Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ukimezeshwa betri ukariri maneno unafikiri inakuaje? Wanasema wasichokijua wala kukielewa kama parrotsYaani shida ya mtoa hoja ni miti mil.3 iliyokatwa ndio isababishe mabadiriko ya tabia ya nchi duh. Hibi unajua ni kiasi gani cha misitu kinapotea kwa mwaka pasipo na manufaa yoyote yakitaifa sembuse hiyo miti iliyokatwa kwa kujenga bwawa.
Halafu kujenga bwawa sio maji yatakauka maji yataendelea kuwepo kitakachofanyika ni control ya maji iki kuzalisha umeme si sawa na maji yanayotumika kwenye umwagiliaji yanapotea ardhini na sio kwenye kuzalisha umeme. Mtoa hoja hebu njoo na hoja za kitaalam sio siasa.
Hao hao wachina hivi karibuni wamejenga bwawa kubwa la kuzalisha umeme kuliko letu, unazani hiyo ecology walikuwa hawaijui.We naye unampoteza tu!! Nani kakwambia madhara ya tabianchi yanakua felt ndani ya mwaka mmoja?? Ukataji miti unaosifia siku ukijibu ni miaka hata 30 ijayo ndio utaona madhara yake.
Tukubali kwamba tumeona faida za umeme ni kubwa kuliko madhara ya ikolojia ila kupinga hakuna madhara kisa "mbona tumeshakata sana" sio logic kabisa.
Hii kitu ilimcost Mao Zedong, kasome the Great leap forward jinsi kuua "wadudu watambaao" kulileta ukame mkubwa sana china almost 50 million walikufa!! Imagine unaua mende na nzi ila anayeathirika ni binadamu tokea pale ndio nikaelewa kwanini hata majoka makubwa yakidakwa hayauawi yanarudishwa msituni. Simple answer ni Ecology!!
6T sio 11 mkuuJifunze ku attach hizo picha vizuri.
Anyway watakuja na blaa blaa za kusema gas imeuzwa na umeme wa gas Ni ghali Sana 😂😂.
Ila Hilo bwawa ni expensive Sana kuliko uhalisia wake.Til.11 Ni Pesa nyingi Sana aisee..
Huna gas ww? Kipindi kile bungeni uliambiwa umeme ukizalishwa kwa kutumia gas, bei zitashuka vip tokea waanze kuzalisha umeme wa gesi Cost per unit imeshuka?
Hapo ndipo utapata majibu gas ni ya nani na nani ana control bei ya hiyo gas.
Mbona unahamisha magoli? Huwezi fananisha ndege na nishati ambayo ina impact kwa kila raia mmoja mmoja.Ndege ni zetu, mbona nauli ni ghali kuliko ilivyokuwa fast jet? Au hizo ndege nazo zina wenyewe kama hiyo gas?
Waethiopia sahv wanakazana kupanda miti kwaoThe main point I have seen in your opinions ni MITI ILIYOKATWA.
Serikali ianze kampeni ya kupanda MITI Ili tufanye recovery ya MITI iliyopotea.
Ethiopians ambao Wana mradi kama huu wanasema nini?
Bandiko nyingine tunazianzisha bila kuwa na exposure.
Everything has merits and demerits for this project merits is very high.
Mtoa mada Mimi siungani na hayo mawazo yako.
Kabla ya umeme wa mafuta mazito, na gas tulikuwa tunatumia umeme wa maji, mbona haukuwa wa bei rahisi? Au huo ni umeme wa maji gani labda. Ukakope fedha zote hizo, kisha utegemee umeme wa bei rahisi?Mbona unahamisha magoli? Huwezi fananisha ndege na nishati ambayo ina impact kwa kila raia mmoja mmoja.
Waethiopia wako kwenye phase 3 ya kulijaza maji bwawa laoEthiopia eneo kubwa ni jangwa sidhani wanahitaji kukata miti, walicholaumiwa ni kuwa waki divert Maji wanaweza risk watumishi wengine kwenye kilimo n.k. so na wao wanapigiwa kelele sana tu.
Tusipende kukataa madhara eti kisa Ethiopia sijui nani naye kakata miti!! Haya mazoea ndio yanasababisha Leo hii mvua hazinyeshi tunaanza lalamika.
LEO Rais Samia Suluhu Hassan, atakuwa mgeni rasmi katika tukio la kujaza maji kwenye Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere (JNHPP). Hatua muhimu kwenda kuzalisha umeme.
JNHPP itakuwa na uwezo wa kufua umeme megawati 2,100 na kuuingiza gridi ya taifa kila siku. Hatua kubwa kuelekea nchi kujitosheleza katika nishati ya umeme.
Kukamilika kwa JNHPP bila shaka utakuwa mwanzo wa kupotea kwa hisia na maneno kuwa mradi huo ulikuwa unahujumiwa usifike mwisho. Muda ni tiba thabiti.
Pamoja na kipengele hicho chanya, upo ukweli ambao si Rais Samia Suluhu Hassan wala Waziri wa Nishati, January Makamba, wanaweza kuusema.
Kwamba JNHPP ni mradi ambao hawakuwa na namna zaidi ya kuukamilisha kwa sababu waliukuta umeshakaribia nusu na tayari ulishateketeza fedha nyingi za Watanzania.
Ukweli ni kuwa mradi wa JNHPP ulikuwa uamuzi wa hovyo kuwahi kutokea. Kwanza unakuja na athari kubwa ya kimazingira. Ushauri wa wataalamu ulipuuzwa. Mradi ukajengwa kwa kulazimisha.
Karibu miti milioni tatu imekatwa. Eneo la msitu la kilometa za mraba 1,500 limeharibiwa (deforestation).
Yaani, Serikali iliamua kujenga mradi wa umeme wa maji kwa kuharibu vyanzo vya maji.
Hivi sasa kuna mabadiliko ya tabia nchi. Mvua hazinyeshi. Mto Rufiji umekuwa mkavu. Je, sio athari za kuharibu msitu wa Selous.
Mtangulizi wa Rais Samia, Dk John Magufuli, alipoingia madarakani, alikuta mradi mkubwa wa gesi Mtwara. Nchi ilikuwa ina tabasamu kuelekea uchumi wa gesi.
Fedha zaidi ya Sh11 trilioni zilizotumika kujenga JNHPP, nusu yake tu ungewekezwa kwenye gesi Mtwara, sasa hivi nchi ingekuwa na umeme wa gesi, nishati ya kupikia ya gesi na kufanya mauzo ya gesi nje ya nchi. Tungeepuka janga la vita ya Ukraine na Urusi.
Umeme wa gesi ndio wa kisasa. Umeme wa maji sio wa uhakika. Ndio maana mara kwa mara nchi ikitetereka kidogo kupata mvua, umeme unakuwa shida.
Changamoto ya umeme wa maji na kukauka kwa mabwawa ya kuzalishia umeme ndio matokeo ya nchi kuingia mikataba ya hovyo ya IPTL na Richmond kwa sababu ya uhitaji wa umeme wa dharura.
Pamoja na kutambua hayo, bado Serikali ya Magufuli ikafanya uamuzi wa kujenga mradi wa umeme wa maji.
Maswali ni mengi mno, unawezaje kujenga mradi wa umeme wa maji katika nchi ambayo tayari ina gesi ya kutosha?
Kuutelekeza mradi wa gesi Mtwara, ilikuwa kumkomoa nani? Hii hulka ya Rais akiingia madarakani anatelekeza miradi ya mtangulizi wake inaumiza mno wananchi.
Ingekuwaje Rais Samia angeamua kutoendelea na JNHPP? Fedha za Watanzania zingetolewa maelezo gani? Yatolewe maelezo ya kutelekezwa gesi Mtwara na miradi mingine yote ambayo ipo njiani miaka saba sasa.
Mwisho tuhoji; miti milioni tatu iliyokatwa Msitu wa Selous kupisha mradi wa JNHPP, ilipelekwa wapi? Iliuzwa? Fedha ilikwenda wapi? Uchunguzi maalum unahitajika katika hili.
Kuna harufu kubwa ya ufisadi wa miti milioni tatu iliyokatwa Selous.
Ndimi Luqman MALOTO
View attachment 2454151View attachment 2454152
Ndiyo mpande miti sasaKama swala ni upatikanaji wa hewa safi. Bahari ipo na ndio inatoa 80% ya oksijeni tunayovuta.
Umetoa wazo zuri sana mkuu. Tupande miti kufidia iliyokatwa problem solved.
Hili dude si mchezoDah,yaani kama ulaya,Mungu ambariki magufuli,
mleta mada kama umeishajenga au unapanga,hata hapo ulipojenga lazima kuna mimea ilikatwa ili upate pa kuishi
unless unaleta uzi huu kutokea porini kama ngedere hapo nitakuelewa.
Hivi unatizamaga bunge wakati wa sekeseke lile la gesi?Kabla ya umeme wa mafuta mazito, na gas tulikuwa tunatumia umeme wa maji, mbona haukuwa wa bei rahisi? Au huo ni umeme wa maji gani labda. Ukakope fedha zote hizo, kisha utegemee umeme wa bei rahisi?
Nchi hii siasa imeshika hatamuSiasa, siasa,siasa. Mambo ya kitaalamu ukiingiza siasa bado kutakuwa na maneme meeeennnnggiiii.
Punguzeni siasa kwenye mambo ya kitaalam,hivi wakati wanatandaza bomba la gesi kutoka urusi hadi ulaya magharibi huko hawakufyeka mitiNInakazia;
"Mwisho tuhoji; miti milioni tatu iliyokatwa Msitu wa Selous kupisha mradi wa JNHPP, ilipelekwa wapi? Iliuzwa? Fedha ilikwenda wapi? Uchunguzi maalum unahitajika katika hili."
Hivi unatizamaga bunge wakati wa sekeseke lile la gesi?
Huja msikia waziri wako akisema umeme wa gas utapunguza gharama za umeme kwa unit? au ndio oya oya.
Ila duniani kote umeme wa maji uzalishwaji wake ni cheap na ndio maana hata China nae kakimbilia huko huko hivi karibuni kazindua bwawa kubwa kuliko letu la kuzalisha umeme,kwani unazani China alishindwa kuweka power plant ya nuclear.
Umeme wa gas ni gharama pili gas sio yako labda sijajua hiyo gas iliyo gunduliwa kipindi cha Magu hapo Ruvu, mikataba yao ipoje.