Nimekuelewa mkuu, hapo mwanzo nimesema kama unasimama nafasi ya Mwananchi wa kawaida nilikuwa na maana kubwa sana.... Tukiachana na hilo kuhusu Msumbiji kikubwa ni usimamizi mzuri usio na ubabaishaji mfano kwenye pembejeo serikali ya Msumbiji huwa inasimama kidete kuhakikisha si tu pembejeo zinapatikana kwa wakati bali pia zenye ubora, viuatilifu vyote ambavyo tunavipata kutoka Msumbiji huwa ni bora sana sana sana ukilinganisha na vya kwetu, SERIKALI YETU haina nia ya dhati ya kutusaidia, wanachohakikisha wao ni neema za matumbo yao tu!
Mfano huo wa "pembejeo, na ubora wa wa viutilifu", ni mfano mzuri sana, kwa maana unawagusa wananchi moja kwa moja.
Tunalia na ukosefu wa mafuta ya kula, kila mwaka. Ukisikiliza kelele zinazopigwa na viongozi wetu juu ya uwezekano wetu kujitosheleza na kuuza nje bidhaa hiyo, utadhani Tanzania tuna nema ya ajabu sana.
Leo hii rais anasimama mbele za wananchi anazungumzia uhaba wa bidhaa hiyo hiyo. Anatoa amri bidhaa hiyo iagizwe toka nje kwa bei yoyote ile..., halafu anaishia hapo!
Kwani alizeti, karanga, pamba ..., mazao haya yanahitaji muda mrefu kiasi gani kuweza kuyazalisha ya kutosha ili tupate mafuta ya kutosha? Kwa nini tumeshindwa kila mwaka kuwahudumia wakulima ili wazalishe mazao haya kwa wingi ili tuondokane na adha hii ya kila mwaka?
Rais kasema, viwanda vipo, lakini havizalishi mafuta! Anaamrisha mafuta yaagizwe..., anaishia hapo! Huu ndio uongozi? Kweli anao moyo wa kujali maslahi ya nchi hii?
Kinachoonekana hapa, rais anao watu wake walio mstarini tayari kuagiza mafuta. Hawa ndio anaowajali. Wakulima na hivyo viwanda vilivyopo yeye hana habari navyo kabisa!
Samia ataididmiza Tanzania. Anaua kabisa hata ule moyo wa kudhani tunaweza kufanya na kujitegemea katika mambo kadhaa. Kujitegemea na Kujitosheleza katika mambo tuliyo nayo uwezo ndiyo njia sahihi kabisa ya nchi yetu kuendelea. Hatuwezi kuwa nchi ya kutegemea wachuuzi ndio watuletee maendeleo.