Ukweli usiosemwa juu ya dini za Kiafrika

Wahindu na mabudha si ndio wanaabudu ng"ombe,watu na sanamu.Huoni kwao kukiwa na ushirikina??

Kulala chini ng"ombe akubariki na mguu au kumsujudia mtu hio nayo ni akili??

Dini za asili si ndio zimewafanya baadhi ya waarusha watoboe masikio yao na chuma yakawa mabaya kama ya tembo?

Hivi unajua jamii zote za kiafrika ziliwakeketa watoto wa kike kwa kuufyeka utamu wao.Huo si ushirikina wa dini mbovu za asili.??

Dini mpya zimetutoa kwenye ushirikina mwingi sana,,ile evil forest ya kitabu cha okonkwo unajua ni msitu wa ukweli? Na watu waliopotoka na mizimu walitupa huko mapacha ya watoto?

 

Ukijifunza zaidi juu ya Hindunism au Budism..haya unayoyaona ni ushirikina yatabadili mawazo yako..

Ngombe/Torus/Bull ni symbol kama alivyo yesu..
Sasa kama nyny pia mnaabudu ushirikina kwa kusujudia masanamu na mapicha ya mzungu mliekaririshwa kua ni yesu hamna tofauti
 
Yesu sio symbol,,na ng"ombe anaetembea pia hawezi kuwa symbol..Japo uzuri kuna wahindu wengi wamezikataa hizo dini za asili za kishirikina.

 
Ulichoandika kama ww ni wa Asia upo sahihi sana. Unatumia knowledge ya dini za Asia kuponda dini zetu, ila jua sio kila kitu kilichofanywa na waafrika( e.g kuua mtu mweupe kwa madai ni dhambi. ) ilikuwa ni dini hapana mambo mengine yalifanywa kinyume na dini. Mabaya ya hao waAsia huyajui? au Kwa kuwa dini yao hairuhusu kuihoji na kuichambua?
Sioni ubaya wowote wa dini zetu ila kama utazitazama kwa mtazamo wa kikristo au kiislamu basi utaona hizi dini za Afrika ni rubbish (upuuzi). Na mm ninaetazama dini za Asia kwa mtazamo wa dini za Afrika pia naziona ni upuuzi tena mkubwa tu. Mfumo wao ni waukandamizaji na unyonyaji huku hofu ndio lengo kuu la dini na sio tumaini la maisha baada ya maisha. Mambo

Wameweka masharti mengi ili kuenda mbinguni au peponi hadi unahisi huyo mungu anatukomoa au aliumba ili awatese watu. Mungu wa Afrika ametueleza tufanye yale tunayoyafanya na hayana shida kwake na ndio maana tulikuwa tunaishi kwa amani sana.

Wamekuja mabanditi wakapora kila kitu, dini, elimu, biashara, mazao, madini, etc na nashangaa wengi walalama juu ya unyonyaji wa mtu mweupe kwa mwafrika ila upande wa dini wanaona wamefanya sawa.
Wametuachia mfumo feki wa elimu na hadi Sasa tunazalisha mapropesa tu.

Ushahidi wa dunia ni duara, moja ya sababu ni uduara(mviringo) wa sayari zingine kwenye mfumo wa solar, hizo hii inafanya kueleweka kuwa dunia pia ni duara. Hivyo hivyo kwa kuwa elimu walioleta ni feki, maadili yao ni feki na kila kitu walichofanya Afrika ni kwa malengo ya kuitesa na kuikandamiza Afrika, tunaweza sasa sema pia hata dini zao ni feki.

Biashara ya utumwa ilianzishwa na dini baada ya kuona wao ni binadamu na wasio wao ni wanyama kama wanyama wengine hivyo hata mungu wao alihalalisha biashara ile ya utumwa na ukoloni.
 
 
Yesu sio symbol,,na ng"ombe anaetembea pia hawezi kuwa symbol..Japo uzuri kuna wahindu wengi wamezikataa hizo dini za asili za kishirikina.
Ww yesu ni symbol ya mungu wa asia yaani yy(yesu)alisimama badala ya mungu wao. Yesu ni kiwakilishi cha mungu wa Asia.
 
Mimi hapo tu mwisho alipotupia na kakingereza tena,ndio aliponivuruga. Tutawapingaje sasa kama hivyo,mnashuka tena kwa lugha zao?
 
Mimi hapo tu mwisho alipotupia na kakingereza tena,ndio aliponivuruga. Tutawapingaje sasa kama hivyo,mnashuka tena kwa lugha zao?
Lugha ni namna ya mawasiliano kwa mada hii Lugha sio tatizo tatizo ni baada ya maisha haya ni kweli tutakuwa hatujawaudhi hata waliotangulia? pamoja na mungu wetu?.

Kuna vitu sisi tumevipata kwa kufanya biashara na hao wazungu, e. g nguo, lugha, technology etc. na hata wao wanavyakwetu huko makwao ila still wanazichukia dini zetu.
 
Mimi ni mzaliwa huku huku Africa mbagala kibonde maji..ila sijaona uzuri wa dini ya kiafrika.Kama dini ndio iliwasukuma hao watu watufanye watumwa basi jua tungekuwa tunaenda kufanya kazi mashamba ya kanisa au msikiti,,Mbona babu zetu wakaenda kufanya kazi mashamba ya watu binafsi.

Mbona waliokuja kukomesha hio biashara huku walikuwa wamishenari.

Tuna bahati ya kuwa na lugha ya kiswahili,,hivi kwa nini hatuna herufi zetu.Hizi dini ya asili zilisaidiaje kielimu na kuweka hata kumbukumbu ya civilization yetu yoyote,,?? Au kumbukumbu yake ni kwa makungwi kukata visi.mi vya dada zetu ambavyo ni utamu wao.?

Dini za asili zilikuwa janga kubwa sana,,kwa mfano mimi ni mkristo sijaona popote Mungu akasema yeye ni wa Asia pekee,,ila ni Mungu wa mbingu na dunia nzima.
Ww yesu ni symbol ya mungu wa asia yaani yy(yesu)alisimama badala ya mungu wao. Yesu ni kiwakilishi cha mungu wa Asia.
 

Ndugu huo ukristo mpaka unafika hapo ulipo umefanyiwa masahihisho kibao, hata sisi with time tungefanya marekebisho. Hiyo Roman yenyewe imefanyiwa marekebisho kibao mpaka ikafika mahali Martin Luther akaamua kuanzisha Uprotestant nae akaja na marekebisho kibao. Na mpaka sasa naskia wanajadili mapadri kuoa japo kabla walikua wanaoa ila Pope flani akakatanza.

So tusidanganyane tukajidharau kisa hao wazungu na huo utamaduni wao wanao tuaminisha, hata sisi wazee wetu walikua wamestaarabika. Hata hao wazungu walitoboa sana maskio na mpaka leo nadhani kunamachizi wanashindana kutoboa miili. Imani tulikua nazo tena nzuri tu kwa wakati wake. Wakiabudu ng'ombe wanapungukiwa nini??!! Wanakua masikini na kupigana vita na magonjwa kama Africa?

Hao wazungu na ukristo wao mbona ndo washenzi kabisa. Marekebisho mapya kwenye Ukristo ndoa za jinsia moja zinafungwa kanisani na mistari inasomwa kwenye Biblia. Bure kabisa.
 
Je hao wahindu kufuata asili ndio chanzo cha wao kuwa na maisha mazuri?? Ninavyojua nao wanastrugle,,

Kwani ubaya wa ukristo ni nini kwetu sisi? Ndio umetuletea umaskini.
Huoni chanzo cha umaskini wetu ni zaidi ya dini?

Wazungu wameamua kufanya haramu na jinai ya ndoa za jinsia moja,, huoni ni jambo lililoanzia kwenye mfumo wa kiserikali zaidi ya Kanisani??

Huoni kwamba kanisa limekuwa victim mkubwa wa jinai hii??Kwa kutokana na kila mahali kuwa na wanafki wakubwa tena wanaopaswa kifo huoni ndio walioanzisha makanisa mapya yenye agenda sawa na hii hali ya kukubaliana na jinai hii??

Nikimaanisha wakristo wa kweli wasio wanafki na wapumbaf hawakubali hata kutaka kusikia ndoa za jinsia moja...
Je unajua kwa serikali ya marekani kwa sasa kuwa na baadhi ya wakristo ndio kitu kimepunguza kutangaza na kuendelea kueneza jinai hii??

Na watu waliokuwa wakristo wakauacha kurudia dini zao za asili ndio hao wasioogopa kushabikia suala la ndoa za jinsia moja ambazo zimekatazwa ndani ya biblia.
 
Hoja ya nani binadamu na nani sio binadamu ilisababisha waliojioma binadamu kuwa wao ndio watawala wa dunia hii. Katika biashara ya utumwa wazungu hawakujua kama mtu mweusi ni mtu kama wao na wao waliona waafrika kama punda, ng'ombe etc. Ss walituita wanyama pori (wild beast) nenda google kasechi Africans are wild beast na utakuta mengi tu ya juu ya namna walivyotuzania.

Mungu wa Asia anajinadi kuwa yy ni mungu wa miungu yote yaani ni mungu mkuu. Sasa katika hili ww ulitaka waseme vipi? Huyo mungu angekuwa wa dunia yote basi angewatuma mitume na manabii wazunguke dunia yote kuhubiri.

Mungu wa Asia ndio maana hajibu maombi na mlichobakia nacho ni tumaini tu feki la ukifa utakuwa salama mbele ya safari. Mungu wa Asia ni mpenda sifa mambo yote mema ni yake na mabaya yote ni ya shetani how come this my fellow?

Tena anajinadi kamuumba hadi shetani ilihali shetani sio kiumbe Cha kuumbwa . Dini haina msaada kwa maisha ya mwanadamu na huu ni ushaidi mwingine kuwa dini zao ni feki na ni project tu dhidi ya mataifa.
 
Wanaziba pamba masikio yao, maaskofu mashoga wapo wengi ila hili utasikia ni suala la mtu binafsi. Dini sa Asia ni siasa na uwongo mwingi na uhariri mwingi.
 
Sijajua umelewa kiasi gani ila unatakiwa pia kujua upande wa pili upo vipi
 
Hayupo mtu hata mmoja Duniani ambaye huwa anabisha kuwa Yesu hakuwahi kuwepo. Angalia Kalenda tunayotumia mapak leo Dunia nzima
 

Nielewe ndugu, ukristo mpaka umefika hapa umepitia marekebisho mengi sana, hata dini zetu za asili zingepitia marekesho tungeendana na wakati tu, tatizo tuliaminishwa vyekwetu ni upuuzi mtupu wakati kulikua na mazuri mengi tu.

Matekeo yake tumekuaa watumwa wa kifikra na kitamaduni. Halafu ndoa za jinsia moja ziko kanisani sio kwa wapinga ukristo. Askofu Tutu mwanae msagaji na hakuwahi kumsema vibaya. Anglikan wameruhusu au wao sio wakristo? Ishu ni kwamba dini zetu zilikua na maana na kama zingepitia marekebisho kama RC na Uprotestant tungekua poa tu. siukatai Ukristo ila usiwe zana ya kuhukumu utu wangu kihistoria.
 
Niliwahi kuandika kuhusu Ubuntu, harakati ya kufufua dini za kiasili za kiafrika zinazoendelea Afrika Kusini.

Marekani pia kuna jamaa anaitwa Maulana Karenga na yeye pia ameanzisha harakati ya kufufua utamaduni za kiasili. Ulianzishwa mwaka 1966 na inaitwaa KWANZAA na imebase juu ya lugha adhimu ya kiswahili. Wikipedia inaeleza kuwa "Kwanzaa celebrates what its founder called the seven principles of Kwanzaa, or Nguzo Saba (the seven principles of African Heritage), which Karenga said "is a communitarian African philosophy," consisting of what Karenga called "the best of African thought and practice in constant exchange with the world."
Nguzo hizi saba ni:

l Umoja (Unity): To strive for and to maintain unity in the family, community, nation, and race. l Kujichagulia (Self-Determination): To define and name ourselves, as well as to create and speak for ourselves.

l Ujima (Collective Work and Responsibility): To build and maintain our community together and make our brothers' and sisters' problems our problems and to solve them together.
l Ujamaa (Cooperative Economics): To build and maintain our own stores, shops, and other businesses and to profit from them together.

l Nia (Purpose): To make our collective vocation the building and developing of our community in order to restore our people to their traditional greatness.

l Kuumba (Creativity): To do always as much as we can, in the way we can, in order to leave our community more beautiful and beneficial than we inherited it.

l Imani (Faith): To believe with all our hearts in our people, our parents, our teachers, our leaders, and the righteousness and victory of our struggle. Wikipedia inasema watu millioni sita huko marekani na duniani kote ni millioni 20, wanasheherekea sikukuu ya Kwanzaa kila mwaka kuanzia Dec 26 mpaka Jan 01. Mkuu Frustration, baada ya safari ya bondeni kuchunguza Ubuntu, nashauri uende Marekani ukachunguze na hii ya Kwanzaa!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…