Ukweli usemwe: Lissu yupo kwenye mission ya kuiua CHADEMA

Ukweli usemwe: Lissu yupo kwenye mission ya kuiua CHADEMA

Tundu Lissu ameamua kuia CHADEMA kwa mikono yake mwenyewe.

Anapita kila kona kukishambulia chama chake hadharani. Ameunda mtandao kukishambulia chama chake.

Anasema chama chake kinanuka rushwa. Anasema chama chake hakina mipango ya kueleweka ili kuiondoa CCM madarakani.

Anasema chama chake kimekosa kiongozi mwenye quality ya kuongoza mapambano na CCM.

Anakosoa process ya maridhiano ambayo alishiriki kuiratibu.

Na mengine mengi. Anasema haya hadharani wakati anajua fika yeye ni makamu mwenyekiti anaeweza kutumia mifumo ya chama kufikisha malalamiko yake.

Lissu anaisaliti CHADEMA either unaamini au auamini Lissu ni mwanasiasa anajua anachokifanya. Lissu ni kirusi yupo kazini.

Alisema alifatwa na Abdul waonane na alipelekewa pesa akazikataa . Je hizo pesa kazi yake ilikuwa nini? Tutajuaje kama Abdul hakurudi na dau zito zaidi ambalo ndio linamsukuma kukishambulia chama chake hadharani? Lissu yupo kazini.

Nashauri kabla hajaleta madhara zaidi chama chake kimchukulie hatua za kinidhamu, hii anayoifanya sio demokrasia ni fujo.

Heshimu kiongozi wako mfichie msitili madhaifu yake kama anavyostri ya kwako. Nani asiyejua wewe ni mwezi mchanga?

CHADEMA hata kama inatakiwa ifanye mabadiliko ya mwenyekiti Lissu hafai tafuteni watu wenye koromeo tafute viongozi sio wafanya vurugu.

CHADEMA ni chama kikubwa any day inaweza kuchukua nchi lakini kwa viongozi kama Lissu hata deep state haiwezi ruhusu.
Lissu ndio mwanasiasa mwenye mvuto chadema,wakati huu chadema inamuhitaji Lissu kuliko wakati wowote,Lissu ana wafuasi wengi wa wapenda mabadiliko kuliko cdm hii iliyolala usingizi na kusubiri fikra za mwenyekiti pekee.
 
Alisema alifatwa na Abdul waonane na alipelekewa pesa akazikataa . Je hizo pesa kazi yake ilikuwa nini? Tutajuaje kama Abdul hakurudi na dau zito zaidi ambalo ndio linamsukuma kukishambulia chama chake hadharani? Lissu yupo kazini.

Yericko Nyerere ebu ingia chimbo utupatie taarifa kama Abdul alimtembezea miamala kama ulivyochunguza Mialama kutoka Ujerumani kwenda kwa nusu kipenyo jepesi tozi bweka.
 
Lissu ni tapeli la kisiasa anapolalamika kuwa anataka uongozi uwe na kikomo wakati huo yeye alipokuwa chawa wa mbowe alipendekeza na kupigia kura ya kunyofoa kipengele cha ukomo kwenye katiba ili Mbowe atawale milele leo hii nae anataka kuingia kwa katiba ile ile......Nimesema Mbowe aendelee ni sababu mpaka leo Chadema ipo pale ilipo kwa hekima,busara na uvumilivu wa kamanda mbowe zaidi ya hapo ingekuwa kama Nccr tu!
Aliuzwa swali hilo akakwepa wakati anajua bila Mbowe, Chadema isingekuwepo. Hafai wamuachie tu aende anakotaka kwenda.
 
Amechangiwa kununua gari akauchuna
Huyu anaangalia maslahi yake tu akidhani atakuwa mwenyekiti ili ale mali pia
Sijawahi kuwaamini wanasiasa kabisa na hata huyu hana uzalendo bali njaa tu
Wawe chama tawala wala upinzani wote ni sawa tu
Kila mmoja anaangalia tumbo lake tu
 
Back
Top Bottom