Ukweli usemwe: P Funk ndio mtu mnyonyaji zaidi kuwahi tokea kwenye historia ya Bongofleva

Ukweli usemwe: P Funk ndio mtu mnyonyaji zaidi kuwahi tokea kwenye historia ya Bongofleva

Wakuu kuna wakati ukweli lazima usemwe. Mambo ya kusema mtu aheshimiwe kwa kuwa alikuwa anatengeneza beats nzuri hizo ni heshima za uoga.

P Funk ambaye kiukweli zaidi ya kufanya production ya muziki na kupokea malipo hana jingine kubwa alilolifanyia bongofleva.

Kwa wasiofahamu wasanii wote waliokuwa chini ya bongo records hawana nyimbo au album wanazomiliki vyote anamiliki P Funk.

Ngwea amekufa maskini huku muziki wake unamilikiwa na P Funk mpaka leo anakula hela ya Ngwea.

Ukiona wimbo wa Juma Nature au Feruzi kwenye YouTube, Boomplay au digital platform yoyote usidhani ukisapoti unamsaidia msanii hiyo ni pesa ya Majani. Leo hii ikitokea bahati mbaya Juma Nature hatupo nae watoto wake watarithi nothing utajiri wake wa nyimbo ni mali ya watoto wa Majani kina Paula.

Huyu P Funk aliyekuwa anawapiga ngumi na mitama watoto wa kimaskini wakienda kuomba msaada wa kurekodi nyimbo zao.

Kumbuka pale bongo records kwenye utengenezaji wa beats waliusika watu wengi zeze ilitengenezwa na bizimani ila achukui hata sh 10, beat ya mikasi alitengeneza prof ludigo ila achukui hata sh 10 kina Marlon linje walikuwa wanapiga vinanda na vyombo vingine kwenye kutengeneza instrumental za wasanii haki zao za ubunifu anachukua nani kama sio mnyonyaji p Funk?

P Funk tunamuheshimu kwa kutengeneza beats ila zaidi ya production kaufanyia nini huu muziki?
P Funk uwa wakiitwa wasanii walipwe yeye anaenda kuchukua malipo kama nani? Kina Daz Baba wamekuwa vituko mtaani hela zao kwa nini unakula wewe PFunk?

Hii thread haiusiani na tukio lolote bali ukweli usiozungumzwa.
Sikia mi pia ni mdau wa muziki especially wa kizazi kipya nishawasimamia wasanii halikadhalik kujitolea pesa zang mfukon ku support msanii na hata mchakato was Tuzo za TMA 2020 nilihusika, p funk na bongo record zili conquer muziki was bongo late 90's Kuja early 20's kipindi hcho studio chache na wasanii wengi wakina nigger Jay,afande sele, solo thank walifanyaje muziki km passion kutok moyon kutokan na vipaji vyao, pia mfumo uliwalazimu yaan tangu zaman pata umaarufu kafanye shoo ndo ule daz mwalimu, daz maskin jeur, dullysykes walifanyaje shoo kuishi inamaan hakukuwa na mambo ya digital marketing Wala mirabaha inamaan hata producer mwenyee alitegemea pesa ya umeme kutok kmwa wasanii ndo aishi,
P funk angekuw Tajiri km alidhulum pesa ya juma nature, Albert mangwea, Na hakuwa kwny mfumo wowote Zaid ya composer mambo ya digital yamekuja hivi karibuni na ndomaan serikali umevumbua na mirabaha
Hao waliokufa maskini wamewaacha wasanii na producers wakongwe maskini, ndomaan diamond,ay walipamban kupeleka muziki international ukitambulika na tutapata pesa
 
Wakati hao wasanii wanasaini mkataba hawakuona vigezo na masharti?
Kama mkataba uliandikwa kijanja hakuna namna unaweza kuona vigezo na masharti
Walimu na usomi wao wanapigwa kila siku na bayport , terms and conditions
 
Mleta mada unasumbuliwa na nini? Siku zote Producer hua ndio mmiliki halali wa kazi ya sana. Hilo lipo worldwide ndugu, kama unataka kazi yako uimiliki mwenyewe anzisha kampuni mwenyewe utengeneze kazi zako.

Ila suala la kunyang'nya watu hela zao wanazopata kwenye endorsement wanazofanya ambazo zinatokana na nje ya Company ni utapeli.
 
Wakuu kuna wakati ukweli lazima usemwe. Mambo ya kusema mtu aheshimiwe kwa kuwa alikuwa anatengeneza beats nzuri hizo ni heshima za uoga.

P Funk ambaye kiukweli zaidi ya kufanya production ya muziki na kupokea malipo hana jingine kubwa alilolifanyia bongofleva.

Kwa wasiofahamu wasanii wote waliokuwa chini ya bongo records hawana nyimbo au album wanazomiliki vyote anamiliki P Funk.

Ngwea amekufa maskini huku muziki wake unamilikiwa na P Funk mpaka leo anakula hela ya Ngwea.

Ukiona wimbo wa Juma Nature au Feruzi kwenye YouTube, Boomplay au digital platform yoyote usidhani ukisapoti unamsaidia msanii hiyo ni pesa ya Majani. Leo hii ikitokea bahati mbaya Juma Nature hatupo nae watoto wake watarithi nothing utajiri wake wa nyimbo ni mali ya watoto wa Majani kina Paula.

Huyu P Funk aliyekuwa anawapiga ngumi na mitama watoto wa kimaskini wakienda kuomba msaada wa kurekodi nyimbo zao.

Kumbuka pale bongo records kwenye utengenezaji wa beats waliusika watu wengi zeze ilitengenezwa na bizimani ila achukui hata sh 10, beat ya mikasi alitengeneza prof ludigo ila achukui hata sh 10 kina Marlon linje walikuwa wanapiga vinanda na vyombo vingine kwenye kutengeneza instrumental za wasanii haki zao za ubunifu anachukua nani kama sio mnyonyaji p Funk?

P Funk tunamuheshimu kwa kutengeneza beats ila zaidi ya production kaufanyia nini huu muziki?
P Funk uwa wakiitwa wasanii walipwe yeye anaenda kuchukua malipo kama nani? Kina Daz Baba wamekuwa vituko mtaani hela zao kwa nini unakula wewe PFunk?

Hii thread haiusiani na tukio lolote bali ukweli usiozungumzwa.
Sawa Babu tale
 
Kisheria kuna ile haki inaitwa exclusive right, kwamba kama msanii ameuza mpaka exclusive right basi anakuwa hana haki tena na hiyo kazi.

Mfano, nasikia Darassa aliuza album yake boomplay kwa milioni 140 hivi (na exclusive right), baadae wimbo wake wa I Like It ukatumika kwenye movie na boomplay wakalipwa milioni 600, akaanza kujilaumu.
Darassa anajilaumu vipi sasa?

Na kwenye hiyo album kampiga dogo aliyefanya mixing and mastering young keys morento a.k.a themixkiller hakumlipa hafi anaenda kulalamika insta na clouds
 
Unajua nini Ndugu Mdau!? "Haki Haiombwi" Bali "Inapiganiwa". Kama Prof. Jay anaamini ana Haki yake imedhulumiwa, hakuna aliyemkataza kuipigania. Majani alisafiri mpaka Uganda kuipigania haki yake.
Professor J , alishasema yeye sio kwamba alikuwa anataka hizo hela bali, huko bungeni kuna watu walikuwa wanaropoka kuwa serikali imemsaidia prof kupata stahiki za huo wimbo! Ndipo prof aka clarify kuwa yeye hakulipwa ,ili asije daiwa kodi kwa kitu ambacho hajapokea malipo, maana kipindi kile wapinzani bungeni huko walikuwa kwenye vita na serikali ile ya awamu ya 5... !,
 
Li jizi na nyonyaji likubwa kabisa kwa kazi za wasanii wa kiTz lipo limetulia tuu yaani lina wang’ang”ania wasanii kama luba, wasanii walio fanikiwa kutoka kwenye lebo yake walitoka kwa mbinde kweli kweli, limejaxa ma chawa kila kona adi humu JF…. ila siku zake zinahesabika, pumbavuu zake yeye, mama yake, wake zake na machawa wake wootee!
 
Wewe kiumbe mwenye chuki wivu na roho mbaya kwa kila binadamu aliyefanikiwa tunaongea tunayoyafaamu P Funk ana miliki rights za nyimbo za wasanii wote waliokuwa bongo records. Unaita watu machawa alafu unawashwa unajisogeza.

Mama yake Ngwea alifatilia hela za mwanae akaambiwa zipo kwa p funk akaenda kupewa kama msaada. Tena mil 1 baada ya hapo hela za marehemu anakula p funk bila hata aibu wala utu.

Hizo beats zenyewe alikuwa anatengeneza peke yake? Kinanda chenyewe hajui kupiga, anamgawia nani hela za ubunifu mbona anakula zote peke yake mnyonyaji mkubwa yule?
Acha uongo Familia ya ngwair walikuwa hawjaui hata Kama pesa zipo alipelekewa mama yake Milion. 4 hakuwa anajua Kama kuna pesa acha Upuuzi na uongo Kama hajui mambo kaaa Kimya na Alishangaa Nina clip hiyo ntaitafta
 
Je commision za Mikka Mwamba anachukua nani?
Mikka hao hao kina Majani na wenzake walimfsnyia figisu jamaa akakosa vibali vya kazi na kuondoshwa nchini, sawa na Produsa Dunga. Yaani uwepo wao ukawa ni kama tishio kwa maprodusa wazawa, zikafanyika figisu za muziki Mikka Mwamba akaondoka kurudi kwao. Wasanii wakimtaka wamfuate huko, ila jamaa ni kama alipenda sana kuishi Tanzania. Alipokuja 2017 au 2018 kama sikosei, interview yake na Millard ayo, unaona kabisa jamaa hakupenda kuondoka. Commission zake zitakuwa zinachukuliwa na FM
 
Sasa kama ni vibali si angetafuta vibali.

Sababu zako hazina mashiko
 
Back
Top Bottom