Ukweli wa uwepo wa Mungu na Makazi yake upo hapa

Ukweli wa uwepo wa Mungu na Makazi yake upo hapa

Tofauti ni iliyopo ni kwamba ukiamini kitu hupelekea usiwe na uhakika kama hicho kitu kipo au hakipo.

Ila usipoamini hapo utakuwa unahitaji ujue ukweli wa hicho kitu kiundani zaidi.
Na pia nisipoamini huenda nisihitaji kuumiza kichwa...
 
Ni kila chenye utata kimeundwa na kila kitu ktk ulimwengu huu ni kazi ya Mungu.
Kwa mantiki hiyo utakuwa unasema hata Mungu mwenyewe kaumbwa, na aliyemuumba kaumbwa, na aliyemuumba aliyemuumba kaumbwa, bila mwisho.

Ad infinitum, ad nausea.
 
Kuanzia 1999 mpaka sasa zaidi ya miaka 16 nimekuwa nikifanya utafiti wapi yalipo makazi ya Mwenyezi Mungu Kisayansi na Kutumia Vitabu vitakatifu hasahasa Biblia Takatifu nimepata majibu pasina shaka kila mumoja wetu atakubaliana nayo.

Utafiti huu haulengi kumchafua mtu mtu yeyote kwa imani yake naomba atakayeshindwa kuelewa asiwe na jaziba maana ni utafiti wangu binafsi.

KISAYANSI; Mpangilio na Usanifu wa muundo wa Ulimwengu wetu ni mpangilio uliofanywa kwa usahihi ndio maana kila kitu kipo katika sehemu yake bila kuathiri kingine kwa mfano; Dunia na Sayari zote katika mfumo wa Jua letu zinalizunguka Jua kwa kasi lakini haziwezi kugongana Na katika Anga yetu kuna Nyota mamilioni na pia Kuna Majua Mengine yametengeneza mifumo mifumo ya Sayari kama tuliyo nayo katika Jua letu, Vitu hivi vinaonekana kwa mbali na haviwezi kufikika kwa urahisi kwa akili za Kibinadamu.

Nina hakika Mwenyezi Mungu anaishi katika mojawapo ya Nyota za Jua kwa kuwa hakuwezi kufikika kwakua kuna joto {moto} kali sana hakuna chochote kinaweza kukaribia hata kwa kilometa milioni moja.

Katika Jua ndimo kulimo uhai Jua ndicho kitu ambacho hakiwezi kusogelewa wala kuchunguzwa na kitu chochote hata kama utatumia kiona mbali utaishia kuvaa miwani ya kuzuia mwanga ili macho yako yasipofuke kwa miale mikali ya Mwanga wa jua.

Hata Uhai wa viumbe wote hai hutegemea Jua ndiyo maana katika Bara Antaktika uwezekano wa viumbe hai kuishi ni mdogo kwa sababu hupata kiasi kidogo cha jua katika msimu wa mzunguko wa Dunia Ni aina Flani ya Bakteria huweza kuishi katika eneo hilo na Samaki wanaositahimili baridi kari INAYOPELEKEA MAJI KUGANDA NA KUWA BARAFU, NA ENEO LOTE LA BARA ANTAKTIKA NI BARAFU NA MVUA INAYONYESHA NI KWA MARA MOJA KATIKA msimu wa Mwaka.

Jua haliwezi kukalibiwa na kitu chochote kwa maana hiyo Jua linatunza Nafsi Takatifu iliyo hai hakuna chochote chenye mwili au Kitu kinacho weza kusogelea jua kikawa salama kitaungua na kunasa katika Jua.

JUA ndio kitu Kitukufu ambacho mwanadamu kwa uelewa wake hawezi kufikia wala kujaribu kufanyia utafiti.

Katika utafiti wangu nimejifunza kwa kuwa Jua ndilo lina Uhai kwa Viumbe basi kuna uwezekana mkubwa wa 94.6% Muumba anaishi katika Jua Sehemu Tukufu isiyoweza kusogelewa na uchafu wa aina yoyote ya mwanadam.

BIBLIA TAKATIFU (UTAFITI)

Katika vitabu Agano la kale Mwenyezi Mungu anatolewa Sadaka za kuteketezwa, Wanafukiza ubani katika sehemu walizojenga Nyumba za Ibada kwaajiri ya MWENYEZI MUNGU.

Kwanini aunguziwe vitu apokee sadaka kwa moshi?

Kwanini asipewe ng'ombe au Kondoo mzima mpaka achomwe aunguzwe? Ni kwasababu Nafsi ya Mungu inaishi katika moto na Inapokea katika moto.

Kwanini makanisa Mengi yanachoma Ubani katika Nyumba zao za Ibada, Kwanini wasitengeneze Marashi yenye harufu ya Ubani?

Wanachoma kwa kuwa mlengwa Mtukufu anapokea Vitukufu katika moto mjue ya kuwa kila kitu kikichomwa kinatoka katika hali hali nzuri au mbaya hata Dhahabu ili Ing'ae ni lazima ichomwe katika moto.

Kutoka 19: 16-20 Inaelezea jinsi musa anapewa Amri 10 na Mungu na Mwenyezi Mungu anamwambia Musa watu wajitakase kabla ya kukalibia mlima na Mawinguni Kunatokea Radi, Ngurumo na Umeme na Mungu anashuka katika moto na kumpa amri Musa Mlima Sinai unatetemeka kwa utisho Unafuka moshi mkali kama moshi wa tanuu unafunika Mlima wote.

Kwanini Mungu atokee katika moto?

Ni kwa sababu anataka watu wajue Nafsi Tukufu ya Mungu inaishi katika Moto ANAKUJA KWA STAILI YA MAISHA YAKE KWA MAZINGIRA ANAYO ISHI LAKINI WANADAMU WANASHINDWA KULIJUA HILO.

KAMA MUNGU ANALETA AMRI 10 KWA STAILI YA MOTO BASI YEYE ANAISHI KATIKA MOTO KWA HIYO UTUKUFU WA MUNGU HATUWEZI KUUFIKIA BILA MWILI KUFA IKABAKI NAFSI.

Kwa hiyo KIFO NI FAIDA NA NDIO STAREHE YA PEKEE ALIYOTUZAWADIA MWENYEZI MUNGU KWA KUWA TUTAISHI KATIKA UTUKUFU KAMA NAFSI ILIYO KARIBU NA MUNGU BILA KUFA WEWE NI MTUMWA WA DUNIA.
Uwe TAJIRI, uwe MASIKINI wewe ni MTUMWA wa DUNIA hakuna RAHA UTAKULA KWA JASHO, UTALALA KWA KUJIGEUZA GEUZA USIUMIZE UPANDE MMOJA WA MWILI,

Duniani hapa tupo kwa ajili ya kuandaa Maisha ya Utukufu wa milele kama nafsi Katika Jua.

Utafiti wangu unaendelea kadiri Mungu atakavyonijalia ntawaletea ninayoendelea kujifunza Pia ninajitahidi kutafuta njia ya Kitaalamu ya kuweka Video katika kiona mbali ili niweze kuwashirikisha kwa yale ambayo mimi naendelea kuyavumbua kwa kutumia kiona mbali Ninazunguka sehemu mbali mbali kujifunza jinsi Dunia yetu ilivyo na ni kazi ngumu ila ninapata michango ya mawazo kwa watu wengi sana ambao ninawashirikisha sehemu mbalimbali za Dunia.

KARIBUNI KWA MAONI NA USHAURI..
Aisee unawaza kama Mimi, nilishawahi sumbua sana walimu wangu wa dini juu ya hili. Mungu katutofautisha na wanyama wengine kwa kutuwekea "intellect".... Sasa swala la kufikilia exact location ya Mungu anakoishi ni Uhuru wa Mawazo aliyopewa mwanadamu. Ukilitizama jua kwa macho yako utaishia kutoa machozi tu. Miaka mingi kabla hata imani hizi hazijaja...watu walikuwa wanabudu Jua. Ndio maana sehemu ambazo jua linaangaza (tropics, ikweta) kisawasawa zimebarikiwa na utajili wa Madini na uoto wa asili, wanyama ambao sehemu zingine haupo. Masaa 12 ya mwanga, 12 ya Giza. Kwa maana hiyo, tukichukulia kuwa Kweli Mungu yupo kwenye Jua ...nchi za Africa zipo karibu na Mungu kuliko zingine. Sayari zote na nyota zategemea jua....watu Mawazo yako kitumwa, wanaweza mzungu asemacho ndicho sahihi,ndio unasikia wanakuuliza methodology, sijui NASA...
 
Tofauti ni iliyopo ni kwamba ukiamini kitu hupelekea usiwe na uhakika kama hicho kitu kipo au hakipo.

Ila usipoamini hapo utakuwa unahitaji ujue ukweli wa hicho kitu kiundani zaidi.
Tofauti ni iliyopo ni kwamba ukiamini kitu hupelekea usiwe na uhakika kama hicho kitu kipo au hakipo.

Ila usipoamini hapo utakuwa unahitaji ujue ukweli wa hicho kitu kiundani zaidi.
Mkuu ni kweli mtu ukiwa hauna msimamo wakiita wanawake , wanaume, watoto, utaenda kwa kuwa hujui unachokifanya
 
Kwa mantiki hiyo utakuwa unasema hata Mungu mwenyewe kaumbwa, na aliyemuumba kaumbwa, na aliyemuumba aliyemuumba kaumbwa, bila mwisho.

Ad infinitum, ad nausea.

Mkuu, wewe unafahamu mengi sana una uelewa mkubwa sana, ni vile unaumiza kichwa chako kwa vitu vilivyo wazi ama kwa kusudi ya dhamira ya kimsongo naamini unafaham nn unafanya.

Lakini sijui kwanini ukweli wako wa kumjua Mungu una uficha?

Naomba unijibu; Unadhani Dunia imeumbwa?

Au Dunia imekuwapo tuu?
 
Dunia imeumbwa au imekuwapo tu?

Majibu yote mawili hayakubali kuwapo kwa Mungu.

Kama dunia imeumbwa, kwa sababu hakuma chenye maajabu mengi kama ya dunia na complexity ya hali ya juu kinaweza kutokea chenyewe, basi aliyeiumba atakuwa na maajabu na complexity zaidi.

Tukitumia kanuni yetu ya kwamba hamna chenye complexity kinachoweza kutokea chenyewe, aliyeiumba dunia naye atahitaji kuwa kaumbwa, aliyemuumba aliyemuumba naye atakuwa kaumba, aliyemuumba aliyemuumba aliyemuumba naye atakuwa kaumbwa na msururu huu hautakuwa na mwisho.

Katika ulimwengu kama huo hakuna Mungu.

Kama dunia haijaumbwa, ipo tu, then katika ulimwengu huo hatumuhitaji Mungu kwa sababu vitu vinaweza kutokea vyenyewe tu na sababu kubwa ya Mungu ya "creatir and first mover" inaondolewa.

Ulimwengu huu nao haumuhitaji Mungu.

Kwa hiyobutaona jibu lolote la swali lako linaturudisha kwenye ukweli mmoja tu.

Mungu hayupo.
 
Kwa mantiki hiyo utakuwa unasema hata Mungu mwenyewe kaumbwa, na aliyemuumba kaumbwa, na aliyemuumba aliyemuumba kaumbwa, bila mwisho.

Ad infinitum, ad nausea.
Umungu ni Ukuu usio na mwanzo wala mwisho ni kile kilichopelelekea Ulimwengu kuwepo Dunia yetu katika Ulimwengu huu ni sawa na yai la mjusi labda ktk Africa nzima ni namba zisizohesabika ukiamua ukiamua kuyapanga bara zima la Africa.

Mungu hakuumbwa yupo ni yuleyule milele na milele.

Umungu ni uweza usiopimika vyote vimekuwapo kwa yeye.
 
Hujathibitisha, umesema tu.

Ni kama mimi nikwambie Mungu ni mnazi uliopo shambani kwetu.

Mimi kusema hivyo hakuthibitishi mnazi huo ndio Mungu.

Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
 
Sunia imeumbwa au imekuwapo tu?

Majibu yote mawili hayakubali kuwapo kwa Mungu.

Kama dunia imeumbwa, kwa sababu hakuma chenye maajabu mengi kama ya dunia na complexity ya hali ya juu kinaweza kutokea chenyewe, basi aliyeiumba atakuwa na maajabu na complexity zaidi.

Tukitumia kanuni yetu ya kwamba hamna chenye complexity kinachoweza kutokea chenyewe, aliyeiumba dunia naye atahitaji kuwa kaumbwa, aliyemuumba aliyemuumba naye atakuwa kaumba, aliyemuumba aliyemuumba aliyemuumba naye atakuwa kaumbwa na msururu huu hautakuwa na mwisho.

Katika ulimwengu kama huo hakuna Mungu.

Kama dunia haijaumbwa, ipo tu, then katika ulimwengu huo hatumuhitaji Mungu kwa sababu vitu vinaweza kutokea vyenyewe tu na sababu kubwa ya Mungu ya "creatir and first mover" inaondolewa.

Ulimwengu huu nao haumuhitaji Mungu.

Kwa hiyobutaona jibu lolote la swali lako linaturudisha kwenye ukweli mmoja tu.

Mungu hayupo.
Unaamini Ulimwengu upo umekuwapo kwa sababu gani?
 
Unaamini Ulimwengu upo umekuwapo kwa sababu gani?
Sitaki kuamini, nataka kujua.

Ulimwengu upo kwa sababu Mungu wenu wa vitabuni mwenye ujuzi wote, uwezo wote na upendo wote hayupo.

Unajua kwa nini?
 
Hujathibitisha, umesema tu.

Ni kama mimi nikwambie Mungu ni mnazi uliopo shambani kwetu.

Mimi kusema hivyo hakuthibitishi mnazi huo ndio Mungu.

Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
Mungu yupo kwa sababu kila kilichotokea kina usanifu na msanifu ni Mungu.

Unafahamu uhai ulipandikizwa?
 
Mungu yupo kwa sababu kila kilichotokea kina usanifu na msanifu ni Mungu.

Unafahamu uhai ulipandikizwa?
Kama kila kilichotopo kina msanifu, na Mungu naye atahitaji msanifu, na msanifu wake atahitaji msanifu hivyo hivyo bila mwisho.

Na kama Mungu hana msanifu, basi si kweli kwamba kila kilichopo kinahitaji msanifu na hata Mungu mwenyewe kama msanifu hahitajiki kuwepo.
 
Aisee unawaza kama Mimi, nilishawahi sumbua sana walimu wangu wa dini juu ya hili. Mungu katutofautisha na wanyama wengine kwa kutuwekea "intellect".... Sasa swala la kufikilia exact location ya Mungu anakoishi ni Uhuru wa Mawazo aliyopewa mwanadamu. Ukilitizama jua kwa macho yako utaishia kutoa machozi tu. Miaka mingi kabla hata imani hizi hazijaja...watu walikuwa wanabudu Jua. Ndio maana sehemu ambazo jua linaangaza (tropics, ikweta) kisawasawa zimebarikiwa na utajili wa Madini na uoto wa asili, wanyama ambao sehemu zingine haupo. Masaa 12 ya mwanga, 12 ya Giza. Kwa maana hiyo, tukichukulia kuwa Kweli Mungu yupo kwenye Jua ...nchi za Africa zipo karibu na Mungu kuliko zingine. Sayari zote na nyota zategemea jua....watu Mawazo yako kitumwa, wanaweza mzungu asemacho ndicho sahihi,ndio unasikia wanakuuliza methodology, sijui NASA...
Ni mengi sana kuhusu Jua( nyota ) yanafikirisha sana.
 
Mkuu huo itakuwa ni uwezo wako kufikiri ni mdogo ukaamua usijue chochote
Lakini pia nao ni uchaguzi .
Hautaji kuniambia ni uwezo mdogo... kwani followers wa udini ni wenye uelewa duni. Dini haitaji uwe na akili dana bali ukiwa mpumbavu sana ndio unaielewa vizuri....
 
Mkuu, wewe unafahamu mengi sana una uelewa mkubwa sana, ni vile unaumiza kichwa chako kwa vitu vilivyo wazi ama kwa kusudi ya dhamira ya kimsongo naamini unafaham nn unafanya.

Lakini sijui kwanini ukweli wako wa kumjua Mungu una uficha?

Naomba unijibu; Unadhani Dunia imeumbwa?

Au Dunia imekuwapo tuu?
Imekuwepo tu... utasemaje imeumbwa wakati inaumbwa haukuwepo... why unafanya imaginations.
 
Umungu ni Ukuu usio na mwanzo wala mwisho ni kile kilichopelelekea Ulimwengu kuwepo Dunia yetu katika Ulimwengu huu ni sawa na yai la mjusi labda ktk Africa nzima ni namba zisizohesabika ukiamua ukiamua kuyapanga bara zima la Africa.

Mungu hakuumbwa yupo ni yuleyule milele na milele.

Umungu ni uweza usiopimika vyote vimekuwapo kwa yeye.
Kama mungu hakuumbwa... why dunia na vinginevyo viwe vimeumbwa???
 
Back
Top Bottom