Ukweli usiosemwa juu ya dini za Kiafrika

Ukweli usiosemwa juu ya dini za Kiafrika

I used first person plural rather than singular because we're many. Even you you don't know about 'resurrection " I don't know even the meaning of the "the sign of the cross " I was even baptized blindly, I have realized that is better you understand before you believe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuna sababu kwanini imani za kiafrika hazikuwa na nguvu, nazo ni;

1) hazikuwa zikijitambua kama dini, kila kabila liliamini mizimu ya mababu zao kuwa iliwaunganisha na mungu (ni kama saints ktk ukatoliki), hivyo kila kabila na kila mtu alitegemea mababu zake, hakuna aliyeamini mababu wa wezake wangeweza kumsaidia

hiyo ikapelekea kujengeka kwa utamaduni wa kutotafuta wafuasi na waumini, (wakati uislamu na ukristo ni imani zinazotamani dunia nzima wafuate imani hizo)

hiyo ilipelekea kutokuwa na umoja miongoni mwa waafrika maana ilikuwa mtu akiacha kuamini mababu zake ama jamii nzima ikiacha kuamini mizimu ya mababu haikuwa ikionekana kama tatizo kwa wengine ambao wao hawakuona kitisho katika idadi yao, maana wao wakijiona hawahusiki na kuamuni mababu wa wezao , lilikuwa jambo lisilowahusu, hivyo hawakupinga ushawishi wa wamishionari katika kuwabadili waafrika wezao kufuata imani zisizo za kiafrika ( tofauti na ilivyo kusambaza dini mpya huko asia ama ulaya, ni kazi ngumu kila muumini hapendi kusikia wezie wa imani moja wana imani mpya, wao wana hamu dunia nzima waamini chao wao)

pia sie hatuna scriptures, wezenu wana bibbles, qurani, wahindu wana veda, pia wana makanisa, misikitu, temples nk

sisi hatuna

wezetu wana sikukuu zao sie hatuna

wezetu wana siku za ibada sie hatuna

wana miezi ya mfungo, japokuwa unaweza kudharau funga za waja kipindi cha mifungo ila huo huwa ni muda wa kuwakumbusha imani yao, mavazi nk, hivyo kuzidi kuwasimika na identity ya umani yao, kitu hicho afrika pia hatuna

halafu dini zetu zilikuwa ni za sababu maalum, huna mtoto, kuna magonjwa na vifo ndio unaenda kuabudu sio kwenda kuabudu kila jpili ama kila ijumaa

zilikuwa ni imani zisizoeleweka na viongizi wa dini hawakuwa na elimu hiyo ilipelekea kutumia vitisho na kutishatisha kuimarisha taswira zao. plus mambo ya kafara na uchawi, imani hazikueleweka zikaachwa
Ahsante sana
Nalog off
 
Ukienda kuhiji Makka unasamehewa dhambi zako unakuwa kama mtoto , !! jamani huu siupuuzi yaani unafanywa mtalii wenyewe wanapiga pesa wewe unadanganywa kusamehewa dhambi ahahahah
😂😂😂 Kumbe ndivyo ilivyo!
Nalog off
 
Rais moja Mzungu wa Afrika Kusini aliwahi kufanya utafiti juu uwezo wa Mwafrika Mweusi katika kufikiri, kutenda na kuongoza wengine .
Utafiti huu ulimwezesha kupata PHD.
Katika utafiti wake alihitimisha kwa kusema kuwa , " Mwafrika Mweusi mwenye Akili kuliko wote hawezi kufikiri zaidi ya mwaka moja. (The most Intelligent black African can not think beyond one year).
Hata hivyo hii sio asilimia mia moja kwa sababu bado wazungu walikiri kuwa Viongozi kama Hayati Mwalimu J.K.Nyerere walikuwa tofauti sana na dhana hii ya utafiti wa Mzungu huyu.
Mwafrika akikukuta unakula usipomkaripisha atakuita mlafi. Mwafrika akikukuta unafanya kazi akikusaidia atadai pesa.
Mzungu akikukuta unakula hata ukimkaribisha hatokula kama ulikuwa hujamwalika. Mzungu akikukuta unafanya kazi atakusaidia na hatakudai pesa.
Kuna kabila moja siwezi kulitaja jina, Vijana wao wakiwa sita wakienda kuiba ng'ombe, wataiba ng'ombe na watamuua mwenye Ng'ombe.
Baadaye wakiwa safarini kurudi kwao watatu watafanya hila na kuwaua wenzao watu.
Watatu wakifika salama na ng'ombe wa wizi mgawo unakuwa mzuri na hutoa taaifa kuwa wenzao wameuwawa wakati wanaiba ng'ombe.
Nataka niseme tu kuwa nasononeka sana na hulka ya Mtu mweusi kuhusu uchoyo, fitina, wivu, ulafi, majivuno, ukatili, uonevu na mengine mengi.
Udhaifu huu ndiyo unatufanya tusiendee pamoja na kuwa na raslimali nyingi.
Sasa hili Kabila si litaisha kwa kuuana wenyewe kwa wenyewe,😂😂😂
Nalog off
 
Mwandishi mwenyewe anajiita frustration badala ya kujiita majina kama Ngwanalabaka, Masopakyindi,Bujurugwa au Kereng'ende.

Uchawi walileta wazungu? Mwandishi hujasoma.nenda kasome the River Between na Things Fall Apart. Kapate hbr za kuabudu Mizimu n.k.

Mwandishi hujui kuwa uchawi,ushirikina ulikuwa Dunia nzima hata kwa hao wazungu. Nao walikuwa wana miungu yao na imani zao za hovyo hovyo. Za kutoa kafara binadamu kuuana n.k. na unatakiwa ufahamu hata wao Ukristo uliingiia kwao kwa shida sana na mateso. Kasome ufahamu Dark Ages ilikuwa ni nini.

Ni ukosefu wa fikra sahihi kukaa kulaumu wazungu kila wakati na tunafahamu madhara makubwa ya dini za kale.nenda kaangalie mabaki ya dini hizi shinyanga wanakoamini mtu mwenye macho mekundu ni mchawi. Nenda kaangalie watendaji wa dini hizi waganga,wapiga ramli n.k

Kaangalie imani za kutupa mapacha au kuua albino na walemavu. Kutoa sadaka watoto au binadamu.haya ni matatizo ambayo yalikuwepo hata ulaya na asia.dini hizi zilikuja kuyaondoa kwa kiasi kikubwa na kujenga ustaarabu ambao at least unaheshimu ubinadamu km ktk amri 10 za Mungu ni universal.

Waafrika tuache kulalamika na kulia lia hata kwa mambo yasiyo na msingi.kama kuna mabaya ktk dini hizi si tuyaache na tuyafanye mema?na mazuri ktk imani za kiafrika tuyachukue pia?

Suala ni kuanzia asia?then why wazungu hawalalamiki coz hawa wao si zao?mbona sisi afrika tuna mlima kilimanjaro na asia hawana husikii wakilalamika?nao wanakuja kuhiji(kutaliii tanzania)?

Waafrika mmpewa roho ya ulalamishi wa kipuuzi.basi tungekuwa tunajikwamua kuliko kukaa kulalamika.hii dini like ukristo siyo dini ya mataifa ya wazungu.wapo wengi tu wanaupinga.wapo waarabu uislamu ni utamaduni ndo hao wanaofurahi kukata vichwa au kuua wenzao.

Kama ilivyo tu nchi zetu za kiafrika.why malalamiko kila kona miaka nenda rudi?ugumu upo wapi waaafrika kuanzisha dini zao?nani kawazuia?kama kitu kipo strong kitasimama na kama ni weak kitajifia chenyewe au kitashindwa ku nourish/kustawi/kusurvive.

Tufanyeni kazi,tugundue vitu tuacheni kulalamika kila siku. Imani zetu za kiafrika ndizo zilitusaidia kubadilisha risasi ziwe maji katika majimaji war?na unadhani wazungi waliokuwa wanapigana nasi walikuwa na dini?kuitwa john speke ,david au hussein siyo kuwa dini hiyo yenye jina.

Na ndo maana umejiita frustration ila bado umebaki wewe mswahili.
 
Katika kitu kigumu sana kufanya katika karne hii ni kumwambia & kumbadilisha mwafrika atoke kwenye mlengo wake wa mawazo uliopandikizwa na mzungu na kurudi kwenye mlengo huru.
Sio kila Mtu yupo free kuruhusu mawazo huru.....


Sure
 
Mimi huwa wananichanganya tu pale mtu anaposema flani alikufa kwa dhambi zetu yani hizi dini jamani ni kuongopeana ty
 
Mkuu
Tutakaokuelewa ni wachache sana humu, watu wengi walishafanyiwa kitu ninachookiita " kuuwawa kwa tabia zao halisi" Yaani karibu kila kitu hapa Afrika kimeharibiwa. Angalia maisha yetu, mathalani lugha zetu, mavazi yetu, sayansi yetu, dini zetu, usomaji wetu, majina yetu n.k hadi unajiuliza hivi sisi watu weusi tutaacha alama gani hapa duniani!!!???

Kuna jamaa mmoja nilimponda tukiwa wengi kwa kumwita mtoto wake mchanga jina la kiingereza la ajabu ajabu kisa tu eti ni zuri (si ni la kizungu bwana) nilipomwambia kuwa asiendekeze utumwa wa fikra aliniita mimi mshamba yaani akasema sijaelemika! Nikamtazamaaaa, nikamwambia waziwazi mimi naitwa TATA MKURIA na najisikia fahari kuwaita watoto wangu majina yao kama Bhoke, Ghati,Marwa, Mwita n.k.

Mkuu Frustration hakuna bara linadharauliwa kidini kama Afrika! Yaani ni aibu, halafu waafrika hawa wa sasa tena wasomi wanaendelea kuwatumikia wale jamaa wakidhani wapo sahihi yaani waafrika tumeenda hatua zaidi ya wao kujiona hizi dini zao ni bora sana hadi zinatugombanisha! Zinafanya tuuwane! Ni aibu.

Ukienda mabara mengine, huwaambii kitu kuhusu dini zao! Kama hujui nenda nchi za Ulaya, nenda nchi za Uarabuni, nenda Uhindini, nk. Ila sasa njoo Afrika! Yaani akili zetu ni nyepesi nyepesi mno. Kila kitu kinaaminika kirahisi tu, tumesoma sasa lakini bado tunaendekeza yale yale yaliyotuletea madhila siku za nyuma. Tumelala fofofo tunadhani kila kitu kipo sawa. Yaani hadi nimewakumbuka Prof Ngugi wa Thiong'o na maelekezo yake katika kitabu cha "Decolonizing the Mind" pamoja na Okoth p'Bitek na vile vitabu vyake pendwa (najua wengi mlisoma kile maarufu Song of Lawino na Song of Ocol) hawa waafrika wenzetu wametuandikia tushtuke kidogo lakini bado tupo ziii!

Wale wenzangu wanaopenda dini zetu, tuendelee nazo ingawa tunaitwa washirikina mi nasema ni sawa tu nitaendelea kutambika ila siyo kwa kafara za watu kama hawa washenzi wa baadhi ya dini hizi za kisasa wanavyofanya!

Najua tupo wengi tu ingawa makanisani na misikitini pia tunaingia mara kwa mara ila mioyoni mwetu tunaujua ukweli na pia tumeisha enda wapi na wapi kupata tiba zetu za kujikinga na mabalaa. Ukituona kwa nje tuna heshima lukuki katika jamii ila kiundani tunaamini dini za Kiafrika kimya kimya.

Tata mkuria.
Tuko pamoja mkuu... Tawileeeee
 
kila siku watu wanajiuliza nani katuroga? hatujarogwa ila tumelaaniwa na mababu na miungu yetu kwa kuisaliti, kuikana na kiita 'imani potofu' kisha tumekumbatia miungu/mizimu ya kigeni. badala ya kuongea na 'mzimu' wa bibi yako anayekujua unakomaa na 'mzimu' wa bikira maria. Turudi kwenye njia zetu za mababu zetu.
Aisee safi Sana
 
mabara yote duniani yana mfumo wao wa kuabudu ambao ni tofauti na mabara mengine. Hii sio tu Afrika, hadi Amerika, Australia, Europe etc. Asia wameiteka sana Africa na ndio maana tamaduni za America mnaona kama wanakufuru hivi kwa imani za Asia. Ukiwa wa Asia anayofanya American ukitenda ww ni kosa na kinyume chake. Sasa sisi wa Africa tumeacha ya kwetu tunatenda ya Asia huoni ni kosa?. Kwa hiyo huyo Mungu alikaa miaka mingapi hadi alipowaambia watu sasa waweza enda Afrika nao mkawape habari zangu? Baada ya kutuumba tuliachwa wapi? Kwa imani uliyonayo basi tuseme GOD IS UNFAIR. katika nyanja zote eg kupendelea manabii na mitume katika bara la Asia tu.
Mbaya zaidi tunawaomba watakatifu wa kizungu watuombee, kwani Afrika hapakuwahi kuwa na watakatifu. China, Japan na nchi nyingine za bara la Asia wana practice dini zao na wako mbali kimaendeleo. Wazungu wenyewe hata kanisani hawaendi na wengi ukiwauliza wanasema hawana dini. Angalia diplomatic community za kutoka Ulaya, Marekani, yaani wengi hawana dini. Halafu wao mtu kuwa shoga ni human rights etc.

Pia watanzaniaa wengi wana practice dini 2. Yaani kila kukicha matatizo lukuki Africa huku viongozi wakijinasibu wanamjua Mungu kumbe unafiki tu. Nilishawahi kwenda Fiji, wale watu ni full mila zao. Kwenye ufunguzi wa hafla za kitaifa na kimataifa yanapigwa matambiko ya kufa mtu. Yaani more than one hour, tena yanafanywa public huku raisi akishuhidia.
 
Big up! Ila ulipochanganya tena kizungu umeshaingi utamadumi wao. Kuna mambo mazuri ya kuiga kutoka kwao achilia mbali mambo ya imani. Kwa imani tumepigwa sana.
 
Back
Top Bottom