Naunga mkono hoja, huu ndio ukweli wenyewe halisi, wanaopinga ni wanapinga tuu for the sake of kupinga tuu lakini ukweli huu nao wanauona kwa macho yao wenyewe!.
CCM inazidi kuimarika, kupendwa na kukubalika, hadi makapi ya ndani ya chama, yameanza kujichuja yenyewe!!, si mnaona!.
Na hapa ndio mwanzo tuu wa hizi amsha amsha!, kama ni mvua, hii ni rasha rasha tuu!, mvua halisi ni 2025!.
Ila pia kijana ni msikivu sana, alianza kwa moto sana, tukampooza
Pongezi Paul Makonda kuifufua CCM kwa amsha amsha. Twende mdogomdogo ngoma ikivuma sana inakaribia kupasuka! sasa anakwenda vizuri!.
Na kwa vile humu umezuka mtindo ukimkubali mtu ukamsifia na kumpongeza, huchelewi kuitwa chawa!,
angalia huyu dogo sisi kaka zake, tumeanza nae wapi.
Mimi nilianza nae hapa
Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam
Nikaja hapa
Mafanikio ya Makonda ni Uthibitisho Wa Jiwe walilolikataa Waashi litafanywa kuwa Jiwe Kuu la Pembeni
Alipopitia misukosuko tukasimama nae kwanza kwa kutoa wito
Ndugu, Jamaa na Marafiki, Njooni Tumtetee Makonda Dhidi ya Mapapa Wauza Unga Wanaomzushia... kisha tukamshauri
Kumbe ni Uongo, Uzushi, Fitna, Majungu, Wivu na Kijicho Dhidi ya Mafanikio Yake!. Makonda Wapuuze! .
Kuna watu wenye roho za kwanini tukawaambia
Wale mnaosubiri kwa hamu Makonda atumbuliwe, mtasubiri sana!. Ukiwa ni mpakwa mafuta, ni mpakwa mafuta!
Na mwisho nikapendekeza
Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana, kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!. Apunguze...
Hivyo mheshimiwa sana Mwenezi Makonda, piga kazi, tuko nyuma yako!
P