Ukweli usemwe: Joseph Haule (Profesa Jay) anahitaji utulivu, hizi pilikapilika za muziki na siasa angeachana nazo

Ukweli usemwe: Joseph Haule (Profesa Jay) anahitaji utulivu, hizi pilikapilika za muziki na siasa angeachana nazo

View attachment 3158050

Kwanza nna declare interest mimi ni shabiki mkubwa wa Professor Jay na kwenye list yangu ya MCs bora wa muda wote nimemuweka nafasi ya pili.

Napenda sana muziki wake hata siasa zake nilikuwa nazipenda.

Ila kuna kitu nakiona hakipo sawa baada ya yeye kurudi kwenye ugonjwa uliomuweka kitandani kwa muda mrefu mpaka kuchungulia kaburi, nilitegemea angetulia na apate shughuli za kumuingizia kipato zisizohitaji mikiki mikiki. Wazo lake la Foundation lilikuwa bora kabisa.

Soma Pia: Joseph Haule 'Prof. Jay: Nitagombea Ubunge Mikumi 2025

Nasikitika kumuona kwenye majukwaa ya muziki akifanya performance na pia kwenye majukwaa ya siasa akifanya mikutano.

Kwa yoyote anayemshauri au kumuunga mkono kurudi kwenye hizi shughuli basi hana nia njema na hampendi anataka kumtumia.

Prof pumzika tunaona unavyo struggle kuwasiliana na watu na kujichanganya bado haupo sawa.

Tunaokupenda tunaomba upumzike. Mungu amekutoa kwenye hali ambayo kuendelea kuishi ni kama muujiza. Pesa zipo huwezi kuwa nazo vile vile kila siku kubali ndio maisha na upumzike.

Natoa ushauri huu kwa kuwa nakukubali.
Usipangie wati namna yao ya kuendesha maisha
 
Sometimes when it comes to money you have to risk your life,ni juzi tu hapa umeona Mike Tyson amepigana na kijana mdogo wa miaka 27,kwa umri wake wa miaka 58 alikuwa anacheza na uhai wake,pamoja na mkewe kumuonya asipigane aliziba masikio,leo hii acc.yake inasoma Tshs Bil.53.....
Kuna video niliona jamaa analia kwenye kona yake, vitasa noma.
 
😂😂😂😂😂😂😂😂 Ila life cycle ya mzee Yusuf inachekesha sana! Yani alipopata 200M akaona na astaafu mziki kabisa kwamba zingemtosha kuendesha maisha yake hadi afe. Too bad alipokea ushauri wa kipumbavu, if he could still hustle angekuwa mara 2 ya pale alipokuwa but he quit and lost the grip.

Sahizi atakuwa anapiga show kwenye mabar ya uchochoroni tu.😁
🤣🤣🤣🤣🤣
 
Sometimes when it comes to money you have to risk your life,ni juzi tu hapa umeona Mike Tyson amepigana na kijana mdogo wa miaka 27,kwa umri wake wa miaka 58 alikuwa anacheza na uhai wake,pamoja na mkewe kumuonya asipigane aliziba masikio,leo hii acc.yake inasoma Tshs Bil.53.....
Eeh maisha ya mwanaume ni kutafuta tu, unazaliwa unatafuta elimu, unatafuta maisha kwa kutafuta hela, unatafuta mali, unatafta mwanamke, unatafta watoto, unatafuta nyumba, unatafuta gari, unatafuta magonjwa ,unatafta kuuguzwa yani we ni kutafuta tu mpaka utapokutana na kifo.
 
Prof Jize bado ana vitu vya Ku offer so aendelee kupambania legacy

Ushauri wako ni mzuri Sana .
Ila pia Kama kuongea Anaweza aendelee kupambania legacy yake.
 
Alipojitangaza kuacha ya dunia wakamsifu sana. Zikasomwa dua, wakawa wanashinda kibarazani kwake, kila mara wanapita kumsaidia kuiimarisha imani asije ibilisi akamrudia, kabla ya chai wameshifika kwake, na wao wapo kwenye ratiba ya chai, wanaendelea kugalagala kibarazani wakisimuliaana khadithi za zama hizo, mchana wapo kwenye ratiba ya chakula cha mchana kama kawaida.

Jamaa akastuka bajeti imemuelemea, maana kwake paligeuzwa kama mgahawa, akanadilisha, wakawa wakija anawalisha kashata za machicha ya nazi, wakaanza kupungua huku wanamlalamikia kuwa ana choyo, haitakiwi mtu aliyeshika dini kuwa na choyo.
Alipoanza kukamatiwa mali zake ili alipe madeni ndiyo wakamkimbia mazima wakidai hayo ndiyo malipo yake kwa kuwalisha Kashata watu wanaoshinda naye kwakekumsaidia kuilinda imani.
Jamaa akauona huuu mbona ni umaandazi sasa, akatafuta mike, gitaa, vinanda akarudi mjini.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣 aisee nimecheka sanaaaa dah kashata za nazi zimemtoa utu mtu
 
Mkisema anatafuta mkate wake na familia yake ina maana huko nyuma na ubunge hakupata fedha za kuishi muda mrefu bila kufanya hizo kazi tena? Anahitaji kupata utulivu muoneeni huruma. Yule si hohehahe kiuchumi mpaka arudi mbilingeni, huko ni kujitaabisha kulingana na hali yake ya kiafya aliyonayo
 
Ni kama unaishi nje ya tz mkuu hivi unaelewa pesa unavyochomoka kama sungura isitoshe kuumwa . The world doesn't stop cause something show up.
 
ha
Ni kama unaishi nje ya tz mkuu hivi unaelewa pesa unavyochomoka kama sungura isitoshe kuumwa . The world doesn't stop cause something show up
Hajawahi kuuguza hata mgonjwa wa malaria huyu ndio maana hajui ni namna gani maladhi yanafilisi,siku 400+ kitandani hajui ni usiku ama mchana anadhania mchezo mchezo tena figo,yeye mwenyewe akienda hospital akipewa bili laki tu ananena kwa lugha kisa hela nyingi ,kalaki tu,ili hali mwenzake ilikuwa inateketea zaidi ya 8M kwa siku
 
Mwache atafute ugari wake,siasa ndo kazi yake.Ila prof dhis time ukipata ubunge jipange ndugu yangu najua unajua nini cha kufanya.
 
Kwa mara ya kwanza tangu nikujue leo ndio umeongea point
 
View attachment 3158050

Kwanza nna declare interest mimi ni shabiki mkubwa wa Professor Jay na kwenye list yangu ya MCs bora wa muda wote nimemuweka nafasi ya pili.

Napenda sana muziki wake hata siasa zake nilikuwa nazipenda.

Ila kuna kitu nakiona hakipo sawa baada ya yeye kurudi kwenye ugonjwa uliomuweka kitandani kwa muda mrefu mpaka kuchungulia kaburi, nilitegemea angetulia na apate shughuli za kumuingizia kipato zisizohitaji mikiki mikiki. Wazo lake la Foundation lilikuwa bora kabisa.

Soma Pia: Joseph Haule 'Prof. Jay: Nitagombea Ubunge Mikumi 2025

Nasikitika kumuona kwenye majukwaa ya muziki akifanya performance na pia kwenye majukwaa ya siasa akifanya mikutano.

Kwa yoyote anayemshauri au kumuunga mkono kurudi kwenye hizi shughuli basi hana nia njema na hampendi anatakangiwa. kumtumia.

Prof pumzika tunaona unavyo struggle kuwasiliana na watu na kujichanganya bado haupo sawa.

Tunaokupenda tunaomba upumzike. Mungu amekutoa kwenye hali ambayo kuendelea kuishi ni kama muujiza. Pesa zipo huwezi kuwa nazo vile vile kila siku kubali ndio maisha na upumzike.

Natoa ushauri huu kwa kuwa nakukubali.
Akamatwe mara moja na kufungiwa ndani takriban miaka 10 au zaidi mpaka afya yake itakapotengemaa.
 
Mungu ndiyo anajua hatima ya kila mtu ,inawezekana ukaona kama Prof yupo dhaifu kwa mtazamo wako kumbe akawa imara kukuzidi wewe unayejiona hupo fit.
 
Back
Top Bottom