Ukweli usemwe: P Funk ndio mtu mnyonyaji zaidi kuwahi tokea kwenye historia ya Bongofleva

Ukweli usemwe: P Funk ndio mtu mnyonyaji zaidi kuwahi tokea kwenye historia ya Bongofleva

Lete ushahidi kuwa Bizman kalalamika kudhulumiwa au co_producers (hao akina Soggy , Lamar..) unaodai hapa kudhulumiwa.
Soggy hata juzi kama miezi miwili imepita alikuwa anaongea kuwa waliingia mgogoro na P Funk baada ya ngoma ya Darubini Kali ya Afande Sele, beat aliifanya Soggy ila credit hakupewa na vitu kama hivyo.
 
Mchezo ulikuwa hivi. Chamilion alifuatwa kwa kuwa ulitumika wimbo aliouimba yeye. Ila yeye akafanya uhuni wa kutosema ukweli juu ya nani hasa alietengeneza hiyo beat. Na ndiyo maana P Funk ilimuuma sana hii kwani binafsi yeye anafahamu sheria. Kiasi Cha kuamua kwenda Uganda kupigania haki yake.
hapo ndo nasema bado kuna shidaa maana prof j alichomiliki ni maneno tu au??
 
Wakati hao wasanii wanasaini mkataba hawakuona vigezo na masharti?
ignorance of law can't be used as a defence.

vipi kama wengi wao walikuwa hawana uelewa wa sheria za kusimamia haki zao?.

kumbuka akina nature wakati ule walikuwa bado wadogo na wengine kama hao akina daz baba ndio kwanza walikuwa wanahaingaika na elimu ya sekondari.

jaribu kuvaa viatu vyao.
 
noma sana label hizii ukiwa hujatoka ndo unaona zina msaada ila ukishahit ukaanza kuingiza mawe ndo unajua unapigwaaa
Ila wasanii nao wanatakiwa wajue wakishakuwa kwenye label ni kama waajiriwa wengine hawawezi kwenda 50/50 na boss wako na hii ni duniani kote
Mfanyakazi umeambiwa mshahara wako utakuwa 200k baada ya kuanza kazi unagundua ofisi inaingiza faida bil unaanza malalamiko nyongeza ya mshahara hii sio sawa
 
Wenyewe wataalamu wa production wanakuambia msanii anacholipia ni studio time ila "haki ya ubunifu" inabaki kwa producer. Msanii anaweza kumruhusu msanii mwingine atumie mashairi yake ila sio beat ya wimbo huo bila producer kuhusishwa.
Sheria ya haki miliki inasema mbunifu wa sanaa anapata umiliki wa 100% kwa kazi yake aliyobuni, na hapa ndipo changamoto inapojitokeza.

Produsa anachobuni ni beat kwa hiyo anasema kuwa haiuzi ile beat bali anaikodisha tu kwa msanii, na hivyo anaweza kuikodisha kwa mwingine na mwingine na mwingine bila kuomba ruhusa kwa msanii wa kwanza. Ni kama muuza kitabu cha riwaya, anakiuza kwq wasomaji wengi bila kuomba ruhusa kwa wasomaji walionunua mwanzoni kitabu chake

Wakati huo, msanii wa kwanza anasema kuwa ameweka maneno kwenye beat na hivyo kuipa thamani, kazi iliyotoka mwishoni sio beat bali ni muungano wa beat na maneno. Ukimpa beat mtu mwingine, yeye msanii wa kwanza kazi yake inaathirika kimauzo nk, kwa hiyo anasema hauwezi kuiuza bila yeye kufaidika au kutoa ridhaa

Hapo ndipo penye mgogoro
 
Ila wasanii nao wanatakiwa wajue wakishakuwa kwenye label ni kama waajiriwa wengine hawawezi kwenda 50/50 na boss wako na hii ni duniani kote
Mfanyakazi umeambiwa mshahara wako utakuwa 200k baada ya kuanza kazi unagundua ofisi inaingiza faida bil unaanza malalamiko nyongeza ya mshahara hii sio sawa
yaah POINT KUBWA SANA HII.. kiukweli ukienda kihaki hata serikali inanyonya sana wafanyakazii.. hizi private ndo balaa ukiandikiwa mshahara laki 5 ukija kuangalia mauzo ya siku inaingia mil 10 unapataa motoo 😀 😀 😀 😀 unaweza acha kazi yani ila ndio CAPITALISM.
 
hapo ndo nasema bado kuna shidaa maana prof j alichomiliki ni maneno tu au??
Anacholalamika Jay ni kuwa uuzwaji wa beat kwa msanii mwingine unaathiri mapato yake. Mfano hiyo nikusaidiaje huenda ndiyo ingetumika kwenye movie badala ya bombo clat - kwa hiyo Jay angepata mapato badala ya Chameleone

Kwamba, msanii akishatumia beat basi anakuwa ni mmiliki mwenza na produsa.
 
yaah POINT KUBWA SANA HII.. kiukweli ukienda kihaki hata serikali inanyonya sana wafanyakazii.. hizi private ndo balaa ukiandikiwa mshahara laki 5 ukija kuangalia mauzo ya siku inaingia mil 10 unapataa motoo 😀 😀 😀 😀 unaweza acha kazi yani ila ndio CAPITALISM.
Inaitwa tamaa.😃😃

Wewe umeona kabisa kulipwa laki 2 inakulipa, halafu unaanza kuangalia kinachozalishwa na kuona unadhulumiwa, unadhulumika vipi wakati mshahara umetaja mwenyewe na ukaridhika nao?? Hizo ni tamaa
 
Hivi mkuu naomba unieleweshe, ina maana ukitoka WCB hata ukiwalipa bado nyimbo zinabaki kuwa za kwao?
Kila kona kuna unyonyaji ila mimi kinachonichekesha ni mashabiki wa WCB kutetea yale wanayofanya wcb wakati hao hao walikuwa wanaponda clouds kwa mambo hayo hayo.

Huwezi kupatana vizuri ukiwa na njaa na hawa wasanii uwa wakiwa hawajatoka wana sign mikataba wakiwa wanawaza kuwa na majina na kumiliki magari, wakishapata hivyo na kugundua pesa wanayotengeneza na wanachoambulia ni mbingu na mafuta, basi hapo ndipo wanachanganyikiwa.

Kuhusu kupata pesa ni kweli walipata sana sema walikuwa wanaishi lifestyle flani la movie na usela mavi
Wazee mbna mnaendeleza chuki sana na WCB, wapi wameandika ukilipa bado nyimbo zinakuwa za kwao? Aisee watu mnaongeza chumvi Sana , Harmonize accnt zote aliachiwa unataka kunambia , nyimbo zote alizoimba WCB pesa hapati , inaingia anatoa anapeleka WCB ? Maana ya kuvunja mkataba na kulipa ni nini? Acheni hzo , Watanzania fanyeni kazi , hamna mtu wa kukupambania bure , hata kumuabudu Mungu ni costfull sembuse mtu akushike mkono
 
Sheria ya haki miliki inasema mbunifu wa sanaa anapata umiliki wa 100% kwa kazi yake aliyobuni, na hapa ndipo changamoto inapojitokeza.

Produsa anachobuni ni beat kwa hiyo anasema kuwa haiuzi ile beat bali anaikodisha tu kwa msanii, na hivyo anaweza kuikodisha kwa mwingine na mwingine na mwingine bila kuomba ruhusa kwa msanii wa kwanza. Ni kama muuza kitabu cha riwaya, anakiuza kwq wasomaji wengi bila kuomba ruhusa kwa wasomaji walionunua mwanzoni kitabu chake

Wakati huo, msanii wa kwanza anasema kuwa ameweka maneno kwenye beat na hivyo kuipa thamani, kazi iliyotoka mwishoni sio beat bali ni muungano wa beat na maneno. Ukimpa beat mtu mwingine, yeye msanii wa kwanza kazi yake inaathirika kimauzo nk, kwa hiyo anasema hauwezi kuiuza bila yeye kufaidika au kutoa ridhaa

Hapo ndipo penye mgogoro
Mgogoro upo sababu sheria inazingua umiliki inabdi uwekwe kwa namna ya kuwa PRODUCER anaweza kuuza beat pia iwe ya msaniii kwani mbona MAGARI YANAUZWA na ukinunua linakuwa lako why not BEATS???
 
Hivyo ndivyo P. Funk anavyosema na kuuaminisha umma. Anasema kuw msanii hanunui beat ya produsa bali analipia muda wa studio, beat inakuwa mali ya produsa.

Sasa ili uitwe wimbo, maana yake kuna vocals na beat, kwa pamoja ndio vinafanya uitwe wimbo. Kuna msikikizaji atapenda mdundo na kununua huo wimbo, kuna mwingine atapenda maneno na kununua huo wimbo, ni ngumu kujua mtu anaponunua wimbo anakuwa amevutiwa na mdundo au vocals (maneno) au vyote. Ndio maana mgao huenda kwa wahusika wote wa wimbo, waandishi, waandaaji, waimbaji nk

Hii ishu ya Nikusaidiaje, Jay ndie aliyepambana na Chameleone, tafsiri ni kwamba, P Funk alikuwa ameuza beat yake na akaona ni sawa kwa Jay kulalamika, baadae akamzunguka Jay na kuchukua mpunga kwa wamarekani, ndipo hapo mtafaruku ulipoibuka
Hili suala hata Master Jay mwenyewe kashalizungumza Sana tu. Kumbuka pia Kuna wasanii wanakwenda kushinda studio wakipitia ma_beat ambayo ma_producer wanakuwa wameyatengeneza ila hayajatumika bado na wanawaka nayo na hapo hapo wanapata idea ya wimbo .

Ila Yote kwa yote, CoSoTa ndiye msimamizi wa haki za Sanaa na ubunifu, mpaka kufikia kumpa P Funk haki yake ni wazi wanajua sheria, otherwise Prof. Jay asingekubali kudhulumiwa.
 
Anacholalamika Jay ni kuwa uuzwaji wa beat kwa msanii mwingine unaathiri mapato yake. Mfano hiyo nikusaidiaje huenda ndiyo ingetumika kwenye movie badala ya bombo clat - kwa hiyo Jay angepata mapato badala ya Chameleone

Kwamba, msanii akishatumia beat basi anakuwa ni mmiliki mwenza na produsa.
daah bhasi noma sana maana chameleo asingedanganya helaa zote angepewa majani... shida hii
 
Hili suala hata Master Jay mwenyewe kashalizungumza Sana tu. Kumbuka pia Kuna wasanii wanakwenda kushinda studio wakipitia ma_beat ambayo ma_producer wanakuwa wameyatengeneza ila hayajatumika bado na wanawaka nayo na hapo hapo wanapata idea ya wimbo .

Ila Yote kwa yote, CoSoTa ndiye msimamizi wa haki za Sanaa na ubunifu, mpaka kufikia kumpa P Funk haki yake ni wazi wanajua sheria, otherwise Prof. Jay asingekubali kudhulumiwa.
Cosota hawajui kitu kabisa. Ni wasomi wanaoajiriwa kwa elimu ya vyeti tu ila hawajui vitu kimtaa.

Walichoenda kufanya ni kuthibitisha kuwa kazi ilisajiliwa cosota hicho tu ndicho walichofanya. Kumbuka wenye movie hawataki milolongo na makesi kesi kwa hiyo wakatoa mpunga kama ambavyo walimtoa Chameleone kiholela, hata Profesa Jay huenda angekomaa nao naye wangemtoa pia. Ila Jay alimind kuwa P Funk alimzunguka, hakumshirikisha na hakumtoa hata baada ya kulipwa
 
Wakuu kuna wakati ukweli lazima usemwe. Mambo ya kusema mtu aheshimiwe kwa kuwa alikuwa anatengeneza beats nzuri hizo ni heshima za uoga.

P Funk ambaye kiukweli zaidi ya kufanya production ya muziki na kupokea malipo hana jingine kubwa alilolifanyia bongofleva.

Kwa wasiofahamu wasanii wote waliokuwa chini ya bongo records hawana nyimbo au album wanazomiliki vyote anamiliki P Funk.

Ngwea amekufa maskini huku muziki wake unamilikiwa na P Funk mpaka leo anakula hela ya Ngwea.

Ukiona wimbo wa Juma Nature au Feruzi kwenye YouTube, Boomplay au digital platform yoyote usidhani ukisapoti unamsaidia msanii hiyo ni pesa ya Majani. Leo hii ikitokea bahati mbaya Juma Nature hatupo nae watoto wake watarithi nothing utajiri wake wa nyimbo ni mali ya watoto wa Majani kina Paula.

Huyu P Funk aliyekuwa anawapiga ngumi na mitama watoto wa kimaskini wakienda kuomba msaada wa kurekodi nyimbo zao.

Kumbuka pale bongo records kwenye utengenezaji wa beats waliusika watu wengi zeze ilitengenezwa na bizimani ila achukui hata sh 10, beat ya mikasi alitengeneza prof ludigo ila achukui hata sh 10 kina Marlon linje walikuwa wanapiga vinanda na vyombo vingine kwenye kutengeneza instrumental za wasanii haki zao za ubunifu anachukua nani kama sio mnyonyaji p Funk?

P Funk tunamuheshimu kwa kutengeneza beats ila zaidi ya production kaufanyia nini huu muziki?
P Funk uwa wakiitwa wasanii walipwe yeye anaenda kuchukua malipo kama nani? Kina Daz Baba wamekuwa vituko mtaani hela zao kwa nini unakula wewe PFunk?

Hii thread haiusiani na tukio lolote bali ukweli usiozungumzwa
Sikiliza interview za wasanii wa zamani mfano Ferouz, anasema P. Funk aliwasaidia mawazo na kuwapeleka mpaka kuuuza albam kwa mdosi, maana walikuwa hawajui waanzie wap baada ya hapo wakawa wanaenda wenyewe
 
Cosota hawajui kitu kabisa. Ni wasomi wanaoajiriwa kwa elimu ya vyeti tu ila hawajui vitu kimtaa.

Walichoenda kufanya ni kuthibitisha kuwa kazi ilisajiliwa cosota hicho tu ndicho walichofanya. Kumbuka wenye movie hawataki milolongo na makesi kesi kwa hiyo wakatoa mpunga kama ambavyo walimtoa Chameleone kiholela, hata Profesa Jay huenda angekomaa nao naye wangemtoa pia. Ila Jay alimind kuwa P Funk alimzunguka, hakumshirikisha na hakumtoa hata baada ya kulipwa
p funk alikosa utuu aiseee angemgawia mwana hata kidogooo... nadhani hii ndo inamfanya DIAMOND AWE BORAAA.. japo nae anawapiga wasanii wake ukilinganisha hata na kina MKUBWA FELA... ndo maana diamond akaona aajiri mamenegar sio wao ndo wamtawalee... yamoto band mkubw amepigaa za kichwa hawana hamu...
 
Mgogoro upo sababu sheria inazingua umiliki inabdi uwekwe kwa namna ya kuwa PRODUCER anaweza kuuza beat pia iwe ya msaniii kwani mbona MAGARI YANAUZWA na ukinunua linakuwa lako why not BEATS???
Producer anasema ile beat aliyokupa unaweza kuitumia utakavyo (sasa ile sio master) lakini master anayo yeye na anasema anastahili kuitumia atakavyo.

Yaani ni sawa na kitabu, ukishanunua unaweza hata kukichana na kuwashia moto lakini mtunzi au mchapaji atauza nakala nyingine (sio nakala yako) ila ni nakala nyingine ya kitabu hichohicho. Kwa hiyo hata magari, unanunua na kumiliki nakala lakini kumiliki kwako wewe hakuwazuii toyota kumuuzia jirani yako gari kama unalomiliki wewe. Ndio muono wa maprodusa
 
hivi producer si anasikiliza wimbo na idea ya msanii ndo anatengeneza beat?? au msanii anapewa beat aweke mashairi??? maana kama unamlipa akutengenezee beat means utakuwa unaimiliki...lakini pia unaweza nunua beat may b kama huwa hela yake ni mamilion
Kuna wasanii wanazikuta beats mbalimbali studio wanawaka na Mona wapo, ngoma inatengenezwa.

Producers kumi wakimsikiliza msanii mmoja maneno yake na idea yake, kila producer atakuja na mdundo ambao haufanani na wa mwenzie. Wimbo mmoja unaweza kutoboa katika hizo nyimbo kumi kwa kubebwa na beat moja wapo. Hapo ndipo "haki ya ubunifu" ya producer inapoanzia.
 
Producer anasema ile beat aliyokupa unaweza kuitumia utakavyo (sasa ile sio master) lakini master anayo yeye na anasema anastahili kuitumia atakavyo.

Yaani ni sawa na kitabu, ukishanunua unaweza hata kukichana na kuwashia moto lakini mtunzi au mchapaji atauza nakala nyingine (sio nakala yako) ila ni nakala nyingine ya kitabu hichohicho. Kwa hiyo hata magari, unanunua na kumiliki nakala lakini kumiliki kwako wewe hakuwazuii toyota kumuuzia jirani yako gari kama unalomiliki wewe. Ndio muono wa maprodusa
ahaa ok so ile beat huwezi kuipata kwingine isipokuwa kwa majani???
 
Back
Top Bottom