Ukweli usemwe: Joseph Haule (Profesa Jay) anahitaji utulivu, hizi pilikapilika za muziki na siasa angeachana nazo

Ukweli usemwe: Joseph Haule (Profesa Jay) anahitaji utulivu, hizi pilikapilika za muziki na siasa angeachana nazo

Kwani Daktari wake anasemaje?kwahyo ukiumwa sana ukapona hutakiwi kurudi tena kwenye mihangaiko yako?
 
Hawa hawa ndio walimponza mzee Yusuph akajidai na kulia kabisa weee ila alipoanza kushindia vitumbua kama dozi kutwa mara tatu mpaka akikohoa mzee Yusuph alikua anakohoa vitumbua akaona cha kufia na njaa nini
Hahaha Aseee nimecheka sana
Gily Gru siku na ww ukishika mill 300 ndo siku utakayo staafu na kupata ukimwi hapo hapo 🤣🤣
 
Alipojitangaza kuacha ya dunia wakamsifu sana. Zikasomwa dua, wakawa wanashinda kibarazani kwake, kila mara wanapita kumsaidia kuiimarisha imani asije ibilisi akamrudia, kabla ya chai wameshifika kwake, na wao wapo kwenye ratiba ya chai, wanaendelea kugalagala kibarazani wakisimuliaana khadithi za zama hizo, mchana wapo kwenye ratiba ya chakula cha mchana kama kawaida.

Jamaa akastuka bajeti imemuelemea, maana kwake paligeuzwa kama mgahawa, akanadilisha, wakawa wakija anawalisha kashata za machicha ya nazi, wakaanza kupungua huku wanamlalamikia kuwa ana choyo, haitakiwi mtu aliyeshika dini kuwa na choyo.
Alipoanza kukamatiwa mali zake ili alipe madeni ndiyo wakamkimbia mazima wakidai hayo ndiyo malipo yake kwa kuwalisha Kashata watu wanaoshinda naye kwakekumsaidia kuilinda imani.
Jamaa akauona huuu mbona ni umaandazi sasa, akatafuta mike, gitaa, vinanda akarudi mjini.
Hahaha Extrovert ukishika hela na wewe utakuwa na huu ufala!?
 
Professor J, a.k.a nigger J, the heavy weight MC, mwanalizombe, J wa mitulinga na mengine mengi mengi kaimba nyimbo nyingi sana maarufu.

Miongoni mwa nyimbo alizoimba ni pamoja na;

Zari la mentali
Bongo Dar es Salaam
Chemsha bongo na nyinginezo
Prof Jay ni overrated tu ila ni wa kawaida though ni rapper mzuri. Level yake hiyo watu kama wakina Nikki mbishi na Fid Q walipita kitambo tu.
 
Utamtunzia mke na watoto ?
Watu hawajui kuwa ule ugonjwa ulikomba kila senti aliyokuwanayo mpaka akaanza kutembeza bakuli! Yaani!! Wee acha tuu! Alikuwa anatia huruma! Sasa baada ya kurudi na kusimama kwa miguu yake lazima apambane! Ata kama atapata maswaibu ili mradi anatafuta hela kihalali haina shida! "Be rich or die trying" by 50cent! Ana mke na watoto na yeye music na siasa ndo vilimpa jina ni lazima arudi katika asili yake broh!
 
Back
Top Bottom