Ukweli unaoogopwa kusemwa kuhusu bwawa la umeme la Nyerere

Ukweli unaoogopwa kusemwa kuhusu bwawa la umeme la Nyerere

Kwani umeme wa Gas Principle ni ipi? Si kuchemsha maji? Sasa kama hamna maji ya kuchemsha si sawa tu kukosa maji kwa ukame? Ile mitungi mirefu inawekwa nini...
Uzuri wa gas ni kwamba ukisha heat up maji ukapata mvuke ukaendesha turbines,ule mvuke unakuwa condensed halafu the process starts all over again,that is the water is recycled, so you need little water. Kwa hiyo power generation using gas has very efficient water usage.

With Hydropower, maji ndiyo yanayoendesha turbines, na yakishapita unahitaji mengine, so there is alot of water wastage I can say.So kwa mazingira ya sasa where they are Geo-engineering Climate for the worst, and hence Climate Change,gas ingetusaidia sana for power generation.
 
LEO Rais Samia Suluhu Hassan, atakuwa mgeni rasmi katika tukio la kujaza maji kwenye Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere (JNHPP). Hatua muhimu kwenda kuzalisha umeme....
So hapo "tunachokijua" ni kipi?
 
Badala ya kuitwa Bwawa la Nyerere liitwe Bwawa la Magufuli


Elitwege
Kwanza ilitakiwa kuitwa jina la aliyeliandika kwenye vitabu nae Ni Stiglaz ,kwa Nini kuua historia?
Screenshot_20221222-091839.png
 
Sasa hapa Kuna hoja gani ya kujenga umeiweka wewe?

Ni kweli mradi huwezi kuacha kwa Sasa lakini haiondoi ukweli kwamba Mwendazake alikosea Sana na kaisababishia Nchi hasara..

Unatumia Til.11 kuzalisha megwt 2113 na kuharibu Mamilioni ya hekta za misitu na vyanzo vya maji.

Ni akili hiyo?
Hilo bwawa utafiti wake ulifanywa tangu 1970s na report nyingine baadaye za Environmental Impact Assessment (EIA). Ni dhahiri kuna miti lazima ingekatwa. Hilo lisingeepukika.

Duniani kote mabwawa yaliyojengwa hilo lilifanyika. Muhimu ni kufanya reforestation siyo story nyingi. Huu mradi ni muhimu kwa maslahi makubwa ya nchi.

Nampongeza sana Mhe. Rais Dk. Samia kwa kasi kubwa ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati, ukiwemo wa JNHPP.🙏🙏🙏
 
KAMPENI YA KUPANDA MITI YA ASILI MILIONI TANO IANZE, GESI ILISHAINGIWA MIKATABA YA HOVYO NA MIGUMU KUVUNJWA, THATS WHY?
Kwa sasa tujibidishe tu kwenye kuponya hasa athari za kimazingira.
Kosa haliwezi rekebisha kosa.
Mkuu kuna jua la bure usisahau wenzetu wameona kuna ukame huko nje yanaset power plant kwa nini hapa kwetu hatubadiliki
 
Sasa hapa Kuna hoja gani ya kujenga umeiweka wewe?

Ni kweli mradi huwezi kuacha kwa Sasa lakini haiondoi ukweli kwamba Mwendazake alikosea Sana na kaisababishia Nchi hasara..

Unatumia Til.11 kuzalisha megwt 2113 na kuharibu Mamilioni ya hekta za misitu na vyanzo vya maji.

Ni akili hiyo?
Wewe bogus kaa kimya, mkaa unakatwa toka miaka ya 90 hadi leo. Lini mvua iliacha kunyesha? Una record ya miti million ngapi imekatwa toka 1991 hadi leo kwa ajili ya mkaa?
 
LEO Rais Samia Suluhu Hassan, atakuwa mgeni rasmi katika tukio la kujaza maji kwenye Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere (JNHPP). Hatua muhimu kwenda kuzalisha umeme....
Kiufupi ni kwamba huko ulaya walisha haribu mazingira sana na bado wanaendelea kuharibu kupiti mioshi ya viwandani.

Lakini Africa ikitaka kufanya jambo la maendeleo utasikia wana harakati wanapinga sababu wanajua mradi ukikamilika kwa namna flani tutapunguza utegemezi.

Bomba la mafuta wanapinga lakini waulize bomba la mafuta kutoka Urusi kwenye Germany pamoja na kupita baharini eneo flani lakini limepita pia aridhini hilo hawakumbuki. Waulize kuhusu miradi mikubwa ya nyukria inafanyikaje?. Kama inafanyika bila kukata miti sawa itakua ni huko angani.

Siku ukijua kwa nini wanasema kuoa wanawake wengi ni vibaya lakini mwanaume kuolewa na mwanaume mwenzake ni haki za binadamu basi utaelewa hii post.

Tuache kushikiwa akili. Ndio maana hata neno 'democracy' inatakiwa tulitafsiri kiafrica sio kimagharibi. Sio kila kitu kinachofanya kazi Europe kinaweza kufanya kazi africa pia.

Tumevunja utaratibu wetu wa zamani wa chiefdom tukaanz akufuata sijui ndio democracy kwamba tunachagua viongozi lakini wao hapo uingereza tu wana endelea na utaratibu wao wa kuwa na mfalme au malkia.

Kuna watu wanajfanya wanaharakati kwa kua wanapata vihela vya NGOs kutoka nje ndio wanaleta agenda zao z kijinga humu.

Kila siku mikutano ya kulinda mazingira haipati suluhisho sababu wakiacha kuzalisha viwandani uchumi wao utashuka sana. Sasa ikiwa wao wanaharibu mazingira kwa 78 Africa kwa asilimia 8 nani anatakiwa kuangaliwa zaidi
 
Nilimpinga JPM mambo mengi ila kuna jambo moja ambalo nilikubaliana naye 100%! Ni ujenzi wa hilo Bwawa, alifanya maamuzi sahihi 100%

Hizo km za mraba 1500 ni sehemu ndogo sana kulinganisha na misitu tuliyo nayo. Ukiona watu wanapinga ujenzi wa hilo Bwawa ni kwa maslahi yao wenyewe. Wanajua kabisa umeme wao wa magenerator hawatauza tena sasa watapigia wapi hela?

Pili hiyo gas yenyewe ilishapigwa mikataba ambayo wewe mtanzania huwezi faidi chochote hapo!! Sana sana utaishia kuwafaidisha ambao wamepewa mkataba kuchimba na atakupangia bei anavyotaka yeye!! At the end umeme utauziwa juuu, gharama za uzalishaji nchini zitanenda juu, uharibifu wa uchumi utakuwa mkubwa sana

Chanzo sahihi kilikuwa ni hilo Bwawa!! Apokee kongole 👏👏huko alipo kwa hili hata kama mengi aliharibu
 
Misri lile bwawa lao la kufua umeme katika mto Nile walijenga juu ya miti?. Ghana na zimbabwe yale mabwa makubwa walijenga kwenye hewa bila kukata miti?.
Ulaya miradk mikubwa ya nyukria wanajenga hewani? Acha kushikiwa akili we dogo

Sisi hatukuwa na ulazima wa kukata miti wakati tayari tulikuwa na umeme wa gas, na bomba la gasi tayari lilikuwa hapa Dar. Mpango wa gas ilikuwa ni kuzalisha 5,000mg, kwanini tusingewekeza 3t kwenye gas kufikia hizo 2,115mg, badala yake tukaweka 11t kwenye mg chache kwa uharibifu wa mazingira?
 
Sasa hapa Kuna hoja gani ya kujenga umeiweka wewe?

Ni kweli mradi huwezi kuacha kwa Sasa lakini haiondoi ukweli kwamba Mwendazake alikosea Sana na kaisababishia Nchi hasara..

Unatumia Til.11 kuzalisha megwt 2115 na kuharibu Mamilioni ya hekta za misitu na vyanzo vya maji.

Ni akili hiyo?
Acha uongo wewe?

Til 11 ni za gesi. Bwana ni Til 6.5+. Labda kama walamba asali watakuwa wameongeza Chao.

Maana hata kwenye SGR wameshaongeza tayari.
 
Una uhakika Gas ya Mtwara ni ya Watanzania????? Una uhakika ??.


UCHINA Kila mwaka wanakata miti zaidi ya million 5, sijagusa Brazil, US ,N.k.

Hivi Sasa Wanaanzisha maujenzi ya Vinu vya Nyukilia, hii yote nikwenda kuharibu Tabaka la Ozone .

Lkn kwann wanafanya hivo?? Ni Ile wajihakikishie Energy, simply because Energy is a driving force of the economy.

Unadhan Kukosekana Kwa Mwamvua ,hapa Tanzania kumesababishwa na Kukatwa na Miti hiyo million 3???

Fanya Utafiti angalau Kwa Nchi za hapahapa Afrika ,zikizokumbwa na ukame ,je zilikata miti??.

NCHI YA ETHIOPIA, KUPITIA MRADI WAO WA "GERD"...wao walikata miti zaidi ya million 2 ,ujenzinwa bwawa lao Hilo, linawapa Ethiopia MEGAWATS ZAIDI YA 5000,, ELFU TANOOO, ELFU TANOOO.

Sasa Ethiopia Umeme wao watauuza mpaka Misri, Sudan n.k.

Tunahitaji Umeme wa uhakika ambao utaimarisha SEKTA YA UWEKEZAJI, VIWANDA, NA UCHUMI KWA UJUMLA.

Wacha kuangalia Miti, mabadiliko ya Hali ya Nchi , yamefanywa na WAZUNGU , Waafrika bado hatuna hata project Moja ambayo unaweza sema imechangia haya mabadiliko
 
Nilimpinga JPM mambo mengi ila kuna jambo moja ambalo nilikubaliana naye 100%! Ni ujenzi wa hilo Bwawa, alifanya maamuzi sahihi 100%...

Ni hatua gani wamechukuliwa waliongia mkataba wa hiyo gas mnayosema imepigwa? Mbona kila siku mnasema wapinzani wakichukua nchi wataiuza kwa wageni, inakuwaje CCM tayari wameshaiuza na bado wako madarakani?

Tunataka maelezo na hatua stahiki kuhusu waliouza gas, na sio kutuambia gas imeshauzwa kisha iwe ndio basi. Hakuna namna mtatuambua uharibifu wa mazingira ni maamuzi sahihi, wakati gas yetu ipo.
 
Eti ukame. Ukame limekuwa ni janga la kidunia karibu robo karne sasa kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani kote. Hata hapa Tz sio mara ya kwanza miaka hii miwili kutopata mvua za kutosha. Wacha kushikiwa akili kipuuzi
 
Ni hatua gani wamechukuliwa waliongia mkataba wa hiyo gas mnayosema imepigwa? Mbona kila siku mnasema wapinzani wakichukua nchi wataiuza kwa wageni, inakuwaje CCM tayari wameshaiuza na bado wako madarakani? Tunataka maelezo na hatua stahiki kuhusu waliouza gas, na sio kutuambia gas imeshauzwa kisha iwe ndio basi. Hakuna namna mtatuambua uharibifu wa mazingira ni maamuzi sahihi, wakati gas yetu ipo.
Sasa kama haijapigwa unaiona wapi wewe?
 
Back
Top Bottom