Ukweli Usemwe: Uongozi wa Rais Samia ni Changamoto

Ukweli Usemwe: Uongozi wa Rais Samia ni Changamoto

Umenena swai mama imagine kauli kama hizi 'Oh nikiwasema wananuna na kuhoji huna imani na vyombo vyako'.

Wacha wanune wapasuke fukuzia mbali huko wameshindwa kazi watimuliwe haraka sana unawabembeleza walevi wa madaraka kwa gharama ya watz milioni 60 kweli????!!!!!!
Eti anaogopa ataitwa dikteta.
Maajabu ya mfalme Zumaridi haya.
 
Uchaguzi unaofata mambo ni yale yale, kiongozi yule yule.

Kiufupi hakutakuwa na maajabu.

Kazi iendelee
Kwa miongozo ya nchi hii ndivyo ilivyo.. Au kunamtu anataraji mabadiliko? Yeye ndo m/Kiti ashindwe kujiteua ama
 
Bora upande bei lakini uwe na ubora. Tabora bakery mikate inauzwa sh 1000, imeandikwa uzito 400g, lakini ukiupima ni 150g! Ukiuminya unaishia kwenye kiganja. Maafisa vipimo wapo, wamekataa maofisini wanasubiri kugonga mizani mihuri.
Kwetu sisi huku mkate una viwango, ukila unaona raha kweli kweli
 
Mkuu 'GAZETI' tatizo letu wengi, nikiwemo mimi na wewe ni hili ulilolionyesha kwenye mada yako hii!

Yaani tunamtazama kiongozi kwa darubini hafifu mno, kama hii ya bei za vitu, basi, tunaishia hapo. Hizo bei zikiwa chini kwa hiyo kiongozi anakuwa bora?

Naomba sana unielewe, sisemi kamwe kwamba bei za vitu kwa wananchi siyo swala muhimu, ni muhimu sana, lakini ni sehemu ndogo sana katika kumfanya kiongozi awe ni kiongozi mzuri.

Samia hana sifa za kuwa kiongozi mzuri, siyo tu kwa sababu anaruhusu bei zipande juu. Samia hana sifa za uongozi bora kwa sababu hajui anataka nchi hii ielekee wapi; hana dira., na kama anayo ni dira potofu ya kudhani kwamba nchi itaendelea kwa kutegemea watu toka nje kuleta maendeleo hapa.

Sasa hilo la Msumbiji, ulikotembelea, umeuliza kwa nini bei zao zipo chini? Mada yako ingesaidia sana hoja zako kama ungeeleza kinagaubaga kinachofanywa na viongozi wa Msumbiji, na kisichofanywa na Tanzania. Ungefanya hivyo, ingesaidia sana mada yako kueleweka.
Nimekuelewa mkuu, hapo mwanzo nimesema kama unasimama nafasi ya Mwananchi wa kawaida nilikuwa na maana kubwa sana.... Tukiachana na hilo kuhusu Msumbiji kikubwa ni usimamizi mzuri usio na ubabaishaji mfano kwenye pembejeo serikali ya Msumbiji huwa inasimama kidete kuhakikisha si tu pembejeo zinapatikana kwa wakati bali pia zenye ubora, viuatilifu vyote ambavyo tunavipata kutoka Msumbiji huwa ni bora sana sana sana ukilinganisha na vya kwetu, SERIKALI YETU haina nia ya dhati ya kutusaidia, wanachohakikisha wao ni neema za matumbo yao tu!
 
Conflict of interest, ndio kinaumiza wananchi Tanzania. Biashara kubwa zote nchini wakubwa wamo.
 
Unaposimama katika nafasi ya mwananchi wa kawaida ndio utaelewa ninachomaanisha.

Ni majuzi tu nilisafiri kwenda Mozambique.

Ile nchi haijatulia na haijawahi kutulia lakini nimeshangaa kukuta bei ya mafuta ya kula ikiwa ni nafuu mno.

Bei ya mafuta ya Kula ya Tanzania ni zaidi ya mara mbili ya ile ya Msumbiji.

Dizeli, Petrol na Mbolea Msumbiji ni nafuu sana ukilinganisha na Tanzania, wanatuzidi wapi?

Nikirudi kwa mama, Mwaka mmoja wa kuwa madarakani kila kitu kimebadilika gharama za Maisha zimepanda mno, uonevu kwa wakulima wa Korosho umerudi upya.

Bei ya magari, TV, Computer n.k zimekuwa juu kabisa.

Kama hali itaendelea hivi uchaguzi unaofuata.
Mungu mbariki sana Rais wetu Mama Samia Hassan Suluhu
 
Wakubwa wanajikatia minyama kwani wao pia ni shareholders wa biashara nyingi kubwa hapa nyumbani...
 
Asilimia zote ni zipi na unajiridhisha vipi na kujua ni zote na hujaacha kuzielewa nyingine ambazo huzijui?
kwa utafiti wangu mm asilimia kubwa ya wa tz hawamkubali huyu mama watu wanamlalamikia huku mitaani hali ya maisha imekuwa ngumu kila ki2 kimepanda wafanyabiashara wanapandisha bei vi2 kiholela,cjui hi nchi anaipeleka wap shida moja ukiwa juu humkumbuki wachini wamezidi ubinafsi,ningependa siku moja hi nchi tuwape japo upnzani miaka mitano alafu tuwaangalie tukiona wanazingua tuwatoe au ikiwezekana ccm watafute mtu mwngine wamumweke awe rais
 
Unaposimama katika nafasi ya mwananchi wa kawaida ndio utaelewa ninachomaanisha.

Ni majuzi tu nilisafiri kwenda Mozambique.

Ile nchi haijatulia na haijawahi kutulia lakini nimeshangaa kukuta bei ya mafuta ya kula ikiwa ni nafuu mno.

Bei ya mafuta ya Kula ya Tanzania ni zaidi ya mara mbili ya ile ya Msumbiji.

Dizeli, Petrol na Mbolea Msumbiji ni nafuu sana ukilinganisha na Tanzania, wanatuzidi wapi?

Nikirudi kwa mama, Mwaka mmoja wa kuwa madarakani kila kitu kimebadilika gharama za Maisha zimepanda mno, uonevu kwa wakulima wa Korosho umerudi upya.

Bei ya magari, TV, Computer n.k zimekuwa juu kabisa.

Kama hali itaendelea hivi uchaguzi unaofuata.
Still Kuna waimba mapambio wanapiga kelele za kinafiki, eti kaupiga mwingi. Kwa unafiki huu hata Mwenyezi Mungu tuna muudhi.
 
Unaposimama katika nafasi ya mwananchi wa kawaida ndio utaelewa ninachomaanisha.

Ni majuzi tu nilisafiri kwenda Mozambique.

Ile nchi haijatulia na haijawahi kutulia lakini nimeshangaa kukuta bei ya mafuta ya kula ikiwa ni nafuu mno.

Bei ya mafuta ya Kula ya Tanzania ni zaidi ya mara mbili ya ile ya Msumbiji.

Dizeli, Petrol na Mbolea Msumbiji ni nafuu sana ukilinganisha na Tanzania, wanatuzidi wapi?

Nikirudi kwa mama, Mwaka mmoja wa kuwa madarakani kila kitu kimebadilika gharama za Maisha zimepanda mno, uonevu kwa wakulima wa Korosho umerudi upya.

Bei ya magari, TV, Computer n.k zimekuwa juu kabisa.

Kama hali itaendelea hivi uchaguzi unaofuata.
Tozooo
 
Na ubaya wa vitu kupanda bei ni kwamba hata vikishuka havitarudi kwenye bei ile ya zamani, yani hapo mjue mambo ndo yanasonga mbele hivyo.

Mtu alikuwa analipwa 500K enzi za sabuni 200sh, leo hii sabuni ni 600 na mshara wake ni uleule.
 
Hata baadhi ya benki kuanzia tarehe 24 april wameweka matangazo kutakuwa na ongezeko la gharama za huduma.

Kuna mtu sehemu hana uwezo wa kutatua changamoto ni either waziri wa fedha au Gavana. Raisi yeye anapewa mapemdekezo tuu. Cha ajabu mishahara hata kutajwa juu juu tu kuwa itapanda kufidia gharama za bidhaa na huduma. Watu wetu wataishije zaidi ya rushwa na utapeli.
 
Kwa ufupi nionavyo mimi serikali ya ccm imeshindwa na haitaweza kuleta maendeleo tz kwasababu hawana sera nzuri ya kumkomboa mwananchi wa kawaida na utitili wa kodi.

Serikali ina matumizi makubwa sana. Wanatumia magari yenye gharama kubwa nayenye kutumia mafuta mengi. Rais wa ccm kitu kikubwa anachofikiria ni uchaguzi tu na kukibakiza chama madarakani kwa njia yoyote ile maana kuna genge kubwa lililojihalalisha kwamba keki ya taifa wanayokula isiwaponyoke kwa namna yoyote ile.

Mbaya zaidi serikali ya ccm sio wabunifu wa kujipatia mapato. Inchi ina rasilimali nyingi sana lakini linapokuja swala la kuongeza mapato ya Serikali, wanachoangalia ni kumkandamiza mwananchi wa kawaida kwa kumuwekea kodi lukuki na ndio sababu kubwa ya kila kitu kuwa na bei kubwa
 
Back
Top Bottom