Ukweli wa alichokisema Sheikh Kipozeo kuhusu Diamond

Ukweli wa alichokisema Sheikh Kipozeo kuhusu Diamond

Wewe na huyo Kipozeo wote mambumbu hamjui kitu, mmedandia treni la waarabu tu mnapelekwa kama ng'ombe. Ule msalaba aliovaa Diamond sio wa Yesu, ile inaitwa Ethiopian cross na Rastafari wengi wanavaa ile kitu. Naweza kusema aina ya muziki na collable na Morgan Heritage ndio maana Diamond akavaa kwenye video. Mwambie Kipozeo atafute kazi ya kufanya maana hajui kitu.
Kipozeo kafanya kazi sahihi. Yeye ni mwalimu wa dini na ni jukumu lake kumkumbusha diamond kama muislam mwenzie. Msalaba iwe wa marasta au wa mapasta kwenye uislam haukubalik. Msalaba ni ishara ya laana. Kipozeo sio wa kutafuta kazi ya kufanya. Hapo kafanya kazi yake
 
Huyu nae kaona Diamond ndio muislamu wa kwanza kuvaa msalaba? by The way Mungu wetu Sote! Kinachonikera toka kwa Waislamu ni Ubaguzi wao! Sasa huyo anaongelea nn hapo
Kwa upuuzi wako huwezi kuelewa. Ile ni dini yenye utaratibu wake. Na moja kati ya utaratibu ni kukumbushana. Sometimes sio lazima utangaze ujinga na chuki zako
 
Ona maswali yako ya kizwazwa shehe mmoja alipata kusema [emoji117]
69a689b4fc9221911a3e201542423118.jpg
hebu kachukue udhu dogo[emoji12]
Huyo SHEHE UBWABWA ,,si kila mwenye kanzu ni shehe.....hakuna kitu kama hicho....
 
Yes u ni Mungu Kamili na Mwanadamu Kamili[emoji123] [emoji106] kataa sasa MWENYEZI Kihivyo Uwezo huo Hana [emoji4]
Hivi MUNGU amezaliwa? MUNGU kabebwa,,,MUNGU anakula na kujisaidia kama binadamu wengine?MUNGU analala?MUNGU anapigwa makofi na kusulubiwa? hivi mnajuwa sifa za MUNGU?kama YESU NI MUNGU basi hata wale wanaochonga KINYAGO na kusema ni MUNGU wapo sahihi,, labda nikueleze sifa za MUNGU, ,,KWANZA MUNGU ni mmoja tu....hana mshirika,,.hana rafiki wala hakuzaa wala hakuzaliwa,,,,hanywi wala hali wala halali,, na hafanani na chochote na AKISEMA KUWA INAKUWA......YESU ni mtume wa MUNGU kama mitume mingine iliyopita......aliyeletewa INJILI...NA ALIKUJA KWA MATAIFA 12 ya wana wa ISRAEL....
 
kiukweli wabongo tunapenda kushabikia stori za ajabu-ajabu sana.
ona kama hivi watu wanabishana kuhusu mshenzi-mshenzi taipu tu mnamuita MUNGU
 
Wewe na huyo Kipozeo wote mambumbu hamjui kitu, mmedandia treni la waarabu tu mnapelekwa kama ng'ombe. Ule msalaba aliovaa Diamond sio wa Yesu, ile inaitwa Ethiopian cross na Rastafari wengi wanavaa ile kitu. Naweza kusema aina ya muziki na collable na Morgan Heritage ndio maana Diamond akavaa kwenye video. Mwambie Kipozeo atafute kazi ya kufanya maana hajui kitu.

Wewe unaejua hebu tueleze historia ya msalaba na utatu mtakatifu. Kama unasema kweli kwamba msalaba wa yesu ni tofauti na msalaba wa Ethiopia tueleze ni lini wakristo walianza kutumia msalaba kama kweli wewe ni mkweli
 
Adhabu ya msalaba ni kwa watu walio mkufuru Mungu (kukana hakuna Mungu au kuabudu sanamu). Musa aliwaadhibu baadhi ya wana Israel kwa kuwasulubu msalabani baada kufanya ibada ile ya ng'ombe.
Ndio maana Yesu alipopelekwa kwa Pilato 'charge sheet' yake ilikuwa 'amekufuru kwa kujifanya mwana mungu'. Alipo ulizwa juu ya hilo, Yesu alikana kwa kusema 'hayo ni madai yao ni si yeye aliyedai hivyo ! (alijibu; wewe wasema !) na imeandikwa katiaka Kumbukumbu 20;22. Amelaaniwa awaye yeyote awambwaye msalabani.
Utawasikia Wakiristo wanasema 'Yesu alifanywa laana' ili sisi tuokoke !
Uislaam unakataa, Yesu hawezi kufa kifo cha laana kwani alikuwa ni Nabii wa haki kwa wana israeli (bani israel)
eden kimario
We jamaa ni muongo mpaka basi kumbukumbu tangu lini ikawa na habari za Pilato na yesu
 
Luka anaandika Injil kama nani !?
Alikuwa miongoni mwa wanafunzi 12 !?
Soma Luka 1;1
Yesu hakuwa na wanafunzi hao 12 tu
Walikuwa zaidi ya 70
Hao 12 ni wale walioapa kufa nae tu
 
MWANA WA MUNGU WA PEKEE



5- MWANA WA MUNGU WA PEKEE

Katika Injili nne ziliomo katika Biblia Yesu Kristo ametajwa mara kadhaa wa kadhaa kwa jina la "Mwana wa Mungu". Ifuatayo ni baadhi ya mifano yake:



Basi yule akida, aliyesimama hapo akimwelekea, alipoona ya kuwa alikata roho jinsi hii, akasema, Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu.

Marko 15.39



Huyo akida anayetajwa hapo juu ni mpagani wa Kirumi mwenye kuamini wanaadamu wanakuwa miungu, hata mfalme wao wakimwita kuwa ni mungu na mwana wa mungu.



Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.

Luka 1.35



Wakasema wote, Basi, wewe ndiwe Mwana wa Mungu? Akawaambia, Ninyi mwasema kwamba mimi ndiye.

Luka 22.70



Amemtegemea Mungu; na amwokoe sasa, kama anamtaka; kwa maana alisema, Mimi ni Mwana wa Mungu.

Mathayo 27.43



Na pepo wachafu, kila walipmwona, walianguka mbele yake, wakalia wakisema, Wewe ndiwe Mwana wa Mungu. Akawakataza sana, wasimdhihirishe.

Marko 3.11-12



Naye alipofika ng'ambo, katika nchi ya Wagerasi, watu wawili wenye pepo walikutana naye, wanatoka makaburini, wakali mno, hata mtu asiweze kupitia njia ile. Na tazama, wakapiga kelele, wakisema, Tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je! umekuja kututesa kabla ya muhula wetu?

Mathayo 8.28-29



Katika Injili za Mathayo, Marko na Luka, Yesu ameitwa mara 22 kwa jina la "Mwana wa Mungu", lakini hata mara moja yeye mwenyewe hakujiita kwa jina hilo. Katika Mathayo 27.43 tuliyonukulu hapo juu yanatajwa maneno ya wakuu wa makuhani wa Kiyahudi pamoja na waandishi na wazee waliokuwa wakimdhihaki, si maneno yake yeye Yesu. Hao walikuwa wakimzulia kuwa anadai uwana wa Mungu, na anadai kuwa ni Mfalme wa Israeli. Aghlabu waliokuwa wakimwita Mwana wa Mungu walikuwa ama wendawazimu, wenye pepo wachafu, au askari wa Kirumi ambao tokea hapo wao ni washirikina, mapagani. Ama mwenyewe Yesu alikuwa daima akipendelea kujiita mwana wa Adamu kwa Kiebrani, lugha yake, Bin Adam, yaani ni binaadamu, mtu tu. Katika Injili jina hili la Yesu kuitwa mwana wa Adamu limetajwa yapata mara 80. Makhasimu zake wa Kiyahudi walimzulia kuwa alidai kuwa ni Mfalme wa Mayahudi ili kumchongea kwa watawala wa Kirumi, na kuwa alidai kuwa ni Mwana wa Mungu ili apate kuchusha kwa Mayahudi.


Francis Young, Mwalimu wa mafunzo ya Agano Jipya katika Chuo Kikuu cha Birmingham, Uingereza, akiandika katika kitabu kinachoitwa The Myth of God Incarnate (Uwongo wa Mungu kuwa Mtu) anasema:



"Isipokuwa katika Injili ya Yohana, ambako maneno ya maelezo yamewekwa kwenye mdomo wa Yesu, injili zote nyengine zinaeleza kuwa wenye kutumia maneno kama 'Mtakatifu wa Mungu', au 'Mwana wa Daudi', au 'Mwana wa Mungu' si Yesu bali wengineo. Jina pekee alilokuwa mwenyewe Yesu daima akilitumia ni 'Mwana wa Adamu'... " Yafaa pia tukumbuke kuwa katika zama za Yesu ilikuwa ni jambo lililoenea kuwabandikiza ungu viumbe vya hadithini na hata wanaadamu wa kweli kweli walio hai. Mwandishi wa kipagani Laertu alieandika kitabu kiitwacho Lives of the Philosophers (Maisha ya Mafailasufi), ameandika kuwa mafailasufi kadhaa wa kadhaa walikuwa wana wa Mungu. Plato amesimuliwa kuwa wazee wake ni miungu; hali kadhaalika Paithagoras akiaminiwa kuwa ni mwana mungu aliyekuwa mwanaadamu na mzazi wake ni mungu aitwae Hermes. Empedokles pia alidaiwa kuwa ni mungu wa milele aliyekuwa akiponyesha wagonjwa, na wafwasi wake wakimuabudu na kumsalia. Plutarch, mwandishi mwengine wa zama hizo, alikuwa anaamini kuwa bila ya shaka yo yote Alexander (Iskandar) Mkubwa ni mwana wa mungu, na Romulus, huyo anayedhaniwa kuwa ndiye baba wa Warumi, alikuwa ni Mwana wa Mars (Marrikh), mungu wa vita. Yeye akiaminiwa kuwa alipaa mbinguni katika kiwingu. Yapo maandishi ya mwaka 48 K.K. (Kabla ya Yesu) yaliyomweleza Juliasi Kaisari, Mtawala maarfu wa Warumi, kuwa ni 'mungu wa kweli, mwana wa Ares na Aphrodites, mwokozi wa wote wa maisha ya wanaadamu.' Maandishi mengine yanamtaja Agosti Kaisari, aliyerithi utawala wa Juliasi, kuwa 'Mfalme wa wafalme, Kaisari, Mwana wa Mungu, mungu Agosti, mwaangalizi wa ardhi na bahari'.


Majina haya, basi, ya "mungu", "mwana wa mungu" na "Bwana" kwa kuwa yalikuwa yameenea na maarufu katika nchi za bahari ya Kati (Mediterranean) katika zama za Yesu haiwezi kukosa kuathiri mawazo ya watu ambao bado haijawavaa imani ya Mwenyezi Mungu Mmoja kama ilivyokuwa ikifunza dini ya Kiyahudi. Majina kama hayo yalikuwa yakitumiliwa ovyo na kila mtu takriban.


Na hizo hadithi za watu kama hao, ikiwa ni watu wa hadithini tu si wa kweli kweli, au watu walioishi kweli kweli duniani, zimefanana mno na hizo ambazo khalafu yake zikaaminiwa na Wakristo kuwa zimemkhusu Yesu Kristo peke yake.


Francis Young katika insha yake inayoitwa Mizizi Miwili au Matatanisho (Two roots or a Tangled Mass) ameandika:



"Tena, hatuwezi kutupilia mbali mawazo kuwa mambo kama hayo yalitokea kwa mintarafu ya Yesu. Kwa mfano, kuna kufanana kukubwa baina ya hadithi ya Romulus, kama alivyoeleza Livy, na baadhi ya hadithi zinavyoelezwa kuwa ni za Yesu katika Injili: kuzaliwa na bikra, kutiwa mimba na mungu, maisha ya kiajabu, kutoonekana mabaki yake baada ya kufa, kutokea tena baada ya kufa na kuwatuma wafuasi wake, kumwomba kwa sala. Itakuwa ni muhali kuleta ushahidi kuwa haya yote yaliigwa tu; lakini watu walioishi wakati mmoja sana huonekana kuwa wanazua hadithi zilizoelekeana."


Tukirejea kuyanukulu yaliyomo katika Biblia tunamwona Yesu mahkamani alikataa kukiri mashtaka aliyoshtakiwa kuwa yeye alidai kuwa ni Mwana wa Mungu, kama wendawazimu na mapagani walivyokuwa wakimuenezea:



Kisha Kuhani Mkuu akasimama akamwambia, Hujibu neno? Hawa wanakushuhudia nini? Lakini, Yesu akanyamaza. Kuhani Mkuu akamwambia, Nakuapisha kwa Mungu aliye hai, utuambie kama wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu. Yesu lakini nawaambieni, Tangu sasa mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija juu ya mawingu ya mbinguni.

Mathayo 26.62-64



Injili tatu za Mathayo, Marko na Luka (ambazo zimefanana) hazimtaji kabisa Yesu kuwa ni Mwana "Pekee" wa Mungu. Ni Injili ya Yohana tu ndiyo iliyokazania kumpa ungu Yesu na kumwita Mwana Pekee wa Mungu. Injili ya Yohana inasema:



Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.

Yohana 1.14



Lugha ya Yohana ni ya namna ya peke yake. Injili tatu za mwanzo, Mathayo, Marko na Luka zinamweleza Yesu ni binaadamu. Lakini Yohana amepindukia mipaka hapa kwa kumweleza Yesu kuwa ni "Neno" kwa maana aliyoipata kutokana na waandishi wa Kigiriki, sio kutokana na maandishi ya Kiyahudi. Kauli hii haikutajwa katika Injili hizo tatu za mwanzo wala katika vitabu vyote vya Agano la Kale. Katika karne ya sita kabla ya Yesu kulizuka katika maifalasufi wa Kigiriki nadhariya ya kuwa uumbaji wa ulimwengu haukuzuka ovyo lakini kwa mpango wa kiakili, na ulimwengu wote unaendeshwa kwa kufuata sharia maalumu. Sharia hii au akili hii au mpango huu waliuwita "Logos", maana yake ni "Neno". Tunaona tamko hilo linatumika katika "Bio-logy" "Geo-logy" "Psycho-logy", kwa maana ya "ilimu". Katika zile zile zama za Yesu alikuwako mwanachuoni wa Kiyahudi katika mji wa Iskandaria katika Misri ambaye alikuwa ni mwanachuoni katika ilimu za Kiyahudi na vile vile ni mtaalamu katika falsafa za Kigiriki. Alijaribu kutaka kueleza mafunzo ya Kiyahudi kwa kutumia hoja za falsafa za Kigiriki. Yeye alitumia hii kauli ya Logos au "Neno" kwa kueleza ile hekima na busara ya Mwenyezi Mungu katika kuumba. Myahudi huyu akiitwa Filo. Yohana aliitumia lugha ya huyo Filo na kuingiza ndani yake mawazo ya kipagani akachanganya falsafa ya Kigiriki kwa kumuambatishia Yesu, na kumfanya yeye Yesu ndiye "Logos" au "Neno" na hilo "Neno" lilikuwapo tangu mwanzo, na hilo "Neno"lilikuwa pamoja na Mungu, bali ndilo khasa likawa ni Mungu. Haya yote hayakusemwa kabisa na Injili zote zilizotangulia, wala Yesu mwenyewe hakuyadai, wala wanafunzi wake hawakupata kumdaia. Tena Yohana alizidi kusema:



Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

Yohana 3.16



Tunaona kwa mara ya kwanza Yesu kuitwa Mwana wa Mungu wa pekee. Lakini hata kulitumia neno "Mwana wa Mungu" kuna maana gani khasa? Tukiipitia Biblia na kufungua sahifa zake tutaona kuwa jina hilo limetumiliwa kwa watu wengi licha Yesu. Katika Agano la Kale ambalo lote limeandikwa hata kabla ya Yesu hajazaliwa tunakuta mifano kama hii:



Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao,wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.

Mwanzo 6.1-2



Misingi yake ilikazwa juu ya kitu gani?Au ni nani aliyeliweka jiwe lake la pembeni,Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja,Na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha?

Ayubu 38.6-7



Tena itakuwa ya kwamba hesabu ya wana wa Israeli itafanana na mchanga wa bahari, usioweza kupimwa wala kuhesabiwa; tena itakuwa, badala ya kuambiwa, Ninyi si watu wangu, wataambiwa, Ninyi ndio wana wa Mungu aliye hai.

Hosea 1.10



Ni dhaahiri tunaona ilikuwa ni jambo la kawaida hata kwa waandishi wa Kiyahudi wanaoamini Mwenyezi Mungu mmoja kutumia maneno kama "wana wa Mungu" kwa kukusudia "vipenzi vya Mungu", au "waja wa Mungu", yaani watu wema.


Mwanachuoni wa Biblia wa Kitaliana, Marcello Craveri, aliyeandika kitabu chake, Maisha ya Yesu (The Life of Jesus), anaamini kuwa neno hilo "Mwana wa Mungu" limegeuka maana kwa kupitiwa na miaka ya makosa ya kufasiri. Ameandika:



"Kwa hakika, Agano la Kale limetumia neno ebed Yahweh, ambalo maana yake ni 'mtumishi wa Mungu', 'mtumwa wa Mungu', 'khaadimu wa Mungu'. Matini ya Kigiriki ya Septuagint imeipa tafsiri ambayo yaweza kuwa na maana mbili, (Pais Theou), hali ya kuwa pais, kama neno puer laweza kuwa maana ya 'mvulana mdogo' au 'mtumwa'. Baada yake ilikuwa ni wepesi kuliondoa neno pais lenye maana ya 'mvulana' likatiwa neno (hyos)ambalo maana yake ni 'Mwana'."


Lugha ya Kiyahudi ya Kiebrani na lugha ya Kiarabu zina asli moja. Mfano wa hayo ni kama mathalan kutumia neno la Kiarabu Abd kama katika "Abdu-Llahi" kwa maana ya "Mtumwa wa Mwenyezi Mungu",na likaja baadae kugeuzwa na kubuniwa neno
"Ghulam" ambalo lina maana ya "Mtumishi" na vile vile "Kijana". Na khatimaye likatumiwa neno "Ibn" ambalo maana yake ni "Mwana" tu.


Hii ndio shida inayompata mtu ye yote anapotaka kujua hakika ya mafunzo ya Kikristo. Hapana kitabu cho chote duniani chenye asli ya matamshi yake Yesu wala wanafunzi wake. Wao wakisema Kiaramia, lugha ya mazungumzo zama zile huko Palastini, kama ilivyo lugha ya Kiswahili kwetu. Na lugha yao ya dini ni Kiebrania, kama ilivyo lugha ya Kiarabu kwa Waislamu po pote pale walipo, au Kilatini kwa Wakatoliki. Injili zote ziliopo hapana hata moja iliyoandikwa na kubaki katika lugha ya Kiebrania ya asli, ambayo tungeweza kuirejea tupate ukweli wa kauli za Yesu. Ziliopo zote ni tafsiri za Kigiriki. Injili za Kiebrania ziliamrishwa zote zichomwe moto. Hiyo ni amri ya Wazee wa Kanisa, na ye yote aliyeonakana nayo hukumu yake ilikuwa kifo. Inakubaliwa pia kuwa Injili zote zimeandikwa miaka mingi baada ya Yesu kwisha ondoka duniani, na zimeandikwa na watu ambao hawakumwona bali ni kwa kufuata masimulizi waliyoyasikia. Na ziliopo ni tafsiri, na tafsiri za tafsiri. Yesu hakusema maneno yake kwa Kiswahili, wala Kiingereza, wala Kilatini wala Kigiriki. Kama si kwa Kiebrania basi akifunza kwa lugha iliyofanana nayo, nayo ni Kiaramia.
Hata bila ya ubabaishi wa tafsiri ni jambo la hakika kuwa katika maandishi ya vitabu vya Biblia hili neno "mungu" likitumiwa ovyo. Tunasoma katika Agano la Kale Mwenyezi Mungu anamwambia Musa vipi yatavyokuwa makhusiano yake na nduguye Haruni:



Naye (Haruni) atakuwa msemaji wako kwa watu, hata yeye atakuwa mfano wa kinywa kwako, nawe (Musa) utakuwa mfano wa Mungu kwake.

Kutoka 4.16



Angalia tena isemavyo Zaburi:



Mimi nimesema, Ndinyi miungu, Na wana wa Aliye juu, nyote pia.

Zaburi 82.6



Utumiaji ovyo ovyo maneno hayo matakatifu kama "Mungu" au ya kufuru kama "mwana wa Mungu" yaliyotumiwa na waandishi wa Biblia yaonyesha wazi vipi imani na agano la Ibrahimu na Manabii wengine walilofungamana kwalo na Mwenyezi Mungu lilivyopotoshwa. Mayahudi ambao kumshirikisha Mwenyezi Mungu na cho chote ni mwiko walishawishiwa na watawala wao na makafiri waliokuwa wakikaa nao kutumia lugha na maneno ya kikafiri bila ya wenyewe kutambua. Sisi tunaona vipi hii leo tulivyoharibiwa hata Kiswahili chetu na watawala ambao mila na dini zao ni mbali na yetu.



Tunaona vipi maneno kama "Halali na Haramu" yalivyopotoshwa hata imekuwa yanatumiwa kuwa ni kilichoruhusiwa au kukatazwa na serikali au chama kinachotawala, wala sio kama ilivyo asli kuwa alichohalalisha na kuharimisha Mwenyezi Mungu. Tunasikia inasemwa kuna pombe ya "halali", yaani inayoruhusiwa na serikali. Tunasikia kuna majumba au mashamba yaliyopokonywa (kughusubiwa) na serikali yanaambiwa ati "yametaifishwa" kihalali. Na ilhali hapana unyan'ganyi, au wizi wa halali. Yote ni haramu. Hata hili neno "sharia" limepotoshwa pia. Sharia ni sharia ya Kiislamu tu. Ya Serikali ni "Kanuni" si sharia. Sharia ni ya Mwenyezi Mungu. Makosa anayoyafanya mcheza mpira (faul) sasa yanaitwa: Dhambi. Badala ya Nguzo Tano za Uislamu watoto wetu wanafunzwa "Nguzo tano za ujamaa".


Ni namna hivyo basi waandishi wa Biblia wa Kiyahudi ambao walikuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu mmoja waliikoroga lugha yao kwa kuwa maneno ya kikafiri ya watawala wao wa kipagani wa Kirumi na jirani zao mapagani wa Kigiriki, wa Kimisri na wengineo waliokuwa katika pande zile za mashariki ya Bahari ya Kati (Mediterranean Sea) yaliwaathiri hata wao wakawa wanayatumia kama jambo la dasturi.


Tuliyokwisha kuyanukulu ni maneno ya kutokana na sehemu ya Biblia iitwayo Agano la Kale, yaani ile sehemu iliyoandikwa kueleza mambo ya Manabii waliokuwa kabla ya Yesu. Hebu tuangalie sasa yaliyosemwa na Agano Jipya lilioandikwa baada ya Yesu. Luka anatusimulia katika Injili yake alivyohubiri Yesu:



Bali wapendeni adui zenu, tendeni mema, na kukopesha msitumaini kupata malipo, na thawabu yenu itakuwa nyingi; nanyi mtakuwa wana wa Aliye juu, kwa kuwa yeye ni mwema kwa wasiomshukuru na waovu.

Luka 6.35



Hapo twaona Yesu anawaambia wafwasi wake kuwa katika malipo ya watendao mema na kuwapenda maadui zao ni kuwa watakuwa "wana wa Aliye juu" yaani Mwenyezi Mungu. Katika Injili ya Mathayo Yesu anasema:


Heri wapatanishi;

Maana hao wataitwa wana wa Mungu.

Mathayo 5.9



Ni wazi kwa maneno haya kuwa Yesu hakujiona yeye kuwa ni "mwana wa Mungu" kwa maana ya namna ya peke yake kama linavyofundisha Kanisa. Kwa mujibu wa Biblia wote watendao mema, wapatanishi, wanaokopesha bila ya kutaraji kulipwa n.k. ni "wana wa Mungu". Hiyo ndiyo lugha ya Kibiblia, ndiyo lugha iliyokuwa ikitumiwa wakati huo. Nasi tutakuwa wajinga tukimsikia mtangazaji wa redio au T.V. kwenye uwanja wa futboli akisema: "Kafanya dhambi" kwa kuwa mchezaji kaugusa mpira kwa mkono, nasi tukaamini kuwa yule mtu kweli kafanya dhambi tunayoijua sisi, yaani kamkosa Mwenyezi Mungu na hivyo anastahiki kutiwa katika jahannam! Haya yanadhihirika wazi katika hadithi hii inayosimuliwa katika Injili ya Yohana. Mayahudi walipotaka kumpiga mawe Yesu aliwauliza kwa vitendo gani vyema alivyowaonyesha ndio wanampiga?



Wayahudi wakamjibu, Kwa ajili ya kazi njema hatukupigi kwa mawe; bali kwa kukufuru, na kwa sababu wewe uliye mwanadamu wajifanya mwenyewe u Mungu. Yesu akawajibu, Je! haikuandikwa katika torati yenu ya kwamba, Mimi nimesema, Ninyi miungu? Ikiwa aliwaita miungu wale waliojiliwa na neno la Mungu; (na maandiko hayawezi kutanguka); je! yeye ambaye Baba alimtakasa, akamtuma ulimwenguni, ninyi mnamwambia, Unakufuru; kwa sababu nalisema, Mimi ni Mwana wa Mungu?

Yohana 10.33-36



Kwa mujibu wa kauli hiyo iliyoelezwa na Yohana tunafahamu kuwa Yesu anawaambia Mayahudi kuwa ikiwa katika vitabu vyao watu wema wote wameitwa "wana wa Mungu" pana ajabu gani basi kuwa Mtume wa Mungu aliyetakasika akaitwa vile vile ni "mwana wa Mungu" kwa maana hiyo ya jumla jamala. Na haya yanawekwa wazi na maneno aliyoyanukulu huyo huyo Yohana kuwa Yesu akimwambia Mariamu Magdalene:



Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu.

Yohana 20.17



Hata Paulo naye amesema katika barua yake aliyowapelekea Warumi:



Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.

Warumi 8.14



Yohana na Paulo ndio wakubwa wa kumfanya Yesu ni Mungu, au mwana wa Mungu, lakini hata wao wametoa ushahidi wa kutosha kuwa huo "uwanamngu" wa Yesu ndio ule ule kama walio nao wote walio wema.


Mwandishi wa Kimarekani maarufu, Upton Sinclair, akiandika katika kitabu chake A Personal Jesus (Yesu Mtu) amesema:



"Na ili asidhani mtu ye yote kuwa kwa kumuita Mungu kuwa ni Baba yake, Yesu akijitangaza kuwa yeye ni Mwana wa Mungu, yafaa ibainishwe wazi ya kuwa vile vile alimwita Mungu 'Baba yenu.' Aliyasema hayo mara kumi na nane katika Agano Jipya: 'Baba yenu wa mbinguni anajua,' na kadhaalika. Alikusudia ya kuwa sote sisi ni wana wa Mungu, na yeye (Yesu) ni mmoja wao."
Ukiwa huna roho Mtakatifu ni ngumu kukubali Yesu Kristo ni mwana wa Mungu mwenye mamlaka mbinguni na duniani mpaka hapo mwisho wa huu ulimwengu utakapofika
Na pia ukiwa hauna roho Mtakatifu ni ngumu kukubali Bikira Maria ni mama wa Mungu kama alivyotamka elizabeti
 
Kwa Hiyo yesu anavyosema hakuja kuleta Amani bali upanga anamaanisha nini
Anamaanisha kila neno lake litaibua sintofahamu kati ya watu kutokana na kupotea kwa watu
Maneno yake yatawachoma watu na wale watakaoelewa na Kuwafundisha wengine habari njema basi watazua vita kati ya watu na huenda wakauawa kabisa
Ndio maana alisema anaetaka kunifuata ajikane mwenyewe kwanza na aubebe msalaba wake na kumfuata
Ndio maana akasema atakayetaka kuyaokoa maisha yake atakufa na yule ambaye yuko tayari kuyapoteza ataishi
Hii ni falsafa ya Yesu na kazi yake ya ukombozi wa dhambi
 
Ungekuwa wa maana kama ungeyuletea Sura zilizosema hayo uliyoandika. Vinginevyo ukae kimya tu.
 
Wewe unapayuka tu ndugu Ila hata Diamond anaelewa kwamba alichokumbushwa na kiongozi wake wa dini ni sahihi. Kilichobaki ni kufuata tu amri ya Shetani.
 
Back
Top Bottom