Mkuu
Tutakaokuelewa ni wachache sana humu, watu wengi walishafanyiwa kitu ninachookiita " kuuwawa kwa tabia zao halisi" Yaani karibu kila kitu hapa Afrika kimeharibiwa. Angalia maisha yetu, mathalani lugha zetu, mavazi yetu, sayansi yetu, dini zetu, usomaji wetu, majina yetu n.k hadi unajiuliza hivi sisi watu weusi tutaacha alama gani hapa duniani!!!???
Kuna jamaa mmoja nilimponda tukiwa wengi kwa kumwita mtoto wake mchanga jina la kiingereza la ajabu ajabu kisa tu eti ni zuri (si ni la kizungu bwana) nilipomwambia kuwa asiendekeze utumwa wa fikra aliniita mimi mshamba yaani akasema sijaelemika! Nikamtazamaaaa, nikamwambia waziwazi mimi naitwa TATA MKURIA na najisikia fahari kuwaita watoto wangu majina yao kama Bhoke, Ghati,Marwa, Mwita n.k.
Mkuu
Frustration hakuna bara linadharauliwa kidini kama Afrika! Yaani ni aibu, halafu waafrika hawa wa sasa tena wasomi wanaendelea kuwatumikia wale jamaa wakidhani wapo sahihi yaani waafrika tumeenda hatua zaidi ya wao kujiona hizi dini zao ni bora sana hadi zinatugombanisha! Zinafanya tuuwane! Ni aibu.
Ukienda mabara mengine, huwaambii kitu kuhusu dini zao! Kama hujui nenda nchi za Ulaya, nenda nchi za Uarabuni, nenda Uhindini, nk. Ila sasa njoo Afrika! Yaani akili zetu ni nyepesi nyepesi mno. Kila kitu kinaaminika kirahisi tu, tumesoma sasa lakini bado tunaendekeza yale yale yaliyotuletea madhila siku za nyuma. Tumelala fofofo tunadhani kila kitu kipo sawa. Yaani hadi nimewakumbuka Prof Ngugi wa Thiong'o na maelekezo yake katika kitabu cha "Decolonizing the Mind" pamoja na Okoth p'Bitek na vile vitabu vyake pendwa (najua wengi mlisoma kile maarufu Song of Lawino na Song of Ocol) hawa waafrika wenzetu wametuandikia tushtuke kidogo lakini bado tupo ziii!
Wale wenzangu wanaopenda dini zetu, tuendelee nazo ingawa tunaitwa washirikina mi nasema ni sawa tu nitaendelea kutambika ila siyo kwa kafara za watu kama hawa washenzi wa baadhi ya dini hizi za kisasa wanavyofanya!
Najua tupo wengi tu ingawa makanisani na misikitini pia tunaingia mara kwa mara ila mioyoni mwetu tunaujua ukweli na pia tumeisha enda wapi na wapi kupata tiba zetu za kujikinga na mabalaa. Ukituona kwa nje tuna heshima lukuki katika jamii ila kiundani tunaamini dini za Kiafrika kimya kimya.
Tata mkuria.