Mkuu Tata, hata hao wazungu unaowalaumu walikua na dini zao kama ambavyo wafrika wanavyodai wana dini yao. Lakini swali la kujiuliza: je, ni dini ipi ya wafrika ambayo wafrika wanadai ni yao, ambayo wazungu hawakuwa nayo?
Kwa hakika hakuna dini kwa maana ya Mungu au miungu ambayo wafrika wanasema ni yao ambayo wazungu hawajakuwa nayo. Hakuna!
Kama ni dini za uongo-miungu, wazungu ndiyo wameanza.
Kilichopo leo Afrika, ambacho wafrika wanadai kuwa ni dini yao na kuitumikia ni uongo. Kama ilivyo kwa wafrika nyakati zetu na hata mababu zetu waliotutangulia walikataa ukristo kwa uongo huo wa kuwa tuna dini yetu. Hata wazungu walikataa ukristo kwa madai, dhana na upotofu kama huu huu tulionao Afrika.
Shida kubwa ya Afrika ni elimu. Wafrika hatujawa na elimu. Hatuelewi dini ni nini, inaundwa na mini na ina sifa gani. Lakini pia wafrika siyo tu kwamba hatujaweza kuandika historia ya maisha ya vizazi vyetu, lakini hatuna elimu ya historia ya ulimwengu na mwanadamu.
Sasa kama hatuna tu elimu na uelewa wa jambo dogo la historia ya ulimwengu na maisha ya mwanadamu yalivyoanza itawezekanaje kwa jambo kama dini?