Habari za Sasa hivi hope everyone is fine,
Bhana eeh siku moja, nilikuwa naongea na rafiki yangu wa muda mrefu, Rasi. Nilijua kuwa alikuwa ameanza kufanya kazi online, lakini sikuwahi kuelewa vizuri ni kazi gani hasa alikuwa anafanya. Tulikuwa tunakutana mara chache, lakini kila tukikutana, maisha yake yalikuwa yanabadilika kwa kasi sana.
Nilianza kushangaa baada ya kuona mabadiliko yake—kutoka kwa kuvaa kawaida hadi kuvaa mavazi ya kifahari, kutoka kwa kutumia simu ya kawaida hadi kuwa na flagship ya iPhone mpya kila mwaka.
Siku moja, nilimkazia macho na kumwambia, “Rasi eeh, sikuelewi kabisa. Juzi tu tulikuwa tunahangaika wote kutafuta hela, leo hii maisha yako ni kama ya mtu aliyeshinda jackpot. Nifungukie basi, unafanya nini?”
Alitabasamu, kisha akasema kwa sauti ya utulivu, “Bro, ni cryptocurrency. Hapa ndipo pesa ipo.”
Nilishtuka kidogo. Nilishasikia kuhusu crypto mara nyingi, lakini sikuwahi kuichukulia kwa uzito. “Basi nifundishe nami nianze?” nilimuuliza kwa hamu.
Alitingisha kichwa na kunitazama kwa macho makali. “Hapana bro, hii mishe si ya kila mtu. Ukiingia bila kuelewa, unaweza kupoteza kila kitu.”
Nilimsihi, nikamwambia niko tayari kujifunza, lakini bado hakutaka kunifundisha. Nilijaribu kumuuliza jamaa zetu wa karibu kama wanajua anachofanya hasa, lakini hakuna aliyekuwa na majibu kamili.
Ndipo nikajua kuwa si kila mtu atakusaidia kwenye njia ya mafanikio. Nikasema, ikiwa Rasi hataki kunifundisha, basi siwezi kukata tamaa. Nikaamua kutafuta njia mbadala.
Nikajiunga na magroup mbalimbali, nikasoma makala, na nikaanza kufuatilia mijadala ya cryptocurrency. Hatimaye, nikagundua kuwa wadau wengi wanashare maarifa kwenye forum kama Jamii Forums. Nikajiambia, kama kuna mtu anayeweza kutufundisha, basi ni wadau wa JF.
Sasa, wadau, njooni hapa mtufundishe. Crypto ni real, lakini bila mwongozo, mtu anaweza kuingia kichwa kichwa na kuumia. Kama kuna mtu mwenye maarifa ya kutosha kuhusu crypto, mining, staking, trading, na hata airdrops, tafadhali tujuzeni!
Wadau mpo?