Ukweli usiosemwa juu ya dini za Kiafrika

Ukweli usiosemwa juu ya dini za Kiafrika

Wapi ambapo wewe umepata hayo maelezo ya kuhusu makusudio ya Mungu kutuumba? Kwa sababu kuna wengine wanasema Mungu hajaeleza makusudio ya yeye kutuumba sisi hivyo hatuwezi kujua Mungu anatutaka tuishi vipi ila wewe unasema Mungu katuumba ili tuishi kwa upendo na umoja ndio maana nakuuliza wewe mwenzetu una connection gani hadi umeweza kujua kusudio la Mungu kutuumba?
Hakutakuwa na maana ya maisha bila ya upendo na amani
 
Sawa ila kusudio la Mungu kutuumba umejuaje kuwa ni hilo?
Tuliumbwa ili tuishi na thamani ya maisha ni upendo,furaha na amani. Vyote tunavyovifanya duniani ni kwa sababu ya upendo,furaha na amani
 
Tuliumbwa ili tuishi na thamani ya maisha ni upendo,furaha na amani. Vyote tunavyovifanya duniani ni kwa sababu ya upendo,furaha na amani
Mkuu unanilisha mawazo yako wakati unajua kila mtu anaweza kuwaza kivyake na ndiyo maana nimeeleza hapo watu wengine husema kuwa hajaweka wazi kusudio la kutuumba na wala hajishughulishi na jinsi tuishivyo.
 
Hicho kitabu unataka aandike nani ili kiwe reference kwako? Nambie ntampa material ili ukiona handwriting yake uamini.
Sasa mzee si ndio yaleyale uliyokuwa unasema kuwa mwafrika hataamini hadi reference itoke kwenye kitabu cha mzungu. Kwani andiko lako haliwezi kuwa reference kwa wengine siku za usoni?
 
Mimi naona hakuna jambo baya waafrika kuacha mila zetu kwa sababu siku zote inabid kufwata vitu vya mtu aliyekuzidi.

Tunafwata vya wazungu kwa sababu wametuzidi na kuwafwata na sisi twaweza barikiwa kama wao. Endapo tungewatawala basi wao ndo wangefwata mila zeti na tamaduni
 
Mimi naona hakuna jambo baya waafrika kuacha mila zetu kwa sababu siku zote inabid kufwata vitu vya mtu aliyekuzidi.
Tunafwata vya wazungu kwa sababu wametuzidi na kuwafwata na sisi twaweza barikiwa kama wao.
Endapo tungewatawala basi wao ndo wangefwata mila zeti na tamaduni
Wahindi, Wachina hawawafuata wao. Vipi una maoni gani juu ya hilo?
 
Dini za Waafrika ni vigumu sana kuzitenganisha na Mila na Desturi zao, hivyo mimi naona dini za kiafrika na Mila na desturi zao ni kitu kimoja kilekile. Waafrika tuna mila na desturi nyingi toifauti tofauti sana ambazo ni vigumu kuiita dini moja kama ilivyo kwa dini nyingine kubwa mbalimbalui duniani. Na katika mchanganyiko wa mila na desturi hizo mbalimbali zipo baadhi ni nzuri lakini pia ni lazima tukubali ukweli kwamba kuna nyingi mbaya zisizostahili kabisa kuwepo. Nitatoa baadhi ya mifano ya mila hizo mbaya na nzuri,

Mfano wa mila nzuri ni kama vile, kutahiri wanaume, kufanya matambiko ya kuchinja wanyama kama wafanyavyo makabila mengi mfano wachagga huomba miungu yao kwa kuchinja mbuzi, kondoo au ngombe sambamba na kuandaa pombe ya kienyeji(Mbege), mimi sioni mila kama hii ni mbaya hata kidogo kwani haimdhuru mtu yeyote na tena ilileta nidhamu kwa watu kuamini Ipo Nguvu juu yenye uwezo wa kuwaadhibu watendapo mabaya.

Kwa upande mwingine wa shilingi Waafrika tulikuwa na mila nyingine kwa kweli hata Wazungu kuita zilikuwa ni za kishenzi mimi sioni kama walituonea, kuna mila nyingine kwa akili ya kawaida kabisa huwezi ukazikubali, mila mfano ya kutahiri wanawake, kuzika machifu waliokufa wakiwa na watu waliokuwa hai, hebu imagine ni wewe unaambiwa eti uzikwe na maiti ya chifu ungali hai unapumua tena la kushangaza zaidi unaambiwa baadhi ya waliotakiwa kuzikwa na machifu, wenyewe walifurahia kitendo hicho! Kuna mila kama za kuua maalbino pindi tu walipokuwa wakizaliwa hivi, au kuwatupa misituni nk. Tukienda mbali zaidi kuna imani ambazo hata leo hii bado watu wanazo, imani za kishirikina hamna asiyetambua madhara yake katika jamii. Sasa utasemaje kuwa dini hizi zilikuwa zinatufaa?

Dini au mila za Waafrika hazina Mungu mmoja, kuna Miungu mingi kitu kinachosababisha mtu kushindwa kuziweka katika kundi moja, Tunachoweza kufanya Waafrika ni kuendeleza zile mila na tamaduni nzuri tu ambazo hazina madhara kwa binadamu. Kwa mfano mambo ya uganga na uchawi hayaeleweki, ni vitu vinavyofanyika kwa sirisiri, na ndio uliokuwa msingi wa dini zetu Waafrika. Sasa mambo kama hayo ya kifichoficho unawezaje kuyaita ni dini inayoweza kumsaidia mwanadamu? Huwezi kumtofautisha mganga na mchawi ni yupi kwani wote wanawadhuru binadamu. Wakati wachawi wakidaiwa kuwaloga watu lakini waganga nao wanalaumiwa sana kwa kusababisha uchonganishi, mauaji na machungu mengine mengi kwa kisingizio cha kuagua watu.

Kingine ni kwamba dini za Kiafrika hazikuwa na miongozo ya maandishi wala vitabu kama zilivyo za wenzetu, miongozo hiyo huwa ndio kama katiba au kanuni za kuziongoza.

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, dini hizi za Wazungum, Waarabu na Waasia japo nazo hazipo sahihi kwa asilimia mia moja lakini hauwezi ukazilinganisha na dini za Waafrika, inawezekana nazo zimesababisha madhara fulani kwa wanadamu lakini ni ukweli pia mafundisho yake yameleta ustaarabu kwa kiasi fulani Duniani. Kwanza zimeweza kuwaunganisha idadi kubwa ya watu duniani, zinahubiri kuwepo kwa NGUVU kuu kuliko zote(MUNGU), Zinahubiri ustawi wa binadamu kama suala la watu kuwa na afya njema, elimu na watu kutendeana mema. Dini ya namna hiyo sidhani kama ina ubaya kwa mtu labda tu kuwe na wapotoshaji katika dini husika wanaohubiri vitu vinavyoleta madhara mabaya kwa binadamu wengine.
 
Umu ndani kila mtu anamlalamikia muafrcia, ni muafrica yupi uyo? aya tusaidiane kwasisi wachache tuliokua apa ni hatua gani za awali mmeanza kuchukua ndugu zangu? maana uyo beberu katushika pabaya sana, 90% ya tunachotumia kimehusika na mzungu, Wengi mnalalamika utafikiri uyo muafrica hatokani na sisi, kama vijana waelewa ni solution ipi mmekuja nayo na mmeanza na hatua zipi za awali.
 
Hii sababu ya kutawaliwa, kutawaliwa ni kubaya sana, waafrika tumepoteza vitu vingi sana vya maana. Usidanganyike ndugu waafrika tuna dini zetu nzuri sana kutojua na hazina tofauti yoyote ile kubwa na hizi dini za mapokeo.
 
Mkuu
Tutakaokuelewa ni wachache sana humu, watu wengi walishafanyiwa kitu ninachookiita " kuuwawa kwa tabia zao halisi" Yaani karibu kila kitu hapa Afrika kimeharibiwa. Angalia maisha yetu, mathalani lugha zetu, mavazi yetu, sayansi yetu, dini zetu, usomaji wetu, majina yetu n.k hadi unajiuliza hivi sisi watu weusi tutaacha alama gani hapa duniani!!!???

Kuna jamaa mmoja nilimponda tukiwa wengi kwa kumwita mtoto wake mchanga jina la kiingereza la ajabu ajabu kisa tu eti ni zuri (si ni la kizungu bwana) nilipomwambia kuwa asiendekeze utumwa wa fikra aliniita mimi mshamba yaani akasema sijaelemika! Nikamtazamaaaa, nikamwambia waziwazi mimi naitwa TATA MKURIA na najisikia fahari kuwaita watoto wangu majina yao kama Bhoke, Ghati,Marwa, Mwita n.k.

Mkuu Frustration hakuna bara linadharauliwa kidini kama Afrika! Yaani ni aibu, halafu waafrika hawa wa sasa tena wasomi wanaendelea kuwatumikia wale jamaa wakidhani wapo sahihi yaani waafrika tumeenda hatua zaidi ya wao kujiona hizi dini zao ni bora sana hadi zinatugombanisha! Zinafanya tuuwane! Ni aibu.

Ukienda mabara mengine, huwaambii kitu kuhusu dini zao! Kama hujui nenda nchi za Ulaya, nenda nchi za Uarabuni, nenda Uhindini, nk. Ila sasa njoo Afrika! Yaani akili zetu ni nyepesi nyepesi mno. Kila kitu kinaaminika kirahisi tu, tumesoma sasa lakini bado tunaendekeza yale yale yaliyotuletea madhila siku za nyuma. Tumelala fofofo tunadhani kila kitu kipo sawa. Yaani hadi nimewakumbuka Prof Ngugi wa Thiong'o na maelekezo yake katika kitabu cha "Decolonizing the Mind" pamoja na Okoth p'Bitek na vile vitabu vyake pendwa (najua wengi mlisoma kile maarufu Song of Lawino na Song of Ocol) hawa waafrika wenzetu wametuandikia tushtuke kidogo lakini bado tupo ziii!

Wale wenzangu wanaopenda dini zetu, tuendelee nazo ingawa tunaitwa washirikina mi nasema ni sawa tu nitaendelea kutambika ila siyo kwa kafara za watu kama hawa washenzi wa baadhi ya dini hizi za kisasa wanavyofanya!

Najua tupo wengi tu ingawa makanisani na misikitini pia tunaingia mara kwa mara ila mioyoni mwetu tunaujua ukweli na pia tumeisha enda wapi na wapi kupata tiba zetu za kujikinga na mabalaa. Ukituona kwa nje tuna heshima lukuki katika jamii ila kiundani tunaamini dini za Kiafrika kimya kimya.

Tata mkuria.
Mkuu mko sawa kabisa. Miaka ya hivi karibuni namimi nimestuka, baada ya kuona hali inavyokwenda. Kiukweli Niseme kuwa ' Things has fallen apart' Ukichanganya Rangi, Ufukara ni wepesi mtu mjanja kupandikiza uongo ikawa kama gundi kichwani.

Just imagini kuna Mchungaji alikuwa hana kitu, kaja na mbwembwe za kuombea watu wenye shida mbalimbali, alikuwa wakawaida lakini alifanikiwa kuwa anakuja na wazungu anawaita mbele wanasalimia waumini, ila malazi nachakula, Kanisa lina wahudumia. Mbaya zaidi huwezi kutaja mchango kimya kimya, unapewa microphone ukiwa mbele ya waumini, ili ushangiliwe.

Niseme tu kwa ufupi, sasahivi huyo mchungaji amenunua Gorofa Masaki na anaendesha ' HAMA" na VX magari ya kifahari. Mishahara yao naijua ukifanya hesabu mpaka kustaafu kwake hata bei ya gari moja haitoshi. Sasa najiuliza Msisitizo wa saadaka mbona ni kila wakati? Kumbe walio wengi wanadhani wanamtolea Mungu kumbe ni zake na ni Tax free!!!
Waafrika tumeshachemka tayari, bora Mababu zetu hawakuwahi kukutana na utapeli kwa kusingizia Mungu na kuwaambia walipe fungu la kumi na malimbuko na sadaka rukuki huku wakiendelea kuwa masikini wa kutupwa, huku wachungaji wakifanikiwa kuwa matajiri wa kutupwa.

Kwa hali iliyopo sasa Viongozi wa kiserikali wasipoingilia kati, umasikini utaongezeka kwani hata katikati ya wiki kuanzia saa 4 za asubuhi kuna kuwa na Ibada na maombi siku 40. Sasa najiuliza, hivi ni Mungu gani anayetumia muda mwingi kwenye maombi? Kazi za kumletea mtu kipato zinafanyika saa ngapi?. ' HILI NI JANGA JIPYA KWENYE HIZI DINI ZA KIDHUNGU"
 
Inategemeana na Kabila lako,ongea na wazee watakupa dini na usipate tabu kwa sababu dini ni jina tu ila ni namna ya kufanikisha mambo kiimani na kiroho. Mfano mila ya mti aina ya Horo na matambiko. Mungu wa Afrika anapenda yale mambo na ndio maana akatuumba black. Miungu iligawana mabara sio kwa bahati mbaya kama udhaniavyo.
Umetowa wpi hii kuwa miungu iligawana mabara? Leteni ushahidi ili mutupe nguvu ya hoja.
 
Afrika ina dini ambazo ni nyingi sana kuliko bara lolote lile Duniani. Dini hizi nyingi zimepigwa ban na watu wa nje (whites) kwa sababu tu ya inferior ya mtu mweusi wa zamani. Kuishi kwa kumtegemea mzungu kwa kila kitu hadi ikapelekea hadi sasa watu wanategemea pia dini za Kizungu.

Hakuna kabila hata moja Afrika ambalo limepoteza imani ya dini yao, ndio maana hata waendao makanisani hutembelea kwa mababu zao kupata kinga. Dini zote Afrika zilikuwa hazihusiani na uchawi ila mtu mweupe ndiye aliempa mtu mweusi uchawi kwa mafunzo maalumu akimdanganya ya kiimani.

Uchawi Afrika uliletwa na mzungu na ukweli huu haupingiki. ukiachana na hayo lakini pia upande wa maadili hapa nianze kwa salamu

U hai? ndugu hata kama haupo hai ila ukweli ukifikie huko huko ulipo. Nani aliyekuambia kuwa Afrika watu walikuwa wanavaa nguo full mwili mzima? Angalia wamasai japo na hao pia wamejaribu kubadilika. Ila hali ilikuwa mbaya sana zamani.

Watu walikuwa wanazuii tupu tu, Vikande vyote vya nyuma vilikuwa wazi na hakukuwa wa kushangaa katika hili kwa sababu ndiko tulikotoka. Ujio wa white man ukatibua hali ya hewa wakabadili,mtindo wa mavazi,dini, elimu, lugha, biashara na kila kitu.

Sasa katika mambo waliobadili pamoja na nidhamu na kusema nchi za Afrika hawajastarabika kwa sababu wanatembea uchi, wanaabudu madudu, wanaongea lugha chafu n.k. Watu wa Afrika walilazimishwa kukopi mila na mitindo yote ya Kizungu.

Unaposema vijana wetu hawana maadili ni kutukana wazee wetu wa zamani ambao walikuwa wanawinda,na kupiga ngoma uchi.

Hawa wapuuzi wa kizungu ndio walioita matabibu wetu kwa jina baya eti Matabibu wa kichawi(witch doctor) na wao kujiita Doctors, physician mara sijui wakemia n.k. Wakasema kupiga ngoma ni ushamba ila tupige miziki ya kisasa n.k.
Sioni jema la wazungu katika imani, wala tamaduni na wala technology kwa sababu naamini tungepigana na hali zetu. Wale wanaoenzi mababu zetu siku hizi wanajiita TIBA MBADALA sijui ndio nini.

Wajiite wauguzi na wataalamu wa tiba na magonjwa mbalimbali.

Afrika without White's countries is possible, hatujachelewa sana tuanze ku uphold vya kwetu ili vitusaidie na sisi kwa masilai yetu. Hivi vya kuletewa havitufai kwani "NGUO YA KUAZIMA HAISITIRI MA**KO" na ndio mana mambo hayaendi kama ilivyotakiwa.

Nawachukia wa Asia na dini zao i.e Christian and Muslims. Wewe ndugu yangu mtoto na mjuu wa Likangamai hayo mambo utayaweza? Ndiyo maana kulikuwa na mabala na aina ya watu na mila tofautitofauti, sasa ya nje ya nini na kuona kama vile ulichelewa kuvipata?

Kwani wao walikuwa hawajui kama Afrika kuna watu? mbona wamefika baada ya manyanyaso mauaji na dhulma kwa ndg zetu? Nini za Asia ni dini za ukweli kwa Asia na dini za Afrika ni za kweli kwa Afrika tu?

Jambo gani jema limewahi semwa na hao watu juu ya mababu zetu? wamewatukana sana kupitia imani zao na leo wamefanikisha kutufanya ndg,jamani tunaenda wapi na ilihali tunakotoka tunakudharau?

NAIPENDA AFRIKA SANA NA HATA NIKIWA JIRANI NA MZUNGU WOTE WE FEEL DIFFERENCES ON EACH AND EVERYTHING.RELIGION, LANGUAGE, STYLES,CUSTOMS, COLOUR, AWARENESS, ASSERTIVENESS STATUS, RECOGNITION e.t.c.
Ukweli haupingiki hata mniue hadi nife

TO MAKE THINGS VERY CLEAR

Wachangiaji wengi ambao hawakubaliani na mtazamo wa mada hii,hoja hii wamejikita kwenye mizimu. Naomba nifahamishe kwamba mizimu ni jina la MTU yeyote wa taifa lolote na Rangi yoyote aliyekufa na kuaminika bado anaishi katika hali ya gesi (invisible & intangible).

GHOST: the soul of a dead person thought of as living in an unseen world or asappearing to living people: .
Hivyo basis neno MIZIMU (GHOST) lisitumike tu negatively kuponda watu waliokufa Afrika.

Pia Milima, miti mikubwa, mapango etc kwa Afrika ilikuwa teknolojia pekee kwa wakati huo kama icon & symbol (alama) ya watu kukutana na siyo walikuwa wanaabudu hivyo vitu vilivyotajwa hapo na vifananavyo.

Watu walikuwa wanaomba Mungu kupitia waliotangulia kwani kwa nyakati hizo walikuwa kioo na dira pekee na walikuwa wanafanikisha kwa imani hiyo.

To be continued soon.

Umejenga hoja murua kuzisemea dini za kiafrika.
Lakini mimi napata shida moja,kule kwetu Giningi kuna mahali wachawi wanakutana kufanya wayafanyayo ya kimila.

Kule Rufiji hujengwa vibanda vya kinyamkela,
Kule moshi ndowatu huenda kwenye mlima Uleee mrefu K/Njaro NK ,lakini waabudu hao wote hakuna andiko wala dalili ya kimaono iliyowazi kushuhudia uwepo wa yule wanayemuabudu.
Wote wanamuabudu au kumtumikia Shetani ambaye hutolewa matambiko na kuondowa mateso kwa wamuaminio.

Kweli watu waliheshimu hizo mila na kuwa na nidhamu fulani,ila hakuna hatua yoyote iliyofuatia baada ya kucheza ngoma na kula vibudu,watu hawa walibaki mafukara ,wagonjwa,na hawakuwa nauwezo wa kuyamudu mazingira yao wenyewe,Mpaka walipokuja wageni wenye dini za kiasia na kuanza kuwaelimisha dini zao na elimu zao na kuwasaidia kujiboresha kimazingira.

Hakuna mwafrika hata mmoja aliyegundua chchote cha kumsaidia binadamu zaidi ya kuvaa magome ya miti na panga na mkuki wa kuwindia ,basi.
Hatukujuwa na bado hatujuwi thamani ya Madini tuliyonayo kwenye nchi zetu wenyewe.Hio miungu yetu haikutusaidia lolote na haitusaidii hadi leo pamoja na kuwa bado baadhi yetu tunaikweza na kuipa matambiko.

Uuwaji wa Maalbino na kutowa kafara mbali mbali kule migodini hakukusaidia kuitowa dhahabu wala Tanzanite kwenye migodi na kuileta juu ili tupate maslahi.lakini Wazungu wameleta Mamashine makubwa ambayo kwayo milima hutawanywa na Dhahabu kutolewa na kuwanufaisha wachimbaji husika.

Magari,Matreni,Ndege,na baskeli zote hutoka kwao.ndo maana wakisema hata wao kuwa ni miungu tunaweza tukawa na sababu ya kuwaabudu.Kwa kuwa wanacho cha kutonesha cha maajabu na ambacho sisi hatuwezi kukitengeneza.Hii computer na Simu ni maajabu tosha ya kuamini kuwa mvumbuzi wake anaweza kuitwa mungu.lakini waungu wale wa kunywa damu na kupigiwa ngoma ni lazima watoweke sasa na hawana tena watu wa kuwaamini isipokuwa mapunguwani.

sasa hapa swali ni moja
NI IPI DINI SAHIHI NA YA KWELI? NITAKUFUNULIA UKINIHOJI
 
Mkuu
Tutakaokuelewa ni wachache sana humu, watu wengi walishafanyiwa kitu ninachookiita " kuuwawa kwa tabia zao halisi" Yaani karibu kila kitu hapa Afrika kimeharibiwa. Angalia maisha yetu, mathalani lugha zetu, mavazi yetu, sayansi yetu, dini zetu, usomaji wetu, majina yetu n.k hadi unajiuliza hivi sisi watu weusi tutaacha alama gani hapa duniani!!!???

Kuna jamaa mmoja nilimponda tukiwa wengi kwa kumwita mtoto wake mchanga jina la kiingereza la ajabu ajabu kisa tu eti ni zuri (si ni la kizungu bwana) nilipomwambia kuwa asiendekeze utumwa wa fikra aliniita mimi mshamba yaani akasema sijaelemika! Nikamtazamaaaa, nikamwambia waziwazi mimi naitwa TATA MKURIA na najisikia fahari kuwaita watoto wangu majina yao kama Bhoke, Ghati,Marwa, Mwita n.k.

Mkuu Frustration hakuna bara linadharauliwa kidini kama Afrika! Yaani ni aibu, halafu waafrika hawa wa sasa tena wasomi wanaendelea kuwatumikia wale jamaa wakidhani wapo sahihi yaani waafrika tumeenda hatua zaidi ya wao kujiona hizi dini zao ni bora sana hadi zinatugombanisha! Zinafanya tuuwane! Ni aibu.

Ukienda mabara mengine, huwaambii kitu kuhusu dini zao! Kama hujui nenda nchi za Ulaya, nenda nchi za Uarabuni, nenda Uhindini, nk. Ila sasa njoo Afrika! Yaani akili zetu ni nyepesi nyepesi mno. Kila kitu kinaaminika kirahisi tu, tumesoma sasa lakini bado tunaendekeza yale yale yaliyotuletea madhila siku za nyuma. Tumelala fofofo tunadhani kila kitu kipo sawa. Yaani hadi nimewakumbuka Prof Ngugi wa Thiong'o na maelekezo yake katika kitabu cha "Decolonizing the Mind" pamoja na Okoth p'Bitek na vile vitabu vyake pendwa (najua wengi mlisoma kile maarufu Song of Lawino na Song of Ocol) hawa waafrika wenzetu wametuandikia tushtuke kidogo lakini bado tupo ziii!

Wale wenzangu wanaopenda dini zetu, tuendelee nazo ingawa tunaitwa washirikina mi nasema ni sawa tu nitaendelea kutambika ila siyo kwa kafara za watu kama hawa washenzi wa baadhi ya dini hizi za kisasa wanavyofanya!

Najua tupo wengi tu ingawa makanisani na misikitini pia tunaingia mara kwa mara ila mioyoni mwetu tunaujua ukweli na pia tumeisha enda wapi na wapi kupata tiba zetu za kujikinga na mabalaa. Ukituona kwa nje tuna heshima lukuki katika jamii ila kiundani tunaamini dini za Kiafrika kimya kimya.

Tata mkuria.
Acha kwenda kanisani kabisa. Uendelee kutambika. Acha kuwa ndumilakuwili. Usiionee haya hiyo imani/dini yako ya Kiafrika unayoipenda huku unaiendea kwa kujificha. Hakuna atakaekuzomea.
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, dini hizi za Wazungum, Waarabu na Waasia japo nazo hazipo sahihi kwa asilimia mia moja lakini hauwezi ukazilinganisha na dini za Waafrika, inawezekana nazo zimesababisha madhara fulani kwa wanadamu lakini ni ukweli pia mafundisho yake yameleta ustaarabu kwa kiasi fulani Duniani. Kwanza zimeweza kuwaunganisha idadi kubwa ya watu duniani, zinahubiri kuwepo kwa NGUVU kuu kuliko zote(MUNGU), Zinahubiri ustawi wa binadamu kama suala la watu kuwa na afya njema, elimu na watu kutendeana mema. Dini ya namna hiyo sidhani kama ina ubaya kwa mtu labda tu kuwe na wapotoshaji katika dini husika wanaohubiri vitu vinavyoleta madhara mabaya kwa binadamu wengine.
umesema sawa 100% niko pamoja na wewe umefafanua vilivyo na nadhani hata mimi umenifilisi. ☑ 👍
lakini hapa kidogo ulipo sema ''japo nazo hazipo sahihi kwa asilimia mia moja'' panahitaji uchambuzi.mdoogo.
Miungu ipo mingi kama zilivyo dini zenyewe,Ila miungu hio inajifafanua kutokana na imani husika nakwa hiyo dini hiyo huwa sahihi kwa mujibu wa hichi kitabu naimani iliyomo humo kwa waamini wake tu.
lakin iko dini Inayoziunganisha dini zooote ambayo imezi taja na kuzikosowa na kutowa njia ya kati iliyo nyooka kwa ini zote ,kwa mujibu wa dini hiyo,hizo dini zote zimejumlishwa na kufanywa moja na Muumba mwenyewe.
 
Back
Top Bottom