Ukweli usemwe: P Funk ndio mtu mnyonyaji zaidi kuwahi tokea kwenye historia ya Bongofleva

Vipi kuhusu Said Commorien pia ni same case?
 
Author wa thread hamjui P.Funk ktk muziki vizuri mfano anasema hajafanyia muziki chochote zaidi ya kutengeneza beat na kuchukua sifa za wenzake, muhimu ajue jamaa ni miongoni mwa pioneers waliousukuma huu muziki katika radios na kuandaa matamasha ya kihistoria kuzindua album mfano Ugali ya Juma Nature....
Mtoa mada anasema P.Funk anamiliki album za wasanii, hili sio kweli P.Funk anamiliki beats...
Co producers kulipwa au kutolipwa mirabaha inategemea, je alikubaliana na one time payment, kumbuka wakati huo hakukuwa na urasmi wala miundombinu ya kufatilia ziada za malipo endelevu.
Kuhusu royalties, mtoa mada ajipe kazi kujua CMEA(Copyright Music East Africa) P.Funk alikuwa miongoni mwa watu wanaopigania hilo japo walifeli kwa sababu nyingi zikiwa nje ya uwezo wao.
Mtoa mada huenda akawa anashindwa kutofautisha mapenzi yake na WCB na jambo la kinyonyaji linalofanywa, ukweli ni kuwa wanawanyonya vijana wale,kwa kisingizio cha kuwasaidia, kama P.Funk alifanya hivyo haimzuii kusema ukweli...
Mwisho serikali imeshindwa kuandaa mifumo mizuri ya kisheria na kucha nafasi ya yote haya kutokea.
 
Acheni uzushi. Majani ana influence gani mpaka azuie watu wasipate vibali? Usikute hao kina Miika walikuwa wanafanya kazi kimagumashi bila vibali ndio maana wakazuiwa kufanya kazi. Huyo Dunga nishamuona anazurula mitaani na demu wake mzungu wala hakufukuzwa labda alikosa tu kibali cha kufanya kazi.
 
P Funk anakula mpaka hela za marehemu Ngwea. Yeye p Funk anajinadi kama anapaza sauti juu ya haki za wasanii vipi mbona yeye anawanyonya mpaka leo?

Haki za ubunifu kwenye midundo mbona anawatapeli wenzie?

Tukemee unyonyaji wa P Funk
uleta ushahidi
 
Hawa jamaa wamerukwa na akili sio bure. Eti P Funk ana influence watu wanyimwe vibali! Hiyo influence kaitoa wapi!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…