Isa = zeruzeru
Yesu = mkombozi
Au Kiebrania yehosua = Mungu mkombozi
Historia inatueleza Isa alizaliwa katika chini ya mti wa mtende lakini qurani haitaji nchi ila inasema alizaliwa mchana na mama yake ni Mariamu
Hii ni stori tofauti na inayotupa bible
Huu ndio uzao wa Issa Bin Mariam according to Quran Sura ya 19.
20. (Malaika) akasema: Hakika mimi ni Mjumbe wa Mola wako; ili nikupe mwana mtakatifu.
21. (Mariamu) akasema: Ninawezaje kupata mtoto hali hajanigusa mwanamume ye yote wala mimi si asherati?
22. (Malaika) akasema: Ni kama hivyo; Mola wako Amesema: Haya ni rahisi Kwangu, na ili Tumfanye Ishara kwa wanadamu na rehema itokayo Kwetu; na ni jambo limekwisha hukumiwa.
23. Basi akambeba mimba, na akaondoka naye mpaka mahali pa mbali.
24.
Kisha uchungu ukampeleka penye shina la mtende, akasema: Laiti ningekufa kabla ya haya, na ningekuwa sahau iliyosahauliwa.
25. Mara ikamfikia sauti kutoka chini yake: Usihuzunike, hakika Mola wako Ameweka kijito chini yako;
26. Na ulitikise kwako shina la mtende, litakuangushia tende nzuri, zilizo mbivu.
27. Basi ule na unywe na uburudishe macho; na kama ukimwona mtu ye yote, useme: Hakika mimi nimeweka nadhiri
kwa Mungu wa rehema ya kufunga saumu, kwa hiyo leo sitasema na mtu.
Biblia nayo, kupitia Matayo 1: 1-7 hivi ndivyo inavyosema:
1 Siku zile, tangazo rasmi lilitolewa na Kaisari Augusto kuwataka watu wote nchini kote wahesabiwe.
2 Sensa hiyo ilikuwa mara ya kwanza, wakati Kurenio alipokuwa mkuu wa mkoa wa Siria.
3 Basi, wote waliohusika walikwenda kuhesabiwa kila mtu katika mji wake.
4 Yosefu pia alifanya safari kutoka mjini Nazareti mkoani Galilaya, na kwa vile alikuwa wa jamaa na ukoo wa Daudi, alikwenda mjini Bethlehemu mkoani Yudea, alikozaliwa mfalme Daudi.
5 Alikwenda kuhesabiwa pamoja na mchumba wake Maria ambaye alikuwa mjamzito.
6 Walipokuwa huko, siku yake ya kujifungua ikawadia,
7
akajifungua mtoto wake wa kwanza wa kiume, akamvika nguo za kitoto, akamlaza horini kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.
Now, hivi jambo la kiroho hasa linapokuja suala la uzao wa Yesu ni sehemu gani alizaliwa au ni wapi na namna gani alizaliwa?! Kwa mfano, ni ipi hoja ya kiroho inayoonesha uwezo wa Mungu kati ya Yesu kuzaliwa kwa mama ambae hakupata kuingiliwa as per bible na Kuran kwa upande wa Issa; au hoja ya kuzaliwa kwenye zizi la kondoo kama inavyodai Bible au kuzaliwa chini ya mtende kama inavyodai Quran?!
Second, ingawaje Waislamu wanaamini kwamba Issa Bin Mariam alizaliwa chini ya mti wa mtende, hapo juu Quran imeishia tu kusema kwamba
uchungu ukampeleka penye shina la mtende na wala haijatuambia kwamba alizalia hapo chini ya mtende!!!
Na hata ukiangalia Quran hapo juu kwenye BLUE, utaona bado Mariamu analalamikia uchungu kwa sababu, mtu ambae tayari ameshajifungua hana sababu ya kusema
Laiti ningekufa kabla ya haya, na ningekuwa sahau iliyosahauliwa.. Hapo inaonesha wazi kwamba bado anaugulia uchungu hapo kwenye mtende!!!
Likewise, wakati Wakristo wanaamini Yesu alizaliwa kwenye zizi la kondoo, hapo juu Biblia inaishia tu kutuambia kwamba
akajifungua mtoto wake wa kwanza wa kiume, akamvika nguo za kitoto,
akamlaza horini! Suala la hori limetajwa kwenye kumlaza mtoto lakini haijatuambia kwamba alimzaa horini unless kama kuna Aya zingine zinasema vinginevyo!
So, what if baada ya Mariam kushikwa uchungu hapo kwenye mtende, hapo hapo alijifungua lakini kwavile asingeweza kukaa na mtoto mchanga sehemu ya wazi, ndipo akaenda kumlaza horini?!
Or, what if baada ya uchungu kumzidi, akajivuta hadi sehemu ambayo si Kuran wala Biblia imepataja, kisha akajifungua hapo lakini kwavile asingeweza kukaa na mtoto mchanga sehemu hiyo, ndipo akaenda kumlaza horini?!
Ukweli mchungu ni kwamba, both Bible na Quran simulizi zao huwa zina-missing pieces!!