Ukweli unaoogopwa kusemwa kuhusu bwawa la umeme la Nyerere

Ukweli unaoogopwa kusemwa kuhusu bwawa la umeme la Nyerere

Ni kweli umeme wa maji ni cheap, lakini uwekezaji wa huo mradi ni fedha za mkopo. Unajua terms za marejesho ya huo mkopo?

Kwani Magu aliwahi kuweka mkataba wowote wazi hadi uwe na imani naye kwenye mikataba?
Kwai umeme wa maji tumeingia na kampuni gani ambayo itazalisha huu umeme?

Maana huu mradi ni wa serikali hamna third part atakaye control huu mradi tofauti na wa gesi, je gas unacontrol nayo?
 
Kwai umeme wa maji tumeingia na kampuni gani ambayo itazalisha huu umeme?

Maana huu mradi ni wa serikali hamna third part atakaye control huu mradi tofauti na wa gesi, je gas unacontrol nayo?

Narudia tena, hizo ni fedha za mkopo, unajua masharti ya huo mkopo?
 
Narudia tena, hizo ni fedha za mkopo, unajua masharti ya huo mkopo?
Sasa fedha ya mkopo uliyokopa ww ambayo unaijua 6.5tn? na fedha ya Mwekezaji ipi ni nyepesi kurudi? Kwanza huna control na gasi yako, pili mwekezaji hata akisema katumia tn 100 huwezi kumkatalia.

Kuhusu mkataba mkopo sijauona ila najua tumekopa 6.5tn,vp ww unaye komaa na umeme wa gasi mikataba ya uzalishaji na ujengwaji wa vinu vyake gharama zake umeziona?
 
Tuongee tu UKWELI.
Kati ya mradi ambao utageuka na kuwa mzigo kwa Taifa ni pamoja na huu wa JNHP.
Mradi mwingine ni wa SGR, baada ya ule wa ndege.
Labda tuboreshe uwezo wetu wa kukabiliana na majanga!
 
Ww una uhakika ni 6.5t?
 
LEO Rais Samia Suluhu Hassan, atakuwa mgeni rasmi katika tukio la kujaza maji kwenye Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere (JNHPP). Hatua muhimu kwenda kuzalisha umeme.

JNHPP itakuwa na uwezo wa kufua umeme megawati 2,100 na kuuingiza gridi ya taifa kila siku. Hatua kubwa kuelekea nchi kujitosheleza katika nishati ya umeme.

Kukamilika kwa JNHPP bila shaka utakuwa mwanzo wa kupotea kwa hisia na maneno kuwa mradi huo ulikuwa unahujumiwa usifike mwisho. Muda ni tiba thabiti.

Pamoja na kipengele hicho chanya, upo ukweli ambao si Rais Samia Suluhu Hassan wala Waziri wa Nishati, January Makamba, wanaweza kuusema.

Kwamba JNHPP ni mradi ambao hawakuwa na namna zaidi ya kuukamilisha kwa sababu waliukuta umeshakaribia nusu na tayari ulishateketeza fedha nyingi za Watanzania.

Ukweli ni kuwa mradi wa JNHPP ulikuwa uamuzi wa hovyo kuwahi kutokea. Kwanza unakuja na athari kubwa ya kimazingira. Ushauri wa wataalamu ulipuuzwa. Mradi ukajengwa kwa kulazimisha.

Karibu miti milioni tatu imekatwa. Eneo la msitu la kilometa za mraba 1,500 limeharibiwa (deforestation).

Yaani, Serikali iliamua kujenga mradi wa umeme wa maji kwa kuharibu vyanzo vya maji.

Hivi sasa kuna mabadiliko ya tabia nchi. Mvua hazinyeshi. Mto Rufiji umekuwa mkavu. Je, sio athari za kuharibu msitu wa Selous.

Mtangulizi wa Rais Samia, Dk John Magufuli, alipoingia madarakani, alikuta mradi mkubwa wa gesi Mtwara. Nchi ilikuwa ina tabasamu kuelekea uchumi wa gesi.

Fedha zaidi ya Sh11 trilioni zilizotumika kujenga JNHPP, nusu yake tu ungewekezwa kwenye gesi Mtwara, sasa hivi nchi ingekuwa na umeme wa gesi, nishati ya kupikia ya gesi na kufanya mauzo ya gesi nje ya nchi. Tungeepuka janga la vita ya Ukraine na Urusi.

Umeme wa gesi ndio wa kisasa. Umeme wa maji sio wa uhakika. Ndio maana mara kwa mara nchi ikitetereka kidogo kupata mvua, umeme unakuwa shida.

Changamoto ya umeme wa maji na kukauka kwa mabwawa ya kuzalishia umeme ndio matokeo ya nchi kuingia mikataba ya hovyo ya IPTL na Richmond kwa sababu ya uhitaji wa umeme wa dharura.

Pamoja na kutambua hayo, bado Serikali ya Magufuli ikafanya uamuzi wa kujenga mradi wa umeme wa maji.

Maswali ni mengi mno, unawezaje kujenga mradi wa umeme wa maji katika nchi ambayo tayari ina gesi ya kutosha?

Kuutelekeza mradi wa gesi Mtwara, ilikuwa kumkomoa nani? Hii hulka ya Rais akiingia madarakani anatelekeza miradi ya mtangulizi wake inaumiza mno wananchi.

Ingekuwaje Rais Samia angeamua kutoendelea na JNHPP? Fedha za Watanzania zingetolewa maelezo gani? Yatolewe maelezo ya kutelekezwa gesi Mtwara na miradi mingine yote ambayo ipo njiani miaka saba sasa.

Mwisho tuhoji; miti milioni tatu iliyokatwa Msitu wa Selous kupisha mradi wa JNHPP, ilipelekwa wapi? Iliuzwa? Fedha ilikwenda wapi? Uchunguzi maalum unahitajika katika hili.

Kuna harufu kubwa ya ufisadi wa miti milioni tatu iliyokatwa Selous.

Ndimi Luqman MALOTO
View attachment 2454151View attachment 2454152
Asali ni TAMU SANA
 
Punguzeni siasa kwenye mambo ya kitaalam,hivi wakati wanatandaza bomba la gesi kutoka urusi hadi ulaya magharibi huko hawakufyeka miti
Ehhh

Ova

Wewe ni mmoja wa wanafamilia wale 12 wanufaika wakuu wa rasilimali hizi?

Su japo mseme tu? Hii miti milioni 3 iliyokatwa huko mliipeleka wapi? Mliitupa baharini?

Au kama mliiuza, mliiuza wapi? Pesa nazo mkapeleka wapi?

Au mngependa tusiwaulize?

Uhuru wote wa majibu tumekupa na tutayazingatia.
 
Sidhani Kama ni vibaya kuwa na sources za kutosha za kuzalisha umeme.Tatizo la gesi ya Mtwara nadhani ni zito.Zipo taarifa kwamba gesi ya Mtwara ilishauzwa for the next 25 years,na ndio maana Magufuli alikuwa anainyanyapaa.Kama hii ni kweli, huu ni ufisadi wa kutisha sana.Ni kweli hata hivyo kwamba gesi ingesaidia nchi sana kupata umeme.

Kuhusu swala la Bwawa la Nyerere,sidhani kama ni mradi worthwhile,eventually it will just be a White Elephant,hasa ukizingatia Climate Change.Water resources are drying up everywhere around the World,and Tanzania will not be an exception.Believe me, there won't be enough water for the dam considering the Climate Change Geo-engineering terrorism going on unabated around the World.The best option would have been Geothermal power.

Tuambie sababu za maji yanakauka
 
JPM alikuwa anawaza mbali sana yule mwamba. Bora kipi pesa zinazoibwa na akina makatani na mwenzie miguru au bora zipotelee kwenye mradi wa Watanzania wote na wanufaike wote.
Mimi hata pesa itumike matrions kwenye miradi kikubwa yenye tija inayoonekana sina tatizo kabisa. Acha pesa itumike kuliko inavyokwapuliwa
 
Sasa hapa Kuna hoja gani ya kujenga umeiweka wewe?

Ni kweli mradi huwezi kuacha kwa Sasa lakini haiondoi ukweli kwamba Mwendazake alikosea Sana na kaisababishia Nchi hasara..

Unatumia Til.11 kuzalisha megwt 2115 na kuharibu Mamilioni ya hekta za misitu na vyanzo vya maji.

Ni akili hiyo?
Uelewa wako ni mdogo
 
Yaah ninao 6.5tn,sababu hata kwenye magazeti walichapisha gharama tulizokopa. Vip ww wa gas na huyo mwekezaji?

Imebidi nicheke tu, eti hata kwenye magazeti wamechapisha. Kwani hayo magazeti yenyewe yanafanya uchunguzi wa ukweli wa kisemwacho, au wao wanaripoti tu wanachosikia toka kwa viongozi?
 
Imebidi nicheke tu, eti hata kwenye magazeti wamechapisha. Kwani hayo magazeti yenyewe yanafanya uchunguzi wa ukweli wa kisemwacho, au wao wanaripoti tu wanachosikia toka kwa viongozi?
So kwa hiyo ulitaka kuuona hebu ni ambie serikali gani duniani ishawahi kureveal mkataba kwa wananchi wake? Zaidi ya kuambiwa tumekopa kiasi gani kupiti kwenye vyombo vya habari.

Nitajie nchi yoyote kwa kinipatia reference (document)ya huo mkataba.
 
Subiri Mkuu uambiwe hivyo hivyo.
 
Tutachukua mkopo himilivu wa mvua kutoka congo
 
Simple nitajie nchi moja ambayo ishawahi ku reveal mkataba wake kwa wanachi?

Wananchi ni bunge boss, kwa bahati mbaya hapa kwetu bunge ni kibogoyo. Ila mikataba yote kwa nchi zinazojitambua hupitia bungeni.
 
Sidhani Kama ni vibaya kuwa na sources za kutosha za kuzalisha umeme.Tatizo la gesi ya Mtwara nadhani ni zito.Zipo taarifa kwamba gesi ya Mtwara ilishauzwa for the next 25 years,na ndio maana Magufuli alikuwa anainyanyapaa.Kama hii ni kweli, huu ni ufisadi wa kutisha sana.Ni kweli hata hivyo kwamba gesi ingesaidia nchi sana kupata umeme.

Kuhusu swala la Bwawa la Nyerere,sidhani kama ni mradi worthwhile,eventually it will just be a White Elephant,hasa ukizingatia Climate Change.Water resources are drying up everywhere around the World,and Tanzania will not be an exception.Believe me, there won't be enough water for the dam considering the Climate Change Geo-engineering terrorism going on unabated around the World.The best option would have been Geothermal power.

Na Mto Nile pia unaelekea kukauka! Ama sivyo?....
 
Back
Top Bottom