Ukweli unaoogopwa kusemwa kuhusu bwawa la umeme la Nyerere

Ethiopia eneo kubwa ni jangwa sidhani wanahitaji kukata miti, walicholaumiwa ni kuwa waki divert Maji wanaweza risk watumishi wengine kwenye kilimo n.k. so na wao wanapigiwa kelele sana tu.

Tusipende kukataa madhara eti kisa Ethiopia sijui nani naye kakata miti!! Haya mazoea ndio yanasababisha Leo hii mvua hazinyeshi tunaanza lalamika.
Madhara Yana solution, hiyo ndio point yangu.

Na faida ya hili Bwawa ni kubwa kuliko unachokiongea
 
LEO Rais Samia Suluhu Hassan, atakuwa mgeni rasmi katika tukio la kujaza maji kwenye Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere (JNHPP). Hatua muhimu kwenda kuzalisha umeme.

JNHPP itakuwa na uwezo wa kufua umeme megawati 2,100 na kuuingiza gridi ya taifa kila siku. Hatua kubwa kuelekea nchi kujitosheleza katika nishati ya umeme.

Kukamilika kwa JNHPP bila shaka utakuwa mwanzo wa kupotea kwa hisia na maneno kuwa mradi huo ulikuwa unahujumiwa usifike mwisho. Muda ni tiba thabiti.

Pamoja na kipengele hicho chanya, upo ukweli ambao si Rais Samia Suluhu Hassan wala Waziri wa Nishati, January Makamba, wanaweza kuusema.

Kwamba JNHPP ni mradi ambao hawakuwa na namna zaidi ya kuukamilisha kwa sababu waliukuta umeshakaribia nusu na tayari ulishateketeza fedha nyingi za Watanzania.

Ukweli ni kuwa mradi wa JNHPP ulikuwa uamuzi wa hovyo kuwahi kutokea. Kwanza unakuja na athari kubwa ya kimazingira. Ushauri wa wataalamu ulipuuzwa. Mradi ukajengwa kwa kulazimisha.

Karibu miti milioni tatu imekatwa. Eneo la msitu la kilometa za mraba 1,500 limeharibiwa (deforestation).

Yaani, Serikali iliamua kujenga mradi wa umeme wa maji kwa kuharibu vyanzo vya maji.

Hivi sasa kuna mabadiliko ya tabia nchi. Mvua hazinyeshi. Mto Rufiji umekuwa mkavu. Je, sio athari za kuharibu msitu wa Selous.

Mtangulizi wa Rais Samia, Dk John Magufuli, alipoingia madarakani, alikuta mradi mkubwa wa gesi Mtwara. Nchi ilikuwa ina tabasamu kuelekea uchumi wa gesi.

Fedha zaidi ya Sh11 trilioni zilizotumika kujenga JNHPP, nusu yake tu ungewekezwa kwenye gesi Mtwara, sasa hivi nchi ingekuwa na umeme wa gesi, nishati ya kupikia ya gesi na kufanya mauzo ya gesi nje ya nchi. Tungeepuka janga la vita ya Ukraine na Urusi.

Umeme wa gesi ndio wa kisasa. Umeme wa maji sio wa uhakika. Ndio maana mara kwa mara nchi ikitetereka kidogo kupata mvua, umeme unakuwa shida.

Changamoto ya umeme wa maji na kukauka kwa mabwawa ya kuzalishia umeme ndio matokeo ya nchi kuingia mikataba ya hovyo ya IPTL na Richmond kwa sababu ya uhitaji wa umeme wa dharura.

Pamoja na kutambua hayo, bado Serikali ya Magufuli ikafanya uamuzi wa kujenga mradi wa umeme wa maji.

Maswali ni mengi mno, unawezaje kujenga mradi wa umeme wa maji katika nchi ambayo tayari ina gesi ya kutosha?

Kuutelekeza mradi wa gesi Mtwara, ilikuwa kumkomoa nani? Hii hulka ya Rais akiingia madarakani anatelekeza miradi ya mtangulizi wake inaumiza mno wananchi.

Ingekuwaje Rais Samia angeamua kutoendelea na JNHPP? Fedha za Watanzania zingetolewa maelezo gani? Yatolewe maelezo ya kutelekezwa gesi Mtwara na miradi mingine yote ambayo ipo njiani miaka saba sasa.

Mwisho tuhoji; miti milioni tatu iliyokatwa Msitu wa Selous kupisha mradi wa JNHPP, ilipelekwa wapi? Iliuzwa? Fedha ilikwenda wapi? Uchunguzi maalum unahitajika katika hili.

Kuna harufu kubwa ya ufisadi wa miti milioni tatu iliyokatwa Selous.

Ndimi Luqman MALOTO
View attachment 2454151View attachment 2454152
Acha UONGO!
Eneo linalojazwa maji na miti kukatwa katika mradi halifiki 2% ya eneo lote la hifadhi ya Selous, actually ni around 1.5% kama sikosei.
KNOW YOUR FACTS!
 
Kuna program za upandaji muti zaidi ya milioni 20 kila mwaka. So inaweza kureplace haraka.

Kinachofanya mvua isinyeshe ni jambo jingine ambalo wazung hawawezi kukwambia.
Unasubiri uambiwe na wazungu kwa nini mvua hazinyeshi?. Pole sana kizazi hiki. Hata babu zetu ambao hawakua na elimu ya kisasa wasingesubiri wazungu wawaambie.

Walikuwa na njia zao za asili za kujua vyanzo vya maji viliko na kuvihifadhi. Huyo tuliyemzika Chato mwaka jana alipkuwa anakata miti zaidi ya Milioni 4 kupisha ujenzi wa bwawa la JNHEPP mlikuwa mnamshangilia.

Sasa hivi mvua hakuna mnataka wazungu ndiyo wawasemee, poor ypu
 
Mradi wa JNHPP upo ktk POINT OF NO RETURN BACK! Acheni maneno mengi yasiyojenga nchi. Serikali za CCM tangu Uhuru viongozi wanaongozwa na Dira ya nchi.

Marais wetu wote waliongoza kwa Dira ya nchi. Mhe. Rais Samia alishasema hakuna mradi wa kimkakati ulioanzishwa na mtangulizi wake utakwama.

Tuwe na hoja za kujenga nchi siyo porojo za uchonganishi kila siku zinakera sana. Jiandae kushuhudia Mhe. Rais akibonyeza kitufe.🙏🙏🙏
Mkuu umesahau kutoa hoja yako....
 
Eti ukame. Ukame limekuwa ni janga la kidunia karibu robo karne sasa kutokana na mabasiliko ya hali ya hewa duniani kote. Hata hapa Tz sio mara ya kwanza miaka hii miwili kutopata mvua za kutosha. Wacha kushikiwa akili kipuuzi
Hayo mabadiliko ndio Sasa yamesababishwa na among other factors shughuli za kibinadamu kwenye maeneo ya misitu n.k mbona simple tu au alichodanganya hapo ni Nini? Ni sawa useme UKIMWI upo dunia nzima kwa hiyo katembee na mwanamke bila Kinga? Hapo umesolve tatizo au umeongeza?

Cha kushauri tu ni kuwa miti iliyokatwa ijaziliziwe upya around the facility Wala hakuna haja ya kupingana kwa kitu kilicho wazi.
 
Unasubiri uambiwe na wazungu kwa nini mvua hazinyeshi?. Pole sana kizazi hiki. Hata babu zetu ambao hawakua na elimu ya kisasa wasingesubiri wazungu wawaambie. Walikuwa na njia zao za asili za kujua vyanzo vya maji viliko na kuvihifadhi. Huyo kichaa tuliyemzika Chato mwaka jana alipkuwa anakata miti zaidi ya Milioni 4 kupisha ujenzi wa bwawa la JNHEPP mlikuwa mnamshangilia. Sasa hivi mvua hakuna mnataka wazungu ndiyo wawasemee, poor ypu
Kwa tamaa ya pesa ulikubali kutatuliwa marinda na kichaa wa chato
 
Everything has merits and demerits for this project merits is very high.

Mtoa mada Mimi siungani na hayo mawazo yako.
Acha kuongea utafikiri ulizaliwa na Magufuli by cloning. Wewe huelewi haya mambo ya long term impacts, unachoona hapa ni suluhisho la load shedding basi unasema project has long merits.

Na kama umeelewa mada, katika case kama hii huwa tunaconsider alternative sources of power generation - natural gas was the obvious option. Na kumbuka kwamba tuna miradi ya HEP ambayo iko well below generation capacity kwa sababu za diminishing of river flow rates, ambapo hata hii Nyerere HEP itakuja kuwa impacted. The fact kwamba kuna concern kuwa hata season mbili zinaweza zisijaze Nyerere dam ni kwa kuwa kuna athari katika river flow rates nchini, kutokana na climate change, uharibifu wa catchment areas na wetlands na siltation kutokana na mashamba upstream

With gas turbines unakuwa na uwezo wa kuongeza generation capacity any time you want. Kwenye Nyerere tupo capped kweye 2100MW, na sijui kama tutafikisha hiyo generation level. Tungechukua option ya gas turbines tungeanza na units za 100MW tukiongeza taratibu hata kufika 5000MW kutokana na national power demand hata na exports kupitia grid ya Southern Africa (SAPP) na hata ya East Africa.

Choosing Nyerere dam over Mtwara gas turbines was one of the many dumb things done by Magufuli. In fact leadtime ya gas turbines is way shorter than HEP ya size ya Nyerere dam. Sasa tuna gas Mtwara lakini haitatusaidia kwa kuwa yote itauzwa nje kama LNG kwa bei ambayo wala sio sisi tutakaopanga. Then people kama Magufuli walijiona wana akili sana kuliko Watanzania wengine? Incompetent fools.
 
LEO Rais Samia Suluhu Hassan, atakuwa mgeni rasmi katika tukio la kujaza maji kwenye Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere (JNHPP). Hatua muhimu kwenda kuzalisha umeme.

JNHPP itakuwa na uwezo wa kufua umeme megawati 2,100 na kuuingiza gridi ya taifa kila siku. Hatua kubwa kuelekea nchi kujitosheleza katika nishati ya umeme.

Kukamilika kwa JNHPP bila shaka utakuwa mwanzo wa kupotea kwa hisia na maneno kuwa mradi huo ulikuwa unahujumiwa usifike mwisho. Muda ni tiba thabiti.

Pamoja na kipengele hicho chanya, upo ukweli ambao si Rais Samia Suluhu Hassan wala Waziri wa Nishati, January Makamba, wanaweza kuusema.

Kwamba JNHPP ni mradi ambao hawakuwa na namna zaidi ya kuukamilisha kwa sababu waliukuta umeshakaribia nusu na tayari ulishateketeza fedha nyingi za Watanzania.

Ukweli ni kuwa mradi wa JNHPP ulikuwa uamuzi wa hovyo kuwahi kutokea. Kwanza unakuja na athari kubwa ya kimazingira. Ushauri wa wataalamu ulipuuzwa. Mradi ukajengwa kwa kulazimisha.

Karibu miti milioni tatu imekatwa. Eneo la msitu la kilometa za mraba 1,500 limeharibiwa (deforestation).

Yaani, Serikali iliamua kujenga mradi wa umeme wa maji kwa kuharibu vyanzo vya maji.

Hivi sasa kuna mabadiliko ya tabia nchi. Mvua hazinyeshi. Mto Rufiji umekuwa mkavu. Je, sio athari za kuharibu msitu wa Selous.

Mtangulizi wa Rais Samia, Dk John Magufuli, alipoingia madarakani, alikuta mradi mkubwa wa gesi Mtwara. Nchi ilikuwa ina tabasamu kuelekea uchumi wa gesi.

Fedha zaidi ya Sh11 trilioni zilizotumika kujenga JNHPP, nusu yake tu ungewekezwa kwenye gesi Mtwara, sasa hivi nchi ingekuwa na umeme wa gesi, nishati ya kupikia ya gesi na kufanya mauzo ya gesi nje ya nchi. Tungeepuka janga la vita ya Ukraine na Urusi.

Umeme wa gesi ndio wa kisasa. Umeme wa maji sio wa uhakika. Ndio maana mara kwa mara nchi ikitetereka kidogo kupata mvua, umeme unakuwa shida.

Changamoto ya umeme wa maji na kukauka kwa mabwawa ya kuzalishia umeme ndio matokeo ya nchi kuingia mikataba ya hovyo ya IPTL na Richmond kwa sababu ya uhitaji wa umeme wa dharura.

Pamoja na kutambua hayo, bado Serikali ya Magufuli ikafanya uamuzi wa kujenga mradi wa umeme wa maji.

Maswali ni mengi mno, unawezaje kujenga mradi wa umeme wa maji katika nchi ambayo tayari ina gesi ya kutosha?

Kuutelekeza mradi wa gesi Mtwara, ilikuwa kumkomoa nani? Hii hulka ya Rais akiingia madarakani anatelekeza miradi ya mtangulizi wake inaumiza mno wananchi.

Ingekuwaje Rais Samia angeamua kutoendelea na JNHPP? Fedha za Watanzania zingetolewa maelezo gani? Yatolewe maelezo ya kutelekezwa gesi Mtwara na miradi mingine yote ambayo ipo njiani miaka saba sasa.

Mwisho tuhoji; miti milioni tatu iliyokatwa Msitu wa Selous kupisha mradi wa JNHPP, ilipelekwa wapi? Iliuzwa? Fedha ilikwenda wapi? Uchunguzi maalum unahitajika katika hili.

Kuna harufu kubwa ya ufisadi wa miti milioni tatu iliyokatwa Selous.

Ndimi Luqman MALOTO
View attachment 2454151View attachment 2454152
nilidhnai nitasoma kitu kipya ambacho hakijawahi kusemwa
 
ujinga ni mzigo mkubwa sana. vyanzo vya maji yale sio kule yanapokusanywa, ni mikoani huko, huko ndiko walikotakiwa kulima miti na kuhifadhi mazingira. kule stigners ni maandalizi ya kumwaga maji baharini yaende zake. hebu tueleze, ni athari gani za mazingira unazozielea ili tuone kama ni tofauti na zile zinazosemwa na wazungu wanaotaka kutuuzia gas wanayoichimba kwetu sisi wenyewe?

weka kwenye mzani, miti hiyo ikikatwa upande mmoja na megawati zaidi ya 2000 za umeme upande mwingine, wapi kuna faida zaidi kwa wananchi? ni kwamba hiyo miti kukatwa ndio kweli kumeharibu kabisa mazingira hatutasavaivu?

Au unaongelea kuharibu mazingira ya wanyama wa selous game reserve ambao ndio watapata raha zaidi kwa kuja kunywa maji pembezoni mwa ziwa, na mamba watashiba sana kwa kuwala hivyo utalii pande ile unaweza kuongezeka pia. ilikuwa ni lazima iwe usiku au mchanga bwawa lile lijengwe ili tuondokane na utumwa wa umeme. umeme ni kitu muhimu kuliko hata hiyo miti unayoipenda ambayo tunaweza kucompensate kupanda sehemu zilizobaki.

mwisho, mapimbi wengi kasori mikia wanaupinga sana huu mradi kwasababu wanataka wazungu wanaochimba gas kwetu watuuzie gas hiyo kwa garama ili wao wapate faida kwasababu wana chao huko, ili umeme wetu utegemee tu gas, ambayo haipo mikononi mwetu, kama gas ipo mikononi mwa wazungu hao ndio watatuamulia chochote watakachotaka, hata wakisema leo hii tuukubali ushoga ama la wataondoka na utaalamu wao hatuna la kufanya. tuna safari ndefu sana kuishi na watu kama wewe.
Mkuu, unawezaje kumudu lundo hilo la chuki?
 
LEO Rais Samia Suluhu Hassan, atakuwa mgeni rasmi katika tukio la kujaza maji kwenye Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere (JNHPP). Hatua muhimu kwenda kuzalisha umeme.

JNHPP itakuwa na uwezo wa kufua umeme megawati 2,100 na kuuingiza gridi ya taifa kila siku. Hatua kubwa kuelekea nchi kujitosheleza katika nishati ya umeme.

Kukamilika kwa JNHPP bila shaka utakuwa mwanzo wa kupotea kwa hisia na maneno kuwa mradi huo ulikuwa unahujumiwa usifike mwisho. Muda ni tiba thabiti.

Pamoja na kipengele hicho chanya, upo ukweli ambao si Rais Samia Suluhu Hassan wala Waziri wa Nishati, January Makamba, wanaweza kuusema.

Kwamba JNHPP ni mradi ambao hawakuwa na namna zaidi ya kuukamilisha kwa sababu waliukuta umeshakaribia nusu na tayari ulishateketeza fedha nyingi za Watanzania.

Ukweli ni kuwa mradi wa JNHPP ulikuwa uamuzi wa hovyo kuwahi kutokea. Kwanza unakuja na athari kubwa ya kimazingira. Ushauri wa wataalamu ulipuuzwa. Mradi ukajengwa kwa kulazimisha.

Karibu miti milioni tatu imekatwa. Eneo la msitu la kilometa za mraba 1,500 limeharibiwa (deforestation).

Yaani, Serikali iliamua kujenga mradi wa umeme wa maji kwa kuharibu vyanzo vya maji.

Hivi sasa kuna mabadiliko ya tabia nchi. Mvua hazinyeshi. Mto Rufiji umekuwa mkavu. Je, sio athari za kuharibu msitu wa Selous.

Mtangulizi wa Rais Samia, Dk John Magufuli, alipoingia madarakani, alikuta mradi mkubwa wa gesi Mtwara. Nchi ilikuwa ina tabasamu kuelekea uchumi wa gesi.

Fedha zaidi ya Sh11 trilioni zilizotumika kujenga JNHPP, nusu yake tu ungewekezwa kwenye gesi Mtwara, sasa hivi nchi ingekuwa na umeme wa gesi, nishati ya kupikia ya gesi na kufanya mauzo ya gesi nje ya nchi. Tungeepuka janga la vita ya Ukraine na Urusi.

Umeme wa gesi ndio wa kisasa. Umeme wa maji sio wa uhakika. Ndio maana mara kwa mara nchi ikitetereka kidogo kupata mvua, umeme unakuwa shida.

Changamoto ya umeme wa maji na kukauka kwa mabwawa ya kuzalishia umeme ndio matokeo ya nchi kuingia mikataba ya hovyo ya IPTL na Richmond kwa sababu ya uhitaji wa umeme wa dharura.

Pamoja na kutambua hayo, bado Serikali ya Magufuli ikafanya uamuzi wa kujenga mradi wa umeme wa maji.

Maswali ni mengi mno, unawezaje kujenga mradi wa umeme wa maji katika nchi ambayo tayari ina gesi ya kutosha?

Kuutelekeza mradi wa gesi Mtwara, ilikuwa kumkomoa nani? Hii hulka ya Rais akiingia madarakani anatelekeza miradi ya mtangulizi wake inaumiza mno wananchi.

Ingekuwaje Rais Samia angeamua kutoendelea na JNHPP? Fedha za Watanzania zingetolewa maelezo gani? Yatolewe maelezo ya kutelekezwa gesi Mtwara na miradi mingine yote ambayo ipo njiani miaka saba sasa.

Mwisho tuhoji; miti milioni tatu iliyokatwa Msitu wa Selous kupisha mradi wa JNHPP, ilipelekwa wapi? Iliuzwa? Fedha ilikwenda wapi? Uchunguzi maalum unahitajika katika hili.

Kuna harufu kubwa ya ufisadi wa miti milioni tatu iliyokatwa Selous.

Ndimi Luqman MALOTO
View attachment 2454151View attachment 2454152
Naona baadhi yetu tuna tatizo la uelewa hafifu hasa kwa kutotembelea nchi za wengine kujifunza. Nenda Dubai tu ,kuna majengo hadi hayakaliwi kwa ajili ya utalii. Kila mradi humu,wapingaji husema gharama,gharama ,gharama.

Maoni yangu,Tuzalishe umeme wa maji, tuzalishe umeme wa gesi, tukiweza tuzalishe wa makaa ya mawe, ziada ya mahitaji ,tutawauzia majirani
 
Binadamu wanaishi hadi jangwani ambako huwezi kuwa na umeme wa maji.
WEKENI ANALYSISI ZA KITAALAMU TUONE HAPA..KAMA MAJI YAKIKOSA HATA BINADAMU WATAKUFA
 
Hiyo miti kama inawauma watuamia Watanzania tuipande ndani ya siku moja tu! Kila miti 200 kila mkoa kwisha! Unahofia miti utafikiri inaumbwa wakati ni ya kupanda tu.
Kama swala ni upatikanaji wa hewa safi. Bahari ipo na ndio inatoa 80% ya oksijeni tunayovuta.

Umetoa wazo zuri sana mkuu. Tupande miti kufidia iliyokatwa problem solved.
 
Misri lile bwawa lao la kufua umeme katika mto Nile walijenga juu ya miti?. Ghana na zimbabwe yale mabwa makubwa walijenga kwenye hewa bila kukata miti?

Ulaya miradk mikubwa ya nyukria wanajenga hewani? Acha kushikiwa akili we dogo
Nadhani Wewe ndiye umeshikiwa akili
 
LEO Rais Samia Suluhu Hassan, atakuwa mgeni rasmi katika tukio la kujaza maji kwenye Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere (JNHPP). Hatua muhimu kwenda kuzalisha umeme.

JNHPP itakuwa na uwezo wa kufua umeme megawati 2,100 na kuuingiza gridi ya taifa kila siku. Hatua kubwa kuelekea nchi kujitosheleza katika nishati ya umeme.

Kukamilika kwa JNHPP bila shaka utakuwa mwanzo wa kupotea kwa hisia na maneno kuwa mradi huo ulikuwa unahujumiwa usifike mwisho. Muda ni tiba thabiti.

Pamoja na kipengele hicho chanya, upo ukweli ambao si Rais Samia Suluhu Hassan wala Waziri wa Nishati, January Makamba, wanaweza kuusema.

Kwamba JNHPP ni mradi ambao hawakuwa na namna zaidi ya kuukamilisha kwa sababu waliukuta umeshakaribia nusu na tayari ulishateketeza fedha nyingi za Watanzania.

Ukweli ni kuwa mradi wa JNHPP ulikuwa uamuzi wa hovyo kuwahi kutokea. Kwanza unakuja na athari kubwa ya kimazingira. Ushauri wa wataalamu ulipuuzwa. Mradi ukajengwa kwa kulazimisha.

Karibu miti milioni tatu imekatwa. Eneo la msitu la kilometa za mraba 1,500 limeharibiwa (deforestation).

Yaani, Serikali iliamua kujenga mradi wa umeme wa maji kwa kuharibu vyanzo vya maji.

Hivi sasa kuna mabadiliko ya tabia nchi. Mvua hazinyeshi. Mto Rufiji umekuwa mkavu. Je, sio athari za kuharibu msitu wa Selous.

Mtangulizi wa Rais Samia, Dk John Magufuli, alipoingia madarakani, alikuta mradi mkubwa wa gesi Mtwara. Nchi ilikuwa ina tabasamu kuelekea uchumi wa gesi.

Fedha zaidi ya Sh11 trilioni zilizotumika kujenga JNHPP, nusu yake tu ungewekezwa kwenye gesi Mtwara, sasa hivi nchi ingekuwa na umeme wa gesi, nishati ya kupikia ya gesi na kufanya mauzo ya gesi nje ya nchi. Tungeepuka janga la vita ya Ukraine na Urusi.

Umeme wa gesi ndio wa kisasa. Umeme wa maji sio wa uhakika. Ndio maana mara kwa mara nchi ikitetereka kidogo kupata mvua, umeme unakuwa shida.

Changamoto ya umeme wa maji na kukauka kwa mabwawa ya kuzalishia umeme ndio matokeo ya nchi kuingia mikataba ya hovyo ya IPTL na Richmond kwa sababu ya uhitaji wa umeme wa dharura.

Pamoja na kutambua hayo, bado Serikali ya Magufuli ikafanya uamuzi wa kujenga mradi wa umeme wa maji.

Maswali ni mengi mno, unawezaje kujenga mradi wa umeme wa maji katika nchi ambayo tayari ina gesi ya kutosha?

Kuutelekeza mradi wa gesi Mtwara, ilikuwa kumkomoa nani? Hii hulka ya Rais akiingia madarakani anatelekeza miradi ya mtangulizi wake inaumiza mno wananchi.

Ingekuwaje Rais Samia angeamua kutoendelea na JNHPP? Fedha za Watanzania zingetolewa maelezo gani? Yatolewe maelezo ya kutelekezwa gesi Mtwara na miradi mingine yote ambayo ipo njiani miaka saba sasa.

Mwisho tuhoji; miti milioni tatu iliyokatwa Msitu wa Selous kupisha mradi wa JNHPP, ilipelekwa wapi? Iliuzwa? Fedha ilikwenda wapi? Uchunguzi maalum unahitajika katika hili.

Kuna harufu kubwa ya ufisadi wa miti milioni tatu iliyokatwa Selous.

Ndimi Luqman MALOTO
View attachment 2454151View attachment 2454152
Wewe Mtanzania una gas gani?,gas yote ni ya wachina,acha kudanganya watu
 
Lawama zote kwa CCM. Hali ya mvua imekuwa kusuasua sana. Wajinga hawa wanatuambia tuombee mvua. Haya maji yakikauka hiyo turbines zitaendeshwa kwa madenda?
 
Kwani umeme wa Gas Principle ni ipi? Si kuchemsha maji? Sasa kama hamna maji ya kuchemsha si sawa tu kukosa maji kwa ukame? Ile mitungi mirefu inawekwa nini?

Hydro haihitaji mitungi na kuchemsha maji, inahitaji "gravity" tu kuziendesha Turbines na umeme unawake, kipi gharama rahisi kati ya hivi viwili?

Mto au bwawa la Maji => Gravity = Turbines au
Gasi = mitungi ya maji kuchemsha mvuke halafu ukapige turbines na coolers vile vile!

Shule nzuri
Wrong. Gas turbines haziendeshwi na mvuke wa maji.
 
Back
Top Bottom