Ukweli usemwe: Joseph Haule (Profesa Jay) anahitaji utulivu, hizi pilikapilika za muziki na siasa angeachana nazo

Ukweli usemwe: Joseph Haule (Profesa Jay) anahitaji utulivu, hizi pilikapilika za muziki na siasa angeachana nazo

Ana madaktari wake na wanafamilia waliokuwa naye wakati wote alipougua ,wakamuuguza hadi afya yake ikaimarika. Sidhani kama watu wote hao wameshindwa kumshauri aachane na harakati zake za muziki na siasa~ kwa maelezo yake yeye mwenyewe anaanza upya.

Kutafuta pesa sio kazi rahisi. Mungu amjaalie azidi kuimarika
 
Huyu aliimba wimbo gani maarufu?
Professor J, a.k.a nigger J, the heavy weight MC, mwanalizombe, J wa mitulinga na mengine mengi mengi kaimba nyimbo nyingi sana maarufu.

Miongoni mwa nyimbo alizoimba ni pamoja na;

Zari la mentali
Bongo Dar es Salaam
Chemsha bongo na nyinginezo
 
Mimi sicoment chochote kwenye my mid 30s nimejifunza kutojudge kitu kabla ya kusikiliza pande zote2.... Unaweza kukaa na jay akakueleza Kwa undani na ukasema ni sawa tu.... Au si sawa .... Maadam hatujamsikia ni fungu jema kunyamaza.
 
Kusema eti anafanyia pesa, sikweli!! Hawezi kukosa biashara inayompa kiasi cha kusurvive...

Sema huyu mwamba ni mwanaharakati, kwasasa lazima aonyeshe ukakamavu kusimama na wananchi ambao walimsaidia katika nyakati ngumu....


He is a Strong Man
 
View attachment 3158050

Kwanza nna declare interest mimi ni shabiki mkubwa wa Professor Jay na kwenye list yangu ya MCs bora wa muda wote nimemuweka nafasi ya pili.

Napenda sana muziki wake hata siasa zake nilikuwa nazipenda.

Ila kuna kitu nakiona hakipo sawa baada ya yeye kurudi kwenye ugonjwa uliomuweka kitandani kwa muda mrefu mpaka kuchungulia kaburi, nilitegemea angetulia na apate shughuli za kumuingizia kipato zisizohitaji mikiki mikiki. Wazo lake la Foundation lilikuwa bora kabisa.

Soma Pia: Joseph Haule 'Prof. Jay: Nitagombea Ubunge Mikumi 2025

Nasikitika kumuona kwenye majukwaa ya muziki akifanya performance na pia kwenye majukwaa ya siasa akifanya mikutano.

Kwa yoyote anayemshauri au kumuunga mkono kurudi kwenye hizi shughuli basi hana nia njema na hampendi anataka kumtumia.

Prof pumzika tunaona unavyo struggle kuwasiliana na watu na kujichanganya bado haupo sawa.

Tunaokupenda tunaomba upumzike. Mungu amekutoa kwenye hali ambayo kuendelea kuishi ni kama muujiza. Pesa zipo huwezi kuwa nazo vile vile kila siku kubali ndio maisha na upumzike.

Natoa ushauri huu kwa kuwa nakukubali.
ni kweli kabisa mkuuu!atulie tuuuu!!!

vipi MC wako no moja unamueka nani mkuu?
 
Back
Top Bottom