Ukweli usemwe: Lissu yupo kwenye mission ya kuiua CHADEMA

Badala ya kupigana chama kiwe cha kitaifa bado mnaendekeza regionalism ,badilikeni aisee eti mwamba wa kaskazini?😭😭😭
 
Ngoja tumsubirie Leo ataongea nini
 
Haya maswala hayakutakiwa kufikia hapa yalipofikia ila yamefikia hapa yalipofikia kwa sababu, madudu ya mbowe ndani ya chama kwa vyovyote vile yamefikia hatua yakutovumilika. Mbowe alikuwa ni mtu anayethaminiwa sana na Lisu na amemsaidia sana Lisu hasa wakati amepigwa Risasi, Ila chama cha kinashindwa kwenda mbele kwa sababu ya Ajenda za siri za Mwanyekiti. Anaonekana anakijenga chama kumbe anawala kisogo wenzake. Yote kwa yote najua pamoja na Mbowe kutotaka kuachia madaraka lakini Mbowe ni mtu mwenye akili sana za kisiasa awezi akakiachia chama kipasuke kama vile Cuf.Kwa vyovyote atafanya juu chini kukinusuru chama kwa maana kukijenga chama kingine kama hiki ni kazi kubwa sana. Najua mpaka Lisu kutoka adharani nakujitoa Muhanga kuna mambo mazito sana yapo ndani ya chama ambayo ameyaona hayavumiliki
 
Lissu kaongea facts ambazo ndivyo siasa inapaswa kuwa hasa kiushindana ndani ya vyama na kuisha dhana ya uhuru na haki ya kidemokrasia.

Na Chadema wakishindwa kwenye hili watapoteza tafsiri ya CHADEMA, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo.

Kutangaza nia ni haki na uzalendo wa kiutumishi na kuwa tayari kubeba mzigo wa kutumikia na kuendeleza Chama.

Je, CHADEMA Chama binafsi Cha kabila la wachagga na familia ya Mzee Mtei na Mbowe? Tusubiri tuone

Mara zote nimesema CHADEMA ni chama Cha wachagga na hizo familia mbili. Sitarajii tofauti na hapo

Pang Fung Mi
 
Ukweli ni kwamba Mbowe hana ushawishi kwa mashabiki wa CDM. Sema wanaomzunguka wana hofu na fursa wanayoitumia kuwepo kwake kwenye kiti.
Anachopaswa kukifanya kukinusuru chama na kuilinda heshima yake ni yeye kuamua kutokugombea uenyekiti.
 
Ndani ya futi sita ya chadrama kuna mambo haswaa.. Hadi wajifukie wenyewe baada ya waliokuwa wanawafukia kuwa panga iwe hivyo.
 
Naunga mkono hoja Lissu asipewe friji lake bovu!
Pale mwanaccm kindakindaki anapoipenda Chadema na kuishauri kuwa isikubali Lissu kuwa Mwenyekiti kwa ana friji bovu!
Hakika huu ni upendo wa ajabu sana, hongera mzee Kipara kwa upendo wako!
Kwi kwi kwi!
Hivi nyie CCM mnatuona sisi ndezi sio? Juzi hapa kila siku ooh Mbowe aondoke anaua chama! Amekaa siku nyingi kama mfalme nk. Leo kila mtu huko kwenu kuanzia wajumbe wa KK hadi wafagizi Lumumba na Chamwino hawataki Lissu kwani "ana friji bovu"?
Poleni sana, naona hata kauli yenu "mitano tena" mmesha sahau kama mlivyo sahau kuwa hamna makamu mwenyekiti. Au makamu mwenyekiti ni Steve Magere aka Nyenyere!
 
Lissu hafai kuwa kiongozi wa juu.
1.Hana shukrani
Rais Samia&Mbowe wanajua hili.
2.Hana adabu
JPM aliliona hili...
3.Hawezi kudhibiti
mdomo wake.
Wana CDM mnalijua...
4.Ana kiburi&ujuaji.
Mungu amsaidie!
Hana shukrani? ulitaka amshukuru nani zaidi ya Mungu hapa duniani au akishukuru inasaidia nini taifa?
Hana adabu? amfanyie adabu nani kwa hawa viongozi wa nchi wanao kandamiza demokras na kufanya ufisadi wa wazi?
Audhibiti mdomo ili iweje? Lini kusema ukweli kukawa kuvunja sheria?
Ujuaji ni muhimu kuliko ujinga, yeye sio maccm ambayo yanaweka brain 🧠 kabatini na kuona ujinga ni muhimu kulinda matumbo yao.
Hapa umekosa hoja kabisa na ulipaswa uishi karne iliyopita na sio hii
 
Lissu ni tapeli la kisiasa anapolalamika kuwa anataka uongozi uwe na kikomo wakati huo yeye alipokuwa chawa wa mbowe alipendekeza na kupigia kura ya kunyofoa kipengele cha ukomo kwenye katiba ili Mbowe atawale milele leo hii nae anataka kuingia kwa katiba ile ile......Nimesema Mbowe aendelee ni sababu mpaka leo Chadema ipo pale ilipo kwa hekima,busara na uvumilivu wa kamanda mbowe zaidi ya hapo ingekuwa kama Nccr tu!
 
Kwahiyo kutangaza nia ni mission ya kukiua chama??

Unataka Mbowe asipate ushindani na awe mwenyekiti mpaka afe?

HUNA AKILI MASTA
 
Deep state my foot. acheni kuwapa vichwa hao watumishi wa CCM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…