nasrimgambo
JF-Expert Member
- Jan 10, 2017
- 1,902
- 2,488
kuna sababu kwanini imani za kiafrika hazikuwa na nguvu, nazo ni;Mkuu
Tutakaokuelewa ni wachache sana humu, watu wengi walishafanyiwa kitu ninachookiita " kuuwawa kwa tabia zao halisi" Yaani karibu kila kitu hapa Afrika kimeharibiwa. Angalia maisha yetu, mathalani lugha zetu, mavazi yetu, sayansi yetu, dini zetu, usomaji wetu, majina yetu n.k hadi unajiuliza hivi sisi watu weusi tutaacha alama gani hapa duniani!!!???
Kuna jamaa mmoja nilimponda tukiwa wengi kwa kumwita mtoto wake mchanga jina la kiingereza la ajabu ajabu kisa tu eti ni zuri (si ni la kizungu bwana) nilipomwambia kuwa asiendekeze utumwa wa fikra aliniita mimi mshamba yaani akasema sijaelemika! Nikamtazamaaaa, nikamwambia waziwazi mimi naitwa TATA MKURIA na najisikia fahari kuwaita watoto wangu majina yao kama Bhoke, Ghati,Marwa, Mwita n.k.
Mkuu Frustration hakuna bara linadharauliwa kidini kama Afrika! Yaani ni aibu, halafu waafrika hawa wa sasa tena wasomi wanaendelea kuwatumikia wale jamaa wakidhani wapo sahihi yaani waafrika tumeenda hatua zaidi ya wao kujiona hizi dini zao ni bora sana hadi zinatugombanisha! Zinafanya tuuwane! Ni aibu.
Ukienda mabara mengine, huwaambii kitu kuhusu dini zao! Kama hujui nenda nchi za Ulaya, nenda nchi za Uarabuni, nenda Uhindini, nk. Ila sasa njoo Afrika! Yaani akili zetu ni nyepesi nyepesi mno. Kila kitu kinaaminika kirahisi tu, tumesoma sasa lakini bado tunaendekeza yale yale yaliyotuletea madhila siku za nyuma. Tumelala fofofo tunadhani kila kitu kipo sawa. Yaani hadi nimewakumbuka Prof Ngugi wa Thiong'o na maelekezo yake katika kitabu cha "Decolonizing the Mind" pamoja na Okoth p'Bitek na vile vitabu vyake pendwa (najua wengi mlisoma kile maarufu Song of Lawino na Song of Ocol) hawa waafrika wenzetu wametuandikia tushtuke kidogo lakini bado tupo ziii!
Wale wenzangu wanaopenda dini zetu, tuendelee nazo ingawa tunaitwa washirikina mi nasema ni sawa tu nitaendelea kutambika ila siyo kwa kafara za watu kama hawa washenzi wa baadhi ya dini hizi za kisasa wanavyofanya!
Najua tupo wengi tu ingawa makanisani na misikitini pia tunaingia mara kwa mara ila mioyoni mwetu tunaujua ukweli na pia tumeisha enda wapi na wapi kupata tiba zetu za kujikinga na mabalaa. Ukituona kwa nje tuna heshima lukuki katika jamii ila kiundani tunaamini dini za Kiafrika kimya kimya.
Tata mkuria.
1) hazikuwa zikijitambua kama dini, kila kabila liliamini mizimu ya mababu zao kuwa iliwaunganisha na mungu (ni kama saints ktk ukatoliki), hivyo kila kabila na kila mtu alitegemea mababu zake, hakuna aliyeamini mababu wa wezake wangeweza kumsaidia
hiyo ikapelekea kujengeka kwa utamaduni wa kutotafuta wafuasi na waumini, (wakati uislamu na ukristo ni imani zinazotamani dunia nzima wafuate imani hizo)
hiyo ilipelekea kutokuwa na umoja miongoni mwa waafrika maana ilikuwa mtu akiacha kuamini mababu zake ama jamii nzima ikiacha kuamini mizimu ya mababu haikuwa ikionekana kama tatizo kwa wengine ambao wao hawakuona kitisho katika idadi yao, maana wao wakijiona hawahusiki na kuamuni mababu wa wezao , lilikuwa jambo lisilowahusu, hivyo hawakupinga ushawishi wa wamishionari katika kuwabadili waafrika wezao kufuata imani zisizo za kiafrika ( tofauti na ilivyo kusambaza dini mpya huko asia ama ulaya, ni kazi ngumu kila muumini hapendi kusikia wezie wa imani moja wana imani mpya, wao wana hamu dunia nzima waamini chao wao)
pia sie hatuna scriptures, wezenu wana bibbles, qurani, wahindu wana veda, pia wana makanisa, misikitu, temples nk
sisi hatuna
wezetu wana sikukuu zao sie hatuna
wezetu wana siku za ibada sie hatuna
wana miezi ya mfungo, japokuwa unaweza kudharau funga za waja kipindi cha mifungo ila huo huwa ni muda wa kuwakumbusha imani yao, mavazi nk, hivyo kuzidi kuwasimika na identity ya umani yao, kitu hicho afrika pia hatuna
halafu dini zetu zilikuwa ni za sababu maalum, huna mtoto, kuna magonjwa na vifo ndio unaenda kuabudu sio kwenda kuabudu kila jpili ama kila ijumaa
zilikuwa ni imani zisizoeleweka na viongizi wa dini hawakuwa na elimu hiyo ilipelekea kutumia vitisho na kutishatisha kuimarisha taswira zao. plus mambo ya kafara na uchawi, imani hazikueleweka zikaachwa