Ukweli usemwe: Chris Brown ni mkali kumzidi Michael Jackson

Unataka kutudanganya kwamba tumekairirishwa wakati wote tunawaona, acha hizo mambo we jamaa, kama unaona Chris brown ni bora bac hio ni preference yako lakini usitake kulazimisha wengine kwa kusingizia tumekaririshwa, hapana wote tumewaona na ukweli unajulikana nani ni bora, hata Chris brown ukimwambia yeye ni bora kuliko MJ atakukataa.
 
Dhaania ❌ dhahania ✅ entrainment ❌ entertainment ✅..... hata sisi tulishajiandaa kisaikolojia kuusoma uzi wako wa kipumbavu baada ya Chris Brown kupost akicheza wimbo wa mumeo Diamond.
 
Vijana wa zamani hakuna kitu chao kimezidiwa na kitu cha sasa 😂😂
Watu kama kina MJ hawatokei hovyohovyo. Unafahamu kwamba rekodi ya mbio za 1500m aliyoweka Mzee Filbert Bayi mwaka 1974 kwenye michezo ya jumuiya ya madola imekuja kuvunjwa mwaka 2022? Hata rekodi alizoweka mumeo Diamond huenda ikachukua muda sana kuja kuvunjwa. Kwahiyo kabla hujaandika fanya utafiti kwanza.
 
Kwenye muziki hakuna mfalme wa milele huko ni kulishana upepo,labda umri ungekuwa hausogei kwamba ukiwa kijana basi utaendelea kuwa kijana milele.Kizazi kimoja kinapita kinakuja kingine na kila kizazi cha muziki kinakuwa na mfalme wake
Watu wanaona ni dhambi kusema Michael Jackson hagusi uwezo wa Chris Brown
 
Ukiweka kigezo cha mauzo ya album basi baada ya Michael Jackson anafata Adele
 
So point yako ya msingi ni umri wangu?
Sio MJ kamzidi nini Chris Brown?
Nadhani amezungumzia umri sababu,kwenye industry ya Music kipindi Michael akiwa at the peak,mapenzi watu waliyokuwa nayo juu Yake ni makubwa mara dufu,kuliko kipindi hiki ambacho Chris akiwa katika peak yake,tukiacha mapenzi tu angalia records zingine kama mauzo etc.Usilinganishe nyimbo za chris na Michael kwa kuzisikiliza ss hv,kuna possibility kubwa ukamuona Chris ana nyimbo kali kutokana na umri wako.Walinganishe kila mtu alivyokuwa kwenye peak yake nn kilitokea dunian.
 
Ukiweka kigezo cha mauzo ya album basi baada ya Michael Jackson anafata Adele

Kwa mindset hii una uhalali wa kuona Chris Brown yupo juu ya Michael Jackson maana Muziki wa huko mbele huujui mkuu.

Maana kwa mtu anaeelewa, unawezaje kumuweka Adele mbele ya Whitney Houston, Celine Dione na Madonna kwenye mauzo ya album 😁😁. Cha kukusaidia tu, kwa hicho kigezo, adele hayupo hata top 5 ya best albums sales by female artists
 
Nina uhakika unatania
 
So point yako ya msingi ni umri wangu?
Sio MJ kamzidi nini Chris Brown?
Acha kujidhalilisha basi, kamuulize boss wako diamond ambaye CB kacheza nyimbo yake juzi atakwambia nani mkali, leo kukiwa na show mbili kwa pamoja yaani ukimbi mmoja wanapiga nyimbo za MJ na ukumbi mwingine kuna show ya CB nakuhakikishia huyo CB ataenda kwa MJ huku akisahau kuwa ana show
 
Embu jistukie basi, peke yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…