Ukweli Usiosemwa Kuhusu Watu Wako wa Karibu Kwenye Safari ya Mafanikio

VN Warehouse Limited

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2023
Posts
1,139
Reaction score
1,156
Habari wana JF,

Kuna jambo wengi huligundua wakiwa wamechelewa -sio kila mtu wa karibu yako atakuwa tayari kukuona ukipiga hatua kubwa kuliko yeye.

Na hapa nisisemee vibaya:
Watu wengi wa karibu wanaweza wakawa wanakutakia mema kwa dhati. Wanapenda ufanikiwe. Wanakuombea. Wanakutia moyo.

Lakini kuna tofauti kubwa kati ya:

•Kutaka ufanikiwe

na

•Kuwa tayari kukuona ukizidi mafanikio yao.

Hapo ndipo ukweli mchungu unapojitokeza.

Saikolojia ya kulinganisha (Comparison effect)

Kibinadamu, watu hujilinganisha na waliokaribu nao - ndugu, marafiki, wanaokulia nao pamoja.
Ukianza kupiga hatua kubwa, mafanikio yako yanakuwa kama kioo kinachoonyesha hali zao.

Sio kwamba wanakuchukia.
Lakini maendeleo yako yanawakumbusha maeneo ambayo wao hawajafika.

Na hilo linaweza kuzaa:

•Wivu wa kimya kimya
•Maneno ya kukukatisha tamaa
•Au ushauri unaokurudisha nyuma

2. Comfort zone ya kijamii

Kila kundi la watu lina kiwango chake cha kawaida cha maisha.
Mnapokuwa wote mko level moja, hakuna presha.

Lakini mmoja akianza kubadilika:

•Anabadilisha mindset
•Anabadilisha marafiki
•Anabadilisha malengo
•Anabadilisha matumizi

Ghafla anaonekana “amebadilika”.

Ukweli ni kwamba hajabadilika vibaya - amekua.
Lakini ukuaji wako unaweza kuvuruga utulivu wa wengine.

3. Historia yenu inawafanya wakuzoee

Watu waliokujua kabla hujafanikiwa wana picha ya zamani yako.
Wanakuona kama yule mtu wa jana.

Hivyo wakikuona leo unafanya makubwa, akili zao zinapata shida ku-update hiyo picha.

Ndiyo maana mara nyingi support ya kweli huja kutoka kwa watu wasiojua historia yako ya zamani.

4. Hofu ya kupoteza nafasi

Wakati mwingine mtu wa karibu anaweza kuogopa:

•Utamzidi kipato
•Utabadilisha circle
•Utapunguza muda nao
•Au hata utapoteza utegemezi fulani waliokuwa nao

Hivyo bila kujua, wanaanza kukudrag chini kwa maneno kama:

•Hiyo biashara si rahisi
•Usijitie presha sana
•Mbona unakimbilia sana mafanikio?

Wanaweza wasijue wanachofanya, lakini matokeo yake ni kukurudisha kwenye kiwango chao cha comfort.

Ukweli wa mwisho

Watu wengi wa karibu watakutakia mema - lakini wachache sana watasherehekea mafanikio yako bila kujisikia kuguswa ndani yao.

Hii haimaanishi uwachukie.
Haimaanishi uwatenge.
Haimaanishi uwachukulie vibaya.

Inamaanisha tu ujifunze kitu kimoja muhimu:

Usitarajie support kubwa kutoka kwa kila aliye karibu na wewe.

Maisha yanakuwa rahisi sana pale unapojifunza:

•Kufanya mambo yako bila kutafuta approval
•Kufanya kazi kimya kimya
•Kupunguza matarajio kutoka kwa wengine
•Kujitegemea kihisia

Kadri unavyopunguza matarajio, ndivyo unavyopunguza maumivu.

Na kadri unavyojitegemea zaidi, ndivyo unavyokuwa huru zaidi kupiga hatua.

Safari ya mafanikio si ya kundi kubwa.
Ni safari ya watu wachache wanaoamua kuvumilia upweke, misunderstanding na maneno ya pembeni.

Ukishajua ukweli huu mapema, utaepuka maumivu mengi.
 
Screenshot_20260217_181936_Facebook.jpg
 
Habari wana JF,

Kuna jambo wengi huligundua wakiwa wamechelewa -sio kila mtu wa karibu yako atakuwa tayari kukuona ukipiga hatua kubwa kuliko yeye.

Na hapa nisisemee vibaya:
Watu wengi wa karibu wanaweza wakawa wanakutakia mema kwa dhati. Wanapenda ufanikiwe. Wanakuombea. Wanakutia moyo.

Lakini kuna tofauti kubwa kati ya:

•Kutaka ufanikiwe

na

•Kuwa tayari kukuona ukizidi mafanikio yao.

Hapo ndipo ukweli mchungu unapojitokeza.

1. Saikolojia ya kulinganisha (Comparison effect)

Kibinadamu, watu hujilinganisha na waliokaribu nao - ndugu, marafiki, wanaokulia nao pamoja.
Ukianza kupiga hatua kubwa, mafanikio yako yanakuwa kama kioo kinachoonyesha hali zao.

Sio kwamba wanakuchukia.
Lakini maendeleo yako yanawakumbusha maeneo ambayo wao hawajafika.

Na hilo linaweza kuzaa:

•Wivu wa kimya kimya
•Maneno ya kukukatisha tamaa
•Au ushauri unaokurudisha nyuma

2. Comfort zone ya kijamii

Kila kundi la watu lina kiwango chake cha kawaida cha maisha.
Mnapokuwa wote mko level moja, hakuna presha.

Lakini mmoja akianza kubadilika:

•Anabadilisha mindset
•Anabadilisha marafiki
•Anabadilisha malengo
•Anabadilisha matumizi

Ghafla anaonekana “amebadilika”.

Ukweli ni kwamba hajabadilika vibaya - amekua.
Lakini ukuaji wako unaweza kuvuruga utulivu wa wengine.

3. Historia yenu inawafanya wakuzoee

Watu waliokujua kabla hujafanikiwa wana picha ya zamani yako.
Wanakuona kama yule mtu wa jana.

Hivyo wakikuona leo unafanya makubwa, akili zao zinapata shida ku-update hiyo picha.

Ndiyo maana mara nyingi support ya kweli huja kutoka kwa watu wasiojua historia yako ya zamani.

4. Hofu ya kupoteza nafasi

Wakati mwingine mtu wa karibu anaweza kuogopa:

•Utamzidi kipato
•Utabadilisha circle
•Utapunguza muda nao
•Au hata utapoteza utegemezi fulani waliokuwa nao

Hivyo bila kujua, wanaanza kukudrag chini kwa maneno kama:

•Hiyo biashara si rahisi
•Usijitie presha sana
•Mbona unakimbilia sana mafanikio?

Wanaweza wasijue wanachofanya, lakini matokeo yake ni kukurudisha kwenye kiwango chao cha comfort.

Ukweli wa mwisho

Watu wengi wa karibu watakutakia mema - lakini wachache sana watasherehekea mafanikio yako bila kujisikia kuguswa ndani yao.

Hii haimaanishi uwachukie.
Haimaanishi uwatenge.
Haimaanishi uwachukulie vibaya.

Inamaanisha tu ujifunze kitu kimoja muhimu:

Usitarajie support kubwa kutoka kwa kila aliye karibu na wewe.

Maisha yanakuwa rahisi sana pale unapojifunza:

•Kufanya mambo yako bila •kutafuta approval
•Kufanya kazi kimya kimya
•Kupunguza matarajio kutoka kwa wengine
•Kujitegemea kihisia

Kadri unavyopunguza matarajio, ndivyo unavyopunguza maumivu.

Na kadri unavyojitegemea zaidi, ndivyo unavyokuwa huru zaidi kupiga hatua.

Safari ya mafanikio si ya kundi kubwa.
Ni safari ya watu wachache wanaoamua kuvumilia upweke, misunderstanding na maneno ya pembeni.

Ukishajua ukweli huu mapema, utaepuka maumivu mengi.
madini sana mkuu,hongera sana kwa uwezo wa kuchambua mambo
 
Unaweza ukashangaa unapewa ushauri wa biashara au kazi Fulani kuwa ni mbaya Sana na haifai kabisa, mtu anayekupa huo ushauri hajawahi hata kufanya hiyo biashara au hiyo kazi...Washauri wengi TZ wa kuhusu biashara au kazi wala si wahusika wa hizo sehemu Bali wengi ni maneno ya kusikia na kutabiri Tu...Mada nzuri Sana.

KUSEMA KWELI MCHAKATO WA MAFANIKIO HUWA UNA UPWEKE MWINGI SANA
 
kupunguza upweke kunywa kapombe shomari.....
 
Back
Top Bottom