Ukweli wa alichokisema Sheikh Kipozeo kuhusu Diamond

Ukweli wa alichokisema Sheikh Kipozeo kuhusu Diamond

Wewe na huyo Kipozeo wote mambumbu hamjui kitu, mmedandia treni la waarabu tu mnapelekwa kama ng'ombe. Ule msalaba aliovaa Diamond sio wa Yesu, ile inaitwa Ethiopian cross na Rastafari wengi wanavaa ile kitu. Naweza kusema aina ya muziki na collable na Morgan Heritage ndio maana Diamond akavaa kwenye video. Mwambie Kipozeo atafute kazi ya kufanya maana hajui kitu.

Hahaha cross maana yake nini?
 
Wewe na huyo Kipozeo wote mambumbu hamjui kitu, mmedandia treni la waarabu tu mnapelekwa kama ng'ombe. Ule msalaba aliovaa Diamond sio wa Yesu, ile inaitwa Ethiopian cross na Rastafari wengi wanavaa ile kitu. Naweza kusema aina ya muziki na collable na Morgan Heritage ndio maana Diamond akavaa kwenye video. Mwambie Kipozeo atafute kazi ya kufanya maana hajui kitu.
Safiii
 
MAONI YALIYOKAA SAWA

17- MAONI YALIYOKAA SAWA

Alipokuja Nabii Muhammad s.a.w. mambo yote yaliwekwa sawa. Mafunzo safi ya Musa yalirejeshwa pahala pake, na dini ya Yesu ilisafishwa na kutolewa takataka za Upaulo. Zote dini hizo mbili, Uyahudi na Ukristo, bali dini zote zilizogeuka zilirejeshwa kwenye umbo lao la asli lisiloharibika, umbo la Uislamu. Muhammad s.a.w. alifunza kwa uwazi kabisa juu ya dhambi, na akalegeza mikazo iliyokuwa imewabana Mayahudi. Alifahamisha kuwa baadhi ya mikazo hiyo ni matokeo ya inda yao wenyewe na uasi wao, na mingine ilizuliwa na makuhani wao tu ili wazidi kuwakandamiza na kuwaendesha watakavyo wafuasi wao. Upande mwingine hakuwaacha watu wakitangatanga gizani bila ya uwongozi, wala hakuwaacha watu watende horera watakavyo au kuwaambia watazame maandishi ya kale ambayo jinsi yalivyo chafuliwa kwa maongezo na mabadiliko hata mtu hawezi kutambua lipi la kweli na lipi la uwongo, lipi la Mungu na lipi la matamanio ya binaadamu. Kuachia mambo hivyo huzidisha zogo penye fujo. La! Muhammad alikuja na Qur'ani, kitabu cha kusomwa, au kwa jina jingine, Furqan, yaani Kitabu cha kufarikisha, yaani kupambanua, baina ya haki na baatili, baina ya kweli na uwongo. Alileta Sharia, Sharia ya Kweli ya Mwenyezi Mungu, iliyomkomboa binaadamu kutokana na minyororo iliyowatatiza Mayahudi, lakini haikuacha mambo ovyo kila mtu atende atakavyo kama alivyofanya Paulo kuivunja sharia kabisa. Huo ni utumwa mwingine ambao ni mbaya zaidi, kwa kuwa ni utumwa wa ubongo na roho, kuuwachilia mwili utende upendalo na kuifunga akili isifikiri na roho isinawirike. Sharia ya Qur'ani ni sharia ya kati na kati. Dini ya Kiislamu ni ya kati na kati. Si ya kulia wala kushoto lakini ya kuongoza mbele moja kwa moja kumfikilia Mwenyezi Mungu. Anasema Mola Mlezi katika Qur'ani:



Adhabu yangu nitamfikishia nimtakaye, na rehema yangu imekienea kila kitu. Lakini nitawaandikia wale wanaomcha Mungu, na wanaotoa Zaka na wanaoziamini Aya zetu, ambao wanamfuata Mtume, Nabii asiyejua kusoma na kuandika, ambaye wanamkuta ameandikwa kwao katika Taurati na Injili, ambaye anawaamrisha mema na anawakataza maovu, na anawahalalishia vizuri, na anawaondolea mizigo yao na minyororo iliyokuwa juu yao. Basi wale waliomuamini yeye, na wakamhishimu, na wakamsaidia, na wakaifuata nuru iliyoteremshwa pamoja naye - hao ndio wenye kufanikiwa.

(Qur'ani) Al Aaraf 7.156-57



Huyu ndiye Roho wa Kweli aliyetolewa bishara yake na Yesu kama ilivyo katika Injili ya Yohana sura ya 16. Ni yeye ambaye amesimuliwa kuwa "akisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu...huyo roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote." Ni huyu Muhammad s.a.w. ndiye aliyeambiwa Nabii Musa a.s. na Mwenyezi Mungu katika Kumbukumbu la torati sura ya 18:



Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe.

Kumbukumbu 18.18



Mafunzo ya Nabii Muhammad ndiyo yale ya Nabii Isa na ndio yale ya Nabii Musa na Nabii Ibrahim na kila Nabii aliyetokana na Mwenyezi Mungu. Msingi wao ni mmoja. Sharia zaweza kukhitilafiana kwa mujibu wa zama na hali, ama Imani na mambo ya kiroho na wema na ubaya hayo ni mamoja. Qur'ani imetilia nguvu sana juu ya Imani, Imani ya Mwenyezi Mungu Mmoja, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu, Imani kamili ya fadhila na neema ya Mwenyezi Mungu.



Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake juu yenu asingelitakasika miongoni mwenu kabisa hata mmoja.

(Qur'ani) An Nur 24.21



Lakini kumuamini Mwenyezi Mungu ni kutenda yale ayapendayo. Kama asemavyo Jalaludin Rumi, mshairi sufi mkubwa: "Ukimuamini Mwenyezi Mungu muamini kwa vitendo vyako! Atika mbegu, tena ndio mtegemee Mwenyezi Mungu!" Mswahili akichukua jembe kwenda kondeni husema: "Nenda omba Mungu."


Alikuwapo mtu mmoja akamuuliza Mtume s.a.w. amwachilie ngamia wake naye akimtegemea Mwenyezi Mungu? Mtume alimjibu: "Mfunge ngamia wako, ukisha ndio mtegemee Mwenyezi Mungu."


Qur'ani imejaa maneno kama haya: "Wanaoamini wakatenda mema". Na Yesu naye amefunza haya haya kama yaliyomo katika maneno yake mwenyewe, sio ya Paulo. Na waraka wa Yakobo, nduguye Yesu, unasema hivyo hivyo.
 
Dini zenyewe zote uongo tu.

Ndiyo maana Diamond kaona huu ujinga tu. Natengeneza controversial song mniongelee nibaki juu, huku napiga hela.
 
Allah -kiarabu
God - kizungu
Mungu- kiswahili
Jehova - kiebrania
Mulungu- kichewa
Chiuta - kitumbuka


Ikiwa namaana sawa-Muumba mbigu na ardhi na vilivyomo, most merciful, most powers full, unseen, Almighty nk
Hakuna Mungu isipokuwa allah, fuatilia kwa makini hii nahau.
 
Dah,hapa kunavumbi linakuja ngoja nivae elemet maana sina maji ya kunawa uso mie.
Arab religion Club Vs Europe religion Club,hapa ni zaidi ya yanga na simba.
 
Nilimsikiliza sheikh kipozeo wakati akimzungumzia dimondi
Sina shida na alichosema kuhusu huyu mtoto wa Kiislamu bali kilichonifanya niandike haya ni maneno yake kwamba dimond kuvaa msalaba anakubali kuwa Isa alisulubiwa wakati wao Waislamu wanaamini Isa hakusulubiwa

Huenda alichosema ni sahihi kabisa lakini kuna vitu akawa havielewi

Isa = zeruzeru
Yesu = mkombozi
Au Kiebrania yehosua = Mungu mkombozi

Historia inatueleza Isa alizaliwa katika chini ya mti wa mtende lakini qurani haitaji nchi ila inasema alizaliwa mchana na mama yake ni Mariamu
Hii ni stori tofauti na inayotupa bible

Kiarabu Yesu inatamkwa Yasu na sio Isa kama Waislamu wanavyowaaminisha wenzao kuwa ni Isa

Historia ya bible inasema Yesu Kristo au Yasu kwa Kiarabu alizaliwa nchini Israeli,katika mji wa Bethlehemu na katika hori la ngo'mbe hiyo ni bible inasema hivyo

Ukiangalia kwa makini huyu Isa utagundua sio Yesu kabisa na hata kuzaliwa kwao ni tofauti na hata walichokuja kuhubiri ni tofauti

Isa alikuja kuhubiri dini mpya ya mwenyezi Mungu kwa mujibu wa historia
Wakati Yesu alikuja kuwakomboa watu na dhambi zao

So kuanzia leo Waislamu wajue Yesu sio Isa kama wanavyoaminishwa
Na wala Isa sio Yesu kama wanavyoaminishwa

Nawasilisha tu
db22e02e5263d2c889b2e2e4cec506fa.jpg
Nenda upande wa maneno magumu uangalie maana ya holi ni nini?

Halafu rejea kwenye Quran uangalie eneo alilojifungua Mariam kulikuwa na nini?
 
1. Mathayo 22:35-40
35. Mmoja wao, mwana-sheria, akamwuliza, akimjaribu
36. Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu?
37. Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote
38. Hii ndio amri iliyokuu, tena ni ya kwanza.
39. Na ya pili yafanana nayo, nayo ni MPENDE JIRANI YAKO kama Nafsi yako.
40. Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii

2. 1Korintho 13:13
Basi sasa inaumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo

3. 1.Waraka wa Yohana 4:16
Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini.
Mungu ni UPENDO, naye akaaye katika pendo hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake.

Kama wewe ni Christian na humpendi Muslim then you are nothing.
 
Huyu nae kaona Diamond ndio muislamu wa kwanza kuvaa msalaba? by The way Mungu wetu Sote! Kinachonikera toka kwa Waislamu ni Ubaguzi wao! Sasa huyo anaongelea nn hapo
Mkuu unaweza kuongelea huo ubaguzi ulio uona juu ya waislam.
 
Mkuu unaweza kuongelea huo ubaguzi ulio uona juu ya waislam.
Hivi unajua ukinuka kikwapa mara nyingi hujisikii bali uliokaa nao ndio hujua jamaa anatema. Kama kisasi ni suna, basi ubaguzi lazma uwepo.
 
Back
Top Bottom