Ukweli wa uwepo wa Mungu na Makazi yake upo hapa

Tofauti ni iliyopo ni kwamba ukiamini kitu hupelekea usiwe na uhakika kama hicho kitu kipo au hakipo.

Ila usipoamini hapo utakuwa unahitaji ujue ukweli wa hicho kitu kiundani zaidi.
Na pia nisipoamini huenda nisihitaji kuumiza kichwa...
 
Ni kila chenye utata kimeundwa na kila kitu ktk ulimwengu huu ni kazi ya Mungu.
Kwa mantiki hiyo utakuwa unasema hata Mungu mwenyewe kaumbwa, na aliyemuumba kaumbwa, na aliyemuumba aliyemuumba kaumbwa, bila mwisho.

Ad infinitum, ad nausea.
 
Aisee unawaza kama Mimi, nilishawahi sumbua sana walimu wangu wa dini juu ya hili. Mungu katutofautisha na wanyama wengine kwa kutuwekea "intellect".... Sasa swala la kufikilia exact location ya Mungu anakoishi ni Uhuru wa Mawazo aliyopewa mwanadamu. Ukilitizama jua kwa macho yako utaishia kutoa machozi tu. Miaka mingi kabla hata imani hizi hazijaja...watu walikuwa wanabudu Jua. Ndio maana sehemu ambazo jua linaangaza (tropics, ikweta) kisawasawa zimebarikiwa na utajili wa Madini na uoto wa asili, wanyama ambao sehemu zingine haupo. Masaa 12 ya mwanga, 12 ya Giza. Kwa maana hiyo, tukichukulia kuwa Kweli Mungu yupo kwenye Jua ...nchi za Africa zipo karibu na Mungu kuliko zingine. Sayari zote na nyota zategemea jua....watu Mawazo yako kitumwa, wanaweza mzungu asemacho ndicho sahihi,ndio unasikia wanakuuliza methodology, sijui NASA...
 
Tofauti ni iliyopo ni kwamba ukiamini kitu hupelekea usiwe na uhakika kama hicho kitu kipo au hakipo.

Ila usipoamini hapo utakuwa unahitaji ujue ukweli wa hicho kitu kiundani zaidi.
Tofauti ni iliyopo ni kwamba ukiamini kitu hupelekea usiwe na uhakika kama hicho kitu kipo au hakipo.

Ila usipoamini hapo utakuwa unahitaji ujue ukweli wa hicho kitu kiundani zaidi.
Mkuu ni kweli mtu ukiwa hauna msimamo wakiita wanawake , wanaume, watoto, utaenda kwa kuwa hujui unachokifanya
 
Kwa mantiki hiyo utakuwa unasema hata Mungu mwenyewe kaumbwa, na aliyemuumba kaumbwa, na aliyemuumba aliyemuumba kaumbwa, bila mwisho.

Ad infinitum, ad nausea.

Mkuu, wewe unafahamu mengi sana una uelewa mkubwa sana, ni vile unaumiza kichwa chako kwa vitu vilivyo wazi ama kwa kusudi ya dhamira ya kimsongo naamini unafaham nn unafanya.

Lakini sijui kwanini ukweli wako wa kumjua Mungu una uficha?

Naomba unijibu; Unadhani Dunia imeumbwa?

Au Dunia imekuwapo tuu?
 
Dunia imeumbwa au imekuwapo tu?

Majibu yote mawili hayakubali kuwapo kwa Mungu.

Kama dunia imeumbwa, kwa sababu hakuma chenye maajabu mengi kama ya dunia na complexity ya hali ya juu kinaweza kutokea chenyewe, basi aliyeiumba atakuwa na maajabu na complexity zaidi.

Tukitumia kanuni yetu ya kwamba hamna chenye complexity kinachoweza kutokea chenyewe, aliyeiumba dunia naye atahitaji kuwa kaumbwa, aliyemuumba aliyemuumba naye atakuwa kaumba, aliyemuumba aliyemuumba aliyemuumba naye atakuwa kaumbwa na msururu huu hautakuwa na mwisho.

Katika ulimwengu kama huo hakuna Mungu.

Kama dunia haijaumbwa, ipo tu, then katika ulimwengu huo hatumuhitaji Mungu kwa sababu vitu vinaweza kutokea vyenyewe tu na sababu kubwa ya Mungu ya "creatir and first mover" inaondolewa.

Ulimwengu huu nao haumuhitaji Mungu.

Kwa hiyobutaona jibu lolote la swali lako linaturudisha kwenye ukweli mmoja tu.

Mungu hayupo.
 
Kwa mantiki hiyo utakuwa unasema hata Mungu mwenyewe kaumbwa, na aliyemuumba kaumbwa, na aliyemuumba aliyemuumba kaumbwa, bila mwisho.

Ad infinitum, ad nausea.
Umungu ni Ukuu usio na mwanzo wala mwisho ni kile kilichopelelekea Ulimwengu kuwepo Dunia yetu katika Ulimwengu huu ni sawa na yai la mjusi labda ktk Africa nzima ni namba zisizohesabika ukiamua ukiamua kuyapanga bara zima la Africa.

Mungu hakuumbwa yupo ni yuleyule milele na milele.

Umungu ni uweza usiopimika vyote vimekuwapo kwa yeye.
 
Hujathibitisha, umesema tu.

Ni kama mimi nikwambie Mungu ni mnazi uliopo shambani kwetu.

Mimi kusema hivyo hakuthibitishi mnazi huo ndio Mungu.

Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
 
Unaamini Ulimwengu upo umekuwapo kwa sababu gani?
 
Unaamini Ulimwengu upo umekuwapo kwa sababu gani?
Sitaki kuamini, nataka kujua.

Ulimwengu upo kwa sababu Mungu wenu wa vitabuni mwenye ujuzi wote, uwezo wote na upendo wote hayupo.

Unajua kwa nini?
 
Hujathibitisha, umesema tu.

Ni kama mimi nikwambie Mungu ni mnazi uliopo shambani kwetu.

Mimi kusema hivyo hakuthibitishi mnazi huo ndio Mungu.

Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
Mungu yupo kwa sababu kila kilichotokea kina usanifu na msanifu ni Mungu.

Unafahamu uhai ulipandikizwa?
 
Mungu yupo kwa sababu kila kilichotokea kina usanifu na msanifu ni Mungu.

Unafahamu uhai ulipandikizwa?
Kama kila kilichotopo kina msanifu, na Mungu naye atahitaji msanifu, na msanifu wake atahitaji msanifu hivyo hivyo bila mwisho.

Na kama Mungu hana msanifu, basi si kweli kwamba kila kilichopo kinahitaji msanifu na hata Mungu mwenyewe kama msanifu hahitajiki kuwepo.
 
Ni mengi sana kuhusu Jua( nyota ) yanafikirisha sana.
 
Mkuu huo itakuwa ni uwezo wako kufikiri ni mdogo ukaamua usijue chochote
Lakini pia nao ni uchaguzi .
Hautaji kuniambia ni uwezo mdogo... kwani followers wa udini ni wenye uelewa duni. Dini haitaji uwe na akili dana bali ukiwa mpumbavu sana ndio unaielewa vizuri....
 
Imekuwepo tu... utasemaje imeumbwa wakati inaumbwa haukuwepo... why unafanya imaginations.
 
Kama mungu hakuumbwa... why dunia na vinginevyo viwe vimeumbwa???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…