Mkuu 'GAZETI' tatizo letu wengi, nikiwemo mimi na wewe ni hili ulilolionyesha kwenye mada yako hii!
Yaani tunamtazama kiongozi kwa darubini hafifu mno, kama hii ya bei za vitu, basi, tunaishia hapo. Hizo bei zikiwa chini kwa hiyo kiongozi anakuwa bora?
Naomba sana unielewe, sisemi kamwe kwamba bei za vitu kwa wananchi siyo swala muhimu, ni muhimu sana, lakini ni sehemu ndogo sana katika kumfanya kiongozi awe ni kiongozi mzuri.
Samia hana sifa za kuwa kiongozi mzuri, siyo tu kwa sababu anaruhusu bei zipande juu. Samia hana sifa za uongozi bora kwa sababu hajui anataka nchi hii ielekee wapi; hana dira., na kama anayo ni dira potofu ya kudhani kwamba nchi itaendelea kwa kutegemea watu toka nje kuleta maendeleo hapa.
Sasa hilo la Msumbiji, ulikotembelea, umeuliza kwa nini bei zao zipo chini? Mada yako ingesaidia sana hoja zako kama ungeeleza kinagaubaga kinachofanywa na viongozi wa Msumbiji, na kisichofanywa na Tanzania. Ungefanya hivyo, ingesaidia sana mada yako kueleweka.