Ukweli usiosemwa juu ya dini za Kiafrika

Pamoja sana kiongozi.
 
Sisi waafrika tunapoteza vitu vyetu hata leo. Tukubali tu wenzetu wametuzidi katika umakini na kujali iwe kwa sababu ya miungu yao au sababu tofauti..

Suala la ulinzi wa dini,
Mfano. Wayahudi. Kwenye maandishi ya Biblia na historia yao kwa vitabu vingine vinaonesha wamekuwa chini ya tawala nyingine kwa vipindi tofauti tofauti na kwa muda mrefu.
Biblia inawaonesha wakianzia Misri ambako hadi watawala wa Misri wakaona ni jamii tishio kwa utamaduni wao maana waliweza hifadhi mila na dini yao wakiwa ugenini.
Wakiwa chini ya wafilisti, wasirya,wakaaldayo, waajemi na hata warumi bado waliweza kuhifadhi dini yao na tamaduni zao hata kwa kuzipigania.

Hata baada ya ukristo na uislam leo dini ya kiyahudi ipo. Na hawa ukristo haukuanza juzi tulipoletewa sisi, tunongelea miaka karibu 2000 iliyopita. Sisi tulishindwa nini kulinda hizo dini zetu kwa kipindi cha miaka 300 tu?

Kumiliki historia na kuilazimisha dini iendane na matakwa ya tamaduni husika,
Ukiacha wayahudi wagiriki na wazungu kwa walioathiriwa na ukristo na uislam baadaye walitakiwa kulalamika kama sisi. Maana hizi hazikuwa dini zao kabla. Lakini wameweza kutunza tamaduni zao hata bado wana majina yao yasiyo ya kidini mpaka leo pamoja na kwamba ukatoliki ulitawala sana huko kwao. Zaidi waliweka utamaduni wao kwenye dini ya myahudi na kulazimisha wengine kufuata hayo.

Sisi huku utamaduni na dini zimevurugwa na hakuna kumbukumbu maalum za kuhusu hizo dini. Hatuna taarifa sahihi zaidi ni speculations kuhusu dini. Kama wenzetu wanawezaa kufuatilia miungu ya kigiriki, ni nani leo anaweza akatueleza hiyo miungu tulokuwa nayo. Nani anaweza kutuambia miiko ya hizo dini.

Uchawi ni mbadala wa dini sio tu kwetu; Uchawi uko dunia nzima na kila jamii inajua ni namna ya kutafuta roho za kishetani kama mbadala kwenye maisha. Hatuwezi kusema uchawi ni dini.

Wachawi wanatajwa tangu babeli, na viongozi wa kidini wa babeli pia hutajwa. Maana wote walikuwepo. Na sasa hata jamii zingine zinazodini na wachawi wapo na tafsiri zetu zinarandana. Nadhani uchawi wetu haukuathirika ila ulipata adui mwingine.

Ninachokiona tukiri kwa uwazi jamii yetu ilikuwa dhaifu katika misingi ndio maana tumepoteza vitu vingi na bado tunaendelea kupoteza. Hatuwezi rudi nyuma kutumia nyenzo walizoshindwa babu zetu tupigane nazo kwenye mazingira ya leo. Muhimu ni kutengeneza upya historia yetu. Na katika hili, uchumi unaweza kubadilisha historia. Leo watu wanasoma Kichina baada ya china kuwa kinara kwenye uchumi. Miaka 50 nyuma isingekuwa muhimu kabisa.

Tupambane tuache kusukumizia wazungu.
 
Mwandiko wako ni mzuri mkuu ila unaandika haraka haraka unakimbilia wapi sasa kwa maana umeachia uzi hewani bila kuupq sapoti ya kutosha
 
Kwani kuna wanaomjua mungu? akina nani hao wanaomjua mungu. Mungu ni mawazo ya binadamu ili kutatua shida zake

Hili huwezi kuthibitisha mpaka kiyama kinasimama.

Mimi namjua Mola wangu aliyeumba mbingu na ardhi na vyote vilivyomo.
 
Viva mkuu. Na katika hili hatuwezi sema sasa kwa kuwa dini zetu zimepotea basi sasa tufuate tu hizi za majambazi na majangila wa Afrika. Kama tunavyopigania katika raslimali za nchi madini,gas,meno ya wanyama na wanyama, samaki etc zisiendelee kupotea, basi hata dini nazo pia lazima tupiganie. Tutafanya tena tafiti ili kurudisha. Mbona wafuasi wa bible na wao walipoteza? na sasa wapo katika masimulizi(hearsay) tu.
 

Waafrika walithibitisha vipi hili ?
 
Hili huwezi kuthibitisha mpaka kiyama kinasimama.
Mimi namjua Mola wangu aliyeumba mbingu na ardhi na vyote vilivyomo.
Sema mm namjua mola wa Asia kwa masimulizi ya vitabu vyao. Yaani ww umjue Mungu na nikikuuliza yupo vipi na anataka nn huwezi nijibu. Unajifariji tu kusema unamjua hapo ndugu umejificha kwenye kichaka cha karanga kuzani huonikani.
 
Mwandiko wako ni mzuri mkuu ila unaandika haraka haraka unakimbilia wapi sasa kwa maana umeachia uzi hewani bila kuupq sapoti ya kutosha
Nakubali ila kuna uwanja wa kuuliza,kusapoti n.k. Simu ya tecno hii na opera yake.
 
Waafrika walithibitisha vipi hili ?
Kwani wao walithibisha kama watakuwa wanafufuliwa na kugawa katika makundi mawili. Huwezi sibitisha katika hilo ndugu yangu.
 
Sema mm namjua mola wa Asia kwa masimulizi ya vitabu vyao. Yaani ww umjue Mungu na nikikuuliza yupo vipi na anataka nn huwezi nijibu. Unajifariji tu kusema unamjua hapo ndugu umejificha kwenye kichaka cha karanga kuzani huonikani.

Usinichagulie cha kujibu bali mimi ninajua ninachokijibu na kukiamini na kukiandika.

Kama wewe ulishindwa kumkingia kifua Mungu wako wa Afrika na ukakiri ya kuwa humjui sio mimi,kwani mimi nilianza kwanza kusomeshwa ndio nikaamini.

Nakariri tena na tena "MIMI NINA MJUA MOLA WA ULIMWENGU NA VYOTE VILIVYOMO"
 
Dini zote hizo kati ya uislam na uyahudi na ukristo zote ni za kujinufaisha wao kwanza zimekuja kwa masimango

Quran na bible zimejaa uongo zimekithiri stori za abunuwasi lengo wapate kututawala

Kiuhalisia kufata dini za nje ni utumwa wa kifikra na tena ni mbaya sana haiwezekani mtu akae Roma au Makka akupangie uishi vipi huu ni utumwa mkubwa
 
Kwani wao walithibisha kama watakuwa wanafufuliwa na kugawa katika makundi mawili. Huwezi sibitisha katika hilo ndugu yangu.

Umeelewa swali langu ? Inakuwaje unauliza swali unapo ulizwa swali ?
 
Wafuasi wa biblia kwa zama tofauti walikuwa wanajikumbusha na kuanza mianzo mipya.
Wayahudi walikuwa wanarejea maandiko ya mababu wa karne huko na kuamua kubadilika kabisa kiasi cha kuwa tayari kuua, kufukuza na kuharibu.

Sisi mpaka sasa hatuna hata hizo rejea. Hatujui kuelezea namna walivyokuwa wanatunza kumbukumbu kama walikuwa wanatunza.
Tumechanganyika sana.
Mfano. Mimi ni kizazi cha tatu cha mchanganyiko wa makabila na nikijaliwa watoto watakuwa kizazi cha nne.
Tunamfukuza nani? Tunafuata dini ya kabila gani maana hakuna hata fununu za dini iliyohusisha makabila kadhaa. Tunafuata utamaduni wa kabila gani.
Halafu hili sio sisi tu. Wazungu nao walikuwa na jamii ndogo ndogo ambazo zinaendelea kumezwa na jamii kubwa. Kuendekeza kwamba ndio chanzo cha matatizo yetu basi kinamna fulani tunakuwa tumepotoka.

Kama tunaacha labda tufanye walosema hakuna Mungu wakakomaa na maisha halafu pole pole wanaanza kulinda dini za kifamilia kama wachina. Pengine baadaye zitajirudi tena.
 
Hapa tunapaswa kujadili kwa mapana yake tena bila kuchoka ili tuelimike
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…