Ukweli usemwe: P Funk ndio mtu mnyonyaji zaidi kuwahi tokea kwenye historia ya Bongofleva

Wewe kiumbe mwenye chuki wivu na roho mbaya kwa kila binadamu aliyefanikiwa tunaongea tunayoyafaamu P Funk ana miliki rights za nyimbo za wasanii wote waliokuwa bongo records. Unaita watu machawa alafu unawashwa unajisogeza.

Mama yake Ngwea alifatilia hela za mwanae akaambiwa zipo kwa p funk akaenda kupewa kama msaada. Tena mil 1 baada ya hapo hela za marehemu anakula p funk bila hata aibu wala utu.

Hizo beats zenyewe alikuwa anatengeneza peke yake? Kinanda chenyewe hajui kupiga, anamgawia nani hela za ubunifu mbona anakula zote peke yake mnyonyaji mkubwa yule?
Sasa hapo embu elewesha p funk anakula hela za nyimbo za ngwair kama mtengeneza beat sio? Pia inatakiwa ifahamike katika wimbo/nyimbo mtengeneza beat anatakiwa achukue asilimia ngapi na muimbaji asilimia ngapi, muandishi wa nyimbo asilimia ngapi? Huko kwenye digital platform je ni universal kwamba inajulikana ni asilimia ngapi au inategemea na mkataba..? Nauliza haya sababu tofauti na kusikiliza miziki sina mengi ninayoyafahamu...
 
Producer anasema ile beat aliyokupa unaweza kuitumia utakavyo (sasa ile sio master) lakini master anayo yeye na anasema anastahili kuitumia atakavyo.

Yaani ni sawa na kitabu, ukishanunua unaweza hata kukichana na kuwashia moto lakini mtunzi au mchapaji atauza nakala nyingine (sio nakala yako) ila ni nakala nyingine ya kitabu hichohicho. Kwa hiyo hata magari, unanunua na kumiliki nakala lakini kumiliki kwako wewe hakuwazuii toyota kumuuzia jirani yako gari kama unalomiliki wewe. Ndio muono wa maprodusa
Nimebaki nacheka tu hapa Ndugu Mdau. Comment zako zinanifurahisha Sana. Eti "hakuwazuii Toyota kumuuzia jirani yako, gari Kama lako". Sipati picha jamaa anaenda Toyota kupiga mkwara jirani yake asiuziwe gari Kama yake yeye.
 
Wakuu kuna wakati ukweli lazima usemwe. Mambo ya kusema mtu aheshimiwe kwa kuwa alikuwa anatengeneza beats nzuri hizo ni heshima za uoga.

P Funk ambaye kiukweli zaidi ya kufanya production ya muziki na kupokea malipo hana jingine kubwa alilolifanyia bongofleva.

Kwa wasiofahamu wasanii wote waliokuwa chini ya bongo records hawana nyimbo au album wanazomiliki vyote anamiliki P Funk.

Ngwea amekufa maskini huku muziki wake unamilikiwa na P Funk mpaka leo anakula hela ya Ngwea.

Ukiona wimbo wa Juma Nature au Feruzi kwenye YouTube, Boomplay au digital platform yoyote usidhani ukisapoti unamsaidia msanii hiyo ni pesa ya Majani. Leo hii ikitokea bahati mbaya Juma Nature hatupo nae watoto wake watarithi nothing utajiri wake wa nyimbo ni mali ya watoto wa Majani kina Paula.

Huyu P Funk aliyekuwa anawapiga ngumi na mitama watoto wa kimaskini wakienda kuomba msaada wa kurekodi nyimbo zao.

Kumbuka pale bongo records kwenye utengenezaji wa beats waliusika watu wengi zeze ilitengenezwa na bizimani ila achukui hata sh 10, beat ya mikasi alitengeneza prof ludigo ila achukui hata sh 10 kina Marlon linje walikuwa wanapiga vinanda na vyombo vingine kwenye kutengeneza instrumental za wasanii haki zao za ubunifu anachukua nani kama sio mnyonyaji p Funk?

P Funk tunamuheshimu kwa kutengeneza beats ila zaidi ya production kaufanyia nini huu muziki?
P Funk uwa wakiitwa wasanii walipwe yeye anaenda kuchukua malipo kama nani? Kina Daz Baba wamekuwa vituko mtaani hela zao kwa nini unakula wewe PFunk?

Hii thread haiusiani na tukio lolote bali ukweli usiozungumzwa.
Shida inaanziaga kwa wasanii wengi hawajielewi aswa issues za digital products zao na hawajui izo ni digital assets kwao na familia zao ambazo ni urithi kwa vizazi vyao na ndo wasanii wa sasa kama platnumz anapowapiga bao msanii anatakiwa kuwa na umiliki wa contents zake zote kama music wake na ulindwe na copyrights company watu wasijifaidishe wala kuutumia bila idhini yake sasa wasanii wengi wa zamani kama lady jay dee, profesa jay, ngwair, ferooz, wengi ukichunguza nyimbo zao nyingi sio mali zao tena ata malipo ya nyimbo zao hawapokei wao tena bali wapigaji ambao wameziweka kwenye digital platforms zao kama YouTube acc za watu wengine maana wasanii wa zamani walikuwa hawana ata youtube channels ivyo nyimbo zao nyingi zipo kwenye channel za watu wengine 😀😀iyo kitu na inazidi kujirudia hadi leo kuna music labels ni majambazi na matapeli kwa mfano WANENE ENTERTAINMENT, wanatabia ya kuwafanyia production ya music wasanii na kisha music videos zao wanaweka kwenye YouTube channels zao na digital platforms acc zao kwa mfano CHIN BEEZ ukichunguza nyimbo zake zote na music videos zake zote zipo kwenye YouTube channels za wanene kitu ambacho ni unyonyaji kwa wasanii na baadae kinawapelekea stress, depression na kula madawa, kitu diamond achowazidi wasanii wengi ni umiliki wa digital products zake kwa 100% ambapo zinasimamiwa copyrights co kutoka SA inayofuatilia haki zake zote na mtu hawezi kuzichezea ovyo ,
 
Kwenye production na ubunifu kuna hakishiliki... walioshiriki kutengeneza beats mgao wao mbona hawapewi? Nyimbo nyingi pale yeye alikuwa anafanya mastering tu na mixing ila ubunifu wanafanya kina bizimani lakini anatepeli jasho lao. Huo ni unyonyaji na uzuri yeye amejipambanua kama mtetezi wa haki za wabunifu.
Hapa unapiga porojo tu..kama walilipwa je? Au unataka kusema walikuwa wanafanya kaz bure?

Sent from my CPH2219 using JamiiForums mobile app
 
Wakuu kuna wakati ukweli lazima usemwe. Mambo ya kusema mtu aheshimiwe kwa kuwa alikuwa anatengeneza beats nzuri hizo ni heshima za uoga.

P Funk ambaye kiukweli zaidi ya kufanya production ya muziki na kupokea malipo hana jingine kubwa alilolifanyia bongofleva.

Kwa wasiofahamu wasanii wote waliokuwa chini ya bongo records hawana nyimbo au album wanazomiliki vyote anamiliki P Funk.

Ngwea amekufa maskini huku muziki wake unamilikiwa na P Funk mpaka leo anakula hela ya Ngwea.

Ukiona wimbo wa Juma Nature au Feruzi kwenye YouTube, Boomplay au digital platform yoyote usidhani ukisapoti unamsaidia msanii hiyo ni pesa ya Majani. Leo hii ikitokea bahati mbaya Juma Nature hatupo nae watoto wake watarithi nothing utajiri wake wa nyimbo ni mali ya watoto wa Majani kina Paula.

Huyu P Funk aliyekuwa anawapiga ngumi na mitama watoto wa kimaskini wakienda kuomba msaada wa kurekodi nyimbo zao.

Kumbuka pale bongo records kwenye utengenezaji wa beats waliusika watu wengi zeze ilitengenezwa na bizimani ila achukui hata sh 10, beat ya mikasi alitengeneza prof ludigo ila achukui hata sh 10 kina Marlon linje walikuwa wanapiga vinanda na vyombo vingine kwenye kutengeneza instrumental za wasanii haki zao za ubunifu anachukua nani kama sio mnyonyaji p Funk?

P Funk tunamuheshimu kwa kutengeneza beats ila zaidi ya production kaufanyia nini huu muziki?
P Funk uwa wakiitwa wasanii walipwe yeye anaenda kuchukua malipo kama nani? Kina Daz Baba wamekuwa vituko mtaani hela zao kwa nini unakula wewe PFunk?

Hii thread haiusiani na tukio lolote bali ukweli usiozungumzwa.
Huo ni ukweli 100%
 
Kama ile kesi ya MWANA FA NA AY mpaka wakalipwa BIL 2 sijui na tigo ina maana ukitumikaa wimbo bhasi ndo haki ya msanii kulipwa ila likitumiKA BEAT tu bhasi haki ya producer kulipwaa... ngoma ngumu snaa hii 😀 😀 😀
Baada ya kushinda kesi, Hermy B akawaambia beat atakuwa anawauzia milioni 8, wakakasirika mpaka wakagombana nae kabisa😃😃 wao wanataka wawe wanalipa laki 5 mpaka single milioni
 
😀 😀 😀kwa hiyo kesi ya mwana fa walizima producer hakulamba kitu daah
 
Music publishing ni ishu tata sana. Sio huku kwetu tu bali hata huko kwa walioendelea. Kuna mifano kadhaa ya wanamuziki wakubwa ambao walitangaza kufilisika (bankruptcy) licha ya "kuuza" mamilioni ya kopi za rekodi. Mfano Toni Braxton, TLC n.k. Lakini huo ni mjadala wa siku nyingine.

Typical music production (unless kila kitu mpaka kuimba amefanya mtu mmoja) huwa inahusisha producers, composers, melody makers, session musicians na engineers. Hawa huwa wanakuwa na haki zinazoitwa mechanical rights za huo wimbo. Ukiangalia hapo sijamtaja mtu mmoja, MUIMBAJI/WAIMBAJI. Hawa wanakuwa na haki za uimbaji (singing right) kwenye huo wimbo.

Tafsiri ya rights zilizotajwa hapo juu ni kwamba kwa namna fulani KILA mtu aliyeshiriki kutengeneza huo wimbo (unless kwa sababu fulani amekubali kufanya bure) anatakiwa kulipwa. Analipwaje ndio mjadala ninaouona kwenye huu uzi. Suala la mshiriki kwenye production atalipwaje huwa liko kimkataba, inaweza kuwa malipo ya mara moja au percentage fulani ya publishing (wenzetu wanaitaga points). Kuna watu wamesema kwamba P Funk amepora haki ya watu aliofanya nao kazi ya production. Tutajuaje kama P alishamalizana nao kimalipo na wakaachia rights zao za publishing? Je, hizo haki zao zimesajiliwa kisheria? Hii ishu nitaijadili kidogo huko mbele.

Again, typical music production huwa inasimamiwa Producer. Kwenye music production kumekuwa na tatizo la watu kuchanganya producer na beat maker au session musician. Kwa kawaida huwa inategemewa producer awe pia musician ili awe na uwezo wa kuendesha zoezi zima la production. Lakini SIO lazima yeye apige vyombo au kufanya programming kwenye huo wimbo unaotengenezwa. Kuna mtu kasema "P Funk hajui hata kupiga kinanda", kwanza sio kweli, P Funk anaweza kupiga kinanda, pili ili awe ame-produce wimbo fulani sio lazima personally afanye beat making, yeye anahakikisha kila mhusika ana-play role yake na standard ya production inakuwa per exellent. Producers wengi wakubwa huko duniani huwa hawapigi vyombo wao wenyewe bali hutumia session musician au beat makers mfano Quincy Jones, Dr Dre, P Diddy, Irv Gotti etc.

Sasa tuje kwenye ishu tata ya hatimiliki aka publishing. Tofauti na watu wengi wanavyoamini, publishing rights sio automatic. Ni lazima ziwe zimesajiliwa kisheria (registered) ili zilindwe, kama umefanya kazi yoyote ya ubunifu bila kuisajili wakatokea wajanja wakasajili imekula kwako. Jamaa watapiga hela huku wewe ukipiga miayo. Huku kwetu nina uhakika kuanzia wasanii, wapiga vyombo na wengineo walikuwa hawalijui hilo ndio maana watu wengi wakiwemo wasanii wanaamini kwamba akienda studio akalipia kurekodi wimbo automatically unakuwa mali yake. Kitu ambacho sio kweli.

Sijajua mikataba ambayo wasanii wa hapa kwetu (wakiwemo wa WCB) huwa wanaingia na lebo huwa ina-address suala la publishing au hapana. Ambacho nina uhakika nacho ni kwamba wasanii wengi (hasa wa zamani) hawako aware kuhusu ishu ya publishing, na ndio mzozo wa Prof Jay na P Funk ulipoanzia.

Actually ishu ya Prof Jay na P Funk kuhusu beat ya nikusaidiaje haikuanzia kwenye beat hiyo kutumika kwenye movie. Baada ya Prof Jay kurekodi wimbo huo na kuhit, Chameleone akamfuata P akitaka atumie hiyo beat, P akamchaji Chameleone USD 2,000. Prof aliposikia akaja juu na kulalamika kwamba beat yake imeuzwa bila idhini yake. Lakini kiukweli Prof hakuwa ma haki yoyote kwa kuwa Chameleone alitumia beat tu, sio wimbo wote. Wimbo wa Chameleone ukaja kutumika kwenye movie ya Queen of Kitwe iliyotengenezwa na Disney na Chameleone akavuta mpunga. P akakomaa na Disney na kwa kuwa sheria ilikuwa upande wake alalipwa. Again Prof hakuwa na haki kwani wimbo uliotumika ni wa Chameleone na sio wa kwake.

Hitimisho ni kwamba music business is very shady, inatakiwa msanii ajifunze SANA sheria za hatimiliki na ahakikishe haki zake ziko documented na zimesajiliwa kisheria ili zilindwe.
 
hivi producer wa kina mwan fa aliambulia hata mia kwenye zile B2 walizopewa na tigo??
 
Ni movie.

Profesa J alitoa wimbo wa nikusaidiaje, Chameleone akatamani beat akalichukua na kufanya wimbo wake wa bombo clat. Profesa akawa na mgogoro na Chameleone, wakayasolve kwa kufanya wimbo wa Ndivyo Sivyo, wakamalizana kisanii.

Kina Lupita Nyongo wakatengeneza filamu yao na katika soundtracks zilizotumika wakatumia wimbo wa Bombo Clat wa Chameleone Jose, wakamlipa bwana Chameleone. P Funk kujua akamfuata Chameleone amtoe mpunga, Chameleone akampa jamaa USD 4,000 kumbe yeye (Chameleone) amelipwa USD 50,000. P Funk akawafuata Kampuni husika ya movie na kutaka kuwashtaki na hapo wenye kampuni wakampa USD 100,000 kama sikosei na hapo ndio Profesa J akajua kuwa jamaa amekula hela na yeye J hajapata kitu, ingawa alilipia beat husika, hivyo kustahili mapato yatokanayo na beat. Na ndiyo sababu kwa Chameleone mlalamikaji alikuwa ni Jay na sio P Funk
USD 100,000 ni zaidi ya M.200 hata kwa rate ya zamani bado ni mpunga mwingi sana, jamaa alipeleka wapi hii hela?! Kwa hela hiyo now hakutakiwa kua analia lia aseeeh
 
Music publishing ni ishu tata sana. Sio huku kwetu tu bali hata huko kwa walioendelea. Kuna mifano kadhaa ya wanamuziki wakubwa ambao walitangaza kufilisika (bankruptcy) licha ya "kuuza" mamilioni ya kopi za rekodi. Mfano Toni Braxton, TLC n.k. Lakini huo ni mjadala wa siku nyingine.

Typical music production (unless kila kitu mpaka kuimba amefanya mtu mmoja) huwa inahusisha producers, composers, melody makers, session musicians na engineers. Hawa huwa wanakuwa na haki zinazoitwa mechanical rights za huo wimbo. Ukiangalia hapo sijamtaja mtu mmoja, MUIMBAJI/WAIMBAJI. Hawa wanakuwa na haki za uimbaji (singing right) kwenye huo wimbo.

Tafsiri ya rights zilizotajwa hapo juu ni kwamba kwa namna fulani KILA mtu aliyeshiriki kutengeneza huo wimbo (unless kwa sababu fulani amekubali kufanya bure) anatakiwa kulipwa. Analipwaje ndio mjadala ninaouona kwenye huu uzi. Suala la mshiriki kwenye production atalipwaje huwa liko kimkataba, inaweza kuwa malipo ya mara moja au percentage fulani ya publishing (wenzetu wanaitaga points). Kuna watu wamesema kwamba P Funk amepora haki ya watu aliofanya nao kazi ya production. Tutajuaje kama P alishamalizana nao kimalipo na wakaachia rights zao za publishing? Je, hizo haki zao zimesajiliwa kisheria? Hii ishu nitaijadili kidogo huko mbele.

Again, typical music production huwa inasimamiwa Producer. Kwenye music production kumekuwa na tatizo la watu kuchanganya producer na beat maker au session musician. Kwa kawaida huwa inategemewa producer awe pia musician ili awe na uwezo wa kuendesha zoezi zima la production. Lakini SIO lazima yeye apige vyombo au kufanya programming kwenye huo wimbo unaotengenezwa. Kuna mtu kasema "P Funk hajui hata kupiga kinanda", kwanza sio kweli, P Funk anaweza kupiga kinanda, pili ili awe ame-produce wimbo fulani sio lazima personally afanye beat making, yeye anahakikisha kila mhusika ana-play role yake na standard ya production inakuwa per exellent. Producers wengi wakubwa huko duniani huwa hawapigi vyombo wao wenyewe bali hutumia session musician au beat makers mfano Quincy Jones, Dr Dre, P Diddy, Irv Gotti etc.

Sasa tuje kwenye ishu tata ya hatimiliki aka publishing. Tofauti na watu wengi wanavyoamini, publishing rights sio automatic. Ni lazima ziwe zimesajiliwa kisheria (registered) ili zilindwe, kama umefanya kazi yoyote ya ubunifu bila kuisajili wakatokea wajanja wakasajili imekula kwako. Jamaa watapiga hela huku wewe ukipiga miayo. Huku kwetu nina uhakika kuanzia wasanii, wapiga vyombo na wengineo walikuwa hawalijui hilo ndio maana watu wengi wakiwemo wasanii wanaamini kwamba akienda studio akalipia kurekodi wimbo automatically unakuwa mali yake. Kitu ambacho sio kweli.

Sijajua mikataba ambayo wasanii wa hapa kwetu (wakiwemo wa WCB) huwa wanaingia na lebo huwa ina-address suala la publishing au hapana. Ambacho nina uhakika nacho ni kwamba wasanii wengi (hasa wa zamani) hawako aware kuhusu ishu ya publishing, na ndio mzozo wa Prof Jay na P Funk ulipoanzia.

Actually ishu ya Prof Jay na P Funk kuhusu beat ya nikusaidiaje haikuanzia kwenye beat hiyo kutumika kwenye movie. Baada ya Prof Jay kurekodi wimbo huo na kuhit, Chameleone akamfuata P akitaka atumie hiyo beat, P akamchaji Chameleone USD 2,000. Prof aliposikia akaja juu na kulalamika kwamba beat yake imeuzwa bila idhini yake. Lakini kiukweli Prof hakuwa ma haki yoyote kwa kuwa Chameleone alitumia beat tu, sio wimbo wote. Wimbo wa Chameleone ukaja kutumika kwenye movie ya Queen of Kitwe iliyotengenezwa na Disney na Chameleone akavuta mpunga. P akakomaa na Disney na kwa kuwa sheria ilikuwa upande wake alalipwa. Again Prof hakuwa na haki kwani wimbo uliotumika ni wa Chameleone na sio wa kwake.

Hitimisho ni kwamba music business is very shady, inatakiwa msanii ajifunze SANA sheria za hatimiliki na ahakikishe haki zake ziko documented na zimesajiliwa kisheria ili zilindwe.
Ahsante mkuu kwa somo, limenyooka sana.🙏🏿
 
Back
Top Bottom