Ukweli usemwe: P Funk ndio mtu mnyonyaji zaidi kuwahi tokea kwenye historia ya Bongofleva

Juma lokole naona umejiwahi eti "Hii thd haihusiani na tukio lolote"
Naona chawa zimemwagwa kwenye social media kumshambulia Pfunk,unaweka lawama bila ushahidi tukuaminije?
Wewe una ushaidi kwenye kitu gani zaidi ya wivu na chuki za Kiswahili
 
Wasafi washenzi tu
 
Nafikiri waliingia mgogoro na Prof. Jay baada ya P. Funk kuchukua hela kwa kampuni ya movie iliyotumia beat ya bombo clat ambapo original ni beat ya nikusaidiaje. Profesa alilalamika kuwa hakupewa hata senti
 
Isipokuwa wasanii wachache waliokuwa wanalipia kazi zao, mfano Mike Mwakatundu aka Mike T ' Mike Tee' mnyalu - huyu alilipa album zake wakati wa kurekodi - anamiliki ngoma zake yeye mwenyewe

Wasanii wengine waliponzwa na umaskini wao. Walirekodiwa bure na kuambiwa watakua kwenye label kumbe ndio wanasainishwa mikataba ya ki- chifu mangungo
 
Nafikiri waliingia mgogoro na Prof. Jay baada ya P. Funk kuchukua hela kwa kampuni ya movie iliyotumia beat ya bombo clat ambapo original ni beat ya nikusaidiaje. Profesa alilalamika kuwa hakupewa hata senti
Ndio alichukua mabilioni yote mnyonyaji yule
 
Lakini pia Majani alitakiwa afanye kazi yote ile halafu asiwe na chochote cha kupata mbeleni? Mbona angekuwa ndiyo ananyonywa!
Majani anachofanya ni kama kile P Diddy amekifanya kwa wasanii wake, wanamfanya awe rich forever, ndio biashara ya muziki ipo hivyo duniani, ni ya kinyonyaji.

Kilichotakiwa kufanyika awali ilikuwa ni kugawana asilimia za mapato ya wimbo. Producer apate asilimia 50 na mwimbaji apate asilimia 50 kwa kuwa combination yao ndio imetoa wimbo (muziki). Sasa kinachozungumzwa hapa ni kuwa P Funk anamiliki 100% yaani mpaka maneno yaliyoimbwa kwenye nyimbo yeye ndio anayamiliki, hakuna cha mtunzi wala muimbaji.
 
Lakini pia Majani alitakiwa afanye kazi yote ile halafu asiwe na chochote cha kupata mbeleni? Mbona angekuwa ndiyo ananyonywa!
Kwa hiyo yeye kuwanyonya wenzie ndio sawa?
Kazi walizofanya kina Jay Moe, Nature, Feruzi, Mangwea etc unaona ni ndogo wasipate chochote kwenye ubunifu wao. Yeye kama ni producer mzuri angekuwa anatoa album za beats peke yake aone kama kuna mtu angenunua
 
Beef
 
Baba levo akiwa kwenye Harusi ya wale wahuni Ile juzi aliongea akamaliza kila kitu , na akatoa sababu za Diamond kuwanyonga 60/40.....!!! Pfunk na yeye atoe sababu za kuwanyonga wenzake .... Alaf hapa duniani chance ya mtu kukurudishia fadhila baada ya kumsaidia ratio yake ni 1/10 ..... Ni kumnyonga tuu akifanikiwa usitegemee atarudi
 

Hebu twende polepole kwani hio mikataba mnasainishwa kwa shuruti au? Ujue tatizo bongo wasanii wengi nyie ni mamburula mlikimbia shule alafu hamtaki kuajir wasomi kutwa kuja kulalamika kwa upuuzi mliosaini wenyewe.
 
Shida Shida Shida. Atokee msanii au wasanii watunge wimbo kuhusu shida.

Shida huteka maarifa.
 
Music production ina mambo mengi Sana aisee. Beats siku zote ni ubunifu wa producer. Kwa hiyo hakuna tatizo akila faida ya ubunifu wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…