Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nashangaa hizi kelele, tukitaka kupanda miti mipya hata milioni 3 igawanye kwa mikoa hata wanafunzi wa shule ya msingi wanafanya. Watu walihamisha bahari ili wapate ardhi itakuwa kujenga bwawa la umeme?Kama swala ni upatikanaji wa hewa safi. Bahari ipo na ndio inatoa 80% ya oksijeni tunayovuta.
Umetoa wazo zuri sana mkuu. Tupande miti kufidia iliyokatwa problem solved.
Bwawa lipi boss.Fuatilia kule kwenye bwawa tu wewe.
Sasa kama haijapigwa unaiona wapi wewe?
Hilo bwawa sio center ya mambo yote, ni porojo tu kama zile za Muhongo na gesi.1: Maji yatakauka ? Duh sasa yakikauka si tutakufa kabisa hata kabla ya kukosa giza ?
2: Ukame utakuja maji hayana uhakika gesi ndio uhakika ? ; Kwamba hio gesi ndio haitaisha ?
3: Tungekuwa na gesi mpaka ya kupikia ?; Hio gesi ingekuwa bei gani production cost na tunanunua kwa kiasi gasi ili tuuziwe kwa kiasi gani? Na hizo infrastructure za pipes mpaka majumbani kwa watu kule milimani ni kiasi gani and is it even feasible let alone doable ?
4: Sipingi energy mix ila hili Bwawa ndio the centre ya mambo yote na likitumika vizuri linaweza likatutoa hapa na kutupeleka pale....
Jinsi ya kuifanya Kampuni ya Tanesco kuwa Kampuni Bora na ya Kujivunia Tanzania na Afrika kwa Ujumla
Tanzania tumebarikiwa vyanzo vingi vya nishati, Na Tanesco ni kati ya Makampuni mama ya Tanzania ambayo yanaweza yakaitangaza nchi yetu Africa na Pote Duniani (Yaani mfano wa kuigwa) Sio tu kutupatia nishati hapa bali tuweze kuwapa hata majirani zetu na kutuingizia fedha badala ya sasa kutumia...www.jamiiforums.com
Inaweza isiwe centre ya mambo yote (kwa jinsi mambo yanavyokwenda) ila likitumika vema litakuwa centre ya mambo yote - kama tunataka energy mix ya upepo na jua unadhani tutatunza vipi hio energy ili itumike baadae...Hilo bwawa sio center ya mambo yote, ni porojo tu kama zile za Muhongo na gesi.
Unajua wewe ni mjinga ila hujui tu kama ni mjinga, ndiomanaa unaadika upupu kama huu kwa kujiamini kabisa.Sasa hapa Kuna hoja gani ya kujenga umeiweka wewe?
Ni kweli mradi huwezi kuacha kwa Sasa lakini haiondoi ukweli kwamba Mwendazake alikosea Sana na kaisababishia Nchi hasara..
Unatumia Til.11 kuzalisha megwt 2115 na kuharibu Mamilioni ya hekta za misitu na vyanzo vya maji.
Ni akili hiyo?
Wewe jamaa hujui kitu unabwabwaja tu au umetumwa kuja kuangalia hali ya hewa,unajua hiyo gesi ya Mtwara inaenda na Wazungu?LEO Rais Samia Suluhu Hassan, atakuwa mgeni rasmi katika tukio la kujaza maji kwenye Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere (JNHPP). Hatua muhimu kwenda kuzalisha umeme.
JNHPP itakuwa na uwezo wa kufua umeme megawati 2,100 na kuuingiza gridi ya taifa kila siku. Hatua kubwa kuelekea nchi kujitosheleza katika nishati ya umeme.
Kukamilika kwa JNHPP bila shaka utakuwa mwanzo wa kupotea kwa hisia na maneno kuwa mradi huo ulikuwa unahujumiwa usifike mwisho. Muda ni tiba thabiti.
Pamoja na kipengele hicho chanya, upo ukweli ambao si Rais Samia Suluhu Hassan wala Waziri wa Nishati, January Makamba, wanaweza kuusema.
Kwamba JNHPP ni mradi ambao hawakuwa na namna zaidi ya kuukamilisha kwa sababu waliukuta umeshakaribia nusu na tayari ulishateketeza fedha nyingi za Watanzania.
Ukweli ni kuwa mradi wa JNHPP ulikuwa uamuzi wa hovyo kuwahi kutokea. Kwanza unakuja na athari kubwa ya kimazingira. Ushauri wa wataalamu ulipuuzwa. Mradi ukajengwa kwa kulazimisha.
Karibu miti milioni tatu imekatwa. Eneo la msitu la kilometa za mraba 1,500 limeharibiwa (deforestation).
Yaani, Serikali iliamua kujenga mradi wa umeme wa maji kwa kuharibu vyanzo vya maji.
Hivi sasa kuna mabadiliko ya tabia nchi. Mvua hazinyeshi. Mto Rufiji umekuwa mkavu. Je, sio athari za kuharibu msitu wa Selous.
Mtangulizi wa Rais Samia, Dk John Magufuli, alipoingia madarakani, alikuta mradi mkubwa wa gesi Mtwara. Nchi ilikuwa ina tabasamu kuelekea uchumi wa gesi.
Fedha zaidi ya Sh11 trilioni zilizotumika kujenga JNHPP, nusu yake tu ungewekezwa kwenye gesi Mtwara, sasa hivi nchi ingekuwa na umeme wa gesi, nishati ya kupikia ya gesi na kufanya mauzo ya gesi nje ya nchi. Tungeepuka janga la vita ya Ukraine na Urusi.
Umeme wa gesi ndio wa kisasa. Umeme wa maji sio wa uhakika. Ndio maana mara kwa mara nchi ikitetereka kidogo kupata mvua, umeme unakuwa shida.
Changamoto ya umeme wa maji na kukauka kwa mabwawa ya kuzalishia umeme ndio matokeo ya nchi kuingia mikataba ya hovyo ya IPTL na Richmond kwa sababu ya uhitaji wa umeme wa dharura.
Pamoja na kutambua hayo, bado Serikali ya Magufuli ikafanya uamuzi wa kujenga mradi wa umeme wa maji.
Maswali ni mengi mno, unawezaje kujenga mradi wa umeme wa maji katika nchi ambayo tayari ina gesi ya kutosha?
Kuutelekeza mradi wa gesi Mtwara, ilikuwa kumkomoa nani? Hii hulka ya Rais akiingia madarakani anatelekeza miradi ya mtangulizi wake inaumiza mno wananchi.
Ingekuwaje Rais Samia angeamua kutoendelea na JNHPP? Fedha za Watanzania zingetolewa maelezo gani? Yatolewe maelezo ya kutelekezwa gesi Mtwara na miradi mingine yote ambayo ipo njiani miaka saba sasa.
Mwisho tuhoji; miti milioni tatu iliyokatwa Msitu wa Selous kupisha mradi wa JNHPP, ilipelekwa wapi? Iliuzwa? Fedha ilikwenda wapi? Uchunguzi maalum unahitajika katika hili.
Kuna harufu kubwa ya ufisadi wa miti milioni tatu iliyokatwa Selous.
Ndimi Luqman MALOTO
View attachment 2454151View attachment 2454152
Mueleweni huyu Bwana vizuri.Nadhani yeye anachohoji ni miti millioni tatu ilipokwenda.He is not concerned about cutting of trees.He believes kwamba hiyo miti imeuzwa,sasa pesa iko wapi?Misri lile bwawa lao la kufua umeme katika mto Nile walijenga juu ya miti?. Ghana na zimbabwe yale mabwa makubwa walijenga kwenye hewa bila kukata miti?
Ulaya miradk mikubwa ya nyukri hewani? Acha kushikiwa akili we dogo
Acheni uchambuzi wa kichawa. Vipi miti inayokatwa kwa kilimo, mkaa na kusafirisha magogo nje? Mbona haya haujayaandikia aya.LEO Rais Samia Suluhu Hassan, atakuwa mgeni rasmi katika tukio la kujaza maji kwenye Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere (JNHPP). Hatua muhimu kwenda kuzalisha umeme.
JNHPP itakuwa na uwezo wa kufua umeme megawati 2,100 na kuuingiza gridi ya taifa kila siku. Hatua kubwa kuelekea nchi kujitosheleza katika nishati ya umeme.
Kukamilika kwa JNHPP bila shaka utakuwa mwanzo wa kupotea kwa hisia na maneno kuwa mradi huo ulikuwa unahujumiwa usifike mwisho. Muda ni tiba thabiti.
Pamoja na kipengele hicho chanya, upo ukweli ambao si Rais Samia Suluhu Hassan wala Waziri wa Nishati, January Makamba, wanaweza kuusema.
Kwamba JNHPP ni mradi ambao hawakuwa na namna zaidi ya kuukamilisha kwa sababu waliukuta umeshakaribia nusu na tayari ulishateketeza fedha nyingi za Watanzania.
Ukweli ni kuwa mradi wa JNHPP ulikuwa uamuzi wa hovyo kuwahi kutokea. Kwanza unakuja na athari kubwa ya kimazingira. Ushauri wa wataalamu ulipuuzwa. Mradi ukajengwa kwa kulazimisha.
Karibu miti milioni tatu imekatwa. Eneo la msitu la kilometa za mraba 1,500 limeharibiwa (deforestation).
Yaani, Serikali iliamua kujenga mradi wa umeme wa maji kwa kuharibu vyanzo vya maji.
Hivi sasa kuna mabadiliko ya tabia nchi. Mvua hazinyeshi. Mto Rufiji umekuwa mkavu. Je, sio athari za kuharibu msitu wa Selous.
Mtangulizi wa Rais Samia, Dk John Magufuli, alipoingia madarakani, alikuta mradi mkubwa wa gesi Mtwara. Nchi ilikuwa ina tabasamu kuelekea uchumi wa gesi.
Fedha zaidi ya Sh11 trilioni zilizotumika kujenga JNHPP, nusu yake tu ungewekezwa kwenye gesi Mtwara, sasa hivi nchi ingekuwa na umeme wa gesi, nishati ya kupikia ya gesi na kufanya mauzo ya gesi nje ya nchi. Tungeepuka janga la vita ya Ukraine na Urusi.
Umeme wa gesi ndio wa kisasa. Umeme wa maji sio wa uhakika. Ndio maana mara kwa mara nchi ikitetereka kidogo kupata mvua, umeme unakuwa shida.
Changamoto ya umeme wa maji na kukauka kwa mabwawa ya kuzalishia umeme ndio matokeo ya nchi kuingia mikataba ya hovyo ya IPTL na Richmond kwa sababu ya uhitaji wa umeme wa dharura.
Pamoja na kutambua hayo, bado Serikali ya Magufuli ikafanya uamuzi wa kujenga mradi wa umeme wa maji.
Maswali ni mengi mno, unawezaje kujenga mradi wa umeme wa maji katika nchi ambayo tayari ina gesi ya kutosha?
Kuutelekeza mradi wa gesi Mtwara, ilikuwa kumkomoa nani? Hii hulka ya Rais akiingia madarakani anatelekeza miradi ya mtangulizi wake inaumiza mno wananchi.
Ingekuwaje Rais Samia angeamua kutoendelea na JNHPP? Fedha za Watanzania zingetolewa maelezo gani? Yatolewe maelezo ya kutelekezwa gesi Mtwara na miradi mingine yote ambayo ipo njiani miaka saba sasa.
Mwisho tuhoji; miti milioni tatu iliyokatwa Msitu wa Selous kupisha mradi wa JNHPP, ilipelekwa wapi? Iliuzwa? Fedha ilikwenda wapi? Uchunguzi maalum unahitajika katika hili.
Kuna harufu kubwa ya ufisadi wa miti milioni tatu iliyokatwa Selous.
Ndimi Luqman MALOTO
View attachment 2454151View attachment 2454152
Watu wengi hawajui kuwa bei muafaka lazima ihusishe kiasi cha “roc” - return on capital invested. Ikipigwa bei ya uhakika kulingana na matarajio ya urejeshaji wa mitaji uliowekezwa, si ajabu hicho kinachoitwa “umeme wa bei rahisi” kikaonekana enzi za wajukuu. Hapo pia itategemea kama mafisadi wajao hawatachezea miundombinu.Una uhakika gani umeme wa maji hautakuwa bei juu? Unajua terms za mkopo wa ujenzi wa hilo bwawa? Mbona ndege ni zetu, lakini nauli ni bei gali kulinganisha na fastjet? Acheni utapeli wa kijinga.
La Nyerere.. usikie ghalama harisi na na sio unaleta mbwembwe za 11 tl badala ya 6.5 tln.. mweupe sana wewe jamaa.Bwawa lipi boss.
Unataka kujenga nchi sio kubomoa nchi,LAKINI ujenzi wa nchi unahitaji maamuzi sahihi na salama kwa maslahi mapana ya nchi yetu.Mradi wa JNHPP upo ktk POINT OF NO RETURN BACK! Acheni maneno mengi yasiyojenga nchi. Serikali za CCM tangu Uhuru viongozi wanaongozwa na Dira ya nchi.
Marais wetu wote waliongoza kwa Dira ya nchi. Mhe. Rais Samia alishasema hakuna mradi wa kimkakati ulioanzishwa na mtangulizi wake utakwama.
Tuwe na hoja za kujenga nchi siyo porojo za uchonganishi kila siku zinakera sana. Jiandae kushuhudia Mhe. Rais akibonyeza kitufe.🙏🙏🙏
Mjane acha kulialia kwani ni wewe pekee yako ndo mjane? Mfare huko umsaidie kukusanya kuni mbanikwe pamojaWivu tu ..
Mimba ya Mwendazake kiboko
Dah,yaani kama ulaya,Mungu ambariki magufuli,Ndimi Luqman MALOTO
![]()
La Nyerere.. usikie ghalama harisi na na sio unaleta mbwembwe za 11 tl badala ya 6.5 tln.. mweupe sana wewe jamaa.