Ukweli Usemwe: Uongozi wa Rais Samia ni Changamoto

Sisi watumishi wa umma tunamshukuru katupandishia mishahara tuna uwezo wa kumudu gharama za maisha. Wengine mtajua wenyewe
Mkuu Sasa si utatumia pesa nyingi kulipia huduma ya kawaida.
Kuna mtu nilimuuliza ni Bora ulipwe laki 5 kwa mwezi alafu mahitaji gharama iwe laki 4
Au ulipwe laki 3 alafu mahitaji gharama iwe laki 1.
Huwezi amini alichagua laki 5.

Kupandisha mshahara ni jambo zuri, Ila mfumuko ukiwa mkubwa thamani ya pesa inapungua hivyo hata huo mshahara uliopanda unakua hauna maana tena. Anyway......
 
Watanzania tupo radhi tule nyasi CCM iendelee kubaki madarakani.
 
We unashangaa hiyo laki 5 kwa matumizi ya laki 4? Hii bongo mtu analipwa laki 2 matumizi ni milioni 1 mzee.
 
Sio samia sema CCM nzima wameishindwa nchi. Hebu jiulize hivi tuna makamu wa raisi nchi hii?
 
Sio samia sema CCM nzima wameishindwa nchi. Hebu jiulize hivi tuna makamu wa raisi nchi hii?
Makamu kapooza kama mkojo wa ngedere yaani huo umakamu ni kama kapewa ihsani. Tukidai katiba ifanyiwe marekebisho hawa mbwa wa ccm wanabweka humu JF. Wacha twende hivo hivo.
 
Kimsingi Huyu MAMA Hana Huwezo Wa Kumaimaliza Miradi Ya Jpm Kwa Wakati.
.
Na Naona Kabisa Mradi Wa Bwawa La Nyerere Ukisitishwa na Kufa Kabisa.
.
Maana wasiopenda Mradi Ndio Hao Hao wameweka Wizara ya Nishati.
.
Wameanza Issue ya Gesi Asilia Wakijinasibu Eti Wao Watakuwa Monopoly Kwenye Gesi zaidi Ya Urusi na USA.
.
Yetu Macho Achana Tuone
 
Mtanikumbuka
 
Mfano huo wa "pembejeo, na ubora wa wa viutilifu", ni mfano mzuri sana, kwa maana unawagusa wananchi moja kwa moja.
Tunalia na ukosefu wa mafuta ya kula, kila mwaka. Ukisikiliza kelele zinazopigwa na viongozi wetu juu ya uwezekano wetu kujitosheleza na kuuza nje bidhaa hiyo, utadhani Tanzania tuna nema ya ajabu sana.

Leo hii rais anasimama mbele za wananchi anazungumzia uhaba wa bidhaa hiyo hiyo. Anatoa amri bidhaa hiyo iagizwe toka nje kwa bei yoyote ile..., halafu anaishia hapo!

Kwani alizeti, karanga, pamba ..., mazao haya yanahitaji muda mrefu kiasi gani kuweza kuyazalisha ya kutosha ili tupate mafuta ya kutosha? Kwa nini tumeshindwa kila mwaka kuwahudumia wakulima ili wazalishe mazao haya kwa wingi ili tuondokane na adha hii ya kila mwaka?

Rais kasema, viwanda vipo, lakini havizalishi mafuta! Anaamrisha mafuta yaagizwe..., anaishia hapo! Huu ndio uongozi? Kweli anao moyo wa kujali maslahi ya nchi hii?
Kinachoonekana hapa, rais anao watu wake walio mstarini tayari kuagiza mafuta. Hawa ndio anaowajali. Wakulima na hivyo viwanda vilivyopo yeye hana habari navyo kabisa!

Samia ataididmiza Tanzania. Anaua kabisa hata ule moyo wa kudhani tunaweza kufanya na kujitegemea katika mambo kadhaa. Kujitegemea na Kujitosheleza katika mambo tuliyo nayo uwezo ndiyo njia sahihi kabisa ya nchi yetu kuendelea. Hatuwezi kuwa nchi ya kutegemea wachuuzi ndio watuletee maendeleo.
 
Nyumbu wameanza kusafiri kwenda Kenya kuzaa sasa, ilikua wasiojulikana sasa maisha. Kwa hiyo yeye ana kisima cha mafuta
 
Kuna kjj wese la mboga ni 8k kwa lita, kipande cha sabuni kinaanzia 700, ....
Nimekumbuka sehemu ya ule wimbo ..... Bora Nirudi Jela.
 
Hapo nchumbiji ndo vitu viwe bei nafuuuu, in mmakonde voice...
 
"UVIKO-19, ambapo kwa miaka miwili hapakuwa na uzalishaji"? Tanzania gani hiyo iliyozuia watu kwenda shambani na kufanya shughuli zao?

Labda aseme, bidhaa zinazotegemewa na wakulima, zinazoagizwa toka nchi za nje, kama Mbolea haikuweza kuagizwa toka huko, kwa vile nchi hizo zilifunga shughuli na usafirishaji wa bidhaa uliathirika. Lakini kama ni kwa wakulima wetu kulima alizeti, karanga, pamba, hakuna mkulima aliyeacha kwenda shamba kwa sababu ya UVIKO-19.
 
Tozo ya mafuta imerejeshwa upyaaaaa !!
 
Hameni Nchi nyie wazee wakulamu kila awamu, mbuzi nyie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…