa "mbona tumeshakata sana" sio logic kabisa.

Hii kitu ilimcost Mao Zedong, kasome the Great leap forward jinsi kuua "wadudu watambaao" kulileta ukame mkubwa sana china almost 50 million walikufa!! Imagine unaua mende na nzi ila anayeathirika ni binadamu tokea pale ndio nikaelewa kwanini hata majoka makubwa yakidakwa hayauawi yanarudishwa msituni. Simple answer ni Ecology!!
 
LEO Rais Samia Suluhu Hassan, atakuwa mgeni rasmi katika tukio la kujaza maji kwenye Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere (JNHPP). Hatua muhimu kwenda kuzalisha umeme.

JNHPP itakuwa na uwezo wa kufua umeme megawati 2,100 na kuuingiza gridi ya taifa kila siku. Hatua kubwa kuelekea nchi kujitosheleza katika nishati ya umeme.

Kukamilika kwa JNHPP bila shaka utakuwa mwanzo wa kupotea kwa hisia na maneno kuwa mradi huo ulikuwa unahujumiwa usifike mwisho. Muda ni tiba thabiti.

Pamoja na kipengele hicho chanya, upo ukweli ambao si Rais Samia Suluhu Hassan wala Waziri wa Nishati, January Makamba, wanaweza kuusema.

Kwamba JNHPP ni mradi ambao hawakuwa na namna zaidi ya kuukamilisha kwa sababu waliukuta umeshakaribia nusu na tayari ulishateketeza fedha nyingi za Watanzania.

Ukweli ni kuwa mradi wa JNHPP ulikuwa uamuzi wa hovyo kuwahi kutokea. Kwanza unakuja na athari kubwa ya kimazingira. Ushauri wa wataalamu ulipuuzwa. Mradi ukajengwa kwa kulazimisha.

Karibu miti milioni tatu imekatwa. Eneo la msitu la kilometa za mraba 1,500 limeharibiwa (deforestation).

Yaani, Serikali iliamua kujenga mradi wa umeme wa maji kwa kuharibu vyanzo vya maji.

Hivi sasa kuna mabadiliko ya tabia nchi. Mvua hazinyeshi. Mto Rufiji umekuwa mkavu. Je, sio athari za kuharibu msitu wa Selous.

Mtangulizi wa Rais Samia, Dk John Magufuli, alipoingia madarakani, alikuta mradi mkubwa wa gesi Mtwara. Nchi ilikuwa ina tabasamu kuelekea uchumi wa gesi.

Fedha zaidi ya Sh11 trilioni zilizotumika kujenga JNHPP, nusu yake tu ungewekezwa kwenye gesi Mtwara, sasa hivi nchi ingekuwa na umeme wa gesi, nishati ya kupikia ya gesi na kufanya mauzo ya gesi nje ya nchi. Tungeepuka janga la vita ya Ukraine na Urusi.

Umeme wa gesi ndio wa kisasa. Umeme wa maji sio wa uhakika. Ndio maana mara kwa mara nchi ikitetereka kidogo kupata mvua, umeme unakuwa shida.

Changamoto ya umeme wa maji na kukauka kwa mabwawa ya kuzalishia umeme ndio matokeo ya nchi kuingia mikataba ya hovyo ya IPTL na Richmond kwa sababu ya uhitaji wa umeme wa dharura.

Pamoja na kutambua hayo, bado Serikali ya Magufuli ikafanya uamuzi wa kujenga mradi wa umeme wa maji.

Maswali ni mengi mno, unawezaje kujenga mradi wa umeme wa maji katika nchi ambayo tayari ina gesi ya kutosha?

Kuutelekeza mradi wa gesi Mtwara, ilikuwa kumkomoa nani? Hii hulka ya Rais akiingia madarakani anatelekeza miradi ya mtangulizi wake inaumiza mno wananchi.

Ingekuwaje Rais Samia angeamua kutoendelea na JNHPP? Fedha za Watanzania zingetolewa maelezo gani? Yatolewe maelezo ya kutelekezwa gesi Mtwara na miradi mingine yote ambayo ipo njiani miaka saba sasa.

Mwisho tuhoji; miti milioni tatu iliyokatwa Msitu wa Selous kupisha mradi wa JNHPP, ilipelekwa wapi? Iliuzwa? Fedha ilikwenda wapi? Uchunguzi maalum unahitajika katika hili.

Kuna harufu kubwa ya ufisadi wa miti milioni tatu iliyokatwa Selous.

Ndimi Luqman MALOTO
View attachment 2454151View attachment 2454152
Huu ndiyo ikweli mchungu mike2k . Nina unerline maneno yako haya;
Ukweli ni kuwa mradi wa JNHPP ulikuwa uamuzi wa hovyo kuwahi kutokea. Kwanza unakuja na athari kubwa ya kimazingira. Ushauri wa wataalamu ulipuuzwa. Mradi ukajengwa kwa kulazimisha.

Sera ya ya magufuli katika kupumbaza watanzania ilikuwa ni "Give Dog a bad name and kill It". Magufuli aliponda kila alichofanya Kikwette kuwa kina harufu ya rushwa na kisha akapandikiza UHAYAWANI wake wa kukata miti zaidi ya Milioni 4 ya pori la akiba la Selous.
 
The main point I have seen in your opinions ni MITI ILIYOKATWA.

Serikali ianze kampeni ya kupanda MITI Ili tufanye recovery ya MITI iliyopotea.

Ethiopians ambao Wana mradi kama huu wanasema nini?

Bandiko nyingine tunazianzisha bila kuwa na exposure.

Everything has merits and demerits for this project merits is very high.

Mtoa mada Mimi siungani na hayo mawazo yako.
Ethiopia eneo kubwa ni jangwa sidhani wanahitaji kukata miti, walicholaumiwa ni kuwa waki divert Maji wanaweza risk watumishi wengine kwenye kilimo n.k. so na wao wanapigiwa kelele sana tu.

Tusipende kukataa madhara eti kisa Ethiopia sijui nani naye kakata miti!! Haya mazoea ndio yanasababisha Leo hii mvua hazinyeshi tunaanza lalamika.
 
Back
Top Bottom