Ukweli usemwe: P Funk ndio mtu mnyonyaji zaidi kuwahi tokea kwenye historia ya Bongofleva

Ukweli usemwe: P Funk ndio mtu mnyonyaji zaidi kuwahi tokea kwenye historia ya Bongofleva

yaah nakubalii mzee sio kama siku hizi kuna platform na mitandao ya kijami kibao kazi zinajipushi zenyewe maredio ndo usisemee ukiacha station za TV... so producer kama majani au master j walifanya kazi kama sallam anavyofanya leoo..

Halafu unaingia Jf na social media platforms nyingine wanakuambia P Funk ana mchango gani 😁😁😁

Wasijue hao ndio waliotengeneza road map na sound ya bongo flava tunayoiona leo hii inaharabiwa na amapiano na afro pop za kinaija,

Watakuambia tunapeleka muziki mbele, muziki upi,

kwa sasa Tz tuna genre ya kupambana na congo, SA au Nigeria au ndio tunafanya muziki wa kucopy na kupaste

Hawa hawa watakuambia P funk na majani hawana mchango wakati hakuna new sound kwa sasa zaidi ucopy cat.. Ngoja ninyamaze
 
amini mzee sound track za south na nigeriaa tuu...bongo fleva halisi inakufaaa
 
Yule mjanja kaona uhuni wanateswa kwa sifa ya kitaa kuwa wcb, S2KIZZY anatakiwa asign contract kwa kila beats anazomtengenezea mond na kila artist kila itakapotumika apate % kadhaa na sio kupata tu sifa ya kudhurula duniani na kukutanishwa na artists wakubwa na sifa ya kuwa karibu na mond , mark my words siku si nyingi watazinguana na akifulia tutaujua ukweli

Yatamtokea ya Nahreel na weusi, alipoipa ukubwa studio yake na kupandisha bei wakamkimbia

Kiufupi creative industry kwa bongo, vichwa haswaaa havinufaiki na kazi zao ila madalali wenye connections ndio wanatusua na kuishi maisha makubwa

Wanamtumia mtu kwa kumuhaidi jina na wengi wanakubali kwa kudhani wakipata jina washatoboa. Wanapata jina ila wakitaka kupiga pesa kupitia jina lao wanakimbiwa

Afadhali ABBA na hansana wameshtuka mapema kumshikilia marioo na wasanii wengine maana itawahakikishia ugali la sivyo, wangetupwa pembeni baada ya kutaka pesa ya maana

Bongo wamejaa wanyonyaji, wanapiga kelele wakiwa na njaa, wakipata chance wanarudia yale yale
 
amini mzee sound track za south na nigeriaa tuu...bongo fleva halisi inakufaaa
Ngoma za sa hivi bongofleva zinafanana ni mwendo wa matusi tu na contents zinazofanana hakuna jipya ni ngono tu tofauti na music industry za nchi nyingine kila msanii anataka aimbe content kama za wasanii wa wcb , maproducers & music composers hakuna kitu nilikuwa nasikiliza bia tamu ya marioo nikawa naskia kama demo vile imekosa vionjo vya kutosha ila ilivyokuwa kwenye trends sikuona kasoro😀😀
 
Acha marioo atulilie akichoka kupiga amapiano, wakina mbosso wakituliza kichwa watuimbie baibuda na Mimi Mars anaejitahidi kutokwenda na trend 😁😁
marioo amapianoo na sauti yake kama hataki imemkaa poaa sanaa muhuni...
 
Yatamtokea ya Nahreel na weusi, alipoipa ukubwa studio yake na kupandisha bei wakamkimbia

Kiufupi creative industry kwa bongo, vichwa haswaaa havinufaiki na kazi zao ila madalali wenye connections ndio wanatusua na kuishi maisha makubwa

Wanamtumia mtu kwa kumuhaidi jina na wengi wanakubali kwa kudhani wakipata jina washatoboa. Wanapata jina ila wakitaka kupiga pesa kupitia jina lao wanakimbiwa

Afadhali ABBA na hansana wameshtuka mapema kumshikilia marioo na wasanii wengine maana itawahakikishia ugali la sivyo, wangetupwa pembeni baada ya kutaka pesa ya maana

Bongo wamejaa wanyonyaji, wanapiga kelele wakiwa na njaa, wakipata chance wanarudia yale yale
Ni balaa boss uwa hawajiulizi familia za kina michael Jackson, Bob marley, tupac kwa nini hadi leo wanafaidika na sanaa za ndugu zao😀😀mjini kuna wahuni ata sio wasanii ila wanawatumia kupiga pesa, bongo kuna majipu mengi wanayachekea kuna WANENE ENTERTAINMENT pia wanawatumia wasanii vibaya nayo yanakubali tu bila kujitambua kama wakina young killer, chin beez, fid q na wengine kibao
 
Wakuu kuna wakati ukweli lazima usemwe. Mambo ya kusema mtu aheshimiwe kwa kuwa alikuwa anatengeneza beats nzuri hizo ni heshima za uoga.

P Funk ambaye kiukweli zaidi ya kufanya production ya muziki na kupokea malipo hana jingine kubwa alilolifanyia bongofleva.

Kwa wasiofahamu wasanii wote waliokuwa chini ya bongo records hawana nyimbo au album wanazomiliki vyote anamiliki P Funk.

Ngwea amekufa maskini huku muziki wake unamilikiwa na P Funk mpaka leo anakula hela ya Ngwea.

Ukiona wimbo wa Juma Nature au Feruzi kwenye YouTube, Boomplay au digital platform yoyote usidhani ukisapoti unamsaidia msanii hiyo ni pesa ya Majani. Leo hii ikitokea bahati mbaya Juma Nature hatupo nae watoto wake watarithi nothing utajiri wake wa nyimbo ni mali ya watoto wa Majani kina Paula.

Huyu P Funk aliyekuwa anawapiga ngumi na mitama watoto wa kimaskini wakienda kuomba msaada wa kurekodi nyimbo zao.

Kumbuka pale bongo records kwenye utengenezaji wa beats waliusika watu wengi zeze ilitengenezwa na bizimani ila achukui hata sh 10, beat ya mikasi alitengeneza prof ludigo ila achukui hata sh 10 kina Marlon linje walikuwa wanapiga vinanda na vyombo vingine kwenye kutengeneza instrumental za wasanii haki zao za ubunifu anachukua nani kama sio mnyonyaji p Funk?

P Funk tunamuheshimu kwa kutengeneza beats ila zaidi ya production kaufanyia nini huu muziki?
P Funk uwa wakiitwa wasanii walipwe yeye anaenda kuchukua malipo kama nani? Kina Daz Baba wamekuwa vituko mtaani hela zao kwa nini unakula wewe PFunk?

Hii thread haiusiani na tukio lolote bali ukweli usiozungumzwa.
P.FUNK alikuwa Mungu mtu na ili kuwapoteza vijana akawafundisha ulevi wa pombe, bange na unga na ukitaka uamini angalia wasanii wote walikuwa chini ya bongo record wengi Wana kazi nzuri ila walevi kama siyo pombe basi unga au bange aliwafanya wawe wajinga prof jay peke yake ndio alistuka vinginevyo naye tungempoteza P FUNk alikuwa alikuwa BIGWA wa kuuwa makundi ya mziki yani uyu jamaa asiongee Chochote kwa Sasa aliwavuruga Daz nundaz, akawavuluga HBC nk.

Anawavuruga vijana akawanywesha pombe hiki tunachokiona kwa mwanae Paula ni malipo ya zambi mungu anamlipa kwa alivyowafanya watoto wa wenzake kwa kuwaingiza kwenye bange, pombe na unga hawa kina T.I.D kina feruz, Daz baba nk majani ndio chanzo
 
Music publishing ni ishu tata sana. Sio huku kwetu tu bali hata huko kwa walioendelea. Kuna mifano kadhaa ya wanamuziki wakubwa ambao walitangaza kufilisika (bankruptcy) licha ya "kuuza" mamilioni ya kopi za rekodi. Mfano Toni Braxton, TLC n.k. Lakini huo ni mjadala wa siku nyingine.

Typical music production (unless kila kitu mpaka kuimba amefanya mtu mmoja) huwa inahusisha producers, composers, melody makers, session musicians na engineers. Hawa huwa wanakuwa na haki zinazoitwa mechanical rights za huo wimbo. Ukiangalia hapo sijamtaja mtu mmoja, MUIMBAJI/WAIMBAJI. Hawa wanakuwa na haki za uimbaji (singing right) kwenye huo wimbo.

Tafsiri ya rights zilizotajwa hapo juu ni kwamba kwa namna fulani KILA mtu aliyeshiriki kutengeneza huo wimbo (unless kwa sababu fulani amekubali kufanya bure) anatakiwa kulipwa. Analipwaje ndio mjadala ninaouona kwenye huu uzi. Suala la mshiriki kwenye production atalipwaje huwa liko kimkataba, inaweza kuwa malipo ya mara moja au percentage fulani ya publishing (wenzetu wanaitaga points). Kuna watu wamesema kwamba P Funk amepora haki ya watu aliofanya nao kazi ya production. Tutajuaje kama P alishamalizana nao kimalipo na wakaachia rights zao za publishing? Je, hizo haki zao zimesajiliwa kisheria? Hii ishu nitaijadili kidogo huko mbele.

Again, typical music production huwa inasimamiwa Producer. Kwenye music production kumekuwa na tatizo la watu kuchanganya producer na beat maker au session musician. Kwa kawaida huwa inategemewa producer awe pia musician ili awe na uwezo wa kuendesha zoezi zima la production. Lakini SIO lazima yeye apige vyombo au kufanya programming kwenye huo wimbo unaotengenezwa. Kuna mtu kasema "P Funk hajui hata kupiga kinanda", kwanza sio kweli, P Funk anaweza kupiga kinanda, pili ili awe ame-produce wimbo fulani sio lazima personally afanye beat making, yeye anahakikisha kila mhusika ana-play role yake na standard ya production inakuwa per exellent. Producers wengi wakubwa huko duniani huwa hawapigi vyombo wao wenyewe bali hutumia session musician au beat makers mfano Quincy Jones, Dr Dre, P Diddy, Irv Gotti etc.

Sasa tuje kwenye ishu tata ya hatimiliki aka publishing. Tofauti na watu wengi wanavyoamini, publishing rights sio automatic. Ni lazima ziwe zimesajiliwa kisheria (registered) ili zilindwe, kama umefanya kazi yoyote ya ubunifu bila kuisajili wakatokea wajanja wakasajili imekula kwako. Jamaa watapiga hela huku wewe ukipiga miayo. Huku kwetu nina uhakika kuanzia wasanii, wapiga vyombo na wengineo walikuwa hawalijui hilo ndio maana watu wengi wakiwemo wasanii wanaamini kwamba akienda studio akalipia kurekodi wimbo automatically unakuwa mali yake. Kitu ambacho sio kweli.

Sijajua mikataba ambayo wasanii wa hapa kwetu (wakiwemo wa WCB) huwa wanaingia na lebo huwa ina-address suala la publishing au hapana. Ambacho nina uhakika nacho ni kwamba wasanii wengi (hasa wa zamani) hawako aware kuhusu ishu ya publishing, na ndio mzozo wa Prof Jay na P Funk ulipoanzia.

Actually ishu ya Prof Jay na P Funk kuhusu beat ya nikusaidiaje haikuanzia kwenye beat hiyo kutumika kwenye movie. Baada ya Prof Jay kurekodi wimbo huo na kuhit, Chameleone akamfuata P akitaka atumie hiyo beat, P akamchaji Chameleone USD 2,000. Prof aliposikia akaja juu na kulalamika kwamba beat yake imeuzwa bila idhini yake. Lakini kiukweli Prof hakuwa ma haki yoyote kwa kuwa Chameleone alitumia beat tu, sio wimbo wote. Wimbo wa Chameleone ukaja kutumika kwenye movie ya Queen of Kitwe iliyotengenezwa na Disney na Chameleone akavuta mpunga. P akakomaa na Disney na kwa kuwa sheria ilikuwa upande wake alalipwa. Again Prof hakuwa na haki kwani wimbo uliotumika ni wa Chameleone na sio wa kwake.

Hitimisho ni kwamba music business is very shady, inatakiwa msanii ajifunze SANA sheria za hatimiliki na ahakikishe haki zake ziko documented na zimesajiliwa kisheria ili zilindwe.

Ahsante saana. Umetoa Elimu kubwa Sana ambayo sidhani Kama wengi wetu humu tungeweza kuipata kirahisi. Wewe Ni mdau wa sheria za hii industry maana haya madini sio mchezo!?

Cha kuongezea hapo kwenye publishing rights, mpaka leo Mase anapambana na PDiddy kuhusu hizo rights ambazo PDiddy anazimiliki za kazi za Mase, na Mase anajaribu kuzinunua toka kwa jamaa ila jamaa(Diddy) kagoma.
 
P.FUNK alikuwa Mungu mtu na ili kuwapiteza vijana akawafundisha ule wa pombe, bange na unga na ukitaka.aamini angalia wasanii wote walikuwa chini ya bingo record wengi Wana kazi nzuri ila walevi kama siyo pombe basi unga au bange aliwafanya wawe wajinga prof jay peke yake ndio alistuka vinginevyo naye tungempoteza P FUNk alikuwa alikuwa BIGWA wa kuuwa makundi ya mziki yani uyu jamaa asiongee Chochote kwa Sasa aliwavuruga Daz nundaz, akawavuluga HBC nk.

Anawavuruga vijana akawanyesha pombe hiki tunachokiona kwa mwanae Paula ni malipo ya zambi mungu anamlipa kwa alivyowafanya watoto wa wenzake kwa kuwaingiza kwenye bange, pombe na unga hawa kina T.I.D kina feruz, Daz baba nk majani ndio chanzo
Kuna sehemu sijakuelewa mkuu. P alikuwa anawanywesha pombe na kuwavutisha bangi au walikuwa wanatumia wenyewe kwa hiari yao?
 
Sipendi sana kuingilia mada za machawa siku hizi, ila nimona wewe nikujibu.

Kiuhalisia, huyo P Funk ana afadhali kuliko hao WCB.

PF hamiliki Album za wasanii ila anamiliki BEATS. Na ndio maana hujawahi kusikia Msanii analalamika.

Na kiukweli, wasanii wa zamani walipata pesa mnoooo.

Hakuna Msanii ambaye hakupata pesa. Kuna wasanii mpaka walikuwa wanatembea na pesa kwenye but I za gari.

Tatizo kubwa ukiwa msanii WCB ujue Ni Kama unafanya kazi ambayo Ni COMMISSION BASED.

Inatakiwa ufanye kazi halafu, iqe Shows, ngoma mitandaoni au endorsement kila kinachopatikana unakatwa 60% unapewa 40% kwa mkataba wa miaka 10.

Maana yake, unafonzea kila kitu. Miaka 10 kisanii hutakuwa na jipya tena.

Na baada ya kutoka hutakuwa unamiliki nyimbo yoyote Wala digital platform zako.

Kuna vitu watu huwa wanakubali kwasababu ya shida tu.
Wewe nimekuelewa vizuri sasa umenifungua masikio.
Kumbe ndio maana harmonize alifosi kujitoa kule WCB.
 
Nakumbuka sio movie, ni ngoma sijui nikusaidiaje ile biti akauziwa tena chameleone akaimbuia bomboclat.. Jay kuulizia p kaishakula hela, chameleone akataka kumpa tena hela Prof akaamua wapige kolabo, ngoma nimeisahau jina.
beat aliuza Chamilione kwa ajiri ya movie flani waingereza kama sikosei, wimbo ni jose ft joseph haule. Ila beat Majani. Majani akawa anamponda Josee ila mwishoe huko P nafikiri alilipwa. P yy anamiliki beat sio wimbo....ndio haki yake mengine kwa kina Nature, Jay Mo na wengine alisimama kama meneja na produce!!
 
Majani anachofanya ni kama kile P Diddy amekifanya kwa wasanii wake, wanamfanya awe rich forever, ndio biashara ya muziki ipo hivyo duniani, ni ya kinyonyaji.

Kilichotakiwa kufanyika awali ilikuwa ni kugawana asilimia za mapato ya wimbo. Producer apate asilimia 50 na mwimbaji apate asilimia 50 kwa kuwa combination yao ndio imetoa wimbo (muziki). Sasa kinachozungumzwa hapa ni kuwa P Funk anamiliki 100% yaani mpaka maneno yaliyoimbwa kwenye nyimbo yeye ndio anayamiliki, hakuna cha mtunzi wala muimbaji.
Muongo mkubwa weww
 
Kuna sehemu sijakuelewa mkuu. P alikuwa anawanywesha pombe na kuwavutisha bangi au walikuwa wanatumia wenyewe kwa hiari yao?
Yeye ndio alikuwa na exposure katika burudani so kwakua vijana ndio wametoka kimuziki aliwaminisha kulewa ndio ujanja so alichukua wasanii wenye uwezo mkubwa sana kutunga so walipokuwa wazima walifanya kazi nje ya hapo aliwaminisha maisha ni kulewa tu so vijana wakaishiwa kulewa tu nakujisahau mambo ambayo diamond anafanya Leo kwenye uwekezaji nk amini juma nature angekuwa mala mbili yake ila juma nature alishia kuvutishwa bange na kunywa pombe
 
Mfano producer angesajili kazi yake (beat) halafu baada ya kufanya vocal nk msanii nae akaenda kusajili wimbo (vocal na beat) kuwa yeye pekee ndio mmiliki, baadae wimbo ukatumiwa kinyemela, hapo wote watafaidika na kinachopatikana? Producer hakuuza haki zote kwa muimbaji
Usajili wa kazi za ubunifu hauwezi kufanywa zaidi ya mara moja. Wenzetu walioendelea ishu za publishing huwa zinakuwa addressed kwenye mkataba kati ya producer/label na msanii au yeyote anayeshiriki kutengeneza wimbo. Baada ya hapo ndio kila mtu anatakiwa kusajili hizo haki zake kisheria kwenye mamlaka husika.
 
Back
Top Bottom