Ni movie.
Profesa J alitoa wimbo wa nikusaidiaje, Chameleone akatamani beat akalichukua na kufanya wimbo wake wa bombo clat. Profesa akawa na mgogoro na Chameleone, wakayasolve kwa kufanya wimbo wa Ndivyo Sivyo, wakamalizana kisanii.
Kina Lupita Nyongo wakatengeneza filamu yao na katika soundtracks zilizotumika wakatumia wimbo wa Bombo Clat wa Chameleone Jose, wakamlipa bwana Chameleone. P Funk kujua akamfuata Chameleone amtoe mpunga, Chameleone akampa jamaa USD 4,000 kumbe yeye (Chameleone) amelipwa USD 50,000. P Funk akawafuata Kampuni husika ya movie na kutaka kuwashtaki na hapo wenye kampuni wakampa USD 100,000 kama sikosei na hapo ndio Profesa J akajua kuwa jamaa amekula hela na yeye J hajapata kitu, ingawa alilipia beat husika, hivyo kustahili mapato yatokanayo na beat. Na ndiyo sababu kwa Chameleone mlalamikaji alikuwa ni Jay na sio P Funk