Ukweli usemwe: Aliyeharibu nchi hii ni Mwalimu Nyerere kwa kushindwa kuwapa Watanzania Elimu

Sasa mzee wangu unaweka hiyo screenshot haijulikani hata umeitoa wapi. Unazozifanya hapa ni cheap propaganda.

Kizazi cha sasa hakidanganywi kivyo. Weka source ya taarifa zako watu waweze evaluate. Unaogopa nini?
Niliposema wewe umeharibiwa na bangi usidhani nilikuwa natania.

Sasa hebu haya uliyoandika hapa, halafu rudi kwenye takataka zako ulizo andika hapo mwanzo uone kama akili yako kweli inafanya kazi sawasawa.

Hapa unadai kujua hiyo 'screenshot' ilikotolewa; lakini kule kwenye uchafu wote hata hujisumbui kurejea chochote.
 

Lee Kuan Yew anampata huyu PM wa singapore ???​

 
Sawa Nyerere kalikoroga na hayupo na nchi kaiacha nini kinawakwamisha kuifanya mtakavyo?
 
Na likatiba libovu la kumfanya rais mungu mtu
 
Shida
Sawa Nyerere kalikoroga na hayupo na nchi kaiacha nini kinawakwamisha kuifanya mtakavyo?
No mambo alivyo yaseti,yaani Kuna wenye nchi,Wala Nchi na Waliwa na Nchi,Sasa wewe mliwa na nchi huna chako nchini,unatakiwa usubiri kufa tu.yaani wenye nchi ni sawa na miungu,hata wafanye kosa gani huwaambii kitu huwatoi,hawakupendi hawakujali,wanajaliana wenyewe na Wala nchi
 
Kwa mada hii ndugu yangu yafaa Sasa tuwaite hata kenge waje JF kuchukua umember humu na watengeneze ID zao Kama vile Pluto star, Mercury star au Jupiter star! Maana mada Kama hii yako imekaa kikengekenge mnoo!

Ndio, kenge Hana Nidhamu, Kama ambavyo mada yako ilivyokosa Nidhamu kwa mzee wetu mwl Julius Kambarage Nyerere!

Jiulize kwanza Je, familia yako inapaswa kutegemea misingi iliyowekwa na babu yako, kwa ustawi wake?
Je, misingi ileile aliyoweka babu yako ndio ipasayo kuwaongoza wajukuu wako?

Acha ukenge ewe nyota ya Zuhura!
Mpe heshima Nyerere, na kila unapomkumbuka mhurumie kwa kazi mzito aliyofanya kujenga hili Taifa la wahuni Kama ninyi ambao Leo munaishia kumtukana matusi ya nguoni!

Kumbuka yule mzee aliongoza serikali maskini kuliko zote! Kipato Cha serikali yake kilikuwa duni mnoo, si Kama serikali tajiri za akina Kikwete!
Mapato ya miaka mitano ya serikali ya Kikwete, yalizidi mapato ya miaka 24 yote ya serikali ya Nyerere

Zingatia pesa ndogo aliyokuwa nayo, serikali yake iliwajibika kukidhi huduma zote za Jamii, Elimu, afya, maji, umeme, barabara, mishahara, ulinzi na usalama, na mengineyo!

Wewe umesimama na hoja ya miaka 24, vipi huangalii umaskini wa Taifa?
Alikuwa na vyanzo gani hasa kupata fedha lukuki kumwaga mashule Nchi mzima? Enzi zile hata waalimu hawakuwepo, hizo shule angefundisha Nani?

Nyakati zile raia walikataa shule, aliwaswaga wakae kwenye vijiji na aliwahimiza kujenga shule! Walioitika waliweza kukata miti na kujenga shule za udongo na waalimu wawili au watatu waliletwa, na shule ilianza!

Hivi unajua mzigo wa kusambaza vitabu mashuleni Nchi mzima? Hawa marais wako wa siku hizi bado wanashindwa kujaza vitabu mashuleni, ingawa wanaingia madarakani wanakuta shule Zina upungufu wa vitabu na Hadi wanaondoka madarakani wanaacha shule Zina upungufu wa vitabu!
Enzi za Nyerere vitabu vilijaa mashuleni, wanafunzi wanapewa daftari na peni, Elimu bure, si hii ya leo michango miiingi na tunaambiwa Elimu bure!

Mwache yule mzee apumzike!
Wewe na Mimi tulijenge hili Taifa Sasa!
Mambo aliyoanzisha yangedumishwa, Taifa hili lisingekuwa hivi lilivyo!

Watu eti munamlaumu katiba! Hivi Ni kweli? Tunashindwa kuunda katiba? Ule mchakato wa katiba ulisitishwa na Nyerere?
Hio Ni sawa kumlaumu baba yako hajanunua nguo za wewe kuvaa ujanani na uzeeni!
Baba ananunua nguo za utotoni tu, ukikua nunua mwenyewe!

Aliandaa katiba iliyompa uhalali wa vile alivyopenda atawale! Ameondoka hakuwashurutisha watanzania kuendelea kuifuata! Kwani bunge si mnalo? Unapomlaumu Nyerere, huoni unazuia wabunge kuwajibika?
Na ingewezekana vipi abadili katiba ili ang'atuke na kuwaachia marais wenzake msala?
Hilo Ni Jambo la kutekelezwa na wananchi, sikitika kwamba wananchi hawajaamka!

Mataifa mengi, yamebadili katiba, wamejenga uchumi na maendeleo ya Taifa bila kulalama eti Rais wa kwanza hajaweka misingi imara!

Nosense!







Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Huyo si ndie aliesema kwa katiba tuliyonayo Rais anaweza kuwa Dictator lakini hakubadilisha na uwezo alikuwa nao
Je alikuwa anaongozwa kwa remote nae toka nje ?
 
You seems to have a very serious Mental problem. I urge you to visit a nearby Mental Health Hospitali so that you can be treated.
 
Sijakikataa kiswahili , ila sio lugha ambayo inaweza kukujenga kwenye international standards of understanding the world..
Mikataba mingapi tumeingizwa chaka tu kwa sababu watawala hawakusoma na kuelewa those fine prints? Sasa hivi kuna hili la Dp world hali ni ile ile, wengi hata huo mkataba hawajui kinaelezwa nini.
 
Niliwahi kuandika haya kuhusu Nyerere:

 
Shida kubwa ya sera ya ujamaa ni propaganda na unafiki . Na ndio ulikuwa mtaji mkubwa wa the late mwalimu .

Kwamba mwaka 1961 kulikuwa na madokta 12 na mainjinia 2 nchi nzima na wewe unaaamini!
 
Rudi shule! Rudi shule!

Yaani kwa akili yako finyu, unafikiri mikataba mibovu ni kwaajili ya lugha?? 😂 😂

Chenge, mwanasheria mkuu wa serikali kasoma " Ivy League" Harvard University. Hizi ni top vyuo vikuu vya dunia. Lutokea Tanzania, vijana toka Ilboru, Seminary na shule nyingine za serikali za watoto wenye vipaji maalumu. Huko ni waalimu wa nguvu tu hufundisha, Wajerumani, Waingereza na Wamatumbi walio vizuri mno.

Mimi walimu wangu tangu Pre Form One wote walikua Wahindi wenye degree zaidi ya moja.
 
Shida kubwa ya sera ya ujamaa ni propaganda na unafiki . Na ndio ulikuwa mtaji mkubwa wa the late mwalimu .

Kwamba mwaka 1961 kulikuwa na madokta 12 na mainjinia 2 nchi nzima na wewe unaaamini!
Unakichaa! 😂

shule ulikuwa unakula bagia na kalimati😂

Tupe ushahidi kuwa haikuwa hivyo, mimi ninao ushahidi kuwa manesi zaidi ya 36 walikua toka Africa Kusini baada ya kutoroshwa na ANC na kuja Tanzania. Wengi wao bado wanaishi Tanzania, wameolewa na wengine wamekufa.

Toa wako nitakupa wangu😂
 
Huwezi kujadili hoja bila kejeli?
Nyerere wakati anaomba uhuru alikuta kina chifu mareale nao wanaomba uhuru wa ili kaskazini iwe kama nchi .
Sio hayo tu babu zangu miaka hiyo kabla ya uhuru walikuwa na elimu ya zaidi ya dokta. Nina amini sio miongoni mwa hao 12 maana sisi ni kaukoo kadogo sana.
 
Walimu wako wote walikuwa na degree! Yet unachangina hoja na kwa dharau na tambo!!
Huna tofauti na Chenge na Mkapa, watu walisoma top universities, badala ya kuja kulisaidia taifa kwa elimu zao wakaja kuwa chanzo cha sera mbovu zinazoleta umasikini mkubwa hadi leo.
' Kwenye ulimwengu wa vipofu ,chongo huonekana mfalme" hoja zako zinazidi kuji manifest kwenye tatizo alilotuachia the late mwalimu, la kutunyima elimu bora , wachache waliopenya , badala ya kuwa msaada ndo wanakuja kuwa maadui na tambo..
Kungekuwa na elimu bora usingekuja kunitambia mimi st kayumba , kuwa umefundishwa na walimu wenye degree!
 
Kuzipambanisha nchi yawatu weusi na race zingine kwenye issue yamaendeleo niujinga kamwe mtu mweusi hawez kushindanishwa ni automatic failure
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…